Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (09)
    Hadithi

    Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 3, 2024Updated:June 5, 202449 Comments6 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Nyumba Moja Na Majini
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Waliomba sana, kuna wakati mimi nilihisi kuchoka lakini wao waliendelea tu hadi moyoni nikasema kweli ni watu wa Mungu.

    Ghafla nilianza kuona moshi mweusi ukitoka chini ya milango yote ya wale ndugu, mlango wa sebuleni kama sikikosei na mlango wa chumbani. Moshi ulikuwa mzito kiasi kwamba, kuna wakati nilihisi kupaliwa na kukohoa kwa nguvu lakini wao hawakuonesha dalili ya kusumbuliwa na moshi huo ” 

    Endelea

    SEHEMU YA TISA (09)

    Mara, milango yote miwili ikaanza kufunguka yenyewe polepole huku maombi yakiendelea kwa kasi na nguvu ya ajabu. Milango hiyo ilifunguka hadi ikafika mahali ndani kukaonekana.

    Cha ajabu sasa, vyumba vilikuwa vyeupe, ndani yake hakukuwa na kitu chochote, hata karatasi. Ilikuwa kama chumba kilichopigwa deki au kufagiliwa kwa ajili ya maandalizi ya kuingia mkaaji mpya.

    “Ha! Oneni jamani,” nilijikuta nikisema hivyo. Nilibaini kwamba, wale watu hawakuona wakati milango inafunguka kwa vile walipokuwa wakiomba walifumba macho na walikuwa wakijipigapiga kwenye viganja kwa kutumia ngumi.

    Yule mzee alipoona vile akasema:

    “Katika jina la Yesu.”

    “Amiiin.”

    “Sasa tushushe uwepo wa Bwana mahali hapa, kwamba akapafanye pawe mahali salama, penye amani na utulivu wa hali ya juu, kila mmoja sasa amwombe Bwana hivyo.”

    Wakaanza kuomba tena, safari hii si kwa kukemea kama mwanzoni, ilikuwa sauti yenye upole na utii, mara nikasikia mlango mkubwa ukigongwa kwa nguvu.

    “Ngo ngo ngo ngoo.”

    “Ingia,” nilisema lakini huku nikienda mlangoni, nikaufungua! Mbele yangu alisimama yule dalali.

    “Karibu bwana.”

    “Ee bwana nini umefanya sasa?” ndilo swali lake hata kabla ya salamu.

    “Kwa nini?”

    “We hujui umefanya nini? Si wako watu humo ndani, wamekuja kufanya nini hapa? Hujui kama kuna watu umewaumiza? Wewe ungefanyiwa hivyo ungekubali kweli?”  

    “Kaka unajua ukija kwangu njoo kwa heshima zako zote na hoja zenye msingi, usije kama mwendawazimu mpya, wewe unachokisema mimi sijakisema kwako? Ulichukua hatua gani wakati naumia mimi?”

    “Lini umeniambia?”

    “Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari kwa hilo…”

    “Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana.”

    “Sina haja, mimi ndiyo najua.”

    Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba ile.

    Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto, akasimama, akawa kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda kushoto na kuanguka puu!

    Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa moja na matukio yote ya ajabu mle ndani. Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.

    Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo alisema mambo ya ajabu sana. Alisema mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala kujulikana na mtu.

    Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna ila alikuwa anasikia raha.

    “Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu yeye hajui.”

    Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila kulisema kwa mtu.

    Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe, walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua, walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.

    Yule mzee mkubwa wa wale waombaji akamuuliza:

    “Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko wapi?”

    Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.

    Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi:

    “Sasa watu wanasema majini wana uwezo mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli ni kwa nini aliamua uwe dalali?”

    Dalali akajibu: “Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa sababu mimi na mke wangu tulipenda kuwachezea watu wanaoishi ndani.

    “Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya maisha wala ya fedha.”

    Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka. Hata siku ya kwanza nilipokutana naye nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi nikapata nguvu ya kumuuliza swali:

    “Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje kusababisha mimi nipate namba yako ya simu kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf Mwamba?”

    “Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na kukifanyia kazi. Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf.”

    Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema tumwingize ndani maana watu waliokuwa wakipita walianza kukodolea macho pale nje.

    Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna mtu amebandika jiko la mkaa.

    “Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia matendo yako ya nyuma,” alisema yule mzee aliyenisaidia.

    “Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine. Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu.”

    Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali akasema atakwenda kesho yake mapema.

    Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi ulinishika lakini nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba nimsamehe kwa yote yaliyopita.

    Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta dalali ameshafika.

    Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya wiki mbili, dalali alimleta mke wake  na mtoto mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado nasali kulekule Magomeni na yule dalali.

    Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania mpaka kutoka katika nyumba ile. Ile mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu. Nadhani shetani alipanga nife katika nyumba ile lakini ameshindwa katika jina la Yesu. Amina.  MWISHO 

    Tafadhali Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako Simulizi Ijayo Iwe Ya Kitu Gani? MAPENZI UJASUSI au UCHAWI?

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

     

    nyumba na majini Nyumba Ya Majini Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni

    49 Comments

    1. Edwini Elias Nsato on June 3, 2024 5:11 pm

      Mapenzi itakuwa unyama sana mkuu

      Reply
      • Dismas on June 4, 2024 2:07 pm

        Ujasusi

        Reply
      • Hans on July 19, 2024 4:38 pm

        Daah mzee baba umetisha sana yan story iko poa sana haichoshi haiboi yani hongera sana mzee kama unayakijasusi we tupia au yakuruka na maungo usiku we tupia kama utapendezwa lakin.

