Ilipoishia “Usijali Jacklin nipo kwa ajili yako mara zote” alisemaย Mosses na kunifanya nitabasamu kwa uchovu, shughuli ilikuwaย pevu na vile nimetoka kuumwa basi nilichoka sana nikalalaย palepale.ย
Osman alipofika ofisini alihitaji kuniona ila aliambiwa kuwaย nimetoka, akiwa kama Bosi wangu alihitaji kujuwa niko wapi,ย alinipigia sana simu lakini haikupokelewa maana nilikuwaย nimelala chakali, basi alipiga kwa Mama na kumuuliza kamaย nitakuwa nimeenda nyumbani, Mama alimwambia Osman kuwa sipoย nyumbani. Endelea
SEHEMU YA TANO
“Haya Mama nitaendelea kumtafuta” Alisema Osman, alipokataย simu alijiuliza nilikuwa nimeenda wapi, alishikwa na wivuย fulani hata kazi hakufanya naye aliondoka. Mida ya Jioni kamaย saa moja kasoro hivi ndiyo niliamka, nilikuta Mossesย ameniandalia supu, nilikunywa kisha aliniulizaย
“Osman ndiyo Nani? Amepiga sana simu, ilipokata yake iliingiaย ya Mama yako, walikuwa wakipiga kwa kupokezana” Aliniuliza naย kuelezea kuhusu simu zilizokuwa zimeingiaย
“Osman ni Bosi wangu labda amenipigia sababu kuna faili zipoย kwangu, ngoja nimpigie Mama” Nilisema, alinisogezea simu maraย moja kisha nilimpigia Mama, alipokea na kinishushia swali juuย
“Jacklin uko wapi?” Aliuliza kwa sauti iliyoonesha kuwaย alikuwa na shahuku ya kujuwa nilipoย
“Mama mimi siyo Mtoto sasa swali gani hilo alafu kama vileย una hasira na Mimi!”ย
“Ndiyo wewe siyo Mtoto lakini kwanini uondoke kazini kabla yaย muda wa kazi kuisha? Osman amenipigia simu kujuwa kama upoย sawa na upo wapi”ย
“Ulimjibuje Mama”ย
“Nilimwambia kuwa sijui ulipo sasa kwanini niwe muongo kwaย kijana wa Watu, mwisho wote tuje kuonekana hatuna maana?”ย
“Ok Mama usiongee sana nipo kwa Mosses hata hivyo narudi mudaย siyo mrefu” Nilisema, Mama alikata simu.ย
“Huyo Mama yako jinsi anavyonichukia usikute amekasirika hukoย kisa wewe kuja kwangu” Alisema Mossesย
“Ah! Mama yangu nimeshamzoea love, ngoja nirudi tu nyumbaniย ila fanya kama tulivyoongea tafuta nyumba kesho unipe jibu”ย Nilisema kisha nilizama kwenye waleti yangu nikampa Mossesย laki na nusuย
“Hiyo itakusaidia” Nilisema kisha niliondoka zangu pale.ย
Nilipofika nyumbani nilimkuta Mama akiwa amefura kama churaย mwenye njaa, alikuwa amekaa nje akinisubiria. Nilipomfikiaย aliniuliza swali gumu sanaย
“Umesahau kila kitu sababu leo upo hai, huyo Mosses alikataaย kusaidia Maisha yako, alinijibu jeuri lakini wewe unamuona waย maana sana kwako, nimefanya makosa kukupigania Jacklin?”ย
Lilikuwa ni swali gumu kuwahi kuulizwa katika Maisha yangu,ย Mama alidondosha chozi lililochuruzika hadi kwenye mashavuย yake, ilinibidi nikae kwanzaย
“Mama ndiyo maneno gani hayo? Binadamu tunakosea naย kujirekebisha, usimuhukumu Mosses kwa kosa moja tu yule niย Binadamu hajakamilika Mama, hilo haliwezi kuuondoa uthamaniย wake kwangu” Nilimjibu Mama kwa kujikaza sana, hakuna kituย nilikuwa sipendi kama kumuona Mama akilia kwa ajili yangu,ย anagalau ningekuwa mgonjwa lakini ni mzima na analia kwaย ajili yanguย
