Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Sita (06)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Sita (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 16, 2024Updated:October 28, 202418 Comments7 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Sikia Dokta Simon, naomba hili jambo liwe siri Baina yetu.Β  Baba yangu asijuwe chochote wakati ambao tunatafuta Figo kwaΒ  ajili ya kunipandikiza” Alisema OsmanΒ 

    “Naweza kulificha lakini hali yako inaweza ikaniumbua mbeleΒ  ya Baba yako, vyote nitafanya lakini vipi kama JacklinΒ  akazikataa hisia zako huoni kama utakuwa umekula hasara wewe?” Alimuuliza swali gumu sana, Osman alikunbuka namnaΒ  tukivyogombana kule Dubai, aliona Swali la Dokta SimonΒ  lilikuwa na mashiko sana. Endelea

    SEHEMU YA SITA

    “Tuachane na hilo, naomba ufanye siri asijuwe Mtu yeyote naΒ  pia tangaza dau kwa ajili ya kupata figo nyingine”Β 

    “Sawa kama unavyotaka” Alijibu Dokta Simon, Osman alitoa pesaΒ  akampatia Dokta Simon kisha aliondoka hapo na kurudi nyumbaniΒ  kwake.Β 

    Mimi nilikuwa nikifanya kazi zangu kama ambavyo Mama alikuwaΒ  amenisihi nifanye ili nisimvunje moyo Osman, nilichapa kaziΒ  hadi mida ya Jioni, muda wa kazi ulipoisha niliondoka nikiwaΒ  nimechoka sana, nilimtafuta Mosses kisha alinielekeza wapiΒ  natakiwa kwenda, nilipitia Benki kabla ya yote, nilitoa kiasiΒ  kidogo kisha nilienda huko.Β 

    Nyumba ilikuwa nzuri sana, ilikuwa kubwa na yenye viungaΒ  vizuri vya kupumzika. Tuliikagua kwa pamoja, pesaΒ  zilizotakiwa kulipwa pale zote zilikuwa ni pesa zilizotokanaΒ  na Osman, baada ya kuwa tayari tumemaliza kuikagua, nilifanyaΒ  malipo kwa kutumia huduma za kibenki kwa simu. MalipoΒ  yalikamilika, tuliandikiwa mkataba pale kisha zoeziΒ  lililokuwa limebakia lilikuwa ni kununua fenicha zote zaΒ  ndani ili nyumbani ipate kuitwa nyumba wanayoishi Watu.Β 

    Baada ya kuona nina pesa nyingi vile Mosses aliniomba pesa yaΒ  mtaji ili afungue biashara, nilimwambia nitampatia baada yaΒ  siku tatu, kuhusu Mosses nilikuwa sikifirii chochote kileΒ  bali hisia za mapenzi ndizo zilizokuwa zikinisukuma kufanyaΒ  kila kitu kwake.Β 

    Nilipomaliza kila kitu ndipo nilikumbuka kuwa nilikuwa naΒ  maua ndani ya gari ambayo nilitakiwa kumpatia Osman iliΒ  nimuombe msamaha, basi nilimdanganya Mosses kuwa naelekeaΒ  nyumbani, kwa vyovyote asingeliweza kusema anisindikize maanaΒ  alikuwa hapatani na Mama yangu. Nilimuacha hapo kishaΒ  niliingia kwenye gari nikawasiliana na Osman, alinielekezaΒ  mahali anapoishi, lengo langu lilikuwa ni kumuomba msamahaΒ  kama ambavyo nilimuahidi Mama,Β 

    Safari ya kuelekea kwa Osman ilianza nikiwa ndani ya gari yaΒ  kukodi, nikifikiria ni jinsi gani nitaongea na Osman iliΒ  nipate kumuomba msamaha. Alionekana kunisubiria sana sababuΒ  alikuwa akinipigia na kuniuliza nilikuwa nimefika wapi,Β  mwendo wa saa moja na nusu nilifika nyumbani kwa Osman,Β  alikuwa akiishi kwenye Bonge la Kasri, ndioo niliamini kuwaΒ  Mwanaume huyu alikuwa tajiri sana.

