Ilipoishia
Kupitia daraja la Kigamboni, Mzee Shayo aliendesha Subaru kama yupo kwenye mbio za Magari, wakati huo Barabara zilikuwa nyeupe, Watu wengi waliogopa kupoteza uhai wao, walibakia majumbani mwao huku wachache wakiendelea kufanya safari, ilimuwezesha Mzee Shayo kufika Ikulu ya Magogoni haraka sana, alikuta ulinzi umeimarishwa hapo lakini alipowatazama Walinzi hao alijikuta akikata tamaa, aliona ni ngumu sana kupambana na huyo Mwanaume anayeitwa Chogo. Endelea
SEHEMU YA PILI
Aliuliza mahali ambapo Rais wa Nchi alikuwa amehifadhiwa kwa ajili ya usalama, ilikuwa ni ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na milango ya umeme, chumba hicho kilipatikana katikati ya jengo la Ikulu.
Rais akiwa na waziri Mkuu ndani ya chumba hicho walimuona Mzee Shayo akiingia huku sura yake ikionesha kukosa tumaini, Rais alimdaka Mzee Shayo
“Shayo! Nini kinaendelea?” Aliuliza Rais huyo aliyeitwa Martin Bingo
“Ugaidi Mkuu” Alijibu kwa utii Mzee Shayo
“Inakuwaje hadi ugaidi unaingia katika Nchi hii yenye amani kwa zaidi ya Miaka 60 sasa, nyie kama jicho la Taifa mko wapi?” Alihoji Rais akionekana kuchanganikiwa
“Mkuu! Ugaidi huu unaratibiwa na Mtanzania, mkazi wa Jiji la Arusha. Mara moja nitatuma timu kuhakikisha anafuatiliwa mahali alipozaliwa na kupata taarifa zake, kuanzia hapo tutajuwa tunapambana vipi kuhakikisha tunamdhibiti” Alisema Mzee Shayo, maneno yake yalikuwa kama dhihaka kwa Rais Martin Bingo, alimtandika kofi Mzee Shayo
“Tayali kambi la Lugalo lipo chini ya huyo Mtu na kundi lake la ESS, anateka kila sehemu nyeti ya Nchi hii, nimepata taarifa pia kambi la Jeshi la Majimaji nalo lipo chini yake, Shayo uzembe wa aina yoyote utasababisha damu nyingi kumwagika” Alisema kwa hasira huku akimkaripia Mzee Shayo ambaye kiumri alikuwa Mkubwa kuliko Rais Martin
“Mkuu! Naomba niende” alisema Mzee Shayo
“Ndani ya masaa manne nipate majibu ya hili jambo Shayo, vinginevyo utahusishwa pia na Ugaidi huu” Alisema Rais, Mzee Shayo aligeuka na kuondoka Ikulu, alipoingia kwenye gari lake chozi lilimbubujika, alipiga usukani kisha aliondoa gari eneo hilo.
Tuachane na habari za Kitengo na hasira za Rais Martin juu ya uvamizi huu wa kutisha, Ndani ya Jiji la Nairobi, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata kulikuwa na ujio wa Msichana mmoja mzuri sana, Mweupe. Alionekana kuwa makini sana pindi alipokanyaga ardhi hiyo, kutokana na Ugaidi uliokuwa umetanda ndani ya Ardhi ya Tanzania, Ulinzi ulikuwa imara sana ndani ya Uwanja huo, muda mchache baada ya ndege hiyo kutua Taifa la Kenya lilitangaza kusimamisha shughuli zote za anga yaani hakuna ndege nyingine kuingia wala kutoka.
Msichana huyo alikaguliwa kisha aliambiwa avue miwani. “Unaitwa Faudhia?” Aliuliza mmoja wa Askari wa Ukaguzi
“Ndiyo!!” Alijibu Msichana huyo ambaye alifahamika kama Faudhia, askari alimtazama sana Faudhia kabla ya kumruhusu aweze kuondoka Uwanjani hapo, Faudhia aliporuhusiwa baada ya kuwa amekamirisha taratibu zote aliita Taxi
“Nipeleke Nairobi Hotel” alisema Faudhia
“Nairobi Hotel, ni KSH 500” alisema dereva huyo ambaye alikuwa ni Mwanamke, Faudhia alikuwa siti ya nyuma akamwambia
“Muhimu nifike hapo kwa wakati” alisema Faudhia huku Mwanamke huyo akiondoa gari lake katika eneo hilo.
