Ilipoishia “Scola nijibu alikuja Mgeni si ndiyo?” Nilimuuliza tena baadaย ya kuona alikuwa hanipi jibuย
“Lakini Dada..” alisema Scola, nikahisi kuna jamboย
“Sitaki cha lakini nataka uniambie ukweli ni nani alikujaย hapa?” Nilimkazia sauti na jichoย
“Baba alisema nisiseme unanipa wakati mgumu Dada Jacklin”ย Nilimshika mkono Scola nikamuingiza chumbani kwanguย nikamwambiaย
“Tupo Mimi na wewe naomba unieleze ukweli ni nani alikujaย hapa”ย Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA NNE
“Kusema ukweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumuona ilaย nakumbuka Baba alisema nisikwambie wewe, aliniambia niandaeย chakula chenye hadhi ya kuliwa na Bilionea. Aliniambia kuwaย ni Mtoto wa tajiri Mkubwa sana anaitwa Dhabi” Alisema Scolaย
“Basi inatosha, Asante!!” Nilimkatisha Scola, nilifunguaย mlango na kumpa ishara kuwa atoke, alikuwa ameniambia ukweliย ambao nilifichwa na Lidia na Dokta Simon.ย
“Dada naomba Usimwambie Baba” alisema Scolaย
“Usijali Scola siwezi kufanya hivyo, nenda nahitajiย kupumzika” Basi Scola aliondoka zakeย
Unajuwa yale maumivu ya kuchomwa na msumari mguuni? Ndiyoย ambayo nilikuwa nikiyapata kwenye moyo wangu, kulia haikuwaย tiba, kukaa haikuwa tiba, nilitamani nipate sehemu yenyeย utulivu nipige ukunga hadi sauti yangu iishe.ย
Basi siku mbili zilipita, ilikuwa ni tarehe 25/09 ndiyo sikuย ambayo iliandikwa kwenye ile kadi, moyo wangu uliniambia kuwaย ndiyo siku pekee ya kuonana na Osman, nilisoma muda ambaoย Harusi ilikuwa ikifanyika, ilikuwa ni saa 2 Usiku katikaย Hoteli ya nyota tano ya BAMOL DE HOTEL, muda nawaza yoteย ilikuwa ni mchanaย
Nilijaza jina langu kwenye ile kadi, nilijuwa tukioย litawashangaza wengi lakini ili moyo wangu utulie ni lazimaย nionane na Osman na sehemu peke ilikuwa ni kwenye harusiย yake.ย
Niliandaa gauni langu zuri jeusi, mishale ya saa mojaย nililivaa, nilijitazama kwenye kioo niliona jinsiย nilivyopendeza ila nilipofunua gauni nilipata huzuni sana,ย sikuwa na mguu mmoja wa kuvalia kiatu, mkononi nilikuwaย nimeshikilia kiatu cheusi cha kupandaย
Nilikitupa pembeni, nilikusanya magongo yangu, nilimpitaย Scola akiwa anaingia jikoni, niliondoka nyumbani Usiku huoย ili nielekee Hotelini, niliita Tax nikaanza safri huku moyoย wangu ukiwa na maamuzi mawili ya kuacha au kuendelea naย safari, niliazimia ni bora niende tu. Nikiwa kwenye Tax Lidiaย alinipigia simu akaniuliza nipo wapi, nilishangaa sanaย
“Nipo njiani narudi nyumbani” nilimjibuย
“Ulikuwa wapi?” Aliuliza
“Nilikuwa kwenye matembezi kidogo nilichoka kukaa tuย nyumbani”ย
“Sawa ukifika nipigie niongee na Scola”ย
“Sawa!” Alikata simuย
Niliona ni bora niizime simu sikutaka tena kufikiria kuhusuย wao.ย
Nilifika Hotelini mishale ya saa tatu kasoro, palikuwaย pamepambwa sana kwa nje, ulinzi ulikuwa wa kutosha sanaย sababu aliyeko ndani alikuwa ni Bilionea Mkubwa sana.ย
