Ilipoishia “Kwanza pole sana Jacklin, Dunia yako imekugeuka lakiniΒ ndivyo ilivyo sababu siyo Watu wote wanakuwa na simulizi tamuΒ za Maisha yao, yako chungu sana. Osman alikutafuta sana,Β ilisadikika kuwa Mlikuwa mmeuza kila kitu na kuondoka”Β Alisema Dokta Simon, stori yake ilikuwa ngeni masikioniΒ mwanguΒ
“Tuliuza kila kitu?” NilimuulizaΒ
“Ndiyo! Mzee Dhabi pia alihangaika kuwatafuta bila mafanikio,Β mwisho alikata tamaa baada ya kupata taarifa kuwa mliuzaΒ nyumba na kuondoka wewe na Mama yako!”Β
Haraka niligundua kuwa Mzee Dhabi alifanya yote pasipo OsmanΒ kujuwa. Endelea
Sehemu Ya Kumi Na Tatu
“Hapana Baba yake Osman alitumia hasira zake kutuondoshaΒ kwenye ile nyumba na kuchukua kila kitu tulichonunuliwa naΒ Osman, hatukuuza nyumba wala mali yoyote ile vyoteΒ vilichukuliwa na Mzee Dhabi, tuliishi Maisha ya mateso sanaΒ Mimi na Mama yangu” nilisema, nilishindwa kuzuia uchungu ulioΒ ndani ya moyo wangu, nililia sana tena kwa kwikwiΒ
“Usilie Jacklin, kwasasa unaishi wapi?” Alihoji Dokta Simon,Β nilifuta chozi langu nilitulia kwa sekunde kadhaa kishaΒ nilimjibuΒ
“Uswahilini, tulikuwa tunaishi kwa kuuza Mboga mboga mtaani.Β Na hii hali yangu nitaweza vipi kuendesha Maisha yanguΒ Dokta!” Chozi liliendelea kunibubujikaΒ
“Usijali nitakuchukua utaishi kwangu Jacklin wakati tunafanyaΒ utaratibu mwingine” Alisema DoktaΒ
“Samahani hivi Osman yupo wapi?” NiliulizaΒ
“Osman anaishi Marekani..” Alijibu Dokta Simon huku akioneshaΒ kutaka kusema kitu kingine ambacho alijizuia asikisemeΒ
“Anaishi na Zahra?” NilimuulizaΒ
Alishusha pumzi zake kisha alinitazama akanijibuΒ
“Ndio, wanatarajia kufunga ndoa miezi mitatu ijayo hapaΒ Nchini” Alisema Dokta SimonΒ
“Natamani kumuona Osman ili nimwambie kuwa sikukataa kuokoaΒ Maisha yake ila nilikuwa nimechelewa” Nilisema kwa kilioΒ kikubwaΒ
“Jacklin, hayo yameshapita, kwasasa tuangalie Afya yakoΒ kwanza ndiyo jambo lenye umuhimu zaidi kuliko chochote kile”Β Alisema Dokta Simon, nilimkubalia. Hakuchelewa sana aliondokaΒ wodiniΒ
Hakuna aliyekuja kuniona kwa siku nilizokuwa Hospitalini,Β moyo ulijaa upweke na maumivu makali, nilimkumbuka Mama yanguΒ jinsi alivyonilea na kunipigani katika nyakati zote.Β Nilitokwa na machozi kila wakati, Mama yangu aliondoka bilaΒ hata kuniaga, ilinipa shida sana hadi kuwa sawa. Dokta SimonΒ alijitahidi sana kila alipopata muda alikuja kuniangalia naΒ kunipa faraja kwa kuniambia maneno yaliyojaa matumainiΒ makubwa sana japo nilishajuwa kuwa thamani ya Maisha yanguΒ ilikuwa imeshaondoka.