    Jumba lilikuwa likiwaka taa nzuri zenye kuvutia sana, ilikuwaΒ  ndiyo mara ya kwanza nafika kwa Osman, nilivuta picha yaΒ  nyumba aliyotununulia japo ilikuwa ya kifahari ila nilionaΒ  haiifikii hata theluthi nyumba ambayo Osman alikuwa akiishi,Β  nilimpigia simu kisha aliwapa taarifa walinzi kuwa kuna ugeniΒ  nje, nilifunguliwa geti kisha gari liliingia mara moja,Β  ilikuwa ni mishale ya saa moja kasoro.Β 

    Alikuja Mdada mmoja kunipokea, tena alinipokea kwa bashashaΒ  zote kama alikuwa akinifahmu vile, vile nilikuwa muelewaΒ  nilijuwa tu ni kazi yake ya kupokea wageni ndiyo inayomfanyaΒ  awe mchangamfu, nilimruhusu dereva aondoke, Mimi pamoja naΒ  yule mdada tuliongozana kuelekea juu ambako Osman alikuwepo,Β  jumba lake la kifahari lilikuwa la ghorofa tatu tu lakiniΒ  lilikuwa la kisasa mno, ilinifanya niwe na hamu ya kumuonaΒ  Osman.Β 

    “Osman yupo chumba hiki” Alisema Yule Mdada kisha akaongezaΒ  kwa kusemaΒ 

    “Ingia tuu” Yule Mdada aliondoka zake, niliangaza huku naΒ  kule kabla ya kufungua mlango huo ambao ulikuwa na kitasaΒ  chenye mg’ao wa Almasi, ilikuwa ni kwenye floo ya mwisho yaΒ  ghorofa. Nilipofungua mlango nilihisi kama nilikuwa nikiingiaΒ  kwenye bustani fulani hivi, Osman aliidizaini nyumba yakeΒ  mithiri ya Bustan ya Eden.Β 

    Ndani ya chumba hicho kulikuwa na mandhari za kuvutia sana,Β  hewa safi na upepo mwanana, mwenyewe Osman alikuwa amekaa juuΒ  ya Kiti akicheza na samaki walio kwenye bwawa dogo laΒ  kutengeneza. Aliponiona aliacha kila kitu kisha akaweka machoΒ  yake yote kwangu, najuwa moyo wake ulimwambia kuwa Jacklin niΒ  mrembo sana, maana alinitazama kutoka juu hadi chini kishaΒ  chini hadi juu kabla ya kunisemesha chochote. Nilitabasamu tuΒ  huku nikiwa nimeficha Mauwa nyuma kwa kutumia mkono wangu waΒ  kushoto, alinifuata kama vile mzimu, alinisalimia kwaΒ  kuhangaika kama si yeye aliyekuwa akiumwaΒ 

    “Ooh Jacklin! Karibu” Yaani Osman aliongea kama zuzu fulaniΒ  hivi asiyejuwa nini kinaendelea au kama Mtu ambaye hakuwa naΒ  taarifa kuwa ningefika pale wakati nilikuwa nikiwasilianaΒ  naye kuwa naenda.Β 

    “Asante!!” Nilisema kwa tabasamu murua, Osman alihangaikaΒ  kutazama ni wapi tungekaa.Β 

    “Kama hapa si sehemu nzuri tunaweza kwenda chumba kingineΒ  chenye sinema tukaangalia filamu mpya” Alisema Osman

    “Hapana Osman hapa pazuri panatosha, hewa yake ni safi sana”Β  NilisemaΒ 

    “Basi tukae pale” Alinionesha mahali ambapo alikuwaΒ  amepaandaa kwa ajili ya Mimi na yeye, hapo palikuwa na mezaΒ  ya mawe na viti vya mawe, juu yake kulikuwa na juisi mbiliΒ  ambazo ziliwekwa pambo la Ndimu, moyoni nikijikuta nikisemaΒ  “Wow”Β 

