Ilipoishia “Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.Β Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vileΒ vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yanguΒ niteseke.Β
Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuonaΒ Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikuaΒ nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawaΒ anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguoΒ akampa Mzee Mwinyimkuu. Endelea
SEHEMU YA SABA
Walionekana kupiga stori za hapa na pale kana kwamba walijuana muda mrefu, nilijua hii ilikuaΒ ni tabia yake Kaka Hamidu kupenda kuongea sana na Watu tofauti tofauti pasipo kujua kuaΒ aliyekua anaongea naye alikua katili sana na laiti angelijua hata asingelikanyaga mguu wakeΒ ndani ya hii nyumba. Taratibu nilirudi ndani nikaingia chumbani, nikafunga mlango huku choziΒ likinibubujikaΒ Β
Hapakuchukua muda mrefu mlango uligongwa, halafu uligongwa taratibu sana na hapo hapoΒ sauti ya Mzee Mwinyimkuu ikasikika ikiniitaΒ
βMkweβ yaani nilizidi kukereka lakini kwa kuhofia uhai wa Kaka Hamidu ikanilazimu kuitikiaΒ japo kwa shingo upandeΒ
βAbee Babaβ nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango, ghafla akanisukumiza hadi ndani kishaΒ akaufunga mlango na kunishika shingoniΒ
βNilikuonya lakini unaonekana hutaki kusikia si ndiyo, sasa kwa taarifa yako hakunaΒ utakachofanya nisikijue. Ulichojaribu kukifanya leo sokoni kinaweza kukugharimu, subiri KakaΒ yako aondoke nitakuonesha rangi yangu halisi na yule Mtu wako anakufuatilia sasa nayeΒ arobaini yake imefikaβ alisema kisha akanitupa pembeni, kwakuwa nilikua mwembamba ikawaΒ rahisi sana kwake kunisukuma, nikawa nakohoa ila nikawa nimejua kua nilichokusudia kwa yuleΒ Mwanaume kule Buchani kilifanya kazi ila sasa nikawa naogopa sababu ni lazima atadhurika tu.Β
βJiandae uje uonane na Kaka yako, kumbuka nilichokwambia ukifanye la sivyo naye ataishiaΒ humuβ alisema kwa sauti yenye mikwaruzo huku akimalizia na ishara ya kuweka mkonoΒ
shingoni kuwa atamuuwa. Lugha ya chozi ndiyo Lugha pekee ambayo nilikua naizungumza kilaΒ wakati, umri wangu na yote ninayoyapitia vilinizidi kabisaΒ
Ili kumlinda Kaka Hamidu nililazimika kuigiza kuwa kila kitu kipo sawa, nilifunga vizuriΒ kitambaa mguu ambao ulikatwa kidole kisha nikavalia na soksi, Nikanawa usoni ili kujipaΒ utulivu wa sura yangu iliyochoka mateso na manyanyaso ya Mzee Mwinyimkuu. NilisimamaΒ mbele ya kioo huku kwa mbali nikisikia namna ambavyo Mzee Mwinyimkuu na Kaka HamiduΒ walivyokuwa wakichekeshanaΒ
Nilipohakikisha nimejiweka vizuri, nilitoka chumbani nikaenda sebleni ambapo Kaka HamiduΒ alikuwepo, niliizima hisia ya majonzi nikaingia sebleni, Kaka Hamidu alifurahi sana sababuΒ hakuwahi kuhudhuria harusi yangu na pia ilipita kitambo pasipo kuonana, nilimkaribisha kwaΒ furaha ya kuigiza na kumtaka ajisikie yupo nyumbani kisha nilimuacha na kwenda kumuandaliaΒ chakula.Β
