Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Pigo Takatifu Sehemu Ya Nane (08)
    Hadithi

    Pigo Takatifu Sehemu Ya Nane (08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 19, 2024Updated:September 20, 202411 Comments11 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Pigo Takatifu
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwa  kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua ni  James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee Hospitali  kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. Akaketi kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namna  mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari ya  Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini James  alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepaki  sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingia  akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. Endelea  

    SEHEMU YA NANE

    Hofu ikatanda kwenye moyo wake sababu Neema alishasema kua  atamuuwa Patra, katika hali isiyo ya kawaida James akajikuta  akiumia ndani ya moyo wake, akatamani kushuka ili amfwatilie  lakini moyo wake ukawa unamsuta mara kadhaa huku akimshuhudia  Neema akishuka na kuanza kutembea kwa Mguu kuelekea ndani  zaidi. Akawa kwenye vita kubwa sana ndani yake hadi  aliposhinda na kuamua kushuka kisha akaanza kumfwatilia  Neema, kumbuka Neema alikua amepewa ile dawa na Babu yake  akaiweke katikati ya Hospitali ya Muhimbili ili Mtoto Patra  aonekane kusudi auawe 

    “Huyu amefwata nini hapa Hospitalini?” akajiuliza James akiwa  anaendelea kumfwatilia, James alifahamu mahali alipolazwa  Patra, Neema akawa anaelekea huko pasipo kujua kua ndiko  aliko Patra, lakini baadaye akabadilisha uelekeo kitu ambacho  kilimfanya James ashushe presha yake. Neema alikua makini  sana tena akionekana ni mwenye kujiamini kabisa, James  hakutaka kukubali kushindwa akataka kujua ni jambo gani  limempeleka Neema Hapo Hospitalini. 

    Matilda akiwa katika chumba chenye giza, hakujua mahali hapo  ni wapi isipokua alijua kua alikua amehamishwa kutoka pale  alipokua zamani, alimfikiria sana Binti yake, akawa anasikia  walinzi wakizungumza, tena wakibishana masuala ya Mpira,  Chumba alichopo hakikumpa ruksa ya kuona kilichokua  kikiendelea nje isipokua aliisikia kelele za hao walinzi  pekee, alijua yupo mafichoni, akaanza kupiganisha akili ili  ajue anaweza vipi kutoroka hapo. 

    Basi, James akaendelea kumfwatilia Neema taratibu tena kwa  umakini huku akiwa na maswali mengi sana kichwani. Neema naye  akazidi kuongeza mwendo huku lengo likiwa kufanya kama  ambavyo Babu yake alimwambia, alipofika katikati ya  Hospitali, akageuka huku na kule huku James akijibanza mahali  ili aone Neema anaelekea wapi. 

    Akazuga kidogo kabla ya kuingiza mkono kwenye Mkoba kisha  akatoa hicho alichopewa na Babu yake alafu akakitupa na kukificha kwa Majani kwa kutumia Mguu wake, James alikua  akiona kila kitu, baada ya kumaliza akaangaza tena huku na  kule kisha haraka akageuka na kurudi alipotoka, akampita  James bila kumwona kisha akaelekea Kwenye maegesho lakini  wakati anatoka hapo akaliona gari la James ndipo akapata  uhakika zaidi kua Patra yupo hapo Hospitalini, akatabasamu  kisha akampigia simu Babu yake na kumwambia kua ameshamaliza,  kweli Babu yake alipoangalia tena alimwona Patra kisha  akacheka na kutengeneza bomu kwa ajili ya kummaliza Patra 

    James akafikiria sana ni kitu gani ambacho Neema alikiweka  pale, hakutaka kukipa uzito sana badala yake akarudi nyuma  kisha akaelekea ilipo wodi ambayo Patra amelazwa, kumbuka  ndani ya wodi hiyo alikuwepo Mama yake Mzazi 