“Mama yako nilisemewa vibaya, Kijana wa Watu alikusaidiaย hakuangalia nyuma. Bila Osman ingekuwa inasimuliwa hadithiย yako Jacklin, lakini leo Mtu aliyekusaidia akabadilisha naย Maisha yetu kututoa kwenye umasikini hadi kwenye hali hiiย haupokei simu zake, unaacha kazi yake na kwenda kwa Mosses?”ย Alisema Mama, nilihema kwa uchungu na maumivu, ni kweli Osmanย alisaidia Maisha yangu lakini hakusaidia ili niwe mtumwaย kwakeย
“Mama msaada ambao unakuwa Mtumwa ni msaada wa kizandiki tuu,ย kama alinisaidia kwa moyo wake hakupaswa kuhitaji malipo,ย mbona anajuwa kila kitu sasa kwanini apige simu kwako?ย Amenikosea sana”ย
“Unajisikiliza Jacklin au unaongea kwasababu unayo nafasi yaย kufanya hivyo? Hajakusaidia tu bali ameweka maisha yakeย rehani, anatembea na figo moja kwa ajili yako, hupaswiย kumsumbua hivi kijana wa Watu na kama huitaji kazi basiย mwambie ili amtafute Mtu mwingine” Mama alisema kwa hisiaย kaliย
“Sawa Mama sipendi ukwazike kwa ajili yangu. Nitamuombaย msamaha Osman, kuwa na amani Mama nakupenda sana” Nilisemaย kisha nilinyanyuka na kuingia ndani, nilimuacha Mama akiwaย amekaa nje peke yake, najuwa jinsi alivyokuwa anajisikia ilaย ningefanya nini wakati moyo wangu upo kwa mwingine? Nilizionaย ishara zote kuwa Osman ananipenda ila tayari hisia zangu zipoย kwa Mosses.ย
Nilipofika chumbani kwangu niliyatafakari maneno ya Mamaย ambayo ni wazi aliyasema kutoka ndani ya nafsi yake,ย nilijisikia vibaya, nilitamani kumtumia meseji Osman nimuombeย msamaha ila niliona ni bora nimuombe msamaha kesho yakeย Ofisini, nilizitazama Missed Calls zake nilimuonea hurumaย Kijana wa Watu, nilifunua shati langu nikaangalia eneo laย tumbo, nilitabasamu tu hata sijui kwanini nilifanya hivyo.
Kesho yake kabla ya kwenda ofisini nilipitia duka la Mauaย nikanunua ua zuri kwa ajili ya kumpatia Osman ili anisameheย kwa kilichotokea. Nilichagua ua zuri ambalo niliamini litampaย furaha Osman, mvua zilikuwa zinaendelea kunyesha, hali yaย hewa ilikuwa nzuri sana ikanikumbusha siku ya kwanzaย Nilipoanza kuumwa nikasaidiwa na Osman, nilianza kutabasamuย tu hadi Muuza Maua alinishtukia akasemaย
“Inaelekea unampenda sana Mtu ambaye unampelekea ua hili,ย Nawaombea penzi lenu lichipue mithiri ya Mtende jangwani”ย Alisema kisha alinitazama usoni, ghafla sura yangu ilikosaย uchangamfu. Sijui kwanini kila nilipomfikiria Osmanย nilijikuta nikiishia kwenye huzuni. Mara muda huo huo Osmanย alipiga simu kama vile alikuwa akijuwa nilikuwa nikimuwaza,ย niliiacha iite kidogo kisha niliipokea huku yule Muuza dukaย akinitazama tuย
“Hello Osman” Nilimsalimia Osman mara baada ya kuwaย nimeshapokea simu na kusikia sauti yakeย
“Jacklin, leo sijisikii vizuri naomba usimamie kazi zakoย vizuri” Alisema Osman, ni kweli hata sauti yake haikuwa naย uchangamfuย
“Una shida gani Osman?” Nilimuulizaย
“Nahisi hali ya Homa tuu Jacklin” Alisema tena Osmanย
“Haya nitafanya hivyo lakini baadaye….” Nilitaka kumwambiaย kuwa nahitaji kuonana naye ila nilisita nikamwambiaย
“Ugua pole Osman” Nilisema kisha simu ilikatika, nilirudiย kulipia ua lile kisha niliondoka nalo hadi kazini.ย
Mdada wa mapokezi aliponiona alinisimamisha, alinifuataย niliposimama akaniulizaย
“Umempa nini Bosi Osman? Yaani alivyo mkali yule lakini janaย alinywea kabisa, aliposikia haupo naye aliondoka naย alionekana hana raha” Alisema, dakika moja tu ilitoshaย kumtambua alikuwa ni Mtu wa aina gani, alionekana kuwaย mshakunaku, nilitabasamu kisha nikamwambiaย
