Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya saba
Siku iliyofuata, Serikali iliongeza Watu zaidi ili kumsaidia Waziri kazi ya utafiti eneo la tukio, sio TU wataalam kutokea Ganza bali Afrika nzima pamoja na Mataifa kadhaa ya
Ulaya. Sayansi ilikataa kutoweka kwa Kijiji hicho lakini shahidi za kimazingira ikiwemo ramani pamoja na Wakazi wa vijiji jirani zilichagiza uzito wa jambo lenyewe.
Pamoja na uwepo wa Sayansi lakini nyuma ya pazia Waziri Majula Majula alikua akishirikiana na Mganga aliyemwamini huku akiwa amepoteza Imani na Sayansi ya Mazingira ambayo ilikua ikiendelea Kuchunguza kupotea kwa Kijiji Cha Nzena.
SEHEMU YA NANE
Helikopta zilizobeba maafisa ziliendelea kushuka eneo la Tukio, ulinzi ukazidi kuimarishwa huku Waandishi wa Habari wakizuiwa kutoa taarifa yoyote ile inayohusu kupotea kwa Kijiji hicho Hadi pale Serikali ya Ganza itakavyotoa mwelekeo wa Uchunguzi.
Kwenye mitandao ya Kijamii kama X , Facebook na Instagram paliibuka hoja kua ulikua ni Mpango wa Serikali kutengeneza propaganda ili kuchukua Madini na kuuza bila pesa kuingia Serikalini lakini walio eneo la tukio waliishia kujishika vichwa vyao. Mtu pekee ambaye alibeba matumaini Yao alikua ni Zahoro, lakini simu ya Zahoro ilikua haipokelewi tena.
Hisia zao ziliwaambia pengine Mtu huyo alikua tayari ameshafariki Dunia. Hawakua na Uwezo tena wa kupata taarifa kutoka ndani ya Kijiji kisichoonekana.
***
Ndani ya Kijiji Cha Nzena.
“Aaaahgg‼” ilikua ni sauti ya Kugugumia ya Zahoro, alijikuta ndani ya shimo lenye Giza nene kiasi kwamba hakupata nafasi ya kuona chochote. Palikua kimya kuliko kawaida, harufu ya uozo ilikua ikipenyeza pua yake ndogo Iliyo chongoka.
Alijiinua na kuketi chini, kwa mbali alianza kusikia sauti ya utiririko wa Maji. Aliamua kufuata hisia pamoja na sauti hiyo pasipo kuona mbele. Kila alivyojaribu kupiga hatua aliona inawezekana kuifikia sauti hiyo, hakujua Upendo alikua wapi. Kichwa lilikua kinamuuma, akakumbuka kilichokua kimetokea wakati wanakimbizwa na kile kiumbe Cha ajabu.
Alitumbukia ndani ya shimo Hilo kabla hajanaswa na kile kiumbe Cha ajabu. Picha halisi ilikua kichwani pake, akajikuta sasa akiwa na shahuku ya kumtaka kujua alipo Upendo, alianza kumwita kwa sauti ya chini iliyojaa tahadhari sana
“Upendo‼ Upendo‼” hapakua na mwitikio wowote ule, alijihisi kua peke yake ndani ya shimo Hilo lililojaa Giza, shimo lililo chimbwa kuelekea mbele mithiri ya handaki.
Alipoona ukimya ndio ulikua ukimwitikia aliamua kwenda mbele kufuata mtiririko wa Maji, alitembea taratibu akipapasa Kila Kona ya shimo Hilo ili kuhakikisha anafikia lengo lake huku kitendawili kichwani pake kikiwa kama ataweza kutoka nje ya Kijiji Cha Nzena akiwa salama.
Alikua amechoka kwa njaa Kali na kiu cha Maji, alihisi koo lake likiwa limekauka huku akikiri kua mwili wake ulianza kua dhahifu sana. Hakukata tamaa alizidi kwenda mbele bila kuchoka, shimo lilikua na kona nyingi zilizo titia ukimya.
Alitembea kwa hatua nyingi za kuhesabu Hadi pale alipoanza kuhisi mwanga machoni pake, hata sauti ya kutiririka kwa Maji ilikua ikisikika kwa ukaribu zaidi. Alianza
kupepesa macho yake ili aone mbele zaidi, angalau alianza kuona ni wapi alipotoka na wapi anakoelekea.
Alijikuta akiwa amesimama mwisho wa shimo Hilo, mbele yake palikua na korongo kubwa linalotiririsha Maji likiwa limepambwa kwa mawe makubwa na miamba mizito. Hakuweza kuangalia chini kwa jinsi ambavyo palikua mbali, angehisi kizunguzungu.
Hapa kua na dalili ya yeye kutoka eneo Hilo hatari ambalo halikua na njia yoyote tena zaidi ya kurudi alipotoka. Alijikuta chozi likiwa linambubujika
Masikini Zahoro aliketi chini kwa kukata tamaa Kisha alijiinamia huku akitiririsha chozi lake, kushuka kule chini ilikua haiwezekani kabisa sababu palikua na umbali mrefu na hatari zaidi. Alilia kwa uchungu, alikua amekata tamaa ya kuendelea kuishi.
