Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi Na Mbili (12)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi Na Mbili (12)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 25, 2024Updated:October 28, 202420 Comments7 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?ย  Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishiย  wapi?” Nilimuuliza Mossesย 

    “Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pamboย  la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi niย  Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, suraย  yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishanaย  naye nilimkubaliaย 

    “Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.ย  Endeleaย 

    SEHEMU YA KUMI NA MBILI

    Nilimuamini sana Mosses, nilijuwa nitaipata hiyo pesa ilaย  sasa huo muda ambao alisema atanipa nilifikria tutaendaย  kuishi wapi Mimi na Mama yangu? Nilipoongea na Mamaย  sikumwambia kuhusu zile pesa istoshe alikuwa hajui kama kunaย  pesa hiyo. Aliniuliza tu nina akiba gani, kiukweli sikuwaย  hata na hamsini mbovu, maana nilijuwa na tumaini kubwa kwenyeย  zile milioni 60 zilizo kwa Mosses, niliona aibu hata kumjibuย  Mama kuwa sina pesa, nilikaa kimya japo Mama alinielewaย 

    “Mimi nina Milioni moja Jacklin, tufanye mpango wa kutafutaย  chumba kimoja” Alisema Mama huku akitabasamu kwa maumivuย  makali, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kukielezea.ย 

    “Itabidi tutafute mahali pa kuishi Jacklin, imeshatokea niย  lazima tukubaliane na hali halisi” Alisema Mama, nilitamaniย  sana kumwambia tukaishi nilipompangishia nyumba Mosses lakiniย  nilihofia kwa jinsi wawili hao walivyokuwa hawaivi chunguย  kimojaย 

    “Sawa Mama haina shida” Huzuni ilitanda kwenye nyumba yetu.ย 

    Siku iliyofuata Mzee Dhabi alituma Watu, tuliwapa funguo zaย  magari yote kuanzia na lile jipya na mengine ambayo hataย  nilikuwa sijui kuendesha, yaliondoka yote. Nilianza harakatiย  za kutafuta chumba cha kupanga ili niishi na Mama yangu,ย  bahati nzuri nilipata japo uswazi huko ila ndiyo Maishaย  ambayo tulishayaishi hivyo haikuwa shida sana kurudiย  Uswahilini huko.ย 

    Baada ya muda ambao Mzee Dhabi aliusema, alirudi kwa ajili yaย  kuchukua funguo za nyumba, Mama alijitahidi tena kuongea nayeย  ila Mzee huyo hakusikiliza kabisa. Tulihama kwenye jumba laย  kifahari ambalo Osman alitununulia, msichana wa kaziย  aliondoka kwao, hatukujuwa maamuzi hayo yalitoka kwa mwenyeweย  Osman au Mzee Dhabi aliamuwa kutumia hasira zake tu.

    Tuliachaย kila kitu ndani ya Jumba hilo, nguo pekee ndizo tulizoondokaย  nazo. Hatukuwa na godoro, tulinunua baadhi ya vitu kidogo iliย  pesa itusaidie kwenye mahitaji ya hapa na pale, tumainiย  lilibakia kwa Mosses japo kila nilipo mpigia simuย  alinizungusha kuonana naye, nilipoenda anapoishi nilikutaย  pamefungwa, niliishi kwa tumaini tu kuwa Maisha yaleย  yasingekuwa ya muda mrefu.ย 

    Siku zilipita, tuliishi kwa matumaini, tulilala kwenye mkeka,ย  niliona jinsi Mama alivyokuwa akiteseka roho iliniuma sababuย  chanzo cha yote nilikuwa ni Mimi. Namba za Osmanย  hazikupatikana kabisa, hatukujuwa kama alikuwa mzima auย  alikuwa amekufa, mwisho tulifuta namba zake. Miezi ilisonga,ย  Mosses hakupatikana kwenye simu kabisa, hata alipokuwaย  anaishi alihama na sikujuwa ningempata vipi, moyo wanguย  ulijawa na maumivu makali sana, pesa zilianza kuisha,ย  tulishauriana Mimi na Mama tufanye nini kwa pesa iliyobakia,ย  kila nilipojaribu kwenda kuomba kazi nilikosa, Mama alishauriย  tuanze biashara ya Mboga mbogaย 

    Tulikuwa tunaamka asubuhi mapema tunaenda Bustanini,ย  tunanunua mbogamboga tunaenda kuuza, Waliotujuwaย  walitushangaa sana, waliosikia kilichotokea walitucheka naย  kutuona hatuna akili, ningefanya nini zaidi ya kukubaliย  masimango yao ili mkono uwende kinywani, Mimi na uzuri wanguย  na usomi wangu niliishia kutembeza mbogamboga Mitaani.ย 