Bili za Hospitali alizilipa mwenyewe Dokta Simon,Β nilimshukuru sana kwa ubindamu aliouonyesha kwangu.Β Alinichukua na kunipeleka nyumbani kwake baada ya mwezi mmojaΒ kupita, alikuwa akiishi na Mke wake aliyeitwa Lidia. NiliishiΒ kwa upendo na amani ya hali ya juu sana, Mke wa Dokta SimonΒ alikuwa na moyo kama wa Mume wake ndio maana ndege hawaΒ wawili waliruka pamoja sababu walifanana kwa kila kituΒ
“Usijali Jacklin Mungu atakupa ufalme mwingine kupitiaΒ maumivu yako” Alisema Mke wa Dokta Simon wakati nilipokuwaΒ najifunza kutembea kwa kutumia MagongoΒ
“Nashukuru kwa ukarimu wenu Lidia, mmenionesha thamani kubwaΒ iliyo ndani yangu ambayo niliona imeondoka, nilihisiΒ sitotabasamu tena. Mwisho ninekubali hali halisi kuwa siweziΒ kutembea hivyo nashukuru kwa kila kitu Lidia” Nilisema tukiwaΒ tumesimama kando ya Barabara.Β
“Dokta Simon alinieleza kuhusu wewe na Osman, alikutolea figoΒ na kuokoa Maisha yako”Β
“Ni kweli, katika vitu ambavyo ninajuta katika Maisha yanguΒ ni kutomshukuru Osman kwa wema wake alionitendea na kumuombaΒ Msamaha sababu sikuweza kuokoa uhai wake, nilishindwa kulipaΒ fadhila za Ubinadamu wake” Nilisema, nilihisi choziΒ likinilenga taratibuΒ
“Usijali Jacklin, hayo yameshapita. Haina haja tena kuingiaΒ kwenye Maisha ya Mtu nwingine na kumkumbusha yaliyopita.Β Sahau tu na Maisha yaendelee ” Alisema Lidia, tuliendelea naΒ mazoeziΒ
“Pamoja na yote ila uzuri wako Jacklin upo pale pale, wewe niΒ mzuri sana” Alisema Lidia,, alinifanya nitabasamuΒ
“Unanichokoza?” Nilisema kwa utani kisha tulicheka, tulikuwaΒ marafiki wakubwa sana kwa kipindi kifupi ambacho niliishiΒ nyumbani kwao, walijitahidi kuniondoa upweke, walinisaidiaΒ sana sikuwa na mawazo kama Mwanzo.Β
Usiku mmoja nikiwa nimelala, kutokana na dawa kali nilizokuwaΒ nameza kwa ajili ya kupunguza maumivu nilijikuta nikizamaΒ ndotoni. Ndoto ilianza kwa furaha sana, Niliota TukiwaΒ tunacheka na Osman, ghafla alikuja Mwanamke akiwa ameshikiliaΒ Bastola, Mwanamke huyo sikuiyona sura yake ila alisemaΒ
“Jacklin una muda mchache sana wa kuendelea kupumua, siweziΒ kukubali furaha yangu ukaiharibu kirahisi, Pumzi yako yaΒ Mwisho sema neno moja kabla sijakumaliza” Alisema MwanamkeΒ huyo, nilimtazama Osman ambaye alikuwa akishangaa tukio hilo,Β nilisemaΒ
“Nakupenda Osman” Lilikuwa ndiyo neneo langu la Mwisho katikaΒ pumzi yangu ya Mwisho, alinipiga risasi. Ghafla nilishtukaΒ kutoka Usingizini, nilihema sana, Jasho lilikuwaΒ likinibubujika, niliamka na kwenda kuwasha taa. Jumba laΒ kifahari la Dokta Simon lilikuwa kimya sana, sikutakaΒ kuwasunbua ila ndoto niliyoiota ilinishtua mno.Β
Nilijiuliza ndoto hiyo ilikuwa na maana gani, nilisali iliΒ Mungu aniweke mbali na hatari hiyo kabisa. NilikeshaΒ nikimuomba Mungu, Usingizi ulinichukua Alfajiri, AsubuhiΒ nilimsimulia Lidia kuhusu ndoto yangu, alicheka tuu kishaΒ alisemaΒ
“Tatizo rafiki yangu unawaza sana kiasi kwamba unatengenezaΒ hadi picha ya Uwongo kwenye akili yako, kumbuka kilaΒ unachokifikiria hutokea hivyo acha kutengeneza Maisha mabayaΒ ya Baadaye” Alisema akiwa ananiandalia chai, alikuwaΒ akinichukulia kama Mtoto mdogo yani kwa jinsi alivyokuwaΒ akinidekezaΒ
“Nimekuelewa Lidia” Nilisema.Β