Alikumbuka mambo mengi yaliyopita kwenye Maisha yake, wakati mzuri alioishi na Baba yake kabla ya Kijiji chao kukumbwa na laana. Aliwakumbuka marafiki, mandhari nzuri ya Kijiji Cha Nzena ambacho sasa kinateketea.
Hakua na Mtu pembeni yake, alihisi upweke ulio ambatana na hofu isiyo mithirika. Mapigo ya moyo wake yalitoa ishara kua hapakua na tumaini la uhai wake. Akajiuliza
“Kwanini naendelea kuishi kwenye Ulimwengu wa Giza?” ilikua ni sauti kuu iliyopita kwenye akili yake, nafsi yake ikamwambia kua ni Bora kufa kuliko kusubiria kifo Cha mateso hapo mbeleni. Masikini Zahoro aliona ni Bora ajitupe korongoni na afie huko kuliko kufa taratibu kwa njaa, hofu na kiu.
Alipomaliza kutafakari alisimama Kisha alisogea karibu na Mdomo wa Korongo uolikua ukimnong’oneza kua ajitupe na afie humo. Alivuta hewa nyingi ili kujiweka sawa, akafumba macho tayari kwa kujitosa Korongoni.
Mara alianza kusikia sauti kubwa ikija upande wake, sauti hiyo ilimshtua huku masikio yake yakiisikiliza kwa makini. Alipofumbua macho alikua amepata jibu kua ilikua ni sauti ya mashine. Moja kwa Moja alijua kua huwenda alishafika nje ya Kijiji Cha Nzena. Alitabasamu huku chozi likimtoka kwa uchungu na hamu ya kutoka salama.
Macho yake yalimwonesha uhalisia wa alichokisia, ilikua ni sauti ya Helkopta ya Kijeshi iliyobeba Watafiti waliokua waliendelea kukichunguza Kijiji kilichopotea Cha Nzena. Helkopta hiyo ilikua mbali kiasi Cha MITA mia mbili lakini ilikua ikisogea taratibu.
Zahoro akapaza sauti yake huku akinyoosha Mikono yake akiomba msaada, alipunga mikono yake.
Mmoja wa Watafiti alimwona Zahoro, akamwambia rubani asogeze Helkopta hiyo karibu na Korongo ili waone zaidi kama alikua Mtu. Kadili walivyosogea walishangaa kumwona Mtu.
Chozi likimbubujika Zahoro, Helkopta ilikua imeshafika mbele yake. Akapiga goti huku akiwa analia kwa Uchungu na furaha, wale Watafiti walihitaji kumsaidia Zahoro wakiamini anaweza kua miongoni mwa Wahanga wa Kijiji Cha Nzena.
Walisogeza zaidi Helkopta. Mmoja akajaribu kumwambia Zahoro kwa sauti ya Juu kua, ajiandae kurukia kwenye Helkopta. Wakaisogeza zaidi ili iwe rahisi kwake kuingia ndani ya Helkopta.
Ghafla Upepo Mkubwa ukaanza kuvuma na kusababisha rubani ashindwe kuimudu Helkopta, upepo ukaishinikiza Helkopta ianguke lakini Rubani alikua akipambana kuhakisha wanaondoka hapo haraka sana.
Tumaini lilianza kufifia kwa Zahoro, alikua akiushuhudia Upepo katili ukiishinikiza kwa nguvu sana Helkopta hiyo, alijua upepo huo haukua wa kawaida ulikua ni ule upepo wa ajabu. Sauti ya Bibi Lugumi ilianza kusikika na kuzima kabisa ndoto za Zahoro.
Helkopta ilianza kuyumba Kisha iliangukia Korongoni na kuwaka Moto. Hapakua na msaada tena kwa Zahoro lakini alitambua kua alikua ameshafika nje ya Kijiji Cha Nzena, shimo Hilo ilikua NDIYO njia ya kuondoka Kijijini hapo.
Taswira ya sura ya Bibi Lugumi ilionekana katikati ya Upepo huo, Bibi Lugumi hakutaka Mtu yeyote atoke Kijijini hapo. Zahoro alianza kutetemeka huku akirudi nyuma nyuma huku akiushuhudia Upepo huo ukianza kumfuata taratibu.
Alianza kukimbia kuelekea ndani zaidi ya shimo Hilo lenye Giza nene, alikimbia bila kuona mbele huku akiusikia upepo ukivuma nyuma yake. Aliendelea kukimbia kwa Kasi huku akijigonga gonga huku na kule ndani ya shimo Hilo.
Alikimbia bila tahadhari huku akisukumwa na hofu iliyotanda akilini mwake, alikimbia Hadi alipofika mwisho wa shimo. Juu yake akaona Pana mizizi mikubwa akajishikiza hapo Kisha akatokea kwa juu.