    Basi James akasogea hadi mlangoni, Patra alilazwa katika wodi  ambayo ilikua ya hadhi kubwa sana, kitendo cha kufika tu  mlangoni alifanikiwa kumwona Mama yake Mzazi akiwa  anazungumza na Mchungaji, alimwona kupitia kioo cha hapo  Mlangoni, akashtuka sana, Mara akashikwa bega 

    Akageuka na kukutana na Daktari ambaye alikua amezungumza  naye na kumwambia kua kwa lolote litakalo hitajika basi  amweleze, na ndiye aliyekua akimweleza kuhusu hali ya Mtoto 

    “Oooh Mr. James….Karibu sana” Alisema Daktari kisha akampa  mkono James ambaye alikua katika butwaa zito sana 

    “Ndiyo unakuja au unaondoka?” akauliza Daktari huyo, Bado  James alikua kwenye Butwaa maana hakutegemea kumwona Mama  yake pale Wodini. 

    “Nili….kua…Naondoka” Akasema James kwa kujiuma uma 

    “Basi sawa, namshukuru Sana Mungu hali ndiyo kama  ulivyoiyona, Mtoto anaendelea vizuri kwasasa” Akasema Dakatri  kisha akafungua mlango na kuingia wodini, Haraka James  akaondoka 

    “Mmemwona Mfadhili?” akauliza Daktari, wote wakashangaa “Mfadhili?” akauliza Mama yake James 

    “Ndiyo…..si alikua hapa kumwona Mtoto, ametoka sasa hivi  nimepishana naye hapa Mlangoni” 

    “Hapana Dokta, Hakuna Mtu aliyefika hapa wodini tokea  ulipotuacha” Akasema Mama yake James, ikampa Mshangao Dokta,  akaelekea mlangoni kumwangalia James lakini hakufanikiwa  kumwona tena

    “Mbona nimekutana naye mlangoni akanambia kua ametoka hapa  wodini, yeye amekua akichangia pesa za matibabu ya Mtoto”  Alisema, kisha akatoa Kadi ya Biashara ambayo alipewa na  James, akamwonesha Mama James, ndipo Mama James naye  alipogundua kua James alikuja Hospitalini na bila shaka  alimwona Mama yake, lakini kilichomshtua Mama James ni  kusikia kua James anachangia matibabu ya Mtoto. 

    Muda huo tayari James alishaondoka Hospitalini, alikua  Barabarani akiendesha gari yake kwa sapidi sana kuelekea nje  ya Jiji ambako alimwacha Matilda, hakujua kua Matilda  alishaondolewa. Alitumia masaa zaidi ya mawili hadi kufika,  alipoingia ndani ya jumba hilo lililo msituni hakumwona  Matilda pia hakukuta Mtu yeyote yule kitu ambacho kilianza  kumchanganya. Akaingia tena kwenye gari na kurudi Mjini 

    Wakati huo Matilda akiwa bado anapiganisha akili anawezaje  akatoroka hapo ili kunusuru Maisha yake, Walinzi walikua  wakikagua chumba chake mara kwa mara kuhakikisha haondoki  hapo kama ambavyo Neema alikua ameagiza, ilimpa wakati mgumu  sana Matilda 

    Mama yake James aliporudi nyumbani kwake alihisi mwili  ukipata moto, kwanza kujua tu kua James amshamwona pale  Hospitalini kulimpa mashaka makubwa sana sababu hakutaka  ajuwe chochote lakini kingine kilichomuwazisha zaidi ni pale  aliposikia kua James alikua akitoa pesa za matibabu ya Mtoto,  maana yake ni kwamba James alikua na mapenzi na Patra. 