- β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Osman aliwasili Nchini kwa ndege ya shirika la Fly EmirateΒ akitokea Marekani. Alirudi Nchini kwa ajili ya kufunga ndoaΒ na Zahra, tangu alipoondoka kwa ajili ya matibabu miezi kdhaaΒ iliyopita hakurudi tena. Aliwasiliana na Rafiki yake DoktaΒ Simon, ilikuwa ni furaha kwa marafiki hao kukutana tena OsmanΒ akiwa mwenye Afya, katika Maongezi yao Osman aliniuliziaΒ lakini Dokta Simon hakutaka kumwambia Osman kuwa Mimi nipoΒ nyumbani kwake, sina Mguu. Alifanya hivyo ili kuruhusu kilaΒ kilichopita kasirudi tena.Β
Nilishangaa siku hiyo Lidia aliniambia kuwa twende ShambaΒ tukakague, sikuwa na pingamizi sababu nilikuwa sina kaziΒ yoyote ile kumbe ndiyo siku ambayo Osman alikuwa anakujaΒ kutembelea nyumbani kwa Dokta Simon, hawakutaka nionane naΒ Osman, hawakutaka nijisikie vibaya. Basi tulipoondoka nyumaΒ Osman alienda nyumbani kwa Dokta Simon kwa ajili ya kupataΒ chakula cha Mchana na mazungumzo mengine ya kirafiki.Β
Tukiwa njiani tunaenda Shamba nilihisi kama kuna kitu hakipoΒ sawa kwangu, sikuwa na furaha ya kwenda huko shamba,Β nilimwambia Lidia kuwa sijisikii vizuri kuendelea na safariΒ hivyo turudi nyumbani.
“Unaumwa?” Aliniuliza LidiaΒ
“Hapana, sihisi kama natakiwa kuwa sehemu ya safari hii,Β samahani Lidia” nilisema ili kama nitakuwa nitakuwaΒ nimemkwaza anisamehe, Lidia alisemaΒ
“Mbona tumekaribia Jacklin jamani, ni hapo tu wala siyo mbaliΒ hata hivyo hatuchelewi” Alisema Lidia, nilizungumza sasa kamaΒ Binadamu ambaye sijatumia viungo vya mwili, si unajuwa vilemaΒ jinsi ambavyo wanapenda kujiongelea madhaifu yaoΒ
“Turudi Bwana au sababu unajuwa siwezi kutembea ndiyoΒ uniringie hivyo? Sijisikii na safari” Nilisema kishaΒ niliuchuna, niliegemea kwenye kioo huku moyo ukiniambiaΒ niwahi kurudi nyumbani, hata mwenyewe sikujuwa ni kwaniniΒ nilikuwa nataka kurudi nyumbani wakati tulikubaliana kuwaΒ twende Shambani.Β
“Usiseme hivyo Jacklin, Usimkufuru Mungu kiasi hicho, hayaΒ turudi” alisema Lidia kisha aligeuza gari, moyo ulianzaΒ kuchanuaΒ
Sasa kingine nilichokigundua ni kuwa Lidia alikuwa bizeΒ kupiga simu mahali alafu simu ilikuwa haiiti, nilijaribuΒ kuchungulia niliona alikuwa akimpigia Mume wake, nilijulizaΒ alikuwa anataka kumwambia nini?Β
Sikuwa na kifua cha kuweza kukaa na dukuduku, nilimuulizaΒ
“Unampigia nani?” Niliuliza makusudi tu wakati nilishaonaΒ alikuwa akimpigia Mume wake Dokta SimonΒ
“Nampigia Dada atuandalie chakula” Alisema kwa tabasamuΒ ambalo hata yeye mwenyewe aligundua kuwa alikuwa akiongopa,Β niligunaΒ
“Mh! Haya” Wala sikutaka eti kumuuliza zaidi wakati nilionaΒ alikuwa akimpigia Mume wake, hali ile iliendelea kwa mudaΒ mrefu, sijui sasa simu ilikuwa inaita alafu haipokelewi auΒ vipi, sikutaka kuhoji zaidi bali nilihisi jambo ambalo sikuwaΒ na uhakika nalo. Tulipofika Mjini kulikuwa na foleni kiasiΒ hivyo angalau nilimuona akitabasamu hadi nilishangaa yaaniΒ Watu wanakasirika kisa foleni yeye anafurahiaΒ
Nilicheka chini chini baada ya kugundua alikuwa amepagawa,Β Basi haikutukuchukuwa muda mrefu kufika nyumbani. NiliiyonaΒ gari ya kifahari ikiwa imeegeshwa karibu na Bustani ya Mauwa,Β ilikuwa ya kifahari sana.