Akajikuta ndani ya Kijiji Cha Nzena, maiti zilikua Kila mahali. Aliuwona utofauti mkubwa sana wa alipotoka na alipo, alihisi alikua amerudi Kuzimu. Sauti za ajabu zilikua zimetawala
Akiwa hapo alisikia sauti ya Mtoto mchanga kwa mbali, alijikuta akiwa na shahuku ya kuifuata, taratibu alianza safari ya kuifuata sauti hiyo ambayo ilisikika Mita kadha kutoka alipo. Alitembea taratibu na kwa tahadhari kubwa sana Hadi alipofika eneo Hilo, hakuyaamini macho yake
Sauti aliyokua akiisikia haikutoka kwa Mtoto Bali ilikua imetoka kwa Mwanaume mmoja aliyetapakaa Damu, alimwonesha Zahoro tabasamu la kuashiria kua alikua amemnasa kwenye mtego wake.
Mwanaume huyo alikua ameshikilia Upanga mkononi mwake, alikua akimtazama Zahoro kwa jicho la roho mbaya. Alikua tumbo Wazi, Zahoro alianza kurudi nyuma huku akijihadhari na hatari ya Mwanaume huyo wa ajabu.
Basi yule Mwanaume akaanza kumfukuza Zahoro kwa Kasi ya ajabu sana, alionekana Wazi kua alikua na nguvu za Kichawi zisizo za kawaida. Alikua na Kasi sana kuliko Zahoro aliyezorota kwa njaa na kiu, Kijana Zahoro alijitahidi sana kukimbia kwa Kasi ili aokoe Maisha yake
Kila alipogeuka aliziona hatua za yule Mwanaume aliyetapakaa Damu huku Upanga wake ukiwa mkono wa kulia tayari kumshambulia pindi atakapomnasa. Ulikua mtihani mzito kwa Zahoro, bahati mbaya akajikwaa kwenye kisiki na kuanguka.
Hakuweza kunyanyuka kwa haraka, alikua chini akigalagala kwa maumivu makali ya Mguu wake hasa eneo la Goti. Fumba na kufumbua, Alikua amekamatika na yule Mwanaume. Mwanaume huyo alikua akikoroma mithiri ya Simba Dume
Zahoro alikua akitetemeka mwili mzima, aliiona pumzi ya Maisha yake ikikatishwa na Mwanaume huyo wa ajabu sana aliyekua akichecheza kwa Madaha. Zahoro alianza kujiburuza kwa kutumia makalio yake lakini haikumsaidia kufika mbali na kujiokoa.
Macho yalimtoka Zahoro akiushuhudia Upanga wenye Damu ukishuka kuelekea mwilini mwake, alifumba macho asiwe shuhuda wa mateso yake. Damu nzito ikamrukia Zahoro usoni, alihisi pumzi zake zikikata
Lakini alijishangaa kujihisi si mwenye maumivu ya Upanga isipokua Damu pekee iliyomrukia usoni, akapata hamu ya kufumbua macho yake. Akakutana na sura ya Mwanamke akiwa amesimama mbele yake, Mwanamke huyo alivalia suruali na tisheti ya Bluu, chini alikua amevalia kiatu aina ya buti nyeusi. Mkononi alikua ameshika Upanga
Zahoro alistaajabu sana kwa msaada aliokua ameupata, ulikua ni msaada asioutarajia. Kando palikua na mwili wa yule Mwanaume wa ajabu ukivuja Damu. Midomo ya Zahoro ikatamani kumuliza maswali mengi lakini yule Mwanamke wa Makamo aliyemzidi kidogo umri Zahoro akampa mkono ili kumnyanyua Zahoro.
Japo kwa kusita lakini Zahoro aliutoa Mkono wake akampatia Mwanamke huyo. Kisha akainuliwa juu
“Naitwa Anna, Mimi ni mwokozi. Nimekuja kukuokoa hapa” alisema Mwanamke huyo kwa kujiamini sana, Upanga wake Bado ulikua ukitiririsha Damu, Zahoro aliuangalia Upanga Kisha kamjibu kwa hofu
“Naitwa Zahoro”
“Nakufahamu Zahoro, wewe ndiye jibu la Laana hii. Uliiona kabla haijaingia pia utaiona ikiondoka, huwezi kunielewa kwasasa lakini nitakueleza zaidi. Nifuate” alisema Mwanamke huyo, Bado aliacha maswali mengi sana kichwani kwa Zahoro. Taratibu Zahoro alianza kutembea kwa kuchechemea kutokana na majeraha ya Mguu aliyoyapta
Alitembea kidogo Kisha alianguka tena kutokana na kizunguzungu kilichosababishwa na njaa Kali na kiu. Anna akambeba Zahoro na kuondoka naye hapo.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TISA Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
12 Comments
https://shorturl.fm/dctKr
🔥🔥🔥🔥
https://shorturl.fm/0n5Z8
🔥🔥🔥🔥🔥
https://shorturl.fm/bkQi3
Kumeshaanza kichangamka🤦🏻🤦🏻
https://shorturl.fm/8sxMw
https://shorturl.fm/X6uUY
https://shorturl.fm/kNXNF
https://shorturl.fm/r9O4W
https://shorturl.fm/nPm57
https://shorturl.fm/TX5Xn