Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pigo Takatifu Sehemu Ya Tisa (09)
    Hadithi

    Pigo Takatifu Sehemu Ya Tisa (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 20, 2024Updated:September 22, 202418 Comments10 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Pigo Takatifu
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Mama umemyoosha sana”ย 

    “Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kileย  sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufungukaย  kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo Msichanaย  Mshikilie hadi mwisho.”ย 

    “Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno”ย 

    “Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena”ย 

    “Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatuย  kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,ย  akaingia Mwanaume mmoja.. Endeleaย 

     

    SEHEMU YA TISA

    “Nimebwana, naomba kujisaidia” Akasema Matilda huku akianzaย  kujikojolea, Mlinzi akamwambia Matildaย 

    “Nenda haraka” Akasema na kumsindikiza hadi chooni, chooย  hicho kilikua cha ndani.ย 

    Alipoingia huko alikua tayari ameshasoma ni namna ganiย  anaweza akaondoka hapo, akapanda juu ya sinki kisha akapitaย  katika kitundu kidogo ambacho kilikua juu kilichotumika kamaย  Dirisha la Choo, akadondokea chini, yule Mlinzi akaendeleaย  kusubiria hapo huku mwenzake akiwa anamwita. Matilda akapataย maumivu kadhaa, jua lilikua linaanza kuzama, akatazama mbeleย  yake akaona ukuta ambao haukua mrefu sana, akafikiria kutumiaย  ukuta ili atimke hapo, akaparamia ukuta.ย 

    Mlinzi akaona dakika zinasogea akagonga mlango, akajibiwa naย  ukimya huku akianza kupata mashaka juu ya uwepo wa Matilda,ย  ikabidi afungue mlango, hakumkuta Matilda, akatazama paleย  kwenye kitundu akaona dalili za Mtu kupitia hapo, akapandaย  kwenye sinki akamwona Matilda akiwa anamalizia kuteremkaย  ukuta, akagongana naye macho. Matilda akajiachia, Yule Mlinziย  akatoka chooni akampa taarifa yule Mlinzi mwingine kishaย  wakaelekea nje kwa ajili ya kuhakikisha wanamkamata Matildaย  jioni hiyo.ย 

    Matilda akajikuta yupo Msituni, akaanza kukata nyikaย  kuwakimbia walinzi hao ili asalimishe maisha yake, Walinziย  wakiwa na mbwa wakawa wanamfukuzia Matilda ambaye alionekanaย  kua na spidi kubwa sana, alikua kilomita kadhaa kutoka walipoย  walinzi. Akaendelea kukata nyika huku giza likiwa linaingia,ย  akawa amechoka sana, alikua hajui ni mahali gani alipo, hivyoย  alikua akikimbia kama mwendawazimu tu.

    “Mama nilitereza naomba unisamehe kwa hili, nilikosea kabisa,ย  nipo tayari kulipa kwa hili, nakiri Mimi ni Mtoto mpumbavuย  sana” Alisema James akiwa mbele ya Mama yake ambaye alikuaย  amekunja uso wake, watu kadhaa walikua wameshafika hapo kwaย  ajili ya Msiba wa Patra. Chozi na makamasi yalikua yakimtoka,ย  Mama Naomi akamwonea huruma sana, akamtazama Mama Jamesย  lakini hakua na nguvu ya kusema chochoteย 

    “Mamaaaaa!” akaita James huku akizidi kudondosha chozi, Mamaย  yake alikua kimya sana akiwa anatazama pembeni, kwa hasiraย  aliyokua nayo hakutaka kabisa kumtazama Jamesย 

    “Mama James, rudisha moyo wako nyuma, huyu ni Mtoto,ย  ameteleza” Akasema Mchungaji George ambaye alikua bega kwaย  bega na familiaย 

    “Tunazungumzia Maisha ambayo hayawezi kurudi, yule Binti,ย  hawezi kurudi kwa namna yoyote ile, na Mama yake piaย  asirudi?” akauliza Mama yake James huku akiwa amekaza machoย  yake kwa Mchungaji George, Mchungaji akameza funda la mate,ย  swali aliloulizwa lilimfanya akae kimya.ย 