“Ile gari ni ya Nani?” Niliuliza maana sikuwahi kuiyona paleΒ nyumbaniΒ
“Aaah ile?” Aliuliza Lidia kama vile hakuwa na jibu laΒ kunipa, nilimkaziaΒ
“Ndiyo! Ile nyeusi sijapata kuiyona hapa nyumbani, inaonekanaΒ ni ya kifahari sana.” Nilisema huku Lidia akiwa anasogezaΒ gari eneo la maegesho.Β
Kumbe Dokta Simon alikuwa tayari amewasiliana na Mke wake kwaΒ njia ya ujumbe mfupi, lengo lao lilikuwa ni kutotaka Mimi naΒ Osman tuonane pale. Huko ndani sasa ambako Osman na DoktaΒ Simon walikuwepo walikuwa wakizungumza mambo yao ilaΒ waliposikia ngurumo ya gari, Osman alitaka kuchungulia hukuΒ akimuuliza Dokta SimonΒ
“Shemeji Lidia huyo?” Simon alipoulizwa hivi alibakia akiwaΒ anajiuma meno asijuwe ajibu vipi, ni kweli tulikuwa Mimi naΒ Lidia sasa angemjibi vipi ikiwa hataki Mimi na Osman tuonane?Β
“Ndi…ndi…oo”Β
“Mh! Mbona unajibu kama hauna uhakika, ni bora ukaangalieΒ kama ni yeye maana muda wangu umeisha hapa ingawa nilihitajiΒ sana kumuona” Alisema OsmanΒ
“Sawa ngoja nikaangalie, jisikie huru rafiki yangu” alisemaΒ Dokta Simon kisha alikuja kwenye Maegesho akatukuta mimi naΒ Lidia tukizozana maana alikuwa hataki nishuke kwenye gariΒ
“Bora hata Shemu umefika yaani Mkeo simuelewi kabisa, huweziΒ amini ananizuia kushuka kwenye gari” nilisemaΒ
“Aaah Mke wangu kwanini unafanya hivyo?” Aliuliza Dokta SimonΒ
“Jacklin hajanielewa, nilikuwa nimemwambia asubirie weweΒ ufike ili ukamuoneshe sapraizi yake” Alisema Lidia,Β nilijikuta nikitabasamu kusikia kuna SapraizΒ
“Sapraiz gani hiyo?” Niliuliza, mkononi Dokta Simon alikuwaΒ na kitambaa cheusi akaniambia anifunge machoniΒ
“Jamani jamani Sapraizi gani hiyo mbona mnanitisha” NilisemaΒ
“Hebu kwanza nikufunge ili ukaiangalie Sapraiz itakayoΒ kufanya upagawe” Alisema Dokta Simon, Basi nilikubaliΒ kufungwa kitambaa kumbe lengo lao lilikuwa Nisimuone Osman,Β Walinipeleka nyuma ya nyumba
“Jamani nna hamu ya kuona hiyo Sapraiz” NilisemaΒ
“Haya hebu nikufungue” Alisema Dokta Simon, moyo wanguΒ ulijawa na furaha sana nilipomuona Kasuku akiwa kwenye kiziziΒ chake, nilikuwa napenda sana Kasuku, sikuwaza chochote tena.Β Nilivuta Magongo yangu na kulisogelea Zizi la Kasuku, DoktaΒ Simon alimpa Ishara Mke wake kuwa anatoka, muda huo akiliΒ yangu wala haikuwa hapo, walinipeleka sehemu ambayo hataΒ nisingeliweza kusikia sauti ya gariΒ
Osman alikuwa akimsubiria Dokta Simon ndani, alipofikaΒ alimdaka kwa swaliΒ
“Ni yeye?”Β
“Mke wangu?”Β
“Ndiyo!”Β
“Aah hapana, ni Kijana wangu wa kazi alikuwa akileta gari”Β
“Oooh! Sawa Basi ngoja Mimi niende” Osman aliaga, alielekeaΒ lilipo gari lake kisha aliondoka pale nyumbani bila kuhisiΒ wala kujuwa kuwa nilikuwa pale.Β
