Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (02)
    Hadithi

    Nilipanga Nyumba Moja Na Majini (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 26, 2024Updated:May 27, 202431 Comments5 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Nyumba Moja Na Majini
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Nje, nilikuta taa inawaka, ndani pia taa inawaka, lakini si sebuleni bali kwenye korido. Hii iliashiria kwamba, wale wapangaji wenzangu walisharudi kutoka kwenye biashara zao.

    Nilishusha vyombo kwa kusaidiwa na wasaidizi wa dereva wa lile lori, lakini nilishangaa sana kuona kila nikiingia na mizigo, wale wapangaji wenzangu wanacheka sana chumbani kwao. Maana yangu ni kwamba, kwa kawaida walitakiwa hata watoke na kunisalimia ili tufahamiane. Tena kwa wengine, mume angetoka na kunisaidia kubeba hata stuli tu.”

    Endelea SasaΒ 

    SEHEMU YA PILI (02)

    Ilifika mahali, wale vijana waliokuwa wakinisaidia waliniuliza:

    β€œHivi hao majirani zako mbona hawatoki, wanacheka tu chumbani.”

    Niliwajibu mimi mwenyewe sijui, lakini sikumaindi sana. Akaja mama mmoja aliyesema anaishi nyumba ya pili, akasalimia na kuniuliza maswali.

    β€œHamjambo wanangu?”

    Tuliitikia wote, akauliza nani anahamia pale kati ya sisi wote, tulikuwa watano mbali na dereva.

    β€œNi mimi.”

    β€œOoo, mzima baba?”

    β€œMimi mzima mama.”

    β€œUnaitwa nani?”

    β€œHumuli Samaki.”

    β€œUnahamia peke yako au uko na mke na watoto?”

    β€œPeke yangu mama.”

    β€œHumuli Samaki ni mwenyeji wa wapi?”

    β€œUsukumani.”

    β€œHaya, naamini uliaga wakati unaondoka nyumbani.”

    β€œHilo lilikuwa la kwanza mama.”

    β€œHaya, kila la kheri.”

    Tuliendelea na kazi ya kuingiza vyombo ndani hadi tukamaliza. Wale wenye gari wakaondoka, nikabaki mimi peke yangu.

    Nilijiwekea malengo kwamba, nihakikishe naweka sawa kila kitu ili kesho yake nisiwe na kazi hiyo zaidi ya kwenda kazini. Niliifanya kazi kwa muda wa saa tatu, mpaka kwenye saa saba na nusu usiku nikamaliza.

    Nilibadili nguo, nikavaa taulo na kwenda kuoga. Nilikuta bafu limetoka kutumika kama dakika kumi nyuma, sikushangaa kwani si kuna wapangaji wengine ambao tulitakuwa tunatumia bafu moja.

    Usiku kabla ya kuzima taa, nilizima taa, nikapanda kitandani. Kabla sijapata usingizi, niliwasikia wenzangu wakicheka sana na kuongea huku wameweka muziki. Lakini ule muziki haukuwa wa kiarabu, kizungu wala kiswahili.

    Hata maongezo yao, mimi nilisikia sauti tu lakini kusema walikuwa wanatumia lugha gani si rahisi. Kuna wakati kama walikuwa wakiongea kihindi, pia niliwasikia kama wanaongea kiarabu, nikajua ni watu wa namna hiyo.

    Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni weupe au waswahili kama mimi, akasema hata yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku moja.

    Basi, nililala. Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka sana. Wakati nakwenda bafuni kuoga niligundua ni mimi peke yangu ndiye niliyekuwa nimetangulia kuamka, kwani bafuni hakukuwa na maji yaliyomwagika kwa muda huo.

    Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu kujiandaa kwenda kazini. Wakati najiandaa, nilisikia mlango ukifunguliwa, nikajua ni wenzangu wanakwenda kuoga au chooni kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wakiamka asubuhi.

    Niliamua kutumia nafasi hiyo kuwatambua. Nilivizia pale niliposikia mlio wa maji bafuni na mimi nikatoka kwenda kupiga mswaki kwa mara ya pili. Sehemu niliyosimama, mtu akitoka bafuni kwenda ndani ilikuwa lazima nimuone kwani ilikuwa kiasi cha kugeuka tu.

