Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi (10)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi (10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 23, 2024Updated:October 28, 202414 Comments6 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Machoย  angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaย  Dokta Simon

    “Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twendeย  Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,ย  waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simonย 

    Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,ย  aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.ย  Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaย  Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmkeย  ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.ย  Endelea

    SEHEMU YA KUMI

    “Zahra?” Aliita Osman akiwa anaendelea kumuangalia Zahraย  ambaye alikuwa akitembea taratibu kuelekea kilipo kitandaย  alicholala Osman, alitikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa niย  Yeyeย 

    “Baba! Huyu ni Zahra?” Osman alimuuliza Baba yakeย 

    “Ndiyo Osman huyu ni Zahra” Alijibu Mzee Dhabi, Choziย  lilimbubujika Osman, Dokta Simon alikuwa akiangaliaย  kilichokuwa kinaendelea kwa kutumia mlangoย 

    Zahra alisogea na kumkumbatia Osman akiwa analia, Osmanย  aliweka mikono yake kwenye mgongo wa Zahra. Muda huo Mimi naย  Mama tulikuwa tumeingia wodini, tulikuta hali hiyo. Ilitubidiย  Mimi na Mama kusizi kwa dakika ili kuangalia kilichokuwaย  kikiendelea, walipoachana Zahra aligeuka nyuma alimtazamaย  Mzee Dhabi aliyekuwa akipepesa macho yake baada ya kunionaย  Mimiย 

    Macho yangu yaligongana na Macho ya Zahra, nilimtambuwa kuwaย  ndiye Mwanamke aliyekuwa akiuendesha moyo wa Osman lakiniย  nilijiuliza aliweza vipi kurudi tena katika Maisha ya Osman,ย  roho iliniuma sababu alirudi wakati ambao nilikubaliย  kumsaidia Osmanย 

    Osman alinitazama, ukimya ulitawala huku kila Mtu akiwaย  kwenye taharuki ya kilichokuwa kinaendelea pale.ย 

    “Baba! Nimerudi” Alisema Zahra akiwa analia, jinsiย  nilivyomtazama niligundua alikuwa na jambo zito lililomfikaย  ambalo lilimrudisha kwa Osmanย 

    Nilihema sana nikihisi maumivu makali sana kifuani,ย  niliondoka nikaenda nje ambako nilijikuta nikiwa nimekaa pekeย  yangu usiku ule.ย 

    Mama hakuwa na neno la kuzungumza ilimbidi aangalie tuย  kilichokuwa kinaendelea paleย 

    “Zahra” Osman aliita, mara moja Zahra alimgeukia Osman

    “Ulikuwa wapi siku zote, nimekutafuta kila kona ya Dunia hiiย  bila mafanikio yoyote” Alisema Osman, Zahra alidondosha choziย  akasemaย 

    “Nisamehe Osman, najuta kwa Ujinga wangu, najuta sana.ย  Nimerudi kukufuta chozi lako” Alisema Zahra kisha alipigaย  magoti akiwa analia, hata Mama alidondosha chozi lakeย 

    “Niambie nifanye nini Osman ili uamini kuwa nimerudi kwaย  ajili yako, nimekukosea sana” Alisema Zahra akiwa anaendeleaย  kulia, Bilionea Dhabi alimsogelea Zahra na kumyanyua kishaย  alimfuta chozi kwa kutumia mkono wake, akamwambiaย 

    “Osman anaumwa sana, hakuna tumaini la yeye kupona isipokuwaย  kupata Figo na kumuondolea mfadhahiko” Alisema Mzee Dhabi kwaย  sauti yenye kunong’oneza masikio ya Zahra, hii ilimshtua sanaย  Zahra alimfuata Osman alipolala kisha akamwambiaย 

    “Utapona Osman” Zahra alimshika mkono Bilionea Dhabi wakatokaย  ndani, walinipita mahali nilipokuwa nimekaa, walielekeaย  ofisini kwa Dokta Simonย 