Nilikuwa nacheza na kasuku wangu mzuri niliyepewa kamaΒ zawadi, nilisahau kila kitu. Lidia na Mume wake waliingiaΒ ndaniΒ
“Hajashtuka chochote” aliuliza LidiaΒ
“Hapana sijui Jacklin!”Β
“Hapana japo alikuwa na wasiwasi kama nilivyokutumia mesejiΒ kuwa hatukufika shambami aligaili njiani” Alisema LidiaΒ
“Mmmh kuna namna hawa Watu wawili wanawasiliana kifikra,Β sitaki waonane, sitaki turudi tulipotoka. Osman ameamuaΒ kuendelea na Maisha yake, nataka Jacklin naye aendelee naΒ Maisha yake, atapata Mtu atakaye mpenda kwa jinsi alivyo”Β Alisema Dokta Simon, alikuwa ni Mtu safi sana, roho yakeΒ ilikuwa nzuri iliyojaa hurumaΒ
“Cha Msingi ni kuendelea kuhakikisha hajisikii mpweke”Β Alimalizia Dokta Simon.Β
Hayo ndiyo yalikuwa Maisha yangu, mipango ya Harusi ya OsmanΒ iliendelea kufanyika, kumbe katika kipindi hicho chote OsmanΒ alikuwa hajakata tamaa ya kunitafuta japo Baba yakeΒ alimuongopea kuwa tuliuza nyumba na kuhama mji, alinitafutaΒ bila mafanikio lakini alijipa tumaini kuwa ipo siku ataniona,Β
Masikini hakujuwa kama Mimi ni kilema wa Mguu, hakujuwa kuwaΒ Mama yangu ambaye alikuwa akihangaika naye kunitafutia figoΒ alikuwa amefariki siku nyingi. Hakujuwa kama nilikuwaΒ nikiishi kwa rafiki yake.Β
Wazazi wa Osman walikuja kutoka Dubai, Harusi ilipangwa kwaΒ kuzingatia heshima aliyonayo Mzee Dhabi, umaarufu na utajiriΒ wake. Moyo wa Mzee Dhabi ulificha unyama ambao alitutendeaΒ Mimi na Mama yangu.Β
Lidia na Osman walikuwa ni miongoni Mwa Watu wa karibu waΒ Familia ya Mzee Dhabi, walishiriki maandalizi kisiri sanaΒ bila Mimi kujuwa kwa kipindi chote, walikuwa wakiingia naΒ kutoka alafu hakukuwa na stori zozote kuhusu Ndoa ya Osman,Β Β nakumbuka siku moja nilimuuliza Dokta Simon kama ndoa yaΒ Osman ilikuwa imepitaΒ
“Imeshapita, walitaka kufanyia huku lakini walighaili,Β imefanyika huko Dubai ambako anaishi kwasasa” NdichoΒ alichonijibu Dokta Simon, nilikuwa mnyonge baada ya kusikiaΒ hivyoΒ
“Usijali Jacklin, haikuwa ridhki yako ndiyo maana yalitokeaΒ yaliyotokea, sahau kila kitu Maisha yaendelee sawa?” AlisemaΒ tena Dokta SimonΒ
“Sawa” Nilijibu huku moyo wangu ukiwa na maumivu makali sana,Β Osman kuowa haikuwa shida kwangu ila kilichoniuma zaidiΒ ilikuwa ni kushindwa kumshukuru na kumwambia kuwa nipo HaiΒ anisamehe kwa kila kitu.Β
Nilikaa na picha ya Osman kwa muda mrefu, siku mojaΒ niliichoma moto, nilifungua ukurasa mpya wa Maisha yangu,Β niliyapotezea maumivu kwa kucheza na Kasuku wangu, sikutakaΒ kabisa kumfikiria Osman wala kukumbuka kilichomfika MamaΒ yangu maana mambo hayo mawili yalikuwa yakinifanya nakuwaΒ mnyonge sana. Niliamua kujisahaulisha hata alichonifanyiaΒ Mosses..Β