    Kusema ukweli Osman alikuwa romantic sana, alijuwa nini MaanaΒ  ya mapenzi, dakika chache tu za kuwa pale nilianza kuhisiΒ  kumpenda Osman lakini nilimkumbuka Mosses nilisema na moyoΒ  wanguΒ 

    “Hapana Jacklin, hapana una Mpenzi” Nilijisemea kishaΒ  nililazimika kufanya haraka, hata sikusogea kuketiΒ  alipopasema bali nilimwambiaΒ 

    “Osman! Lengo langu la kuja hapa kwanza ni kujuwaΒ  unaendeleaje lakini pili ni kukuomba msamaha kwa kileΒ  kilichotokea jana, haikuwa dhamira yangu. Nimejisikia vibayaΒ  sana tena zaidi ya sana” Nilisema kisha nilimuona OsmanΒ  akionesha kama vile tukio la jana halikumuumiza chochote kileΒ 

    “Aah usijali Jacklin, yameshapita hata hivyo wala sikuwekaΒ  akilini sana, karibu tukae” Alisema Osman, nilitoa mauwaΒ  nyuma yangu nikampatia, alikuwa ameduwaa mithiri yaΒ  Mwendawazimu aliyeona jalala lenye chakula, alikosa hata nenoΒ  la kusema, Mauwa ni ishara ya upendo hivyo ndivyo ilivyoingiaΒ  katika akili yakeΒ 

    “Ja…jac…Jacklin” Aliniita kama Mtu asiye na uhakika waΒ  jina languΒ 

    “Samahani na pia ugua pole” Nilisema kisha niligeuka naΒ  kuondoka nyumbani kwa Bilionea Osman, nikiwa nje nilimuonaΒ  akichungulia dirishani wakati huo giza lilikuwa limeingia.Β  Ilipita Bajaji niliita kisha niliitumia kurudi nyumbani.Β 

    Osman nilimuacha akiwa na furaha ambayo aliipoteza mudaΒ  mrefu, furaha ambayo Zahra aliichukua kwake lakini haikuwaΒ  kwamba ndiyo nilikuwa naanza mapenzi na Osman japoΒ  nilimuonesha ishara ya kumpenda, bado akili na mawazo yanguΒ  yalikuwa kwa Mosses.Β 

    Kabla hata sijafika nyumbani Osman alimpigia simu Mama naΒ  kumwambia kuwa nilienda kwake, Mama na Osman walikuwaΒ  wameivana sana kiasi kwamba Mama alikuwa akinitaka niwe naΒ  Osman. Waliongea kuhusu malengo na mawazo yao, nilipoondokaΒ 

    Hali ya Osman ilibadirika akakimbizwa Hospitalini, alikuwaΒ  mgonjwa japo ugonjwa wake alikuwa hajausema popote zaidi yaΒ  kwa Dokta Simon.Β 

    Nilipofika nyumbani nilishangaa kwa hali ambayo ilikuwepoΒ  jana kati yangu na Mama yangu, nilistaajabu kumkuta akiwa niΒ  mwenye furaha sana tena akiimbaimba nyimbo za kabila letu, niΒ  muda mrefu Mama hakuwahi kuwa kwenye furaha namna hiyo.Β 

    Nililazimika kumfuata na kumuuliza kuliko alikuwa mwenyeΒ  furaha sana.Β 

    “Nina furaha sababu Maombi yangu yanaenda kutoa majibu mudaΒ  siyo mrefu, nilichokiwaza kinaenda kudhihirika hivi karibuni”Β  Alisema Mama akiwa bizeΒ 

    “Mh! Mama uliomba nini na ulikuwa unawaza nini?”Β 

    “Siku zote Mama humuombea Mtoto wake na kumuwazia yaliyoΒ  mema, ni furaha kwa Mama kuona Alichokiwaza kinaendaΒ  kutendekea kwa Mtoto wake” Maneno ya Mama yalinipa tabasamuΒ  japo yalijaa mafumbo, mimi ndiye Mtoto wake wa kipekeeΒ  niliwaza atakuwa ameomba nini au kuniwazia niniΒ 

