Ilipoishia “James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni MtotoΒ wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”Β alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibuΒ walishtukaΒ
“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanyaΒ kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni MtotoΒ wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyoΒ vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”Β alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua naΒ hasira sana.Β
Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, MamaΒ Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakiniΒ ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James nayeΒ aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,Β aliondoa gari haraka sana.Β EndeleaΒ
SEHEMU YA TATU
Mama Naomi akamkimbilia Matilda kujua kwanini James alifikiaΒ uamuzi wa kumpiga, hakuna alichokizungumza Matilda sababuΒ bado alikua akilia kutokana na kilichotokea, MwanaumeΒ aliyesababisha akatoroka kwao, akawapa Mawazo wazazi wakeΒ aliishia kumpiga na siyo kujali hali ya Mtoto kisa tu ulemavuΒ
“Matilda usilie hebu nieleze kimetokea nini hadi akakupiga?”Β aliuliza Mama NaomiΒ
“Niache Mama Naomi, ilipofikia nimechoka na mateso ya hiiΒ Dunia ni bora hata nife tu” Alisema kwa hasira Sana MatildaΒ huku akilia kwa uchungu sana.
“Huo ni uamuzi wa kijinga sana Matilda, ukifa Patra atazidiΒ kuteseka, angalia jinsi anavyoteseka sasa hivi je ukifaΒ itakuwaje?”Β
“Sasa nitakaa nikimwangalia Binti yangu akifa mbele ya machoΒ yangu alafu Baba yake akiwa na uwezo wa kumsaidia lakiniΒ hafanyi hivyo, ni bora kufa kuliko kumwangalia Patra akifa”Β Alisema Matilda.Β
“Nakuomba Matilda kwasasa turudi nyumbani tutafakari jinsi yaΒ kuipata pesa ya Matibabu, hebu nyanyuka” Mama NaomiΒ alimnyanyua Matilda kisha aliondoka naye.Β
********Β
“Mimi nina wao wazo Matilda, kwanini usiende kanisani kwenuΒ ukaomba Msaada kwa waumini wakakusaidia?” alisema Mama Naomi,Β yalipita Masaa matatu baada ya kurejea nyumbaniΒ
“Wataweza nisaidia kweli?”Β
“Ndiyo nina imani kubwa watakusaidia sababu wewe ni MuuminiΒ mwenzao”Β
Ushauri wa Mama Naomi aliufanyia kazi, jioni ilipoingiaΒ alienda kanisani, wengi walimshangaa maana baada yaΒ kujifungua hakuonekana tena kanisani, aliofahamiana naoΒ walikua wakimuuliza jinsia ya Mtoto, Maswali ya kuhusu MtotoΒ yalizidi kumfanya Matilda ajisikie vibaya sana.Β
“Mbona unalia?” aliuliza Mchungaji mara baada ya MatildaΒ kufika ofisini kwa mchungaji wa kanisaΒ
“Mchungaji Mtoto wangu” Alisema Matilda, Mchungaji alishtukaΒ akamuulizaΒ
“Mtoto wako amefanyaje?”Β
“Mchungaji Mtoto wangu Mimi” Sauti ya kilio ya MatildaΒ ilisikikika na kumfanya Mchungaji aingiwe na maswali mengiΒ kichwaniΒ
“Matilda Mtoto wako amefanya nini, hebu punguza kuliaΒ uniambie” Alisema Mchungaji kwa sauti iliyojaa upole wa HaliΒ ya juu sana, kwikwi ilimshika sana Matilda kila alipotakaΒ kusema alijikuta akishindwa, kilio kilimuandama katika kilaΒ neno alilohitaji kuzungumza, Mtandio wake aliutumia kufutaΒ chozi lililomiminika kwa wingi, moyo wake ulijawa na simanziΒ ya hali ya juu sana.Β
“Matilda tambua unanichanganya sana Mimi, sielewi hata niniΒ unataka kuzungumza. Nakuomba acha kulia sababu ukilia MimiΒ siwezi kujua kilichokusibu” Alisema tena Mchungaji wakati huoΒ Matilda akiwa ameegemea Meza akiwa analia, hata MchungajiΒ alilengwa na Mchozi kwa jinsi ambavyo Matilda alikua akiliaΒ kwa uchungu, dakika tano zilikatika Matilda akishindwa kusemaΒ chochoteΒ