Niliporudi nilimpa chakula akaanza kula huku akinisifia kuwa mapishi yangu hayajabadilika,Β yeye alionekana kuwa na amani na furaha ya kweli sababu hakuna alichokuwa anakifahamu hadiΒ muda huo, isipokua mimi niliyejiona nilikua ndani ya shimo refu lililoenea giza zito nisione paΒ kutokea, tabasamu lilitanda kote usoni pangu ili tu kumlinda Kaka Hamidu, na jinsi mudaΒ ulivyokuwa umeenda niliogopa sana kama atalala ndani ya nyumba hii ya Kutisha, nilitamaniΒ aondoke baada ya kumaliza kula tu.Β
Mzee Mwinyimkuu alikua ameketi anasikiliza maongezi yetu, akawa ananikumbusha stori zaΒ zamani na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa nilipokua mdogo nilikua na tabia ya kulialia,Β kwake alichukulia kama ni sehemu ya mazungumzo mazuri lakini kwangu niliona anapotezaΒ muda badala ya kula akamaliza mapema aondoke, baadaye akaniuliza kama naweza kupokeaΒ simu kutoka kwakeΒ
Huwezi amini alininunulia simu ndogo ili nisikae bila simu kwa wakati ambao nilimwambiaΒ Mama kuwa namsubiria Mume wangu Salehe akirudi aninunulie simu mpya. Niliitaka sana ileΒ simu lakini jicho alilonikata Mzee Mwinyimkuu nikajikuta nikimwambiaΒ
βAsante Kaka, muda siyo mrefu Salehe atarudi atanunua simu ni wajibu wake. Hiyo kampe WifiΒ yanguβ nilisema kanakwamba nilikua kwenye utani lakini moyoni nilitamani angenipa kisiri ileΒ simu ila sasa alikua hajui kuwa napitia mateso makali sana na vitisho vya kila aina. MzeeΒ Mwinyimkuu akajikoholesha, jasiri haachi asili yake nikashtuka lakini nikajishtukia na kurudiΒ kwenye hali ya kawaidaΒ
βSaida, Muandalie mgeni sehemu ya kulala. Apumzike akimaliza kula maana anaonekanaΒ amechokaβ alisema Mzee Mwinyimkuu, nilishtuka sana sikutaka Kaka Hamidu asikie vitimbiΒ vya Usiku vya hii nyumba, nikaitikia kwa wasiwasi sanaΒ
βNjoo Mamaβ akasema Mzee Mwinyimkuu, mbele ya Mtu mwingine hujionesha ni Mtu mzuriΒ lakini tukiwa wawili ananitendea unyama na ukatili wa kutisha sana. Nilitabasamu nikiwaΒ
namtazama Kaka Hamidu ambaye naye alikua akitabasamu huku akinitazama, ndani ya moyoΒ wake aliiamini hii picha ya nje kuwa nina amani na furaha lakini niliamini kama atalala hapaΒ basi ataiona picha ya ndani ya Maisha yangu kitu ambacho kitahatarisha Maisha yake.Β
Niliongozana na Mzee Mwinyimkuu hadi kwenye korido, akairudisha ile sura yake ya MbuziΒ ambayo niliizoea japo inatisha, kwa sauti ya chini nzito akaniambiaΒ
βChumba cha mwisho kushoto, muandalie mazingira ya kulala.β Alisema, sijui kwanini alisistiza Kaka Hamidu alale wakati alikuja bila begi lolote lile akionekana amekuja Mara moja tu, lichaΒ ya yote sikutaka alale pale ila sikujua nawezaje kumshawishi aondoke.Β
βSawaβ hakunipa onyo lolote lile baada ya kuitikia aliondoka na kurejea sebleni, nilienda mojaΒ kwa moja kwenye chumba nilichoelekezwa ambacho Kaka Hamidu atalala. SikuwahiΒ kukifungua kile chumba wala kukisogelea, ilikua ndiyo mara ya kwanza nakifunguaΒ