        asante sana

        Reply
      • Fredy on August 6, 2024 12:04 pm

        Dah nimejifunza kitu apa asante San

        Reply
    2. Kaytes on June 3, 2024 5:12 pm

      Ameeeen

      Reply
      • Bintii kimmy on June 4, 2024 8:38 am

        Ameen hii story kalii sanaaa🔥🔥na Mtunzi kaimalizia vizurii 🤗🤗apewe maua yakee👌👌

        Reply
        • Nesterjoseph on June 23, 2024 12:32 am

          Ashukuriwe mungu

          Reply
    3. Tumpe on June 3, 2024 5:12 pm

      Perfect 🥰🥰

      Reply
    4. Lus twaxie on June 3, 2024 5:27 pm

      Nzuri kbsaaaa…. Tuje kwenye mapenzi

      Reply
      • Bintii kimmy on June 4, 2024 8:39 am

        Story ijayoo iwe ya mapenzii ila isiishie hewani kama fungate🤔🤔

        Reply
        • Imma MK on June 4, 2024 11:29 am

          Tuletee za ujasusi sasa kama ile koti jeusi 😎😎

          Reply
      • Egibeth on January 19, 2025 5:59 pm

        Mungu muweza wa yoter

        Reply
    5. Pasua kichwa on June 3, 2024 5:33 pm

      Ujasusi kama Ile ya kwanza koti jeusi

      Reply
    6. Mbele on June 3, 2024 5:45 pm

      Ujasusiii itakuaa poa sana

      Reply
    7. Stuart on June 3, 2024 5:51 pm

      Ubarikiwe

      Reply
    8. Idrissu on June 3, 2024 6:00 pm

      Ujasusi 😇

      Reply
    9. Salumsal on June 3, 2024 6:01 pm

      Uuchawai mkuuu ndo itakuwa bomba sana

      Reply
    10. ATUGONZA on June 3, 2024 6:13 pm

      Asante saana story yako inadhihilisha uwezo na ukubwa wa mwenyezi Mungu.Amina

      Reply
    11. FRANCIS THOMAS on June 3, 2024 6:21 pm

      Mapenziiiiiiiiiiii

      Reply
      • Massay on June 3, 2024 10:56 pm

        Ujasusi

        Reply
    12. FRANCIS THOMAS on June 3, 2024 6:23 pm

      MAPENZIIIIIII

      Reply
    13. Tumain on June 3, 2024 6:35 pm

      Love story plz 😍

      Reply
    14. jacques on June 3, 2024 6:46 pm

      Kijasusi itakuwa makini

      Reply
    15. Zombie on June 3, 2024 6:49 pm

      Ujasusi

      Reply
    16. Zombie on June 3, 2024 6:51 pm

      Hii ilianza vizur
      Huku mwishoni imeisha kizembe kama koti jeusi

      Reply
    17. Zombie on June 3, 2024 6:54 pm

      Stori zote tatu mwishoni huwa zinatoka kwenye uhalisia zinaishia kistori stori
      Jitahid ijayo kuwe na improvement plz

      Reply
    18. PILATO on June 3, 2024 7:38 pm

      Love story jomba

      Reply
    19. Dastan on June 3, 2024 7:59 pm

      Mpenziii

      Reply
    20. Trinity on June 3, 2024 8:24 pm

      ujasusi mara 100

      Reply
    21. Seb Jr. on June 3, 2024 8:48 pm

      Amina admin. Hii Stori ituhamasishe watoto wa Mungu kumtumainia katika yote. Up next, ujasusi itakuwa poa Sana

      Reply
    22. Sadick on June 3, 2024 9:40 pm

      Love story Kali ishuke apo tuendelee kuenjoy wana kijiweni

      Reply
    23. Lizzy on June 3, 2024 9:44 pm

      Mapenzi

      Reply
    24. TJ on June 3, 2024 11:37 pm

      Hii ilikua ya moto sana. Sasa mahaba yaingie kazini

      Reply
    25. Msdandy on June 3, 2024 11:39 pm

      Ujasusi itakua hatari sanaaaa

      Reply
    26. Michael Sarpong on June 4, 2024 1:33 am

      Mapnz

      Reply
    27. Henderson Didas on June 4, 2024 3:35 am

      Weka ya combination yani Love story umo na ujasusi umoumo admin😎

      Reply
    28. Loulou on June 4, 2024 9:49 am

      Kwakweli hii ilikuwa hadith tamu mnoooo. Asante sana admin. Ukipata stori zingine zenye mauzauza usisite kutuletea.

      Reply
    29. Joseph kapange on June 4, 2024 9:52 am

      Daaah hakika Mungu autwe Mungu

      Reply
    30. Calvin's HD on June 4, 2024 2:41 pm

      Admin wewe ni 🔥🔥
      Huna mpinzani

      Ijayo iwe ya ❤️❤️Mapenz ❤️❤️

      Reply
    31. Walter on June 4, 2024 10:28 pm

      Ameen

      Reply
    32. Osward on June 5, 2024 10:19 am

      Kijasusi

      Reply
    33. Abuusantos on June 5, 2024 10:29 am

      Ina funzoo ndanii yke

      Reply
    34. Abuusantos on June 5, 2024 10:29 am

      Inafundishoo

      Reply
    35. Lucky on June 29, 2024 5:19 pm

      Huna jambo dog admin

      Reply
    36. Ashirafu on August 19, 2024 5:28 pm

      Mungu ni mkuu siku zote
      Asante kwa story nzuri sana

      Reply
    37. Zahara on August 27, 2024 12:01 pm

      Mapenzi

      Reply
    38. Laurent Kigufa on September 22, 2024 7:29 pm

      Amina kubwa sana Mungu wetu ni Mungu mkuu awezae yote.

      Reply
    39. Joachimu on November 25, 2024 12:20 pm

      Daah! Hii story imenitoa jasho inatixha pia inavutia

      Reply
    40. Francis pallangyo on January 6, 2025 4:38 pm

      Hakika mungu yupo na tunapomuomba anayasikia maombi yetu

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.