Siku moja ilikuwa Mchana nilimpigia simu Lidia nikamwambiaΒ kuwa nina hamu ya kula Ice Cream, alikuwa kazini hivyoΒ alinitaka nivumilie kidogo, baadaye alimtuma dereva taxi ajeΒ kunichukua anipeleke mahali ambapo Lidia alikuwepo iliΒ tukanunue Ice Cream. Nilipofika niliingia kwenye gari yaΒ Lidia, tulielekea kwenye Ice Cream huku tukipiga stori zaΒ hapa na pale ambazo zilituburudisha kwa kiasi fulani.
Kutoka nilipomkuta Lidia hadi sehemu ambayo Ice creamΒ zilikuwa zinauzwa hapakuwa mbali sana, mwendo mfupi tuΒ tulikuwa tumefika. Kutokana na hali ya Mguu wangu LidiaΒ aliniomba nisishuke kwenye gari badala yake nimsubirie! BasiΒ Lidia alishuka na kuingia zinapouzwa Ice cream ambazoΒ nilikuwa nikizipenda sana, alichelewa sana hadi nilianzaΒ kujiona mpweke ndani ya gariΒ
Nilitamani kushuka lakini kabla wazo la kushuka halijaniingiaΒ sawa sawa, simu ya Lidia iliita, iliita kwa muda mrefu sanaΒ hadi nilitamani kuangalia ni nani alikuwa akipiga ilaΒ nilihisi uvivu fulani, sasa katika angalia angalia nilionaΒ kitu kama kadi hivi. Nilipata shahuku ya kuiangalia,Β nilinyoosha mkono na kuichukua.Β
Nilianza kuisoma, ilikuwa ni kadi ya harusi ya Osman naΒ Zahra, moyo uliniripuka paa! Nikaangalia mlango ambao LidiaΒ aliingia hakukuwa na Mtu aliyekuwa akitoka nikaendeleaΒ kuisoma. Cha ajabu kadi ile ilikuwa haijatumika kabisa yaaniΒ tarehe iliyoandikwa ilikuwa ni siku mbili mbele, zilikuwaΒ kadi kama tano hivi zenye majina ila hiyo moja ilikuwa hainaΒ jina basi niliiweka kwenye mkoba wangu haraka ili nikituliaΒ niisome vizuri, nilijikuta nikianza kuwa na huzuni sana.Β
Punde Lidia alirejea ndani ya gari akiwa na Ice Cream,Β nilimtazama sana hadi aliniulizaΒ
“Vipi kuna tatizo?” Aliniuliza akiwa ananipatia Ice Cream,Β nilitabasamu tu baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikifichwaΒ jambo maana Dokta Simon alisema Harusi imeshapita ila chaΒ ajabu kadi zile zilisema kuwa ni siku mbili baadayeΒ
“Hakuna shida” nilimjibuΒ
“Nimepata hiyo ile nyingine unayoipenda haipo” Alisema LidiaΒ
“Hata hii siyo mbaya kikubwa ni Ice Cream” nilimjibu kishaΒ nilianza kufakamia Ice Cream, nilikula kwa hasira sana baadaΒ ya kugundua Lidia na Mume wake hawakuwa wakweliΒ
“Tunarudi nyumbani au kuna mahali unataka twende” aliulizaΒ Lidia akiwa anawasha gariΒ
“Nafikiri turudi nyumbani tu” Basi Tulirudi nyumbani.Β
Tulipofika nilielekea chumbani kwangu nilihakikisha nimefungaΒ mlango vizuri ili niweze kuisoma ile kadi kwa utulivu,Β nilikaa kitandani, niliitoa na kuanza kuisoma tena. KibayaΒ zaidi ni kuwa waliokuwa wakizisambaza zile kadi walikuwa niΒ Dokta Simon na Mke wake Lidia.