    “Mama unaniwazia nini Mwanao?” NilimuulizaΒ 

    “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaΒ  siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaΒ  kumuuliza, nilimwambiaΒ 

    “Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”Β  Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiΒ  Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. HadiΒ  naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naΒ  kuambiana kuwa nilienda kwa Osman.Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

    Pumzi ya mwisho

    18 Comments

    1. Selestin on October 16, 2024 7:14 pm

      https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J

      Reply
    2. Yudah on October 16, 2024 7:15 pm

      Duuh tamu lkn fupi sanaa admin, all in all mapenzi ni ushetaniπŸ˜… upofuuuu

      Reply
    3. Omary Tiliungwa on October 16, 2024 7:28 pm

      Daaah Jacky hebu amka ktk isingiz huo wenye upof
      Mpaka unaniumiza na mimi

      Reply
      • Abuu bura on October 16, 2024 8:15 pm

        Daaah mpaka najikuta nililia kila nikizidi kuiisoma hii riwaya inafundisha sana

        Reply
    4. Farnoush on October 16, 2024 7:30 pm

      Tupe na ya saba tu kwa leo hahahah πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
      • Siwema malekwa on October 16, 2024 11:28 pm

        Toa mbili mbili jamani

        Reply
    5. Sadick on October 16, 2024 7:54 pm

      Osman nae anaumwa dah!! Hii kweli pumzi ya mwisho this is fantastic story πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

      Reply
    6. Massay on October 16, 2024 8:57 pm

      Nzuri sana πŸ™πŸ™πŸ™

      Reply
    7. Angel on October 16, 2024 9:04 pm

      Admin upewe maua yako… unajua bhan…ila t tunaomb isiwah kuish…ivute vute had tuone jacklin na osman wamependan na kuoan

      Reply
      • Charz jr😎 on October 17, 2024 10:38 am

        Mmoja wao atakufa kati ya jack ama osmanπŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²

        Reply
    8. Irene LiwayaπŸ’ž on October 16, 2024 10:03 pm

      Nzuri sanA natamani ya saba admini🀣🀣🀣🀣🀣🀣

      Reply
    9. Given Gihsy on October 16, 2024 10:59 pm

      ila co kwa wadada wa bongo πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
      admin pongezi sana

      Reply
    10. Jesca mhanga on October 17, 2024 10:19 am

      Kwa kweli jack ni muuaji kabisa kupenda gani huko anakompenda Moses mwanaume aliesema bora afe lakini yeye maisha yaendelee kwake

      Reply
      • Charz jr😎 on October 17, 2024 10:38 am

        Ahahahahhaha eti kisa ndo mwanaume wake wa kwanzaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ huo ni udwanziii

        Reply
    11. Mt boy on October 17, 2024 2:05 pm

      Bora figo yang nkaipa hata mbuzi ntaila hata nyama kuliko mwanamke

      Reply
    12. πŸ—“ ⚠️ Confirmation Pending: 0.2 Bitcoin transaction held. Resume here > https://graph.org/UNLOCK-CRYPTO-ASSETS-07-23?hs=be8ebdf53df99effa031dffa3809ed31& πŸ—“ on September 6, 2025 9:12 am

      5s1klx

      Reply
    13. πŸ—“ πŸ’° BTC Transfer - 1.15 BTC waiting. Go to receive >> https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=be8ebdf53df99effa031dffa3809ed31& πŸ—“ on September 21, 2025 3:08 am

      v087bk

      Reply
    14. πŸ–‡ ❗ Security Needed - 0.7 BTC deposit on hold. Unlock now β†’ https://graph.org/Get-your-BTC-09-11?hs=be8ebdf53df99effa031dffa3809ed31& πŸ–‡ on October 14, 2025 9:33 pm

      5jkdy4

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi October 1, 2025

    In the name of LOVE – 12

    Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE Moyo Wangu na…

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.