Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tatu-03)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Kwanza-01)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 28, 202511 Comments9 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia 

    Kupitia daraja la Kigamboni, Mzee Shayo aliendesha Subaru  kama yupo kwenye mbio za Magari, wakati huo Barabara zilikuwa  nyeupe, Watu wengi waliogopa kupoteza uhai wao, walibakia  majumbani mwao huku wachache wakiendelea kufanya safari,  ilimuwezesha Mzee Shayo kufika Ikulu ya Magogoni haraka sana,  alikuta ulinzi umeimarishwa hapo lakini alipowatazama Walinzi  hao alijikuta akikata tamaa, aliona ni ngumu sana kupambana  na huyo Mwanaume anayeitwa Chogo. Endelea

    SEHEMU YA PILI

    Aliuliza mahali ambapo Rais wa Nchi alikuwa amehifadhiwa kwa  ajili ya usalama, ilikuwa ni ndani ya chumba kimoja ambacho  kilikuwa na milango ya umeme, chumba hicho kilipatikana  katikati ya jengo la Ikulu. 

    Rais akiwa na waziri Mkuu ndani ya chumba hicho walimuona  Mzee Shayo akiingia huku sura yake ikionesha kukosa tumaini,  Rais alimdaka Mzee Shayo 

    “Shayo! Nini kinaendelea?” Aliuliza Rais huyo aliyeitwa  Martin Bingo 

    “Ugaidi Mkuu” Alijibu kwa utii Mzee Shayo 

    “Inakuwaje hadi ugaidi unaingia katika Nchi hii yenye amani  kwa zaidi ya Miaka 60 sasa, nyie kama jicho la Taifa mko  wapi?” Alihoji Rais akionekana kuchanganikiwa 

    “Mkuu! Ugaidi huu unaratibiwa na Mtanzania, mkazi wa Jiji la  Arusha. Mara moja nitatuma timu kuhakikisha anafuatiliwa  mahali alipozaliwa na kupata taarifa zake, kuanzia hapo  tutajuwa tunapambana vipi kuhakikisha tunamdhibiti” Alisema  Mzee Shayo, maneno yake yalikuwa kama dhihaka kwa Rais Martin  Bingo, alimtandika kofi Mzee Shayo 

    “Tayali kambi la Lugalo lipo chini ya huyo Mtu na kundi lake  la ESS, anateka kila sehemu nyeti ya Nchi hii, nimepata  taarifa pia kambi la Jeshi la Majimaji nalo lipo chini yake,  Shayo uzembe wa aina yoyote utasababisha damu nyingi  kumwagika” Alisema kwa hasira huku akimkaripia Mzee Shayo  ambaye kiumri alikuwa Mkubwa kuliko Rais Martin 

    “Mkuu! Naomba niende” alisema Mzee Shayo 

    “Ndani ya masaa manne nipate majibu ya hili jambo Shayo,  vinginevyo utahusishwa pia na Ugaidi huu” Alisema Rais, Mzee  Shayo aligeuka na kuondoka Ikulu, alipoingia kwenye gari lake  chozi lilimbubujika, alipiga usukani kisha aliondoa gari eneo  hilo.

    Tuachane na habari za Kitengo na hasira za Rais Martin juu ya  uvamizi huu wa kutisha, Ndani ya Jiji la Nairobi, Uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata kulikuwa na ujio wa  Msichana mmoja mzuri sana, Mweupe. Alionekana kuwa makini  sana pindi alipokanyaga ardhi hiyo, kutokana na Ugaidi  uliokuwa umetanda ndani ya Ardhi ya Tanzania, Ulinzi ulikuwa  imara sana ndani ya Uwanja huo, muda mchache baada ya ndege  hiyo kutua Taifa la Kenya lilitangaza kusimamisha shughuli  zote za anga yaani hakuna ndege nyingine kuingia wala kutoka. 

    Msichana huyo alikaguliwa kisha aliambiwa avue miwani. “Unaitwa Faudhia?” Aliuliza mmoja wa Askari wa Ukaguzi 

    “Ndiyo!!” Alijibu Msichana huyo ambaye alifahamika kama  Faudhia, askari alimtazama sana Faudhia kabla ya kumruhusu  aweze kuondoka Uwanjani hapo, Faudhia aliporuhusiwa baada ya  kuwa amekamirisha taratibu zote aliita Taxi 

    “Nipeleke Nairobi Hotel” alisema Faudhia 

    “Nairobi Hotel, ni KSH 500” alisema dereva huyo ambaye  alikuwa ni Mwanamke, Faudhia alikuwa siti ya nyuma akamwambia 

    “Muhimu nifike hapo kwa wakati” alisema Faudhia huku Mwanamke  huyo akiondoa gari lake katika eneo hilo. 