Nilipoingia ndani nilianza kuona vitu vilivyoniacha mdomo wazi, huyu Mzee alitaka makusudiΒ nione pia. Palijengwa kitu kama kaburi katikati ya kile chumba, halafu palikua na mifupa mingiΒ sana ya Binadamu, mafuvu ukutani, halafu nikasikia sauti ya kutisha ikisemaΒ
βHiki ni Chumba cha Hamiduβ sauti hiyo ilinipa kiwewe nikajikuta nikipiga yowe nikakimbiaΒ kuelekea sebleni, Kaka Hamidu akawa Mtu wa kwanza kunidaka na kuniuliza kuna nini. HapoΒ akili ikanikaa sawa kuwa sikupaswa kupiga kelele namna ile, nikajitahidi kujikaza lakini tayariΒ Β
nilikua nimezua taharuki halafu cha ajabu Mzee Mwinyimkuu alikua akitabasamu tu kituΒ ambacho kilizidi kunipa maswali yasiyo na majibu.Β
βEti Babu huyu ana nini?β akauliza Kaka Hamidu akiwa amenishika bega huku macho yakeΒ akiyapeleka kwa Mwinyimkuu aliyeketi bila hata kujitingishaΒ
βSaida Bwana, sasa nini kinakufanya unamshtua Kaka yako, hadi leo hujaizoea hii nyumba tu?βΒ Aliniuliza Mzee Mwinyimkuu lakini swali lake lilijaa dhihaka sana kitu ambacho sikukipendaΒ kabisa wakati alijuwa alichokua amekifanya. Bumbuwazi niliyonayo ilinifanya nishindwe kujibuΒ swali lolote lileΒ
βHamidu hebu twende ukaone kilichomshitua huyuβ akasema Mzee Mwinyimkuu, MoyoΒ ulifanya kama unataka kusimama hivi kwa namna nilivyoshituka, nikajiuliza kama Kaka HamiduΒ ataenda kule atakiona kile chumba cha kutisha chenye kaburi ndani na hapo kizaa zaa kitaanzaΒ kwake, nikajitahidi nimzuie nikamwitaΒ
βKaka Hamiduβ¦β alikua tayari ameongozana na Mzee Mwinyimkuu, walikuwa wameshafikaΒ kwenye korido wakiwa wamebakisha hatua chache sana kukifikia kile chumba cha kutisha,Β macho yalinitoka nikiwaangalia walivyokuwa wakienda kisha walisimama mlangoniΒ wakatazamana kwa mshangaoΒ
Halafu Kaka Hamidu akaangua kicheko huku akigeuka na kunitazama nikiwa nimesimamaΒ mlango wa kuingilia sebleni, alicheka kama Mtu aliyepandwa na wendawazimu, hapo hapoΒ
nikaisikia simu yake ikiita maana aliiacha kwenye kochi, nikatamani kurudi niipokee ili nitoeΒ taarifa kusudi akipotea kila Mtu ajue pa kuanzia lakini sikupata hata hiyo nguvu mara akaniitaΒ
βSaida hebu njooβ aliniita Kaka Hamidu, alikua tayari ameacha kucheka. Akaniita tena kwaΒ kunisitiza kuwa niende, nikajikuta bila kujiuliza mara mbili naanza kupiga hatua kama Mgonjwa,Β kumbuka hapo nna maumivu ya Uchi wangu pia kidole kilichokatwa halafu nilishakata tamaaΒ Β
Nilisogea taratibu huku nahesabu hatua zangu kama mwendawazimu, nilijua naenda kuona niniΒ sababu nilichokiona mwanzo ni kile kile. Nilipofika nilishangaa sana, Jamani eti kile chumbaΒ chenye kaburi na mafuvu na mifupa ya Binadamu kilikua hakina chochote zaidi ya kitanda kizuriΒ kilochotandikwa shuka safi sana na zaidi kilikua kinanukia ila chini palikua na paka aliyetuliaΒ zake.Β
Kaka Hamidu akanishika bega akaniulizaΒ