    Siku moja nikiwa nauza Mbogamboga nilimuona Mtu aliyefananaย  sana na Mosses, nilitamani kumuona kwa ukaribu zaidi. Ndio!!ย  Alikuwa ni yeye, alikuwa ameongozana na Mwanamke mmoja.ย  Niliona kama vile nimeokota Almasi kwenye zizi la ng’ombeย  nilimkimbilia Mosses na kumkumbatia. Hakuonekana kunifurahiaย  kabisa, yule Mwanamke aliulizaย 

    “Wewe Dada vipi unakichaa au?” Nilijitoa mwilini mwa Mossesย 

    “Ndio! Mimi ni kichaa sababu Sijamuona huyu Mtu kwa mudaย  mrefu, Mosses haujui ni jinsi gani nimekutafuta” Nilisema,ย  beseni la mbogamboga lilikuwa limeanguka pembeni na mbogaย  zote zilikuwa chini kwa jinsi nilivyokuwa nimefurahiย 

    “Kutokumuona muda mrefu na kumkumbatia mbele ya Mke wake kunaย  husiana nini? Mosses huyu ni Nani?” Aliuliza yule Mwanamkeย 

    “Simjui Mimi” Nilishtukaย 

    “Mosses hunijui Mimi Jacklin? Au kwasababu nimebadilika?”ย  Kiukweli nilikuwa nimebadilika, sio Jacklin yule ambayeย  alikuwa akimfahamu, kutembea kwenye jua ilikuwa ndiyo Maishaย  yangu hadi ngozi yangu ilibadili rangi.

    “Sikujui kabisa, nimeshangaa sana unakuja kunikumbatia mbeleย  ya Mke wangu” Alisema Mosses, nilisogea nyuma, niliokotaย  mboga zangu na kuzirudisha kwenye beseni langu.ย 

    “Samahani nilikufananisha na Mosses wangu, mmefanana,ย  Samahani Dada” Nilisema kijasiri sana kisha niliondoka zangu.ย  Mbele ya macho yangu nilidondosha chozi, nilienda kukaa chiniย  ya Mti nililia mno tena kwa kusaga meno. Niliumia kwa mamboย  mawili kwanza kudharirika na pili kupoteza tumaini la kuipataย  ile Milioni 60 ambayo Mosses aliichukua kwenye akaunti yanguย  ya Benki.ย 

    Jua lilikuwa langu, mvua ilikuwa yangu, nilichotakiwa niย  kuhakikisha napata pesa itakayoendesha Maisha yetu Mimi naย  Mama yangu, nilijiuliza kitu kimoja kama nitaendelea kuliaย  nini kitabadilika kwenye Maisha yangu? Hakuna, basiย  nilinyanyuka na kuondoka zangu, nilirudi nyumbani maana mbogaย  nyingi nilikuwa nimeshaziuza iliyobakia niliipigia mahesabuย  nitakaporudi iwe ndiyo Mboga maana siku hiyo Mama hakwendaย  kuuza mboga alikuwa hajisikii vizuri.ย 

    Mdogo mdogo nilifika nyumbani, kulikuwa na mmama anaitwa Mamaย  Amina alikuwa ni Mpangaji mwenzetu. Alinisimamisha kabla hataย  sijaingia ndani alinipa taarifa kuwa Mama yangu alikuwaย  ameanguka chooni hivyo amekimbizwa Hospitalini, nilishtukaย  sanaย 

    “Hospitali gani?” Nilimuuliza beseni likiwa chiniย 

    “Wamempeleka Kwa Dokta Simon” alipomaliza kunielekezaย  nilitimua mbio kuelekea Hospitalini. Mama yangu alikuwa ndiyeย  Mtu pekee aliyebakia na Mimi, alikuwa ndiye tumaini langu,ย  taarifa ilinichanganya sana. Nilikuwa katika hali yaย  kuchanganikiwa sana, nilijikuta nikigongwa na Pikipiki nikiwaย  nakaribia Hospitalini.ย 

    Nilipoteza fahamu zangu kutokana na ile ajali mbaya yaย  Pikipiki, nilipokuja kurudisha fahamu ilikuwa ni sikuย  iliyofuata, nilijikuta nikiwa Hospitalini, nilihisi maumivuย  makali sana ya Mguu wa kulia, kulikuwa na wepesi sana naย  ubaridi hadi nilishangaa, nilipeleka mkono ili kuugusa mguuย  wangu!! Nilishtuka sana, nilikuwa nimeshakatwa Mguu, nililiaย  sana.ย 