Niliangalia kadi yangu, niliongoza kuelekea kwenye lango kuuย ambalo lilikuwa na walinzi, kumbe nyuma yangu alikuwepo Doktaย Simon alafu sikushtukia ila kwakuwa alikuwa na pirika nyingiย wala hakuniona, nilimshtukia aliponipita.ย
“Kumbe mpo hapa Mjini eeh! Kitakachotokea hamtoamini, kamaย hamtotaka kuishi na Mimi tena ni sawa tu” nilijisemea ndaniย ya moyo wangu! Nilionesha kadi yangu pale mlangoniย nilikaguliwa kisha niliruhusiwa kingia ndani ya Hoteli,ย nilielekezwa mahali ambapo harusi ilikuwa inafanyika.ย
Nilitembea na Magongo yangu kwa tahadhari sana maana kamaย nitakutana na Lidia au Mume wake mpango ungekufa. Watuย walikuwa wamependeza sana, ile nakaribia nilimuona Mzee Dhabiย akizungumza na Simu basi niligeuza haraka kama narudiย nilipotoka maana kama ningeendelea mbele angeniona, bahatiย nzuri kulikuwa na chemba upande wa kushoto niliingia hukoย hadi pale alipomaliza kuongea na kurudi Ukumbini.ย
Nilijitoa na kuelekea Ukumbini, kweli ilikuwa ni harusi yaย Kifahari ambayo hata kwnye Filamu sikupata kuishuhudia, rohoย iliniuma sababu nilipaswa kuolewa mimi, ilipaswa Mama yanguย awepo kwa ajili ya furaha ambayo aliipigania.ย
Nilitafuta Kiti cha nyuma kabisa ili nisije onekana naย wanafamilia, Muda ambao nilikuwa nimefika ndio kwanza ilikuwaย inaanza. Matajiri wenye rangi nyeupe walikuwa wengi mno,ย nilijitahidi kuangaza huku na kule ili nimuone Osman.ย
Kweli nilimuona Osman, huwezi amini nilijikuta nikisimamaย bila kurajia, nilimtazama Osman akionekana kuwa mwenye furahaย sana, pembeni yake alikuwepo Zahra naye akiwa mwingi waย tabasamu. Nilishuka na kuketi bila kutaka, Shughuli ilianzaย kwa kutambulisha baadhi ya Watu wakubwa waliohudhuria pale,ย Dokta Simon na Lidia walikuwa wakizungumza jambo hukuย wakionekana kupiga simu bila kupokea majibu, nilijuwa tuย walikuwa wakinipigia Mimi kujuwa niko wapi naona hata waoย hofu iliwaingia maana Scola sikumuaga kabisa.ย
Nilisubiria muda sahihi wa kuonana na Osman bila kubuguzi mtuย yeyote wala kuharibu chochote kile ila kadili muda ulivyozidiย kwenda ndivyo nilivyogundua kuwa hali yangu ya kuhitajiย kuonana na Osman ilikuwa ikipanda.ย
Muda wa Osman kumvisha pete Zahra ulipowadia roho ilizidiย kuniuma, wengi walisimama na kupiga makofi kwa ajili yaย tukio, ila macho yangu yalikuwa yakibubujikwa na machoziย mfululizo, nilijitahidi kujizuia nilishindwa, nilitamaniย kuondoka pale Ukumbini pia nilishindwa. Katika hali isiyo yaย kawaida nilihisi kuguswa kwenye bega langu, nilipogeukaย nilikutana na Lidia. Nilishtuka sana huku chozi likiendeleaย kunibubujikaย
“Jacklin umefuata nini hapa?” Aliniuliza Lidia kwa sauti yaย Chini ambayo hakuna aliyesikia maana wengi akili yao ilikuwaย kule mbele. Nilimpiga kofi Lidiaย
“Muongo Mkubwa wewe, kama ni furaha kusema uwongo na kufichaย kilicho kizuri basi furaha yako haiwezi kudumu Lidia, wewe niย Muongo na mnafiki Mkubwa” Nilisema kwa sauti ya kawaidaย ambayo baadhi waliisikiaย