    Lakini cha kushangaza, nilikuwa sisikii maji kumwagika, nikageuka na kuona mlango wa bafuni upo wazi. Mbali na mlango kuwa wazi, pia chini nikaona alama za kandambili nne zikiwa zimekanyaga, nikajua wametoka.

    β€œLakini wamepitaje hapa?” nilijiuliza.

    Nilirudi ndani, mlangoni kwao nilikuta kandambili pea mbili zikiwa bado na majimaji kwa mbali, jambo hili lilinifanya nijiulize sana.

    Nilijipa ujasiri na kuamua kuchungulia ndani ya chumba hicho kwa kutumia nafasi ya katikati ya mlango ambapo niliweza kuona hadi kitanda lakini sikumwona mtu mwingine.

    Niliingia kwangu, nikaweka mswaki, nikavaa vizuri na kuondoka zangu. Nilitegemea wenzangu nimewaacha ndani, kwani nilipofika mlangoni nilikuta umefunguliwa na upo wazi. Nilirudi ndani hadi kwenye mlango wao.

    β€œWa ndugu,” niliita kwa sauti.

    β€œJamani wa ndugu.”

    Ukimya ndiyo ulinifanya nibaini walishaondoka. Kwani kulikuwa kimya sana na kandambili zilikuwa pembeni ya mlango si pale pa kwanza.

    Nilifunga mlango mkubwa nikaondoka, mbele nilimwona yule mama aliyekuja usiku kuniuliza maswali. Alikuwa amesimama nje ya nyumba yake, aliponiona akashutuka na kuita majina mawili ya watu. Wakatoka watoto wake wawili, ni mabinti wenye miaka kama kumi na nane na ishirini na mbili hivi.

    β€œHujambo kijana?” yule mama alinisalimia kwa furaha.

    β€œSijambo mama, shikamoo.”

    β€œMarhaba.” Kisha akawaambia kitu wale watoto wake nao wakanikazia macho.

    β€œMama umewaona majirani zangu hapa?”

    β€œMajirani zako akina nani?”

    β€œWapangaji wenzangu.”

    β€œKijana, kua uyaone ya dunia. We si umeshakua, utayaona ya dunia.”

    Kauli hiyo iliniogopesha sana, nikashtuka na kumuuliza mama.

    β€œMama una maana gani?”

    β€œSisi hatutaki umbeya kijana.”

    β€œWe si umeambiwa utayaona kwa hiyo subiri tu,” alidakia binti yake mkubwa.

    Miguu ilitetemeka, mwili uliisha nguvu, nikajikuta nataka kukaa, lakini sikuweza. Nilichoamua ni kuondoka huku nampigia simu yule dalali.

    β€œVipi hujambo bwana?”

    β€œMimi sijambo.”

    β€œZa makazi mapya.”

    β€œSi nzuri bwana.”

    β€œKwa nini tena?”   

    β€œSielewielewi.”

    β€œKivipi?”

    β€œKuna mambo kama si ya kawaida.”

    β€œYapi hayo?”

    β€œWale wapangaji wenzangu siwaelewi kabisa.”

    β€œKivipi?”

    β€œAh! Watu gani mimi mgeni nimehamia washindwe kutoka kunisalimia ili angalau tufahamiane?”

    Dalali alicheka sana kisha akasema:

    β€œWale ndivyo walivyo bwana, si unajua tena malezi, mwingine kalelewa vile, mwingine hivi. Ila ulichokisema ni kweli, haiwezekani nyumba mnayoishi mpate mgeni halafu msitambuane, sasa mkikutana njiani je?”

    β€œSi ndiyo hapo sasa,” nilisema nikijifanya lawama zangu ni kwa ajili ya hilo tu, lakini kumbe nilikuwa na zaidi ya hapo.

    Kazini siku hiyo nilishinda sina amani, sina raha, mwili ulikuwa kama umetoka kufanya kazi nzito ambayo sijawahi kuifanya kwa siku nyingi, wenyeji wa Pwani wanaita mavune.