“Kazi njema” nilimuacha akiwa ameduwaa, pengine alitegemeaย ningemwambua Mimi ni Mwanamke wa Osman nahisi ndichoย alichokuwa anataka kukisikia.ย
Niliketi kwenye kiti, nilishusha pumzi zangu, niliona jinsiย maisha yangu yalivyobadilika. Mara simu yangu iliita,ย aliyekuwa akinipigia alikuwa ni Mosses, aliniambia kuwaย amepata nyumba hivyo ilikuwa ikihitaji pesa kiasi cha Milioniย 14, nilimwambia jioni nitampatia pesa hiyo.ย
Siku hiyo, Osman alienda Hospitalini kuangalia afya yake,ย alienda kwenye Hospitali ya Dokta Simon, Wawili hawa walikuwaย wakifahamiana sana. Alipofika Dokta Simon alimfanyiaย uchunguzi, kwakuwa alikuwa akimfahamu vizuri Osman alijuwa niย kitu gani kilikuwa kikimsumbua Osman, waliketi baada yaย vipimoย
“Osman! Nilikuonya kuhusu kutoa figo yako hukutaka kunisikia”ย Alisema Dokta Simon, Osman alikaa kimya kumsikiliza Doktaย Simonย
“Nilikataa usifanye vile sababu ya tatizo lako, figo mojaย ilikuwa na matatizo hivyo ulikuwa ukitumia zaidi figo mojaย tuu, sasa ile nzima umeiondoa hii iliyobakia inafanya kaziย kwa kiwango kidogo sana na haitokuwa na muda mrefu nayoย itakufa” Alisema Dokta Simonย
“Kwanini umeamua kuhatarisha Maisha yako Osman? Wewe niย Bilionea mkubwa hapa Nchini, una pesa ya kutosha,ย unaheshimika kila kona” Aliendelea kusema Dokta Simonย
“Nilifanya vile kwasababu ya upendo wangu kwa Jacklin,ย nilikuwa na Maisha yaliyojaa huzuni sana baada ya Zahraย kunitenda vibaya, ghafla sura yangu ilijawa tabasamu maraย baada ya kumuona Jacklin, niliapa sitopenda tena ila baada yaย Jacklin kuja katika Maisha yangu nimejihisi tofauti kabisa”ย Alisema Osman kisha alishusha pumzi zakeย
“Kwa mara ya kwanza namuona Bilionea dhahifu zaidi katikaย Maisha yangu, unahatarisha Maisha yako kwa ajili ya Mwanamkeย ambaye unajuwa fika ana Mwanaume wake? Unahatarisha Maishaย kwa ajili ya Mwanamke ambaye hata hujawahi kumtamkiaย chochote? Hiyo ni akili yako Osman?? Laiti kama Mzee Dhabiย akilijuwa hili ulilofanya ataipoteza familia ya Jacklin naย haitokuja ionekane tena, wewe ni Mtoto wa pekee wa yule Mzee,ย siku akiligundua hili anaweza hata akaniuwa Mimi” Alisemaย Dokta Simonย
“Sikia Dokta Simon, naomba hili jambo liwe siri Baina yetu.ย Baba yangu asijuwe chochote wakati ambao tunatafuta Figo kwaย ajili ya kunipandikiza” Alisema Osmanย
“Naweza kulificha lakini hali yako inaweza ikaniumbua mbeleย ya Baba yako, vyote nitafanya lakini vipi kama Jacklinย akazikataa hisia zako huoni kama utakuwa umekula hasara wewe?” Alimuuliza swali gumu sana, Osman alikunbuka namnaย tukivyogombana kule Dubai, aliona Swali la Dokta Simonย lilikuwa na mashiko sana.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
ย
10 Comments
Asante mtunzi, endelea kutupa burudani
Huyu demu ovyoo sana๐๐
Mungu naomb jackline atambue kuw mosses hampend arudi kwa osman
Ivi ni kweli kina mwanamke wa ivi
Noma nomaa…..dis iz goin to be bad๐ฅฒ๐ฅฒ osman his going to lose his life๐ฅบ๐ฅบ
Asitisha mapenzi Kwa Jacklin bn me nakadirishwa na uyu dada duuh
Jacklin hakir hana
endelezen bas
tm1nmm
08l9lu