“Jacklin naomba tutoke tukaongee tusije haribu shughuli yaย Watu” Alisema Lidiaย
“Tayari imesha haribika Lidia, unafikiri nitakubali kuondokaย bila kumwambia Osman kuwa nipo hai, kumwambia kuwa Mimi niย kilema wa Mguu, kumwambia kuwa Mama yangu amefariki,ย kumshukuru na kumuomba Msamaha?” Watu wa karibu walianzaย kututazama, Lidia alishtukia hilo akasemaย
“Nakuelewa Jacklin, naomba tukaongee hilo halina shida”ย akaanza kutaka kunitoa pale kitu ambacho sikukubaliana nachoย
“Niacheeee! Niache Lidia Niache…” nilisema kwa sauti ya Juuย ambayo ilimshtua kila Mtu, macho yote yalikuja upande wetu.ย Bahati nzuri nilikuwa nimeonesha mgongo kule waliko akinaย Osman hivyo aliyeonekana vizuri alikuwa ni Lidia, Dokta Simonย haraka alikuja baada ya kumuona Mke wakeย
“Jacklin hukupaswa kuja hapa kabla mambo hayajaharibikaย nakuomba urudi nyumbani, yote tutayaongea kule” Alisema Doktaย Simon
“Siwezi kuondoka hapa bila kuongea na Osman, hamjui ni jinsiย gani naumia Mimi, hamjui ni jinsi gani Maisha yangu yamejaaย majuto, ili moyo wangu uwe sawa ni lazima nionane na Osmanย leo” nilisema kwa sauti ya Juu, Osman alinisikia, sauti yanguย aliijuwa, alipiga hatua tatu mbele akiwa ameshikilia pete,ย Zahra alimshika mkono kumzuia asije upande wangu! Hakunaย aliyeshtuka kuwa nilikuwa ni Mimiย
Upande wa Familia ya Osman wote walisimama, taa ililetwaย kwangu ili nionekane. Ilibidi nigeuke kutazama mbele ambakoย Osman na Watu wengine walikuwepo, Mzee Dhabi alishtuka sanaย kuniona, Osman alitumbua macho yake kwa Mshangao, hakutegemeaย kama angeniona tena katika Maisha yake.ย
Dokta Simon na Mke wake walitazamana ni wazi hawakufurahiaย Mimi kuwepo pale, chozi lilikuwa likinivuja, nilimtazma Osmanย ambaye naye alikuwa bize kunitazama, Zahra aliuacha Mkono waย Osman. Ukumbi mzima ulikuwa kimya sanaย
Nilichukua magongo yangu nikaanza kujongea kuelekeaย aliposimama Osman, nilimuona akiwa mwenye mshituko mkubwaย baada ya kugundua kuwa nilikuwa kilema wa mguu, hata Mzeeย Dhabi na Mke wake nao walishangaa sana.ย
Nilisogea karibu na Osman nikiwa natabasamu kwa maumivuย makali sana, Osman alidondosha chozi lakeย
“Jacklin?” Aliniita, niliitika kwa kutumia kichwa maana mdomoย ulikuwa mzito sanaย
“Upo hai? Ulipatwa na nini, umepoteza Mguu?” Aliniuliza kwaย hisia kali sana, nilitoa tabasamu lenye maumivu nikamwambiaย
“Nilipata ajali” nilitokwa na machozi nilishindwa kujizuiaย kabisaย
“Mama yupo wapi?”ย
“Mama amefariki Osman”ย
“Mungu wangu! Mlienda wapi?” Aliuliza Osman, nilitaka moyoย wangu uwe safi, nilimuonesha kidole Baba yakeย
“Baba yako alitufukuza kwenye ile nyumba, tulirudi Mtaaniย ndipo yalipotukuta haya yote, naomba unisamehe Osman,ย nilihitaji kukusaidia sana ila nilichelewa” Watu woteย walimtazama Mzee Dhabi, ilitosha kuidhihirishia Dunia kuwaย Baba yake Osman alitutendea Unyama!! Osman alimgeukia Babaย yake akamuuliza
“Baba ni kweli?” Aliuliza Osman akiwa anatiririkwa naย machozi, Mzee Dhabi hakuwa na jibu zaidi ya kuinamia chini.ย