βNi lini utaacha kuogopa paka Mdogo wangu? Wewe ni Mtu mzima sasa pia ni Mke na huwendaΒ ukawa Mama baadaye, unaogopa Paka kweli?β aliniuliza, haikuwa siri ni kweli nilikua naogopaΒ paka lakini nilichokiona mwanzo wala hakuwa paka, sasa nikajiuliza ni mawazo yangu tu auΒ nilichokuwa nimekiona kilikua halisi na hiki tunachokiona ni kiini macho tu.Β
Nilihema mfululizo kama vile moyo ulishusha pumzi na kuamua kurejea kwenye mapigo yaΒ kawaida, basi nilikaa kimya sikusema chochote kile.Β
βUtalala hapa, si ulisema kesho asubuhi unarudi Mbeya?β aliuliza Mzee MwinyimkuuΒ
βEeeh asubuhi narudi ili nijiandae halafu kesho kutwa niende Darβ alijibu Kaka Hamidu,Β akanishika mkono tukarudi sebleni nikiwa kimya. Nilimhurumia sana Kaka Hamidu maanaΒ nilianza kuwa na wasiwasi kuwa Mzee Mwinyimkuu kuna mpango fulani ameupanga dhidiΒ yake. Muda huo huo Mzee Mwinyimkuu akapokea simu halafu akatuacha pale akaelekea njeΒ kuzungumza ikionekana kama kuna Mtu aliyemtarajia alikua amefika nje.Β
Nilipanga kumshawishi Kaka Hamidu asilale ndani ya ile nyumba lakini sikujua naanzia wapiΒ Mimi. Nikiwa natafakari Kaka Hamidu akaniulizaΒ
βHuonekani kuwa sawa Saida, kuna tatizo gani hapa?β aliuliza kama Mtu aliyeanza kuoneshaΒ wasiwasi wa ghafla japo muda wote huo alikua akionesha kutokuwa na wasiwasi kabisa.Β Kwakuwa alionesha kuwa na wasiwasi nikaona ni bora nimueleze ili aokoe uhai wake sababuΒ uhai wa Wazazi wangu ulikua mikononi mwangu.Β
Nilisogea na kupiga magoti mbele yake nikashika na miguu yake huku chozi likinibubujika.Β
βKaka Hamidu, usilale ndani ya hii nyumba na kama utafanya hivyo basi kifo chako kitakuwaΒ karibu zaidi na weweβ nilimwambia chozi likizidi kunibubujika, hata sauti iliyonitokaΒ iliambatana na kilio kisicho na sauti KubwaΒ
βUnamaanisha nini?βΒ
Nikavua soksi na kmwonesha Kaka Hamidu nilivyokatwa kidole ili ayaamini kwa harakaΒ maneno nitakayo mwambia, alishtuka sana.Β
βHuyu Mzee siyo Mtu mzuri Kaka yangu, okoa Maisha yako bado una muda wa kufanya hivyo.Β Hii nyumba imejaa uchawi na mateso makali, hata kile chumba unachoambiwa ulale ni chumbaΒ chenye kaburi ndiyo maana nilishtuka. Ondoka bado una mudaβ Nilimueleza Kaka Hamidu,Β haikuhitaji elimu ya chuo kikuu kujua kua Kaka Hamidu alikua ameshanielewa.Β
Akajawa na taharuki na hasira sababu alikua ananipenda sana na isitoshe hakuna nduguΒ anayeweza kumuacha ndugu yake kwenye shida kiasi kile.Β Β
βSaida siwezi kukuacha hapa, nitamfundisha adabu huyu Mshenziβ akasema Kaka Hamidu,Β kimwili Kaka Hamidu alikua amejazia jazia hivyo kama utamuweka mizani moja na MzeeΒ Mwinyimkuu basi yeye ndiye atazidi. Akanishika mkono kwa nguvu akasemaΒ
βTunaondoka woteβΒ Β
βKaka nenda wewe tu, mimi niache hapa ili Wazazi wangu wawe salamaβ nilisema, sasa KakaΒ Hamidu akaanza kupaza sauti kitu ambacho sikukitaka kabisa. Nilichotaka ni siasa zaidi ili KakaΒ Hamidu aondoke pasipo Mzee Mwinyimkuu kujuwa chochote kile.Β
Mara tukasikia mlango ukifungwa tena siyo kufungwa kawaida ni kule kufungwa kwa kufuriΒ kabisa halafu ni Mlango wa kuingilia nyumba kubwa, Kaka Hamidu akanipa ishara ya kukaaΒ kimya. Alidhamilia kuomdoka na Mimi, nami niliona ni bora niondoke naye kuliko kubaki tenaΒ kwa Mzee MwinyimkuuΒ Β