    Dokta Simon alikuja kuniangalia maana mara nyingi alikuwaย  akipita kukagua Wagonjwa, ndipo aliponiona, alinijuwaย  kutokana na ile iliyotokeaga kati yangu na Osman, alishangaaย  sana, nilikuwa katika maumivu makali na majonzi, alinipa poleย  kisha aliniambia

    “Pole sana kwa kilichokupata na kilichomfika Mama yako” Mwiliย  ulisisimka ghafla sana, wazo la Mama kuwa alikuwa Hospitaliniย  lilinijiaย 

    “Mama yangu anaendeleaje Dokta?” Nilimuuliza huku Kidonda chaย  Mguu kikiwa na maumivu makali sanaย 

    “Mama yako alishafariki tokea jana”ย 

    “Nini?”ย 

    “Ndiyo Pole sana Jacklin, Mwili wa Mama yako umechukuliwa leoย  kwa ajili ya mazishi, umezikwa na Manispaa sababu hakunaย  ndugu aliyejitokeza!” Alisema Dokta Simon, moyo uliloa choziย  la Maumivu, Nilijihukumu sana kwa kilichomfika Mama yangu,ย  Nililia sana.ย 

    “Usilie Jacklin, Maisha ndivyo yalivyo. Kwasasa unaishiย  wapi?” Aliniuliza, nilijawa na kwikwi sana sikuweza kumjibuย  mwisho alisemaย 

    “Tutaongea utakapokuwa sawa Jacklin, pole kwa Msiba na poleย  kwa yaliyokufika” Alisema kisha aliondoka, niligumiaย 

    “Mamaaaaa! Umeniacha kilema Mwanao!! Mamaaa umeondokaย  umeniacha na Nani Mimi” Aaah! Chozi lilikuwa ndiyo rafikiย  yangu, nililia sana, sikuwa na uwezo wa kunyanyuka walaย  kutembea.ย 

    Baada ya wiki mbili kupita Dokta Simon alikuja tena kishaย  aliketi kando yangu, angalau nilikuwa nimetuliza maumivuย  yangu! Alinipa pole kabla ya kuanza kuzungumzia kilichokuwaย  kimemletaย 

    “Kwanza pole sana Jacklin, Dunia yako imekugeuka lakiniย  ndivyo ilivyo sababu siyo Watu wote wanakuwa na simulizi tamuย  za Maisha yao, yako chungu sana. Osman alikutafuta sana,ย  ilisadikika kuwa Mlikuwa mmeuza kila kitu na kuondoka”ย  Alisema Dokta Simon, stori yake ilikuwa ngeni masikioniย  mwanguย 

    “Tuliuza kila kitu?” Nilimuulizaย 

    “Ndiyo! Mzee Dhabi pia alihangaika kuwatafuta bila mafanikio,ย  mwisho alikata tamaa baada ya kupata taarifa kuwa mliuzaย  nyumba na kuondoka wewe na Mama yako!”ย 

    Haraka niligundua kuwa Mzee Dhabi alifanya yote pasipo Osmanย  kujuwaย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA TATU Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย 

    ย ย 

    Pumzi ya mwisho

    20 Comments

    1. Roda on October 25, 2024 7:17 pm

      ๐Ÿ˜ญdunia simama mimi nishuke ๐Ÿšฎ๐Ÿ˜”daah had nmelia aseeeeeee

      Reply
    2. Noush on October 25, 2024 7:34 pm

      Tamu hiyooooo๐Ÿ˜‚

      Reply
      • G shirima on October 25, 2024 8:04 pm

        ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ข

        Reply
    3. yahaya on October 25, 2024 7:50 pm

      akome kabisaa aliyataka mwenyewe

      Reply
    4. Hamis on October 25, 2024 7:53 pm

      Bamu balaha

      Reply
    5. Sir, Yowas on October 25, 2024 8:06 pm

      Hujafa hujaumbika

      Reply
    6. Charz jr๐Ÿ˜Ž on October 25, 2024 10:42 pm

      What goes around is what comes around!!๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ mejaribu kingeresa jamn kama nimekosea mnambiee

      Reply
      • Hamza Mwalyawa on October 25, 2024 11:07 pm

        Hujakosea upo sawa kabisa brother dunia ina zunguka. Ulipo anzia wakati fulani ndipo unapoishia.
        Mara hutokea sivyo. HEBU TUANGALIE KIJACHO………

        Reply
    7. Suhayla on October 25, 2024 11:27 pm

      Hatari Yan jacklin yanamkuta mazito mno

      Reply
      • Jason on October 26, 2024 11:28 pm

        Mmmh ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ’ฅ

        Reply
    8. Luse twaxie on October 26, 2024 6:31 am

      Mm nafurahi sana huyu dada yalomkutaa

      Reply
      • Fawziya Hassan on October 26, 2024 11:51 am

        Mmmh!! Usiombe yakukute kaka au dada sijui
        Tuulize sisi yalotukuta
        Jacklin hana tofauti sana na mm sema yeye mwanaume alompenda alimpa uhuru sana wa mali zake
        Wanaume wa siku hisi wanapenda sana misaada kutoka kwa wanawake wakifanikiwa wanasahau kila kitu.