“Unasikia Matilda, kua na imani hakuna kinachomshinda MunguΒ aliye hai, nijuze Mimi ili tujue tunakusaidiaΒ Β
vipi….Unasikia….” Mchungaji alirudia kumbembelezaΒ Matilda, angalau kilio kilianza kupunguaΒ
“Na hapo shavuni umekumbwa na nini?” Aliuliza Mchungaji,Β shavuni Matilda alikua na alama ya kofi alilopigwa na JamesΒ kule Hospitalini.Β
“Mchungaji napitia wakati Mgumu sana katika Maisha yangu,Β Mtoto wangu yupo Hospitalini..” Matilda alijikaza akazungumzaΒ
“Ulipotea kanisani kila Mtu akawa anajiuliza upo wapiΒ Matilda, kumbe ulijifungua….Enhee nini kinamsumbua MtotoΒ wako?” Aliuliza Mchungaji ambaye alionekana kua na umriΒ mkubwa, ngozi nyeusi na mvi iliyokolea vizuri kichwani, akiwaΒ amevalia mavazi ya kanisa na msalaba mkononi.Β
“Mtoto wangu ni Mlemavu, anasumbuliwa na Mapafu, anahitajikaΒ kufanyiwa upasuaji na kibaya zaidi Baba yake Amemkana”Β Alisema Matilda, kilio kilianza upya baada ya kumalizaΒ kumuelewesha Mchungaji ambaye alishikwa na butwaa, MatildaΒ alikua Muumini wa kabisa hilo sababu hata kwao alikotokaΒ alikua Binti wa kanisa hivyo alivyofika Dar alijiunga naΒ kanisa pia.Β
“Yesu kristo! pole Binti yangu Matilda, hakuna linalomshindaΒ Mungu wetu aliye hai, yeye halali kwa ajili yetu, Mtoto yupoΒ Hospitali gani?”Β
“JM Hospital, inahitajika Milioni nane aweze kufanyiwaΒ upasuaji, hapa nilipo sina hata senti tano na kadiri sikuΒ zinavyozidi kwenda tumaini la Binti yangu kua hai linazidiΒ kupotea” Alisema Matilda akizidi kulia kaa uchungu sana.Β
“Twende kwanza Hospitali kwa ajili ya maombi, baada ya hapoΒ kanisa litaangalia utaratibu wa kukusaidia” Alisema MchungajiΒ akiwa ameshasimama,
“Asante Mchungaji George” Alisema Matilda, waliondoka hapoΒ kanisani kuelekea Magomeni Mapipa ilipo Hospitali ya JM,Β waliondoka kwa gari maalum ya kanisa, Wakiwa barabaraniΒ Mchungaji alimwambia MatildaΒ
“Hili jambo litaisha kwa namna nzuri Matilda, kua na imaniΒ thabiti usitetereke. Kupitia Mtihani huu shetani anawezaΒ akajipenyeza na kukuingiza kubaya zaidi endapoΒ hautojiimarisha kiimani” Matilda aliitikia kwa kichwa kishaΒ alijishika tama.Β
********Β
“Una uhakika?” lilikua ni swali aliloulizwa Neema, alikuaΒ kituo cha polisi.Β
“Ndiyo sababu yeye ndiye anayeishi pale” alisema Neema kwaΒ kujiamini kisha akatoa kitita kidogo cha pesa kwa siri sana,Β Polisi akatabasamu sababu ilikua ni ishara kua alichokuaΒ akikizungumza Neema kilihitaji kutengenezwa zaidi ili kiweΒ kikubwa.Β
“Jina lako?” Aliuliza Polisi akiwa anaandika jalada la kesi “Neema Ngushi, Miaka 32”Β
“Mshtakiwa?”Β
“Matilda John, Miaka 28” Alisema NeemaΒ
“Vitu vilivyopotea vina thamani gani?”Β
“Milioni 16” Alisema tena NeemaΒ
Baada ya kumaliza kuandika maelezo marefu aliyoyatoa, alipewaΒ RB ya kumkamata Matilda, alichofanya Neema ni kwendaΒ kumfungulia kesi ya upotevu wa vitu kwenye nyumba anayoishiΒ Matilda, hakutaka kuendelea kumwona Matilda katika MaishaΒ yake, pembeni alikua amesimama Mwanaume mmoja ambaye kaziΒ yake ilikua ni kutingisha kichwa tu.Β
Alipohakikisha amemfungulia kesi, walitoka na Mwanaume huyoΒ wakaingia kwenye gari, wakaondoka kituo cha polisi.Β
“Unajua huyu Mwanamke anaweza kua kikwazo kikubwa sababuΒ James alikiri kua Mtoto ni wake lakini anaona aibu kuleaΒ Mtoto ambaye ni kiwete, sasa hofu yangu ni kwamba akili yaΒ Matilda ikifunguka alalfu akaenda kudai haki, huwenda JamesΒ akajirudi kwake sababu atatakiwa kumtunza Mtoto kwa lazima naΒ pengine akachukuliwa hatua za kisheria alafu MimiΒ nikahangaika” Alisema Neema akiwa anaendesha gariΒ