Akaingia Mzee Mwinyimkuu pale sebleni, alikua amevalia suruali, singlendi na BalaghashiaΒ kama kawaida yake, hakututazama kabisa akalisogelea kabati na kuiweka funguo kwenye drooΒ kwa mbwembwe sana huku akiwa anapiga zake mluzi.Β
Ilikuwa ndiyo nafasi pekee ambayo Kaka Hamidu alikua ameipata, akachukua jagi la kioo lenyeΒ maji kisha akasogea taratibu hadi nyuma kwa Mzee Mwinyimkuu, akampiga na lile jagi kisogoniΒ kwa nguvu hadi Mzee Mwinyimkuu akagugumia kwa maumivu na damu zikaanza kutokaΒ alipopigwa akaanguka chini huku akionekana kutaka kusema jambo lakini alikua akishindwa.Β Β
Kaka Hamidu alikua akimuangalia Mzee Mwinyimkuu alivyokua anatapa tapa, kwa sekundeΒ kadha tu zilitosha kumnyamazisha akawa ametulia tuli pale chini kama maji ya Mtungi, ikawa niΒ nafasi ya dhahabu sana kuondoka ndani ya ile nyumba.Β Β
βTwendeβ akasema kaka Hamidu akiwa amenishikilia mkono kwa nguvu tukawa tunaelekeaΒ mlangoni ili tuondoke. Tulipofika Mlangoni tukapata akili ya ile funguo, ndiyo! Palikua naΒ kufuri mlangoni, funguo aliiweka kwenye droo kule sebleni,.Β
Hapakuwa na ujanja isipokua Kaka Hamidu kurudi sebleni kuchukua funguo, alipofika SebleniΒ hakumuona tena Mzee Mwinyimkuu pale sakafuni wala sebleni kote, ni kama aliyayuka mithiriΒ
ya Barafu juani. Akaniita, nikakimbilia sebleni nami nikawa shuhuda wa kutoweka kwa MzeeΒ Mwinyimkuu, tulitazama kwa mshangao mkubwa.Β
Tusingeweza kurudi nyuma tena, Kaka Hamidu akafungua droo na kuikuta funguo, akaichukuaΒ kisha akaniambia tuondoke. Cha kushangaza ambacho kilitufanya tugande kama Barafu niΒ kuukuta ule mlango tuliohangaika kuchukua funguo ukiwa wazi kabisa, halafu nje tukisikia sautiΒ ya Mtu kama akichakata kuni hivi.Β Β
Sote tukawa na hofu sana, Nani ameufungua ule mlango bila kusikila sauti yoyote? HakunaΒ aliyekua na jibu la moja kwa moja, Kaka Hamidu akaona ni bora apige simu ili aombe msaada,Β alishaona siyo rahisi kuondoka ndani ya ile nyumba ya kutisha, halafu ilikua mishale ya usikuΒ mchanga kama saa 3 hivi lakini matukio yaliyotokea na ukimya uliokuwa umetanda na gizaΒ ilionesha kama vile ni Usiku mnene.Β
Akajipapasa na kukumbuka simu aliiacha Kwenye kochi, kabla hata hajapiga hatua kurudiΒ sebleni, pale pale taa zote zikazima. Pakawa giza tupu hata nuru moja isionekane, pakawa kimyaΒ kabisa, sikumsikia tena Kaka Hamidu isipokua sauti ya kugugumia ambayo aliitoa kwa nguvu,Β papo hapo nikasikia kitu kikianguka kama Mzigo βPuuhβΒ
βAaaaahβΌβ niligumia kwa hofu lakini ghafla nikabanwa mdomo wangu halafu sauti ya MzeeΒ Mwinyimkuu ikagonga ngoma za Masikio yangu, nilishtuka sana.Β Β
βShiiiiiβΌ!β akanitaka nikae kimya. Nilikuwa nahema juu juu, mara papo hapo taa zikawaka.Β Nilichokiona jamani sitakuja kusahau Maisha yangu yote, nilihisi uchizi, nilihisi wendawazimu.Β Mwili ulipoa kama nimemwagiwa maji ya Baridi. Kaka Hamidu alikua sakafuni, damu nzitoΒ ilikua imetapakaa kila mahali.Β Β