Nilitamani kulia kwa uchungu ambao nilikuwa nikiusikia kwenyeΒ moyo wangu, mara nyingi nilikuwa nikiwauliza kuhusu OsmanΒ lakini walikuwa wakinipa majibu ya Hatuna mawasiliano nayeΒ sana kwa sasaΒ
Nililia sana, niliona nimenyimwa haki ya kumuomba msamaha naΒ kumshukuru Osman, niliihifadhi ile kadi kwenye Begi langu laΒ nguo. Sikutaka kuwauliza chochote kile, siku hiyo Usiku LidiaΒ alikuja chumbani kwangu na kuniambia kuwa anasafiri na MumeΒ wake kwenda Nje ya Jiji watarudi baada ya wiki mojaΒ
“Nitawamiss sana jamani” nilisemaΒ
“Usijali Jacklin hata sisi tutakumiss mno, ubaki salama naΒ kwa chochote usisite kutupigia simu” Alisema LidiaΒ
Alipoondoka nilitafakari nifanye nini maana nilijuwa tuΒ walitengeneza safri feki ili kunizuga kuhusu Ndoa ya Osman.Β Kweli siku iliyofuata asubuhi mapema waliniaga rasmi,Β waliingia kwenye gari niliwapungia mkono wa kuwaaga,Β waliniacha na Mdada wa kazi na Mlinzi.Β
Walipoondoka nilimfuata Mdada wa Kazi aliyekuwa anaitwa ScolaΒ nikamuulizaΒ
“Unakunbuka siku ambayo Mimi na Lidia tulienda Shambani? IleΒ siku ya mwisho?..” nilimuuliza alionekana kutafakari sanaΒ
“Ndio nakumbuka” alinijibu baada ya kuwa tayari amemalizaΒ kutafakariΒ
“Kuna mgeni alikuja hapa si ndiyo?” Scola alinitolea machoΒ yake MakubwaΒ
“Scola nijibu alikuja Mgeni si ndiyo?” Nilimuuliza tena baadaΒ ya kuona alikuwa hanipi jibuΒ
“Lakini Dada..” alisema Scola, nikahisi kuna jamboΒ
“Sitaki cha lakini nataka uniambie ukweli ni nani alikujaΒ hapa?” Nilimkazia sauti na jichoΒ
“Baba alisema nisiseme unanipa wakati mgumu Dada Jacklin”Β Nilimshika mkono Scola nikamuingiza chumbani kwanguΒ nikamwambiaΒ
“Tupo Mimi na wewe naomba unieleze ukweli ni nani alikujaΒ hapa”Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA NNE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho
Β Β




7 Comments
Jamani Jacklineπ’
Mapenzi mabaya sana yasikie tu kwa mwenzako omba yasikukute
Leo umejitahidi sana admini
ππππ
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H
Maisha Kitaa WhatsApp channel
uk4exa
j2zpta
Can you be more specific about the content of your article? After reading it, I still have some doubts. Hope you can help me. https://www.binance.com/es-MX/register?ref=GJY4VW8W