“Hapo usiwe na huruma hakikisha unamsotesha hadi akili imkaeΒ sawa, James akijua itakuaje?”Β
“Hata akijua hawezi kufanya chochote sababu nimeshamwambiaΒ kua nataka nitengeneze mchezo ili Matilda akubali kurudi kwaoΒ Njombe” Alisema NeemaΒ
“Bingoo!!! Sasa tunaenda wapi?”Β
“Naenda kukuacha kwako Sadam alafu Mimi nirudi nyumbani,Β kesho tunamkamata Matilda, naamini kitisho hiki kitamfanyaΒ akubali kurudi kwao”Β
“Umetisha sana hakika wewe ni jembe la kujivunia Neema”Β Alisema Mwanaume huyo kisha akaweka Mkono wake kwenye paja laΒ Neema ambaye alikua na Ujauzito wa Miezi mitatu tu.Β
*****Β
Saa 12 Jioni, Gari ya kanisa ilikua ikiingia kwenye geti laΒ Hospitali ya JM Magomeni Mapipa, Matilda alikua amelia sanaΒ hadi macho yalimvimba, wakashuka na kuelekea Nje ya chumbaΒ ambacho Patra alikua amelazwa, Macho ya Mchungaji na Macho yaΒ Matilda yaligongana na macho ya Daktari ambaye alikua akitokaΒ ndani ya Chumba hicho.Β
“Dokta samahani hali ya Mwanangu inaendeleaje?” aliulizaΒ Matilda kwa presha.Β
“Matilda Mtoto anaendelea vizuri kwasasa, aliamka kishaΒ akalala hadi sasa hivi”Β
“Tunaweza kumwona?”Β
“Ndiyo lakini hampaswi kumsumbua” Alisema Dokta akiwaΒ anaondokaΒ
“Asante Dokta, Mchungaji twende” Alisema Matilda kishaΒ alifungua mlango wa chumba hichoΒ
“Mwanangu!!” Alisema Matilda baada ya kumwona Binti yakeΒ akiwa anapumulia Mashine, Roho ilimuuma sana.
“Oooh Jesus” Alisema Mchungaji, Chozi likaanza kumbubujikaΒ tena Matilda, alikua Mtu wa kulia kila dakika kwa namnaΒ ambavyo hali ya Binti yake ilikua, Mchungaji akamwambiaΒ MatildaΒ
“Kulia hakusaidii chochote, ngoja tufanye kwanza Maombi iliΒ tumkabidhi Mtoto huyu na hali yake mbele za Mungu” AlisemaΒ Mchungaji GeorgeΒ
Alianza kufanya Maombezi kwa Mtoto Patra, aliomba kwa imaniΒ kubwa sana, Matilda naye alizama kwenye Maombi akisaidiana naΒ Mchungaji huyo, maombi yalifanyika kwa sauti ya chini sanaΒ ili wasimsumbue Mtoto kama ambavyo Daktari alikua amewaambia.Β Zilitumika dakika arobaini na tano hadi kumaliza kumwombeaΒ Patra, Jasho lilikua likimvuja Mchungaji huyo ambaye kilaΒ alivyomwangalia Patra alijiskia vibaya sana kwa jinsi hli yaΒ Mtoto huyo ilivyokua.Β
“Mungu amepokea Maombi Matilda, anaenda kutenda kwa ajiliΒ yako na Mtoto, atafungua minyororo ya mateso kwa Mtoto huyu,Β amini kua amekwisha kombolewa” Ilikua ni kauli ya kutia moyoΒ ya Mchungaji huyo ambaye alikua amemshika bega Matilda, maraΒ aliingia Daktari akawaambia Muda umeisha.Β
“Baby leo nimefanya kitu ambacho kitakuondolea hasira sana”Β Alisema Neema akiwa anakula embe bichi, alikua akimwambiaΒ James wakiwa chumbani Usiku.Β
“Jambo gani hilo?”Β
“Ni kuhusu Matilda”Β
“Sitaki hata kumsikia huyo Mwanamke Neema, katika MaishaΒ yangu sijawahi pata ona Mwanamke King’ang’anizi kama Matilda”Β Alisema kwa hasira James, alionesha wazi hataki kusikiaΒ kuhusu Matilda ambaye alitoka kumpiga Kule Hospitalini.Β
“Usikasirike sababu hili jambo litaenda kumfanya aondoke hapaΒ Dar bila kupenda Bby”Β
“Nakusikiliza”Β
“Hii hapa ni RB ya kumkamata kwa kosa la wizi wa vitu kwenyeΒ ile nyumba, naamini akilala polisi siku moja akili itamkaaΒ sawa” Alisema Neema kisha alimpatia Karatasi kutoka polisi,Β James akaisoma kwanza kabla ya kusema Chochote, kishaΒ akamtazama Neema
“Umemfungulia kesi?”Β
“Ndiyo!! lengo langu apate kitisho kitakachomfanya aiyone DarΒ chungu, nimefanya hivyo sababu sitaki kumwona Baba MtotoΒ wangu mtarajiwa anakosa raha” Alisema Neema, JamesΒ alitabasamu sababu aliitwa Baba Mtoto, alihitaji sana MtotoΒ