    Chozi na jasho vilikua vikivuja kwa pamoja, James alijitahidiย  sana kumwomba Mama yake amsamehe lakini Mama Jamesย  akashikilia msimamo kua hawezi kumsamehe hadi Matildaย  aonekane. James akaondoka hapo Usiku

    Hekaheka ndani ya Msitu ilikua ikiendelea, Matilda aliendeleaย  kuwakimbia wale walinzi wa Neema, alichoka akaamua kujibanzaย  nyuma ya Jiwe kubwa, walinzi nao walikua wameshachoka hukuย  wakihimizana kua kabla ya jua kuchomoza wahakikishe kuaย  wamempata Matilda.ย 

    Matilda akalala hapo Msituni hadi siku iliyofuata, alipoamkaย  akaendelea na safari ya kutafuta msaada wa kutoka hapoย  Msituni, akakatiza vijito na majabari makubwa na madogo hukuย  akiwa hajui ni wapi anaelekea.ย 

    Moyoni mwake akawa anasema na Mungu wake kua amlinde Bintiย  yake, Masikini hakujua kua Binti yake alikua ameshafariki,ย  ghafla akasikia sauti za Mbwa akajua anapaswa kuongeza mwendoย  wa kuendelea kuutafuta Msaada, akakimbia umbali mrefu akiwaย  na njaa na kiu ya Maji akajikuta akianguka baada ya kuhisiย  kizunguzungu.ย 

    “Eee Mungu nilinde” Akasema Matilda, akahisi giza kishaย  akapoteza fahamu.ย 

    “Babu kinachofuata ni kitu gani?” Akauliza Neema, Babu naย  Mama yake wakiwa mbele yakeย 

    “Mtoto akizikwa habari yake itakua imeisha pia, James anaendaย  kua mali yako bila kipingamizi chochote kile, hili ndiyoย  jambo kubwa” Akasema Babu yake Neema, wakafurahi sanaย 

    “Yaani Babu kama tutafanikisha hili nakuahidi kua nitakupaย  zawadi ambayo hutonisahau” Akasema Neemaย 

    “Huna haja ya kuahidi sababu wewe ni Mjukuu wangu Neema,ย  kikubwa upate unachohitaji, ukipata wewe Mama yako amepata,ย  basi ndiyo furaha yangu hiyo”ย 

    “Pamoja na hayo Babu nitahakikisha nakujengea nyumba yaย  kifahari, nitakua na pesa nyingi” Alisema Neema. Mama Neemaย  alikua Mtu wa kutabasamu tu akimwangalia Mwanaye na Babu yakeย  wakiwa wanazungumza, kicheko chao kilikua kilio upande waย  Mama James ambaye kila alipofikiria jinsi mambo yalivyoendaย  alijikuta akiangusha kilio cha Mtu mzima.ย 

    Moyoni alijua kua kuendelea kuzuia Mtoto kuzikwa ni sawa naย  kumtesa Mtoto huyo lakini moyoni pia alikua akiumia Mtotoย  kuzikwa bila Mama yake kuwepo, aliona ni sawa na kuzuia hakiย  ya Msingi ya Mama Patra, lakini hakuna aliyejua kilichokuaย  kikiendelea, Matilda alikua akipigana vita Msituni.

    “Nipo wapi?” Akauliza Matilda baada ya kujikuta akiwa kwenyeย  nyumba moja ambayo ilikua imeezekwa makuti, hakuna aliyeย  mbele yake bali kitanda na ukuta uliojengwa kwa udongo waย  kugandika. Akakohoa kidogo, haraka akaingia Mzee Mmoja ambayeย  alikua na ndevu ndefu, chafu zenye Mg’ao wa fedha, alikua naย  rasta pia, Matilda akaogopa sana, wakati anajisogeza pembeniย  akajikuta shuka ikiwa inamvuka, ndipo akagundua kua alikuaย  hana nguo yoyote ile, akarudisha macho kwa mzee kwa Mshangaoย 

    Mara, akaingia Bibi mmoja ambaye alionekana wazi kua ni Mkeย  wa Mzee huyo.ย 

    “Usiogope Binti, Nilikukuta ukiwa hujitambui nikakusaidia”ย  Akasema Mzee huyo, Bibi akaketi pembeniย 