        Reply
        • Dommy on October 27, 2024 10:42 am

          Ila kweli sister umenen huwa tunjisahaulisha sna baada ya kupat mali kutok kwen sas hili limekuw fundishoo

          Reply
    9. Sharo love malkx ๐Ÿ’– on October 26, 2024 3:55 pm

      Dah
      Ebu ngoja nimpigie mama angu๐Ÿ˜’๐Ÿ˜’๐Ÿ˜’

      Reply
    10. Magreth on October 26, 2024 8:06 pm

      Siwezi mlaumu sana Jackline, mana story yake inaendana kidg na yangu
      Mimi Tulipendna sana na mkaka flan ambaye huyo mkaka alikuwa na rafk ake na huyo rafk ake Tulikuwa Majirani nando Mwanaume wa kwanza kunitongoza, Wote tulisoma Pamoja Standard 3, bc nikadate na huyo mkaka Takriban miaka 12
      Lakn lafk ake akiwa bado hajakata tamaa ya kunipenda, nilikuwa nikiumwa kwa haraka sana anafika Hospital nilipo lazwa, Nikiumwa hata kichwa, haraka alifika nyumbn lakn bado sikumkubalia, nilizidi kudate na rafk ake na sio yeye

      2021 nikaumwa Ugonjwa wa MOYO nikalazwa Jakaya Kikwete Cardinal Institute (Muhimbili) Nikafanyiwa Operation da!! Yule Mpenzi wangu Akaniacha na wala hakuwahi kuja hospital wala Nyumban But yule anaye nipenda alikuja kila cku na cku zingne alivuta cku moja tu
      Ndg zangu wakasema wanichangie Damu naye pia akaungana na ndg zangu kunichangia Damu.
      Lakn bado sikumkubalia
      Mwaka jana Mwishoni Nikajikuta nayatafakar Mengi aliyo yafanya kwangu da! Niliumia sana why nimemtenda hivo kwa muda mrefu toka tukiwa watoto wa darasa la 3
      Basi nikajikuta naomba appointment bc tukakutana nikamwambia sorry kwa usumbufu wa miaka yote
      NAKUPENDA NAOMBA TUOWANE TUWE MKE NA MME
      Da!! Akasema Wewe ni msichana pekee niliye kupenda katika hii dunia na niliishi kwa kujipa moyo kuwa wewe ni mke wangu lakn Moyo wangu ukachoka sana baada ya wewe kutoka hospital bado ukawa unampenda mtu aliye kufanyia ukatili hivo ni Mwezi sasa toka niingie kwenye mahusiano na binti niliye muona ananipenda kwa dhati
      Guys nililia sana na bado mpka leo naumia cz Kadi za mwaliko zimesha anza kugawiwa ANAFUNGA HARUSI DECEMBER

      Reply
    11. Sir yowas on October 26, 2024 8:37 pm

      Pole kwa yaliyokupata, haya maisha ni fumbo, laiti tungejua yajayo huenda maisha yetu yangekuwa na raha, yule unaempenda hakupendi,. Usiye mpenda ndie anakupenda, kwa kweli maisha ni kitendawili, Mungu pekee ndie ajuaye mwisho wetu, SS niwakupokea tu

      Reply
      • Junior Mtata on October 26, 2024 10:00 pm

        Admin mbona kuna siku una piga desh

        Reply
    12. Junior Mtata on October 26, 2024 10:01 pm

      Leo nimenunua bando kwa niaba ya Jacklin jamani ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

      Reply
    13. ๐Ÿ—’ + 1.53497 BTC.NEXT - https://yandex.com/poll/enter/DFvfEbpST9kmQ1fXfavNuK?hs=5990a20f09037efba606b437c1f69028& ๐Ÿ—’ on June 19, 2025 11:19 am

      4tbttj

      Reply
    14. ๐Ÿ’Œ ๐Ÿ” Verification Pending: 0.6 BTC transaction blocked. Unlock here > https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=5990a20f09037efba606b437c1f69028& ๐Ÿ’Œ on October 11, 2025 3:22 pm

      pzb5b4

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi October 1, 2025

    In the name of LOVE – 12

    Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE Moyo Wangu na…

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.