    “Unaonekana upo makini sana, nini kimekuleta hapa Kenya?”  Aliuliza Mdada huyo ambaye sura yake haikupata kuonekana kwa  Faudhia, lilikuwa ni swali la mtego ambalo Faudhia alilikwepa  haraka sana 

    “Hiyo Hotel ina huduma zote muhimu ee? Nimepata sifa zake”  Alisema Faudhia 

    “Kenya hakuna Hotel hoi hai, hiyo uliyoitaja ndiyo Hoteli  bora sana hapa Nairobi” Alijibu Mdada huyo ambaye hakupata  kutambulika alikuwa anaitwa nani, hakumuuliza tena kitu  kingine Faudhia hadi pale walipofika katika Hoteli ya Nairobi  ambayo ilikuwa mbali kutokea ulipo Uwanja wa Jomo Kenyata. 

    “Here we goo ( tumeshafika ) ” alisema Mdada huyo huku akiwa  amesimamisha gari mbele ya Hoteli hiyo ambayo kwa muda huo  ilikuwa imefungwa kutokana na tahadhali ambazo Taifa la Kenya  liliamuwa kuchukua. 

    Yule Mdada aliondoka zake, Faudhia alilitazama Tax hadi  lilipozama kisha alisogea getini akatoa kitambulisho maalum  kuwa alishafanya booking ya Chumba Hoteli hiyo, alikaguliwa  na kuruhusiwa kuingia Hotelini.

    Akiwa ndani ya chumba chake alipokea simu ya Mtu  aliyemkusudia ndani ya Hoteli hiyo, jamaa huyo aliitwa Khalid  Bangala, alikuwa dalali maarufu sana ndani ya ukanda wa  Afrika Mashariki, alikuwa ni miongoni mwa wachache ambao  walikuwa wakiwindwa sana na Serikali zote kutokana na  Biashara yake ya kusafirisha mizigo, na biashara haramu ya  usafirishaji wa Binadamu wakiwemo wana mgambo wa kundi la  Kigaidi la ESS ambalo lipo Tanzania. 

    Haraka Faudhia alimfungulia mlango jamaa huyo ambaye alikuja  na Watu watatu ndani ya Chumba hicho 

    “Mna uhakika nitaingia Tanzania Kabla ya mipaka kufungwa?”  Aliuliza Faudhia akiwa makini kumtazama Khalid Bangala, jamaa  huyo alicheka kisha akajibu kwa kujimwambafai 

    “Itakuwa ni Biashara yangu ya kwanza kukwama kwenye maisha  yangu, sijawahi kukwamisha biashara yangu” Alisema kisha  Faudhia alishusha pumzi zake, ilikuwa ni majira ya jioni. 

    “Ulisema ni kiasi gani?” Aliuliza Faudhia baada ya  kuhakikishiwa kuwa angesafiri kutoka Kenya hadi Tanzania bila  tatizo lolote lile 

    “Milioni 10 za Kitanzania, hali si shwari huko mpakani,  Watanzania walio jirani wanakinzana na askari kuihama Nchi”  Alisema Khalid Bangala 

    “Sawa, nitalipa hiyo fedha yote nikifika Tanzania” Alisema  Faudhia, Khalid Bangala alimsogelea na kumuuliza kwa  kumdadisi 

    “Nchi ambayo Watu wanaanza kuikimbia wewe unatoa Milioni 10  kuingia huko, una ajenda gani?” Alihoji Khalid Bangala 

    “Nafikiri tuifanye Biashara yetu kwanza Bosi” Alijibu Faudhia 

    “Haya! Utalazimika kuingia ndani ya Sanduku” alisema Khalid  Bangala 

    “Una maanisha Jeneza? Nasafiri nikiwa mfu?” Alihoji Faudhia 

    “Hapana!! Tunachokifanya kitakusaidia kuingia Tanzania,  vinginevyo itakuwa ngumu kwako” Ilikuwa ni Mtihani mgumu kwa  Faudhia kukubali sharti hilo, haraka alikumbuka jambo fulani 

    Kilichomtoa Mexico kilikuwa ni simu ya dharura kutoka kwa  Mkuu Wa kitengo cha Usalama wa Taifa Mzee Shayo juu ya Ugaidi  Nchini Tanzania. Alishusha pumzi zake akasema

    “Safari itaanza saa ngapi?” 