    Siku iliyofuata mapema sana, taarifa mbaya ilianza kuenea  kwenye simu, ilikua ni kuhusu hali ya Patra ambayo  ilibadilika ghafla sana, tena ikidaiwa kua mapigo yake ya  moyo yalikua yakishuka kwa kasi kitu ambacho kilikua  kinaashiria kifo kwa Mtoto huyo, miongoni mwa waliotumiwa  ujunbe huo alikua ni James, Mama yake James, Mama Naomi, Jack  na Mchungaji George 

    Haraka wote wakafika Hospitalini isipokua James ambaye alikua  akifikiria ni namna gani ataingia hapo kwa ajili ya kumwona  Patra, ilionekana wazi kua Patra anaweza kutangazwa kua  amefariki muda wowote, Mchungaji alijitahidi sana kufanya  maombi lakini Mishale ya saa nne Asubuhi Patra alifariki  Dunia, Daktari akathibitisha hilo

    “Poleni sana, tumejitahidi kuokoa uhai wake lakini juhudi  zetu zimegonga mwamba” Akasema Daktari huku akishuhudia mvua  ya vilio, Mchungaji George akashindwa kuvumilia akakimbilia  kulia nje kama Mwanaume, ilikua ni huzuni kwa kila  aliyesikia. Mama James hakuona kama kulikua na sababu ya  kuendelea kulificha hilo sababu alihitaji msiba ukafanyike  nyumbani kwake, akampigia simu James na kumwambia kua  anahitaji kuonana naye 

    Haraka James akaenda nyumbani kwa Mama yake, akamkuta Mama  yake akiwa mwingi wa huzuni, akaketi kando ya Mama yake kabla  ya kumuuliza kiunyonge kilichopelekea huzuni hiyo 

    “Amekufa” Alisema Mama yake James huku chozi likizidi  kumvuja, James akashtuka sana, moja kwa moja akajua ni Patra  lakini akajikaza huku akizidi kumuuliza Mama yake 

    “Nani huyo Mama” 

    “Mtoto wako, Kwanini ulifanya siri James, Mtoto ameteseka Mno  hadi amefariki” Akasema Mama yake James huku akiangusha  kilio, chozi likambubujika James, hakua na la kufanya,  hakuweza kubeba ukatili wa kukana mbele ya Mama yake 

    “Kisa ulemavu James umegeuka kua Mnyama, Mama wa Mtoto hadi  sasa hajulikani yupo wapi….James, hapana shaka upo nyuma ya  hili jambo, nakuhakikishia kua Patra hatozikwa kama Mama yake  Patra hatopatikana” Alisema Mama yake James, kila jambo  lilikua tayari limefunguka, hapakua na siri tena. James  akainamia chini 

    “Kama kuna siku nimeumia katika Maisha yangu James basi ni  leo, James wewe ni katili sana Mwanangu, hustahili kuitwa  Binadamu, Nenda kamlete Mama yake Patra hapa” Akasema kwa  hasira Mama yake James, Basi James akawa kama Budi akasimama  asijuwe aingilie wapi kumtafuta Matilda, akatoka huku chozi  likiendelea kumbubujika, alipofika getini alipishana na gari  iliyowabeba Mchungaji, Mama Naomi na Jack 

    Alipotoka hapo James akaelekea Baa, akaagiza pombe kali na  kuinywa kama anakunywa maji, alihisi kufanya hivyo kungeondoa  Mawazo yote, licha ya kua na pesa nyingi ambazo wengi huamini  kua na pesa kunamaliza matatizo lakini upande wa James ilikua  tofauti, pesa ndiyo iliyoleta matatizo kwake. 

    Giza liliingia huku James akiendelea kuagiza moja baridi,  moja moto hadi akalewa kabisa na kushindwa kujitambua,  akasaidiwa na baadhi ya waliomjua sababu alikua maarufu,  akarudishwa nyumbani kwake.