Alitenganishwa kichwa na kiwiliwili chake, damu zilikua zinaruka kwenye shingo yake. HataΒ Mzee Mwinyimkuu aliponiachilia sikua na nguvu nilianguka chini nikakalia damu.Β
βNilikuonya hukusikiaβ akasema Mzee Mwinyimkuu, alisema. Mkononi alikua ameshikilia kisuΒ kikubwa chenye damu. Niliishia kudondosha chozi tu, mara akaingia Mwanaume mmoja naΒ kuanza kuuvuta mwili wa Kaka Hamidu kuelekea nje, Mze Mwinyimkuu akakichukua kichwaΒ cha Kaka Hamidu na kukipeleka kwenye kile chumba alichokua amekiandaa kwa ajili ya kulalaΒ Kaka Hamidu.Β
Sijui kilichoendelea baada ya hapo nilijikuta nikizidi kuishiwa nguvu, giza zito likatanda nikahisiΒ usingizi wa ajabu. Nikapoteza uwezo wa kujitambua.Β
**Β
βSaida,Mdogo wangu amka Unisaidieβ ilikua ni sauti ya Kaka Hamidu, alikua amesimamaΒ mbele yangu nikiwa nimekaa kitandani, alikua akivuja damu kila sehemu. Alikua ametisha kiasiΒ kwamba niligugumia hadi nikapaza sauti yangu kwa hofu. Hivyo ndivyo nilivyoamka kutokaΒ Usingizi wa kifoΒ
Nilikua na maumivu makali sana mguuni, ndoto hii mbaya iliniamsha. Eneo lile lile nililokatwaΒ kidole lilikua na maumivu makali sana. Niliusogeza vizuri Mguu wangu na kuangalia kidondaΒ kinaendeleaje, nilipoangalia niliona vidole viwili vikiwa vimeondolewa. Yaani jumla ya vidoleΒ vitatu vinavyofuatana kuanzia cha mwisho vilikuwa havipo.Β
Maumivu yalikua makali, ni bora uyasome kwenye hii hadithi lakini yasikukute, mwili woteΒ ulipandisha homa ya ghafla, kichwa kilikua kinauma sana. Safari hii sikuwa na uhakika kamaΒ ninaweza hata kutembea, eneo lenyewe nililopatia ufahamu sikulijua kabisa.Β
Nilikua sakafuni, chumba kilikua kitupu isipokuwa mimi tu na maumivu yangu. Nilipiga sakafuΒ kwa uchovu nikasemaΒ
βKama uliniumba niteseke hadi nife basi nitakufa na kama huu ni mpango wa shetani basiΒ hawezi kukuzidi maarifaβ nilipomaliza kusema hivi nilijikunyata, Nililia sana. Nilikua tayariΒ nimempoteza Kaka Hamidu na sijui walimpeleka wapiΒ
Eneo lile lilikuwa kimya sana tofauti kabisa na nilivyozoea, sikusikia sauti za Pikipiki walaΒ mazungumzo yoyote yale. Niliona ni bora nilikague eneo lile, nilichungulia dirishani, nililionaΒ Pori la Kubwa, nilishtuka. Nikagundua nilikua nimehamishwa kutoka kwenye nyumba ya MzeeΒ Mwinyimkuu. Nililia sana maana safari hii siwezi kukutana na yeyote yule nikapata msaada,Β Mzee Mwinyimkuu alishagundua kuwa kama ataniacha huru naweza kutoroka, ilifika hatuaΒ nilikua mkali nikajisemeaΒ
βKama kuokoa uhai wangu kutafanya wazazi wangu wafe ni sawa, napaswa kukwepa hayaΒ mateso Makali. Mungu atapigana kwa ajili ya Wazazi wanguβ hayo ndiyo yalikua maamuziΒ yangu.Β
Niliveshwa kaniki pekee halafu nilikua na alama fulani kwenye paja langu, ilikua alama ya ajabuΒ iliyochorwa kwa moto, palikua na maneno ya ajabu. Huu ndiyo wakati mgumu zaidi kuwahiΒ kuupitia katika Maisha yangu yote, haukuwa wakati rahisi kwangu, ulikuwa wakati ambaoΒ nilipoteza tumaini la Maisha yangu lakini sikuweza kufanya chochote isipokua kuuguliaΒ maumivu na kulia.Β