“Unaonekana upo makini sana, nini kimekuleta hapa Kenya?” Aliuliza Mdada huyo ambaye sura yake haikupata kuonekana kwa Faudhia, lilikuwa ni swali la mtego ambalo Faudhia alilikwepa haraka sana
“Hiyo Hotel ina huduma zote muhimu ee? Nimepata sifa zake” Alisema Faudhia
“Kenya hakuna Hotel hoi hai, hiyo uliyoitaja ndiyo Hoteli bora sana hapa Nairobi” Alijibu Mdada huyo ambaye hakupata kutambulika alikuwa anaitwa nani, hakumuuliza tena kitu kingine Faudhia hadi pale walipofika katika Hoteli ya Nairobi ambayo ilikuwa mbali kutokea ulipo Uwanja wa Jomo Kenyata.
“Here we goo ( tumeshafika ) ” alisema Mdada huyo huku akiwa amesimamisha gari mbele ya Hoteli hiyo ambayo kwa muda huo ilikuwa imefungwa kutokana na tahadhali ambazo Taifa la Kenya liliamuwa kuchukua.
Yule Mdada aliondoka zake, Faudhia alilitazama Tax hadi lilipozama kisha alisogea getini akatoa kitambulisho maalum kuwa alishafanya booking ya Chumba Hoteli hiyo, alikaguliwa na kuruhusiwa kuingia Hotelini.
Akiwa ndani ya chumba chake alipokea simu ya Mtu aliyemkusudia ndani ya Hoteli hiyo, jamaa huyo aliitwa Khalid Bangala, alikuwa dalali maarufu sana ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, alikuwa ni miongoni mwa wachache ambao walikuwa wakiwindwa sana na Serikali zote kutokana na Biashara yake ya kusafirisha mizigo, na biashara haramu ya usafirishaji wa Binadamu wakiwemo wana mgambo wa kundi la Kigaidi la ESS ambalo lipo Tanzania.
Haraka Faudhia alimfungulia mlango jamaa huyo ambaye alikuja na Watu watatu ndani ya Chumba hicho
“Mna uhakika nitaingia Tanzania Kabla ya mipaka kufungwa?” Aliuliza Faudhia akiwa makini kumtazama Khalid Bangala, jamaa huyo alicheka kisha akajibu kwa kujimwambafai
“Itakuwa ni Biashara yangu ya kwanza kukwama kwenye maisha yangu, sijawahi kukwamisha biashara yangu” Alisema kisha Faudhia alishusha pumzi zake, ilikuwa ni majira ya jioni.
“Ulisema ni kiasi gani?” Aliuliza Faudhia baada ya kuhakikishiwa kuwa angesafiri kutoka Kenya hadi Tanzania bila tatizo lolote lile
“Milioni 10 za Kitanzania, hali si shwari huko mpakani, Watanzania walio jirani wanakinzana na askari kuihama Nchi” Alisema Khalid Bangala
“Sawa, nitalipa hiyo fedha yote nikifika Tanzania” Alisema Faudhia, Khalid Bangala alimsogelea na kumuuliza kwa kumdadisi
“Nchi ambayo Watu wanaanza kuikimbia wewe unatoa Milioni 10 kuingia huko, una ajenda gani?” Alihoji Khalid Bangala
“Nafikiri tuifanye Biashara yetu kwanza Bosi” Alijibu Faudhia
“Haya! Utalazimika kuingia ndani ya Sanduku” alisema Khalid Bangala
“Una maanisha Jeneza? Nasafiri nikiwa mfu?” Alihoji Faudhia
“Hapana!! Tunachokifanya kitakusaidia kuingia Tanzania, vinginevyo itakuwa ngumu kwako” Ilikuwa ni Mtihani mgumu kwa Faudhia kukubali sharti hilo, haraka alikumbuka jambo fulani
Kilichomtoa Mexico kilikuwa ni simu ya dharura kutoka kwa Mkuu Wa kitengo cha Usalama wa Taifa Mzee Shayo juu ya Ugaidi Nchini Tanzania. Alishusha pumzi zake akasema
“Safari itaanza saa ngapi?”