    Usiku huo tafrani ikawa nzito nyumbani kwa Mama James,  Mchungaji aliomba Patra azikwe lakini Mama James aligomea  kabisa akihitaji kwanza Matilda afike ili amshuhudie Binti  yake, wakambembeleza sana lakini akagoma huku akiwaambia  James atamleta Matilda sababu anajua ni wapi alipo na kama  hatomleta basi Patra hatozikwa. Mama Naomi na Mchungaji  wakatoka kwa ajili ya kuzungumza 

    “Huyu Mama anamaumivu makali sana, amemjua Mjukuu wake tu na  Mjukuu amefariki, hali aliyonayo ni ngumu sana kuelewa  chochote kile, cha Msingi kukipambazuka tumtafute James  pengine anajua ni wapi alipo Matilda” Akasema Mchungaji,  Asbuhi mapema sana wakampigia simu James, wakapanga waonane  ili kuweka mambo sawa, James hakua na ujanja akawaelekeza  mahali anapoishi, walipofika walikuta mazingira ya hovyo sana  sbaabu wafanyakazi wote waliondolewa na Neema, aliyebakia  alikua ni mlinzi tu ambaye alikua hafanyi usafi 

    “Kilichotuleta hapa ni kuhusu Matilda, Mama yako amekataa  kumzika Mjukuu hadi pale Mama yake Patra atakapofika, James  kama unapajua alipo Matilda tafadhali tuambie ili tumsitili  yule Mtoto” Alsema Mchungaji, Mama Naomi akawa anafuta chozi  lake 

    “Mchungaji kiukweli sijui mahali alipo Matilda,, Nimehangaika  sana kumtafuta bila mafanikio yoyote yale, ilipofikia  nimekata tamaa” Akasema James, hakutaka kabisa kusema kua  Neema ndiye anayejua mahali alipo Matilda, sababu alihofia  usalama wa Neema kwakua alikua Mjamzito 

    “Mbona Macho yako yanasema ukweli lakini mdomo wako unaongopa  James, wewe ndiye ulimshtaki Matilda, akaenda polisi lakini  akatoweka katika Mazingira tata, unajua alipo..” akadakia  Mama yake Naomi kwa hasira sana 

    “Jamani ningekua najua alipo ningemleta lakini sijui alipo,  nawaahidi nitaendelea kumtafuta” Akasema James huku akikuna  nywele zake 

    Mchungaji akasimama na kusema 

    “Kumbuka kua Mtoto hatozikwa kama Matilda hatopatikana”  Alisema kisha akaongoza nje, Mama Naomi akamwambia James 

    “Hadi kifo kinamchukua Mtoto ukiwa unaendelea kumkana, hakika  wewe ni miongoni mwa matajiri wajinga sana Duniani” Alisema  kisha naye akaondoka hapo, James hakua na jeuri tena sababu  alikua katika nyakati ngumu sana

    Walipoondoka Mchungaji na Mama Naomi, James akaingia kwenye  gari yake, akampigia Jack kua asimamie majukumu ofisini kisha  akawasha injini ya gari na kutimka hapo, kichwa chake kilijaa  mkanganyiko, zilipita siku mbili bila kuzungumza na Neema,  akili yake ikawa inawaza atafanya nini ikiwa Neema ndiye  anayemshikilia Matilda. 

    Injini ya gari ikazima katika geti la Nyumba ya Neema, Mlinzi  akatoka na kumwambia James kua hapaswi kuingia ndani 

    “Hivi unajua unamzuia Nani, Mimi ndiye niliyeinunua hii  nyumba, hebu pisha” Akasema James kwa hasira, alihitaji  kuzungumza na Neema 

    “Hii siyo amri yangu, nimeambiwa nikuzuie James” Akasema  Mlinzi 

    “Bali ni amri ya Nani?” akahoji James, Mlinzi akachungulia  ndani kisha akamwambia 

    “Neema” 

    “Neema? hebu nipishe..” Akasema James huku akijikuta  akisukumana na Mlinzi pale getini mara gari ya Neema ikafika,  Neema alikua ndani ya gari hiyo, hakutaka kushuka, James  akasogea kisha akamwambia Neena 