    “Baba kama kutoa kiungo changu kutamfanya Osman awe salamaย  nipo tayari hata sasa hivi, pimeni figo zangu zikifaa mnitoe”ย  Alisema Zahra mbele ya Dokta Simon na Bilionea Dhabi ambaoย  walijawa na mshangao, chozi lilimtoka Bilionea Dhabiย 

    “Zahra!” Aliita Bilionea Dhabi kwa sauti ya Chini sana, Zahraย  alitikisa kichwa ishara kuwa alichokisema ndicho alichoย  kimaanisha.ย 

    Mzee Dhabi alimkumbatia Zahra kwa Uchungu sana, alikuwaย  ameshakata tumaini, Ujio wa Zahra ulimfanya Osman arudiย  katika hali ya kawaida hata ile hali ya kunitaja ilikata.ย  Mama alimuuliza Osman kule Wodiniย 

    “Huyu Mwanamke ni nani?”ย 

    “Ni Mwanamke niliyampenda sana lakini alinikimbia na kwendaย  Ughaibuni” Alijibu Osmanย 

    “Osman Mwanangu, Jacklin amekuja kwa ajili yako, yupo tayariย  kufunga ndoa na wewe” Mama alisema kwa uchungu sana, Osmanย  alitikisa kichwa chake ishara ya kukataa huku akisemaย 

    “Jacklin hanipendi Mama, hawezi kukubali nimuowe”ย 

    “Tafadhali sana Osman, Jacklin anakupenda na yupo tayari”ย  Alisema tena Mama wakati huo Mimi nilikuwa ninachunguliaย mlangoni, niliumia sana. Sikuona umuhimu wa kubakia paleย  Hospitali niliondoka zangu. Mama alijitahidi sanaย  kumbembeleza Osman lakini haikusaidia, kilichomtesa Sana Mamaย  yangu ni ule wema ambao Osman alitutendea na jinsi ambavyoย  Mimi niliulipa wema huo kwa ubaya sana, Mama alilia sana hadiย  Mzee Dhabi aliporudi akiwa ameambatana na Dokta Simon naย  Zahra, Mzee Dhabi alimwambia Mama yanguย 

    “Nashukuru kwa msaada na Mchango wako Mama Jacklin lakiniย  kwasasa wewe nenda”ย 

    “Lakini Mzee Dhabi…” Mama alikatishwa na Mzee Dhabi kishaย  alipewa ishara ya kuondoka, chozi lilikuwa linamvuja Masikiniย  Mama yangu, aliondoka zake.ย 

    Mama alilia njia nzima hadi anafika nyumbani nguvu zilikuwaย  zimemuishia, bahati nzuri nilikuwa sebleni. Nilipomuonaย  Nilimkimbilia na kumdaka asianguke, mwili wake ulikuwa waย  moto sana, jasho lilikuwa likimtoka, sikupata kumuona Mamaย  akiwa katika hali hii hata siku moja, nilimlaza kwenye Kochiย  nikawasha Feni ili apate ubaridi kisha niliketi pembeni,ย  ukimya ukatawala huku nafsi yangu ikiwa imejaa majuto makubwaย  sana, niliamini hali ya Mama ilitokana na makosa yangu.ย 

    “Jacklin” Mama aliita kwa Maumivu makali kisha alisemaย 

    “Tumechelewa lakini Mama yako nakupenda sana, Dunia nzimaย  inaweza ikakuona mbaya lakini Mama yako nitahangaikaย  kukusafisha. Osman amekataa kufunga ndoa na wewe” Alisemaย  Mama huku chozi likimbubujika, kusema ule ukweli niliumia mnoย  ndani ya nafsi yangu.ย 

    Moyo wangu nilishaufungua kwa Osman lakini niliufungua nikiwaย  nimechelewa, nilijuwa Zahra ndiye aliyeharibu kila kitu,ย  nilimyanyuka na kuondoka nyumbani kwa hasira na maumivuย  makali, sikutaka kujuwa kuhusu Hali ya Mama tena, kichwaย  changu ni kama kilijaa moshi mkali sana.ย 

    Nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa 6 Usiku, nilimpigia simuย  Mosses, zaidi ya mara sita mara ya saba ndio alipokea simuย  yangu ikionesha kuwa alikuwa amelala. Aliniuliza nataka nini?ย  Nilimwambia nahitaji kuonana naye, aliniambia niende kwake,ย  nilianza safari ya kuelekea huko Usiku huo.ย 

    Nilipofika kwa Mosses kuna hali nilianza kuihisi ndani yaย  nafsi yangu, niliona kabisa mapenzi kwa Mwanaume huyoย  yalianza kuondoka ndani yangu, niliigiza tu na kumwambia kuwaย  nammiss sana ila ukweli ni kwamba akili yangu ilikuwa kwaย  Osman, kila nilipomfikiria Osman nilijikuta nikiumia tenaย kibaya zaidi nilipofikiria kuwa Zahra amechukua nafasi yanguย  ndani ya moyo wa Osman ndiyo nilizidi kupagawa, hali hiiย  Mosses aliiona kwangu kwasababu mara nyingi nilikuwa nikitokaย  kifikra akaniulizaย 

    “Unawaza nini? Haupo kabisa” Aliuliza Mosses, huwezi aminiย  tulikuwa katikati ya tendo lakini akili yangu hata haikuwaย  hapo, Mosses alishuka kisha alielekea Bafuni aliporudiย  alihitaji majibu kutoka kwangu.ย 

    “Sijui Mosses! Najikuta tuu” Nilimjibu nikiwa ninavuta Shuka,ย  kweli mapenzi yanaumiza sana Aisee kumbe Osman aliumia hivi?ย  Sikuwahi kuumia kama ambavyo nilikuwa naumiaย 

    “Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwaย  na tabia ya wivu sanaย 

    “Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanjaย  kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwaย  ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bilaย  kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianzaย  kujichukia Mwenyewe.ย 

    Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, namiย  nilitoa tabasamuย 

    “Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadiย  kulipopambazuka.ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MOJA Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย 

    ย ย 

    Pumzi ya mwisho

    14 Comments

    1. catherine Arod on October 23, 2024 3:07 pm

      Dah fupi sana admin tuma mbili Leo Jana hukutuma hii pumz ya mwisho ni ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    2. Nelca on October 23, 2024 4:14 pm

      Waoooow ๐Ÿฅฐ๐Ÿ’ฏ

      Reply
    3. Happyness on October 23, 2024 4:47 pm

      Admin nyingn jmn ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    4. yulia kimario on October 23, 2024 4:48 pm

      Admini hii ni ya jana bado ya leo

      Reply
    5. Calvin paul on October 23, 2024 5:20 pm

      Atleast sasa nimeanza kufurahi zahra kuwepoo

      Reply
    6. Chamalo on October 23, 2024 5:40 pm

      Jana hujatumia na leo ndio imeishia hapa

      Reply
      • Roda on October 24, 2024 3:56 pm

        Admin umerudia mbn ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญila ๐Ÿคฃjack kaulambaaaaaaa akome ingekua mm toka kitamb san nihsaolewana huyoooo osman๐Ÿคฃhata hila kusem yy ungekuta nishamtongoza zangu๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿ™Œ

        Reply
    7. Guyton on October 23, 2024 6:07 pm

      Hiyo ndo dawa ya wanawake kama kina jacklin….๐Ÿ˜

      Reply
      • Lus twaxie on October 23, 2024 9:20 pm

        Akomee huyu dada ..pumbaf

        Reply
    8. Hamis on October 23, 2024 7:01 pm

      Adimin unasikia oja za ndugu zako tuma nyengne

      Reply
    9. Meows on October 23, 2024 10:24 pm

      Kusema ukwel j kayatimba hapo
      ๐ŸŒ๐ŸŒ Lakini atajua mwenyew cz aliyataka

      Reply
      • esthersafary on October 24, 2024 3:32 pm

        Leo n 11 jamn

        Reply
    10. yahaya on October 24, 2024 4:18 pm

      admn vp ten tuma ya 11 Leo bwan

      Reply
    11. Juju on October 24, 2024 5:42 pm

      Admin umezinguwa see ya 11 pumzi ya mwisho hujatuma ,

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneย  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.