    “Na wale watu waliokua wakinifukuzia?” Kwanza Bibi akacheka “Walishambuliwa na jeshi langu” Akasema Mzee huyo “Jeshi lako, unamaanisha nini?”ย 

    “Siafu waliwashambulia walipotaka kukuchukua, wakakimbiaย  ndipo nikakusaidia” Hadithi hiyo ikamshtua sana Matilda.ย 

    “Umepoteza fahamu kwa zaidi ya masaa matano, unahitajikaย  kupumzika zaidi ili kuvuta nguvu, lakini kwanini wale Watuย  walikua wakikufukuzia?” Akauliza Bibiย 

    “Ni stori ndefu sana” Akasema Matilda baada ya kuona watu haoย  si wabaya kwake, akawasimulia kilichotokeaย 

    “Pole lakini unaonekana bado una tumaini kwa hayo unayopitia,ย  bado una Muda wa kurekebisha mengi” Akasema Babu huyo,ย  Matilda akaketi vizuriย 

    “Unamaanisha nini Babu”ย 

    “Ulipokua umelala nilifanikiwa kuyaona yanayokuzunguka,ย  usishtuke sababu ipo Dunia isiyoonekana, ni Dunia ambayoย  mambo huenda haraka mno, huyo Mtoto unayemzungumzia hapa yupoย  kwenye usingizi mzito sana, hawezi kuamka kirahisi sababuย  nguvu kubwa imetumika kumlaza” Akasema Babu huyo, Matildaย  akashtuka sana

    “Usingizi?, kwanza niko wapi hapa nataka kwenda kumwona Bintiย  yangu”ย 

    “Hapa ni Mkata”ย 

    “Mkata?”ย 

    “Ndiyo, kilomita kadhaa kutoka hapa kuna barabara ambayoย  inaelekea huko ulikotoka”ย 

    “Umesema kuhusu Usingizi, sijakuelewa”ย 

    “Namaanisha Mtoto wako amekufa katika Dunia hii lakiniย  anaishi kuzimu” Matilda akazidi kushtuka, aliyokua akiambiwaย  yalimpa Mshtuko mkubwa sana, chozi likaanza kumtokaย 

    “Mtoto wangu amekufa?”ย 

    “Ndiyo lakini usilie sababu bado hajaondoka, mwili umekufaย  lakini nafsi inaishi kuzimu, kikubwa unatakiwa kuwahi kablaย  hajazikwa”ย 

    Wazee hao wakamwambia mengi sana Matilda, wakampa chupa yaย  Maji, wakamwambia kua akifika anyunyize maji kwenye mwili waย  Binti yake, ataamka na kua sawa kabisa.ย 

    Haikuishia hapo, wakampa nauli ya kurejea Dar.

    “Mchungaji, naona namtesa Mjukuu wangu, hakuwa na kosa loloteย  sitaki aendelee kuteseka zaidi. Kesho Patra azikwe” Akasemaย  Mama yake James, alizungumza mbele ya Jamesย 

    “Asante Mama, najiona nimepoteza thamani kubwa sana katikaย  Maisha yangu. Nitamtafuta Matilda kadiri ya uwezo wangu Mama”ย  Akasema James, Siku iliyofuataย 

    Taratibu za Mazishi zikafanyika, mwili wa Patra ukawekwaย  kwenda sanduku, vilio vilitawala, familia ilizizima, Jamesย  alilia sana mbele ya sanduku la Patra, alijutia sanaย  kumkataa, akatamani hata aamke ili amuombe msamaha Bintiย  yake, kila aliyefika aliona ni jinsi gani James alikua katikaย  hali mbaya sanaย 

    Mchungaji George akaongoza maombi ya ibada ya mazishi yaย  Patra, hatimaye sanduka la Patra likawa linashuka taratibuย  kuelekea chini, ikasikika sauti ikisema

    “Patraaaaaaaa” Ilikua ni sauti iliyotambulika kwenye masikioย  ya walio wengi, vilio vilikoma, hakuna aliyeamini, walimwonaย  Matilda akiwa ameshikilia chupa aliyopewa kule Msituniย 

    “Msimzike Binti yangu bila kumwona” Alisema Matilda,ย  Mchungaji akawaamuru waliokua wakishusha sanduku kulirudishaย  juu, Matilda akakimbia hadi kwenye sanduku la Patra, kishaย  akageuka na kuwaambiaย 