    “Sasa hivi” Alisema Khalid Bangala, mara moja vijana wake  waliingiza sanduku ndani ya Hoteli hiyo kupitia Mlango wa  nyuma wakiwa na mavazi ya waangalizi wa maiti kuhakikisha  Faudhia anaingia Tanzania, jeneza hilo lilikuwa na matundu  

    madogo madogo ya kuhakikisha hewa inaingia humo ndani. 

    Faudhia aliingia ndani ya sanduku akiwa na kibegi chake  kidogo sana, safari ilianza. Walipofika nje ya Hoteli Khalid  aliwatakia vijana wake safari njema, mara moja sanduku  liliingizwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser yenye  nembo ya Hospitali ya Nairobi. Safari ilianza ya kuutafuta  mpaka wa Namanga ambapo Faudhia ataachwa hapo 

    Gari hiyo ilianza safari kwa mwendo wa taratibu ili kutoka  Mjini, ilikuwa ni safari ya hatari sana lakini kwa Khalid  Bangala na vijana wake ilikuwa ni kazi waliyoizoea, gari hilo  lilitambuliwa kama gari ya kubeba maiti zinazoenda masafa ya  mbali. Walipofika kwenye kizuizi cha kutoka na kuingia  Nairobi, polisi walianza kulikagua gari hilo ila  walipojiridhisha kuwa gari hilo lilikuwa na maiti walilipa  ruhusa ya kuendelea na safari. 

    Safari ilikuwa ndefu sana iliyogubikwa na giza, usiku  uliingia huku wakizidi kukata miji na vijiji kuutafuta Mpaka  wa Namanga ambao ulikuwa ndio mpaka salama hadi kufikia muda  huo, mara kadhaa Faudhia akiwa ndani ya Sanduku hilo  aliwasiliana na Mzee Shayo kutoka kitengo kwa njia ya ujumbe  mfupi wa simu, alimueleza nini anatakiwa kufanya, alitakiwa  kuelekea Kwenye pori dogo lililopo wilaya ya Longido, hapo  atakutana na gari kisha ataelekea Jijini Arusha kwa ajili ya  kuanza safari ya kuelekea Dar. 

    Miji mingi ilianza kutekwa na Magaidi hao wa kundi la ESS  pasipo kuwekwa wazi sababu ya wao kufanya hivyo huku  ikifahamika wazi kuwa anayekiongoza kikundi hicho anafahamika  kama Martin Gimbo maarufu kama Chogo. 

    “Ukifika Arusha utapewa kazi ya kufanya huko kwa muda fulani”  Ulikuwa ni ujumbe wa mwisho wa Mzee Shayo, kazi hii ilikuwa  ndiyo kazi ya Kwanza kwa Faudhia baada ya kuhitimu mafunzo  huko Mexico, akiwa ndani ya sanduku alitoa picha ya rafiki  yake aliyeitwa Diana ambaye naye alihusishwa katika ugaidi  huo, alikumbuka maisha ya nyuma walipokuwa wakisoma wote  shule ya Majengo huko Mkoani Mbeya, roho ilimuuma sana lakini  lilikuwa ndiyo jukumu lake. Aliiweka picha hiyo mfukoni kisha  alipaza sauti akawauliza vijana wa Khalidi Bangala 

    “Tupo wapi?” Aliuliza huku akigonga sanduku hilo

    “Tupo Kilomita chache kufika” Alisema mmoja wa vijana hao,  masaa yalizidi kukimbia usiku ulizidi kuwa mwingi sana,  Faudhia aliamua kujipumzisha kidogo. 

    Tuachane na safari ya Faudhia, ndani ya Jiji la Nairobi,  baada ya kupata kazi itakayo muingizia fedha nyingi Khalid  Bangala. Alikuwa amejipumzisha kwenye moja ya Hoteli, ghafla  simu yake iliingia ujumbe mfupi, aliichukua simu na kuanza  kuusoma 

    “Khalid, najuwa una msafirisha Mwanamke kuelekea Tanzania,  mnapitia mpaka upi? Namuhitaji huyo Mwanamke” Khalid Bangala  baada ya kuusoma ujumbe huo alijawa na mshangao ni nani  alikuwa amemtumia ujumbe huo na alijuwaje kuwa usiku huo  alikuwa akimsafirisha mwanamke kuelekea Tanzania, alibonyeza  kitufe cha kupiga kisha akapiga simu kwenye namba hiyo 