“Baba ulisema waliuza kila kitu na kuhama Mji, ulisemaย haijulikani kama wapo hai au wamekufa, walikukosea nini Baba?ย Kumbe mkatili kiasi hicho Baba yangu! Mungu ameamuaย kukudhihirisha mbele za Watu wanaokuheshimu na kutaka kuwaย kama wewe, ulitaka iwe hivi si ndiyo?” Alisema Osman kwaย hisia kali ambayo hakuna aliyeweza kumzuiaย
“Osman imeshatokea! Hayo yamepita, nahitaji msamaha wako tu”ย Nilisema.ย
“Jacklin nilishakusamehe tokea ile siku ambayo ulikataa kuwaย Mke wangu, niliheshimu maamuzi na mawazo yako” Alisema Osman,ย huzuni ilitanda pale ukumbini, wenye mioyo midogo waliliaย
“Baba ulitaka nimuowe Zahra kwasababu alikubali kutoa figoย yake kwa ajili yangu? Ukasahau ndiye aliyesababisha jerahaย ndani ya Moyo wangu, aliniacha katika wakati ambao nilikuwaย sina chaguo lingine. Maumivu na mateso niliyoyapta ameyalipaย kwa kutoa Figo lake, Hata Moyo wangu Baba unajuwa kuwaย nampenda Jacklin, namuhitaji ila ulijaribu kumuweka mbali naย Maisha yangu!” Alisema Osman kisha alinikumbatia, Huweziย amini Zahra alilia sana pale chini, alitoka mbio akakimbiliaย njeย
Mzee Dhabi na Mke wake walilia kwa maumivu makali sana.ย Nilivyomkumbatia Osman nilihisi akiwa anapumua kwa shidaย sana, alikuwa akitaka kusema neno ambalo nilitamaniย kulisikia, neno ambalo hadi hivi leo sijui alikuwa anatakaย kuniambia nini, alisizi kwenye mwili wangu bila kuhema tena,ย ilikuwa ndiyo Pumzi ya Mwisho ya Osman katika hii Dunia,ย hakuna aliyejuwa kuwa Osman alifia kwenye mwili wangu. Mzeeย Dhabi alisogea na kupiga magoti akasemaย
“Osman! Nisamehe Mwanangu,,nisamehe kwa yote, nilifanya kwaย hasira baada ya kuona amekataa kusaidia Maisha yako, nimekupaย hasara Jacklin umempoteza Mama yako na Mguu wako naombaย mnisamehe” Alisema Mzee Dhabi, ukimya wa Osman ulianza kunipaย wasiwasi, nilimuacha lakini cha ajabu alienda chini kamaย Mzigo, haraka gari ya wagonjwa ilifika, Osman alipelekwaย Hospitalini. Sote tulienda kusubiria hatma ya Osman, kilaย mmoja alikuwa kimya, nilikuwa mwingi wa kulia tu.ย
Masaa matatu Baadaye Dokta Simon alitoka chumba cha Wagonjwaย mahututi, alitupa taarifa iliyoondoa uhai wa Bilionea Dhabiย pale pale, Ndio, Osman alikuwa amefariki kwa mshituko naย mfadhahiko. Mzee Dhabi na Osman walizikwa nyumbani kwaย Osman,,,nilimshukuru Mungu kwa kila jambo lililonifika kwenyeย Maisha yangu. Nilipoteza kila kitu lakini Mke wa Bilioneaย Dhabi aliniambia kuwa ananipa Nusu ya mali zote za Bilioneaย Dhabi.ย
Nilipewa kila kitu nilichoahidiwa, japo havikuwa na thamaniย ya kuzidi uhai wa Osman, Bilionea Dhabi, Mama na Mguu wangu.ย Nilijiapiza kuwa sitokuja kupenda tena katika Maishaย yangu.,,,,Miezi mingi ilipita, maumivu ndani yangu yalianzaย kupona, niliwekewa mguu wa Bandia.ย