    “Patra hajafa msimzike” Alisema akiwa anatokwa na mchoziย 

    Ni kama watu walipigwa Bumbuwazi, hakuna aliyesema chochoteย  zaidi ya Mchungaji George ambaye alimuuliza Matildaย 

    “Unasema nini Matilda, Mtoto amekaa kwenye jokofu kwa sikuย  tatu. Ulikua wapi?” Akaulizaย 

    “Mchungaji, moyo wangu unaniambia nimwone kwanza Mtoto ndipoย  nieleze kilichotokea, chozi la James lilijikuta likikaukaย  lenyewe kutokana na Mshangao ambao alikua nao, minong’onoย  ikaanza kusambaa miongoni mwa waliofika Kwenye mazishi.ย 

    Mchungaji akawaambia walifungue sanduku ili Matilda amwoneย  Mtoto wake, sanduku likafunguliwa, Matilda akafungua chupa yaย  Maji akanyunyiza kwenye sandukuย 

    “Unafanya nini?” Akauliza Mchungaji Georgeย 

    “Patra ataamka sasa hivi” Alisema Matilda, Mchungaji akaonaย  Matilda amechanganikiwa, akawaamuru wannaume kumshika Matildaย  ili Sanduku lifungweย 

    “Mchungaji mwanangu ni mzima naomba Msimzike” alisemaย  Matilda, ukimya ukatawala kwenye sanduku, alichotegemeaย  Matilda kilikua ni sawa na njozi ya mchana, Patra hakuamkaย  kama alivyofikiria, akaanza kuona wale wazee walikuaย  wamemuongopea, alilia sana huku utaratibu wa kulifungaย  Sanduku ukifanyika, Mama Naomi akamwambia Matildaย 

    “Mtoto amekufa Matilda hawezi kurudi” Mchungaji akamsogeleaย  Matilda akamwambiaย 

    “Huu ni mwisho wa Patra lakini siyo mwisho wa Maisha yako,ย  pole kwa msiba”ย 

    Katika hali ambayo kila mmoja alistaajabu, Patra akaamkaย  kwenye sanduku na kukaa kitako kitu ambacho si tuย kilimfurahisha Matilda bali kilimshtua, tokea amezaliwaย  hakuwahi hata kukaa lakini aliamka na kuketi kiisha akaanzaย  kushangaa watu. Wasio na moyo wa ujasiri walikimbizanaย  Makuburini, wachache wakabakia.ย 

    Muda huo Babu yake Neema alikua amepata ishara mbayaย  akamwambia Neemaย 

    “Nenda Muhimbili kaokote kile kitu kakitupe jalalani harakaย  sana”ย 

    “Babu kwanini unasema hivyo?” Akauliza Neemaย 

    “Nenda Neema fanya haraka sana” Akasistiza Babu yake Neema,ย  haraka Neema akakodi Pikipiki ili awahi Muhimbili,ย  haikuchukua muda mrefu, akawa amefika Muhimbili, akakimbiliaย  mahali ambapo alitupa kile kitu, kabla hata hajakiokotaย  kikawaka na kumwingia machoni, akawa anapiga keleleย  akilalamika kua haoni, haraka akasadiwa kupelekwa Kwaย  Daktari.ย 

    Familia ikawa imekaa, kila mmoja akistaajabu maajabu ya Mtuย  aliyekufa kurejea tena kwenye Maisha, ukimya ukawa mwingiย  sana. Matilda akaanza kuwasimulia kila kitu, siku hiyo ndiyoย  ikawa siku ya kumwona Mama yake James, huwezi amini Patraย  alikua ni Mtoto mrembo sana, akitabasamu ni James Mtupu,ย  James akaomba Msamaha na kuahidi kua atafunga ndoa na Matildaย  na kumlea Mtoto.ย 

    Zikapita siku tatu mambo yakawa shwari, furaha na amaniย  ikazidi kutamaraki, kwa shukurani, James akampatia Mama Naomiย  ile nyumba aliyokua akiishi Matilda, akampa pesa pia kwaย  ajili ya kuanza Biashara. Siku moja akiwa ofisini akapokeaย  simu ya Mama Neema, alivyopokea akaambiwa kua Neema amepofukaย  macho, James akamwambia kua ataenda kumwona.ย 