“Sasa hivi” Alisema Khalid Bangala, mara moja vijana wake waliingiza sanduku ndani ya Hoteli hiyo kupitia Mlango wa nyuma wakiwa na mavazi ya waangalizi wa maiti kuhakikisha Faudhia anaingia Tanzania, jeneza hilo lilikuwa na matundu
madogo madogo ya kuhakikisha hewa inaingia humo ndani.
Faudhia aliingia ndani ya sanduku akiwa na kibegi chake kidogo sana, safari ilianza. Walipofika nje ya Hoteli Khalid aliwatakia vijana wake safari njema, mara moja sanduku liliingizwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser yenye nembo ya Hospitali ya Nairobi. Safari ilianza ya kuutafuta mpaka wa Namanga ambapo Faudhia ataachwa hapo
Gari hiyo ilianza safari kwa mwendo wa taratibu ili kutoka Mjini, ilikuwa ni safari ya hatari sana lakini kwa Khalid Bangala na vijana wake ilikuwa ni kazi waliyoizoea, gari hilo lilitambuliwa kama gari ya kubeba maiti zinazoenda masafa ya mbali. Walipofika kwenye kizuizi cha kutoka na kuingia Nairobi, polisi walianza kulikagua gari hilo ila walipojiridhisha kuwa gari hilo lilikuwa na maiti walilipa ruhusa ya kuendelea na safari.
Safari ilikuwa ndefu sana iliyogubikwa na giza, usiku uliingia huku wakizidi kukata miji na vijiji kuutafuta Mpaka wa Namanga ambao ulikuwa ndio mpaka salama hadi kufikia muda huo, mara kadhaa Faudhia akiwa ndani ya Sanduku hilo aliwasiliana na Mzee Shayo kutoka kitengo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu, alimueleza nini anatakiwa kufanya, alitakiwa kuelekea Kwenye pori dogo lililopo wilaya ya Longido, hapo atakutana na gari kisha ataelekea Jijini Arusha kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea Dar.
Miji mingi ilianza kutekwa na Magaidi hao wa kundi la ESS pasipo kuwekwa wazi sababu ya wao kufanya hivyo huku ikifahamika wazi kuwa anayekiongoza kikundi hicho anafahamika kama Martin Gimbo maarufu kama Chogo.
“Ukifika Arusha utapewa kazi ya kufanya huko kwa muda fulani” Ulikuwa ni ujumbe wa mwisho wa Mzee Shayo, kazi hii ilikuwa ndiyo kazi ya Kwanza kwa Faudhia baada ya kuhitimu mafunzo huko Mexico, akiwa ndani ya sanduku alitoa picha ya rafiki yake aliyeitwa Diana ambaye naye alihusishwa katika ugaidi huo, alikumbuka maisha ya nyuma walipokuwa wakisoma wote shule ya Majengo huko Mkoani Mbeya, roho ilimuuma sana lakini lilikuwa ndiyo jukumu lake. Aliiweka picha hiyo mfukoni kisha alipaza sauti akawauliza vijana wa Khalidi Bangala
“Tupo wapi?” Aliuliza huku akigonga sanduku hilo
“Tupo Kilomita chache kufika” Alisema mmoja wa vijana hao, masaa yalizidi kukimbia usiku ulizidi kuwa mwingi sana, Faudhia aliamua kujipumzisha kidogo.