“Mbinu yako ni bora sana Neema, naamini kwenye hiliΒ hachomoki, ataondoka hapa Dar atake asitake, tena kwa kuondoaΒ kero nitampatia na pesa ya kuanzia Maisha huko aendapo”Β Alisema James kwa furahaΒ
“Umeona jinsi gani nakupenda, nakuhitaji na pia nakuthamini,Β furaha yako ndiyo furaha yangu Mpenzi” Alisema NeemaΒ akiendelea kula embe kwa chumvi.Β
Neema alishajua udhaifu wa James, wala hakutumia nguvu nyingiΒ kumfanya James afurahi, ni kumweleza tu kuhusu ujauzito,Β alichotaka alipewa bila hata kulazimisha.Β
Siku iliyofuata, Neema alienda kituo cha polisi akaonana naΒ yule polisi ambaye aliandika jarada la kesi ya Matilda,Β akaomba askari kwa ajili ya kwenda kumkamata Matilda, akapewaΒ askari polisi wawili akaenda nao moja kwa moja JM Hospital.Β
Muda huo Matilda alikua kanisani, zoezi la kukusanya pesa kwaΒ ajili ya kuratibu matibabu ya Patra lilikua likiendeleaΒ kanisani hapo chini ya uangalizi wa karibu wa MchungajiΒ George ambayo alimwambia Matilda kua atasimama naye bega kwaΒ bega hadi Patra apone, Mama Naomi alikua miongoni mwa WatuΒ waliofika kanisani hapo baada ya kupewa taarifa na MatildaΒ kua litaendeshwa zoezi la Uchangiaji wa matibabu ya Patra.Β
Chozi halikuacha kutoka kwenye macho ya Matilda baada yaΒ kuona uchangwaji wa pesa hiyo, muitikio ulikua mkubwa sanaΒ kiasi cha kumtia moyo hata Mchungaji wa kanisa hilo ambaye niΒ Mchungaji George. Nyimbo za kusifu zilikua zikiimbwa, kilaΒ mwenye kua nacho alitoa kidogo alicho nacho kwa moyo woteΒ bila kujaliΒ
Waumini waliungana kwa pamoja ili kurejesha furaha ya MatildaΒ ambaye alikua haamini macho yake jinsi kapu lilivyokuaΒ linajaa noti. Mikono ya Matilda ilikua kwenye mdomo wake hukuΒ chozi likiendelea kuvuja, tabasamu pana lilionekana kwenyeΒ sura ya Mama Naomi ambaye alitoa wazo la Matilda kurejeaΒ kanisani. Mchungaji George alimtia moyo sana Matilda katikaΒ kila hatua ambayo walikuwepo, baadaye Mchungaji alikabidhiwaΒ kapu lenye fedha hizo.
Watu maalum wa kuzihesabu walianza kazi hiyo huku MchungajiΒ George akitoa neno kanisani hapoΒ
“Hakika leo Bwana ameinuliwa, kwa moyo huu uliooneshwa hakikaΒ roho mtakatifu yupo ndani yetu, kusimama na Mwenye matatizoΒ kunaongeza Baraka, hamjui ni kiasi gani Mungu anaendaΒ kuongeza kilichopungua kwenu. Mungu awabariki sana kwa jinaΒ la yesu” Alisema Mchungaji huku kanisa likiitika haswa kwaΒ kusemaΒ
“Aaameen” Matilda alizidi kulia kwa uchungu sana,Β kilichomliza siyo tu kuumwa kwa Binti yake bali ni maishaΒ anayopitia baada ya kuitwa Mama, jinsi watu bakiΒ wanavyosimama na yeye wakati Mwanaume aliyemfanya akatorokaΒ kwao hajigusi kwa lolote lile, alipiga magoti na kusemaΒ
“Asante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja naΒ kumwinuaΒ
“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji GeorgeΒ alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti.Β Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umatiΒ ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa MatildaΒ Msichana wa miaka 28Β
Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikuaΒ kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpaΒ ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisaniΒ
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
10 Comments
Daaaah jmn
Kama naangalia tamthia vileeeππ
Wakati wa Mungu ukifika Kila lililoshindikana litafanyika kwani hakuna jambo gumu kwake
Mungu hakosei kwakweli
Mambo Yazidi kuwa motooo
God’s ears are not deaf that he cannot hear your π cry ..
Kuna funzo apa
Mamb ni moto
Am I crying too π
Daah pole san kam wap
ge6l84