    Baada ya kazi akaenda Hospitalini kumwona Neema, Mama Neemaย  akiwa analia sana kwa kile kilichomfika Binti yake.ย 

    “Mama huna haja ya kulia, Mimi nimelia sana, Matilda ameliaย  sana, Mama yangu amelia sana. Siku zote Mshahara wa dhambi niย  umauti Mama”ย 

    “Lakini James, Neema ana Mtoto wako tumboni, hupaswiย  kumhukumu moja kwa moja”

    “Namshukuru Mungu sababu amefumbua fumbo zito sana, sikuwahiย  kuwa na thamani kwenu hata kwa yale makubwa niliyowafanyia,ย  nilikua mjinga sijui hata nilikwama wapi hadi nikamkataaย  Mtoto wangu wa damu” Akasema James kisha akataka kuondokaย 

    “James, naomba msaada kama Mama, Neema anatakiwa kwendaย  kutibiwa India, sina pesa hiyo Mwanangu, msaidie kwa hilo tu”ย 

    “Siwezi kumsadia adui anayewinda Maisha yangu, alie mbele yaย  Mungu wake, amwombe amsamehe” Akasema James kisha akaondoka,ย  Mama Neema akalia sana huku akijilaumu kwa kusema ni ujingaย  wake kwani yeye ndiye aliyekua akimshauri vibaya Binti yake,ย  akaona ni bora kufa kuliko kuendelea kumwona Neema akiwaย  kipofu, akaondoka Hospitalini na kumwacha Neema akitesekaย  kwenye kutanda cha Hospitalini ya Muhimbili.ย 

    MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

    ย 

    Pigo Takatifu Pigo Takatifu Kijiweni Riwaya ya Pigo Takatifu

    18 Comments

    1. Lus twaxie on September 20, 2024 4:14 pm

      Adminiiiiiiiii hongera sanaaa ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ๐Ÿฅณ dah mwisho mzuri ..kesho anza riwaya nyingine

      Reply
      • G shirima on September 20, 2024 7:50 pm

        Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi

        Reply
    2. Daniel on September 20, 2024 4:18 pm

      Kali sana

      Reply
      • Zainabu on September 20, 2024 4:51 pm

        Safi sana mwisho nzur riwaya ilikuwa ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

        Reply
    3. Najma muya on September 20, 2024 4:56 pm

      Daah riwaya nzuri Sana

      Reply
    4. Tyson on September 20, 2024 5:32 pm

      dah story moja nzuri sana

      Reply
    5. Pauline on September 20, 2024 5:40 pm

      Asante Mungu wamepata wanachostahili๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    6. Sir yowas on September 20, 2024 5:43 pm

      Mmmmmmm,, mbona imeisha kama inaendelea????????!!?????

      Reply
    7. Cesilia Nkunga on September 20, 2024 5:45 pm

      Big up Admin!
      Riwaya unazotupatia zinatupa fundisho katika maisha halisi yanayotuzunguka.

      Reply
    8. Dickson kikungwe on September 20, 2024 5:47 pm

      Hongera sana mkuu kwa story nzuri sana

      Reply
    9. Zakayo Mngulu on September 20, 2024 7:01 pm

      Dah hatari sanaaaaa

      Reply
    10. G shirima on September 20, 2024 7:52 pm

      Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi

      Reply
    11. Lucas George on September 20, 2024 8:34 pm

      ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ sio powa imeisha kama utani

      Reply
    12. Xavi on September 20, 2024 8:49 pm

      Hongera san kiongozi ๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š

      Reply
    13. Xavi on September 20, 2024 8:51 pm

      Tujitahid kumtunza admin asivunjike moyo wakutupa madini mazuri kma hya

      Reply
    14. Irene on September 20, 2024 9:27 pm

      ๐Ÿ˜๐Ÿ˜โค๏ธ

      Reply
    15. Muharram on September 20, 2024 10:00 pm

      Admini safi kesho anza nyengine

      Reply
    16. Juma on September 23, 2024 9:30 am

      Imeisha vibaya wazaz wake ma patra je

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.