Kilipita kitambo kirefu cha Ukimya, sijui ilikua ni saa ngapi, siku gani au lile eneo ni wapi.Β Nilichojua ni kuwa bado naendelea kupumua, niliusikia Mlio wa pikipiki. Nikajivuta naΒ kuchungulia dirishani, niliiona pikipiki ikiwa imesimama kando kidogo kama mita chache tu hiviΒ kisha Mtu mmoja alisogea mbele kuelekea nyumba niliyopoΒ
Kumbuka hapo ni Porini, tokea nimezinduka sikuwahi kumuona yeyote yule isipokua sauti zaΒ ndege zilizopita kwenye ngoma za masikio yangu yaliyochoka kusikia sauti za kutisha. NilikuaΒ nimekonda ghafla sana Mimi SaidaΒ
Basi, yule Mtu sikuiona sura yake kwa haraka sababu hata nguvu ya kusimama kwa muda mrefuΒ ilianza kuniisha nikajikuta nikianguka chini, maumivu yalikua makubwa halafu nilikua na njaaΒ
sana. Nilisikia tu akifungua mlango ulioonekana kuwa na komeo nyingi, akaingia hadi chumbaΒ nilichopoΒ
Yule Mtu nilimkumbuka kwa haraka sana, alikua ni yule Bodaboda aliyenipeleka sokoni siku ileΒ ambayo nilikutana na Abuu. Nilikua na wenge zito lakini sikuacha kumtazama kwa makini hadiΒ nikamtambua. Alikuwa amebeba chakula kwenye Hot-potΒ
Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.Β
βKunywa Majiβ alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikuaΒ ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuulizaΒ
βMnanimalizia lini nikapumzike?β Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chacheΒ nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambiaΒ
βKifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwajeβ alisema kisha akanipa maji, sikuwaΒ na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe haiΒ
Comments zikiwa nyingi naachia ya NANE leoleo hapa
Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA NANE YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxΒ
16 Comments
Simulizi tamu Sana haichoshi na haiishi hamu kuifuatilia.
Mola mlezi akubariki mwandishi, aturudhuku neema tuzidi kuwa pamoja Hadi tamati.
Leo nitaota haki mwenyew Nina machungu afu nasoma hii story inatishaa
Jamaniii. Huyo dada akimbieee …
Mpka machozii ilaa naaminii Mungu atamfanyiaa njiaa
Dah inasikitish san ππ₯Ί
Duj umeupiga mwingii sanaa admin
Duh….
Simulizi inanitoa machozi jamani ππya Ajabu sana
Sijawahi kusoma hadithi mfano wake.
Maskini Saida.
Vidole vyake nasikia ganzi jamani
Kaka Hamidu kaenda jamani
ππ
Mzee MwinyiMkuu na Salehe wanafaa kuitwa Nguruwe kwa matendo yao.
E Mwenyezi Mungu
Waangamize Wachawi wote Jehannam.
Ameen.
π₯Ίπ₯Ίπ₯π₯ππ
Sehemu ya nane ata leo hadithi inavutia kusoma inasisimua inahuzunishaa pia
Duh hatari sana hii
Inauma sana binadam sis n wabaya sana
Angekua ni mtoto wa 2000 angekua teal amekatwa vidole vyote maana awa wa kizazi iki ni wakaidi balaa
Looh Kisa kinasisimua km nipo ndani yake
i6kjs2