    “Shuka nahitaji kuzungumza nawe” Licha ya James kusema kwa  jazba lakini Neema hakutaka kutii amri hiyo, alishajua nini  kimemleta James nyumbani kwake, James akafungua mlango na  kumchomoa Neema 

    “Wewe vipi kwani kuna ulazima wa kuzungumza na Mimi?” akahoji  kwa dharau Neema, James akampiga kibao Neema, ilikua ndiyo  mara ya kwanza James anampiga Neema, wakati huo Mama yake  Neema alikua ameshatoka ndani, akamsukuma James 

    “Wewe una Kichaa? unampiga ulimzaa wewe huyu?” akauliza Mama  yake Neema huku akimtaka James ajibu 

    “Mama, Neema ananiletea dharau wakati nataka kuzungumza naye” 

    “Kwahiyo ukidharauliwa ndiyo umpige Mtu, adabu ya wapi hiyo  wewe Kijana, hujui kama upo nyumbani kwa Neema, tena siyo tu  kwa Neema bali Mimi nikiwepo alafu unampiga?” Neema akawa  anajiliza 

    “Mama nataka kujua Matilda yupo wapi” Akauliza James

    “Matilda, ndiyo Nani…si nakuuliza wewe huyo Matilda ni  Nani?” akahoji Mama Neema 

    “Ni Mwanamke niliyezaa naye, Neema anajua yupo wapi!” 

    “Hivi wewe una utimamu wa akili, yaani Mwanamke uzae naye  wewe alafu uje umtafute kwa Neema, Dunia itakushangaa kwa  uzuzu wako, kama Matajiri wote Duniani wana akili kama yako  basi kua na pesa siyo kua na heshima, alafu si ulisema huna  Mtoto, leo unakubali kua una Mtoto tena umekuja kwa Neema  kumtafuta Uliyezaa naye” Akasema Mama yake Neema, James akawa  mpole na mwenye kunywea, Mama Neema akamshika mkono Neema  kisha akaingia naye ndani 

    “Simtaki huyo Mtu, tafadhali muondoe” Mama Neema akatoa  maagizo kwa Mlinzi. James akaingia kwenye gari kisha  akaondoka, Baada ya kusikia kua James ameondoka…Neema  akamwambia Mama yake kama si yeye aliyekua akijiliza 

    “Mama umemyoosha sana” 

    “Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kile  sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufunguka  kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo Msichana  Mshikilie hadi mwisho.” 

    “Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno” 

    “Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena” 

    “Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatu  kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,  akaingia Mwanaume mmoja..

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

     

    Pigo Takatifu Pigo Takatifu Kijiweni Riwaya ya Pigo Takatifu

    11 Comments

    1. Sir yowas on September 19, 2024 5:52 pm

      Jamani, mbona inahuzunisha

      Reply
    2. Hamic on September 19, 2024 6:49 pm

      Ni hataree

      Reply
      • Ibraah on September 19, 2024 11:27 pm

        ℳumetisha xaba

        Reply
    3. Xavi on September 19, 2024 6:53 pm

      Mtunzi upo vzr unajua kugusa hisia za watu

      Reply
    4. Temba on September 19, 2024 7:18 pm

      Alooooh🙌🙌

      Reply
      • G shirima on September 19, 2024 10:32 pm

        Tamu ial fupi sana jamani

        Reply
    5. Exploration on September 19, 2024 7:50 pm

      😨😨😨😨

      Reply
    6. Revina on September 19, 2024 8:15 pm

      Upo vzur san

      Reply
    7. Daud on September 19, 2024 9:01 pm

      Daaah maskini akipata matako hulia mbwata mbwata mbwata 😗

      Reply
    8. Farnoush on September 19, 2024 11:31 pm

      Patra kufa cjapenda😪

      Reply
    9. Noel on September 20, 2024 10:27 pm

      Nimeipendq coz
      inatufundisha sanaaa

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.