    Kwa upande mwingine nilitamani sana jioni ifike ili nikaone siku hiyo kitatokea kitu gani kipya kwenye nyumba ile. Jioni ilifika, nikaondoka kazini, sikutaka kupitia popote, dukuduku langu lilikuwa kwenda nyumbani tu.
    Baada ya kufika nyumbani ilikuaje? Usikose Sehemu ya Tatu

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    Nyumba Ya Majini Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni

    31 Comments

    1. Khalifa on May 26, 2024 5:18 pm

      Iko pw sana kazi nzuri sana mtunzi

      Reply
      • Anthony jaden on May 26, 2024 8:57 pm

        Hey

        Reply
      • John on May 27, 2024 11:31 am

        Tamu

        Reply
    2. Kelvin on May 26, 2024 5:22 pm

      Kipande kingne changamka

      Reply
      • Said on May 26, 2024 6:47 pm

        πŸ™

        Reply
      • Letty on May 26, 2024 9:32 pm

        Usichukue muda mrefu basi kuweka episode ijayo unatuacha na uhondoo πŸ˜… good story

        Reply
    3. Given Gihsy on May 26, 2024 5:26 pm

      Toa na ya tat jan ulipitish kapa au ndo sabato boss

      Reply
    4. Fofana on May 26, 2024 5:27 pm

      Duh so poa

      Reply
    5. Jimmy elias mkanila on May 26, 2024 5:29 pm

      Da ! Mbona kipande kidogo hiki .

      Reply
      • Sabra on May 27, 2024 4:27 pm

        Nshaanza kuogopa

        Reply
        • Calvin on June 4, 2024 2:43 pm

          mmh..acha woga

          Reply
    6. Fofana on May 26, 2024 5:30 pm

      Unajuwa mimi sio mpenzi wakusoma hadithi sema hadithi zako nimezielewa sana ukianzia ile ya fungate ndo imenivutia niwe sahabiki wako namba 1 BIG UP 🫑

      Reply
      • Minally on May 27, 2024 1:58 pm

        Nzurii

        Reply
    7. Ahiya on May 26, 2024 5:41 pm

      Mamb mot

      Reply
    8. Dickson on May 26, 2024 5:44 pm

      Kipande kingine ni lini

      Reply
    9. Mussa on May 26, 2024 5:50 pm

      Iko poa sana

      Reply
    10. Enock S on May 26, 2024 7:43 pm

      Iko poa

      Reply
    11. Hamisi halidi on May 26, 2024 8:06 pm

      Aahaha ameyatimba jamaa uyo

      Reply
    12. Pascal on May 26, 2024 8:46 pm

      Ni hatali sijui itakuaj mwamba akiludi nyumban

      Reply
    13. Valence on May 26, 2024 10:00 pm

      Admin siyo unakaa siku tatu ndo unaleta episode nyingine,, tutakosana admin!

      Reply
    14. Wasna kileo on May 26, 2024 10:06 pm

      πŸ™

      Reply
    15. Seif Haruna on May 26, 2024 10:07 pm

      Admin tulale hautumi episode ya pili??

      Reply
    16. mbega on May 26, 2024 10:43 pm

      nixe

      Reply
    17. Jumaa vesso on May 26, 2024 10:44 pm

      uwakk kitu kikal hongr mtunz

      Reply
    18. Maria on May 27, 2024 12:06 am

      Ni nzuri mnooo

      Reply
    19. Sadick on May 27, 2024 10:31 am

      Weka ya 03 apo mana mzigo umenogo yani so poa weka ata viwili kwa siku basi

      Reply
    20. Lizzy on May 27, 2024 10:35 am

      πŸ˜ƒ Weeeeh! πŸ™Œ
      Admin lakini mbona hii unatoa fupi fupi sana tunaomba uirefushe kidogo please πŸ™πŸ₯Ί

      Reply
    21. Muuh on May 27, 2024 12:51 pm

      Mie kupanga jamn mpaka nijifikilie san maanπŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ₯Ί

      Reply
    22. Pauline on May 27, 2024 1:48 pm

      Alikuwa hajui mizamwamwa eeeeh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hapana chezea misoweto πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™Œ

      Reply
    23. Minally on May 27, 2024 2:32 pm

      Nzurii

      Reply
    24. Rajity on May 27, 2024 2:51 pm

      Em tupe mda maalumu maana unatuacha na shauku San Asee af unachelewa sana kuweka mwendelezo ila stor n tamu balaaa

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.