Siku moja asubuhi nikiwa naelekea JM Motors nikiwa kamaย mmiliki wa kampuni hiyo ya Uuzaji wa magari, nilijikutaย katika foleni eneo lile lile ambalo nilijikuta kwenye Foleniย siku ya kwanza kabisa ambayo nilikuwa naenda JM Motors kuombaย kazi, ndiyo siku ambayo nilikutana na Osman. Moyo wanguย uliingiwa na maumivu makali sana, nikiwa nasubiria gariย zianze kutembea, Mtu mmoja ambaye ni ombaomba aligonga kiooย cha gari yangu! Nilikuwa ni Mtu ninayezijuwa shida sanaย kutokana na Maisha niliyopitia, nilifungua kioo, moyoย uliniripuka sana. Aliyegonga kioo alikuwa ni Mosses Mwanaumeย niliyekuwa nampenda sana katika Maisha yangu, alikuwa haoniย yaani kipofu wa macho yote mawili hivyo yeye hakujuwa alikuwaย akimuomba pesa nani, sikujuwa alikuwa amekutwa na nini ilaย hata vidole vyake vilikuwa vimekatika.ย
Nilimpa noti ya Shilingi Elfu tano, kisha aliondoka zake,ย unajuwa kwanini nilimpa noti ya Elfu tano? Ni kwasababu ileย siku aliniahdi kunitumia pesa ya pikipiki alafu hakunitumiaย wakati huo Elfu tano yangu nilimpa marehemu Osman, nilisemaย
“Malipo ni hapa hapa Duniani Mosses, Kwaheri ya kuonana”ย Nilifunga kioo kisha niliondowa gari yangu.ย
โขโขMWISHOโขโขโข
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kununua SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย 
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho
ย ย
 
		
 
									 
					
24 Comments
Ongera nimeipenda
Ila wewe dada!!!!
So sad ๐ข
Mapenzi ni ugonjwa usio na dawa
Eeee Mwenyezi Mungu naomba unipe atakae nipenda kwa dhati kama mapenzi ya Osman kwa Jacklin.
Stori ya kuhuzunisha yenye Mafundisho tosha na maumivu makali ndani yake.๐ญ
Maskini Jacklin kapoteza kila kitu maishani mwake๐ข
๐ญ๐ญDah wow asee nimeipenda sana๐ฅ๐ฅ๐ฅ hii episode imeniuma sana
๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ
Una jua yale maumivu ya kuchomwa msumari kwenye isia feck ๐๐๐๐
๐ซ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ซ
Appriciated @Kaka mkubwa
Live long…uzidi kutupa madude mkuu๐๐ค
Una jua yale maumivu ya kuchomwa msumari kwenye isia feck ๐๐๐๐
Nampa pongezi mwandishi kalamu yake amejua kuitendea haki Yuko vizuri ๐๐๐
Kiukweli nimejifunza kitu asante mwandishi unajua unastahiri mauwa yako
Tamu sana inajenga hisia fulani
Chukua๐น๐บ๐ท๐ฅ yako
Kali kinoma
Kaka mkubwa KWELI wewe ni kaka mkubwa umeumba ulimwengu wa kufikirika mpaka basi……. SASA WATENGENEZA FILAMU MPOWAPI? HAMONI MNANGOJA NINI?…SHIRIKIANENI NA KAKA MKUBWA!!! MTUTENGENEZEE DUDE JAMANIEE
Inagoma nkitaka kutuma hela….inasema no hii haijathibitishws
Aiseee hii simulizi ni nzuri sanaa ๐
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H
SIMULIZI|Jinsi paka alivyomaliza familia yetu.
Sehemu ya 1 na 2
https://maishakitaaonlinetz.blogspot.com/2024/10/simulizipaka-wa-familia-sehemu-ya-pili.html
SIMULIZI|Jinsi paka alivyomaliza familia yetu.
Sehemu ya 1 na 2
https://maishakitaaonlinetz.blogspot.com/2024/10/simulizipaka-wa-familia-sehemu-ya-pili.html
Simuliz nzuri sanaaa
Umetisha
Daaah nilitaman iendelee ila pongezi Kwa mwandishi kazi umeifanya vyema