Tuachane na safari ya Faudhia, ndani ya Jiji la Nairobi, baada ya kupata kazi itakayo muingizia fedha nyingi Khalid Bangala. Alikuwa amejipumzisha kwenye moja ya Hoteli, ghafla simu yake iliingia ujumbe mfupi, aliichukua simu na kuanza kuusoma
“Khalid, najuwa una msafirisha Mwanamke kuelekea Tanzania, mnapitia mpaka upi? Namuhitaji huyo Mwanamke” Khalid Bangala baada ya kuusoma ujumbe huo alijawa na mshangao ni nani alikuwa amemtumia ujumbe huo na alijuwaje kuwa usiku huo alikuwa akimsafirisha mwanamke kuelekea Tanzania, alibonyeza kitufe cha kupiga kisha akapiga simu kwenye namba hiyo
“Khalid” ilisikika sauti ya kiume
“Nani wewe na umejuwaje?” Aliuliza kwa umakini sana Khalid Bangala kisha alishusha pumzi zake
“Kwasasa siyo muhimu sana kunifahamu, itabidi uchague kimoja, kunipatia msichana nikulipe mara mbili au kunipa Kichwa chako” Ilisikika tena sauti ya Mwanaume huyo na kumfanya Khalid aone jambo hilo lilikuwa siriazi kiasi gani, alikaa kimya bila kutoa jibu lolote
“Kuna kiasi kikubwa cha fedha kwenye gari yako hapo chini, chukua kisha niambie Msichana anapitia Mpaka upi” Alisema tena Mwanaume huyo kisha simu ilikatika, haraka Khalidi alishuka chini ya Hoteli mahali ambapo gari lake lilikuwa limesimama, alifungua mlango wa mbele hakuona kitu, akafungua mlango wa nyuma ndipo alipokutana n begi dogo, alipolifungua begi hilo lilikuwa limejaa noti nyingi, alijikuta akitabasamu Khalid Bangala kwasababu atakuwa ameingiza kiasi kikubwa cha fedha, alitoa simu mfukoni kisha alimpigia huyo Mwanaume asiye mfahamu
“Mpaka wa Namanga, baada ya masaa mawili watakuwa hapo” Alisema Khalid kisha simu ilikatwa na Mwanaume huyo bila hata kujibu chochote, fedha zilimuacha Khalid Bangala akiwa mwenye tabasamu zito sana, alijulikana kuwa ni mpenda pesa ndio maana alikuwa akifanya kazi za kuhatarisha maisha yake ili tu apate pesa.
Akiwa anaendelea kutabasamu na kufurahi ghafla alihisi ujio wa Mtu nyuma yake, alipogeuka tu alikutana na risasi moja kichwani, Habari za Khalid Bangala ziliishia hapo, aliyempiga risasi Khalid alikuwa ni mwanamke mmoja aliyefunga nywele zake vizuri, alikuwa ndani ya Koti jeusi na suruali nyeusi, Huwezi amini Mwanamke huyo ndiye aliyemuendesha Faudhia kutoka Uwanja wa ndege hadi Hotelini, alikuwa ni Diana rafiki wa zamani wa Faudhia, alikuwa ametumwa kuchukua pesa ambazo waliziweka ndani ya gari ya Khalid Bangala
“Kazi imeisha!” Alisema Diana kwa njia ya simu
“Waoo Good Girl ( Vizuri Msichana mzuri ) ” ilisikika sauti nzito ya kizee
“Rudi Tanzania” Alimalizia kusema Mwanaume huyo kwa njia ya simu, simu hiyo ilikatika, tayali polisi walishafika nje ya Hoteli hiyo, Diana alichofanya ni kuingia kwenye chemba ya maji machafu akaenda kutokea mbali na eneo hilo.
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TATU
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
15 Comments
Hatar sana
Next plz
Iko poa xnaa
Huyo Diana na faudhia wapo upande wa serikali au magaidi🤷🏽♂️🤷🏽♂️🥱🥱🥱
Faudhia ndo star wa picha
Nzuri
https://shorturl.fm/N6nl1
https://shorturl.fm/a0B2m
https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/68Y8V
https://shorturl.fm/j3kEj
https://shorturl.fm/hevfE
https://shorturl.fm/fSv4z
https://shorturl.fm/xlGWd