    “Khalid” ilisikika sauti ya kiume 

    “Nani wewe na umejuwaje?” Aliuliza kwa umakini sana Khalid  Bangala kisha alishusha pumzi zake 

    “Kwasasa siyo muhimu sana kunifahamu, itabidi uchague kimoja,  kunipatia msichana nikulipe mara mbili au kunipa Kichwa  chako” Ilisikika tena sauti ya Mwanaume huyo na kumfanya  Khalid aone jambo hilo lilikuwa siriazi kiasi gani, alikaa  kimya bila kutoa jibu lolote 

    “Kuna kiasi kikubwa cha fedha kwenye gari yako hapo chini,  chukua kisha niambie Msichana anapitia Mpaka upi” Alisema  tena Mwanaume huyo kisha simu ilikatika, haraka Khalidi  alishuka chini ya Hoteli mahali ambapo gari lake lilikuwa  limesimama, alifungua mlango wa mbele hakuona kitu, akafungua  mlango wa nyuma ndipo alipokutana n begi dogo, alipolifungua  begi hilo lilikuwa limejaa noti nyingi, alijikuta akitabasamu  Khalid Bangala kwasababu atakuwa ameingiza kiasi kikubwa cha  fedha, alitoa simu mfukoni kisha alimpigia huyo Mwanaume  asiye mfahamu 

    “Mpaka wa Namanga, baada ya masaa mawili watakuwa hapo”  Alisema Khalid kisha simu ilikatwa na Mwanaume huyo bila hata  kujibu chochote, fedha zilimuacha Khalid Bangala akiwa mwenye  tabasamu zito sana, alijulikana kuwa ni mpenda pesa ndio  maana alikuwa akifanya kazi za kuhatarisha maisha yake ili tu  apate pesa. 

    Akiwa anaendelea kutabasamu na kufurahi ghafla alihisi ujio  wa Mtu nyuma yake, alipogeuka tu alikutana na risasi moja  kichwani, Habari za Khalid Bangala ziliishia hapo, aliyempiga risasi Khalid alikuwa ni mwanamke mmoja aliyefunga nywele  zake vizuri, alikuwa ndani ya Koti jeusi na suruali nyeusi,  Huwezi amini Mwanamke huyo ndiye aliyemuendesha Faudhia  kutoka Uwanja wa ndege hadi Hotelini, alikuwa ni Diana rafiki  wa zamani wa Faudhia, alikuwa ametumwa kuchukua pesa ambazo  waliziweka ndani ya gari ya Khalid Bangala 

    “Kazi imeisha!” Alisema Diana kwa njia ya simu 

    “Waoo Good Girl ( Vizuri Msichana mzuri ) ” ilisikika sauti  nzito ya kizee 

    “Rudi Tanzania” Alimalizia kusema Mwanaume huyo kwa njia ya  simu, simu hiyo ilikatika, tayali polisi walishafika nje ya  Hoteli hiyo, Diana alichofanya ni kuingia kwenye chemba ya  maji machafu akaenda kutokea mbali na eneo hilo.  

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TATU

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya za kijasusi

    11 Comments

    1. Verena on May 28, 2025 3:37 pm

      Hatar sana

      Reply
    2. guy on May 28, 2025 5:18 pm

      Next plz

      Reply
    3. Cathbert on May 28, 2025 6:50 pm

      Iko poa xnaa

      Reply
    4. KingzJeelay on May 28, 2025 8:39 pm

      Huyo Diana na faudhia wapo upande wa serikali au magaidi🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️🥱🥱🥱

      Reply
    5. Adam on May 28, 2025 8:50 pm

      Nzuri

      Reply
    6. Harvey875 on May 29, 2025 1:35 am

      https://shorturl.fm/N6nl1

      Reply
    7. Katherine2713 on May 29, 2025 2:19 am

      https://shorturl.fm/a0B2m

      Reply
    8. Jay3701 on May 29, 2025 3:42 am

      https://shorturl.fm/9fnIC

      Reply
    9. Sam2353 on May 30, 2025 11:12 am

      https://shorturl.fm/6539m

      Reply
    10. Ronald4025 on May 30, 2025 11:45 am

      https://shorturl.fm/68Y8V

      Reply
    11. Katelyn459 on May 30, 2025 1:27 pm

      https://shorturl.fm/j3kEj

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi May 29, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tatu-03)

    Ilipoishia Sehemu Ya Pili “Kazi imeisha!” Alisema Diana kwa njia ya simu  “Waoo Good Girl…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Kwanza-01)

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Kumi Na Moja-11)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.