Ilipoishia “Mh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi waΒ Elfu Kumiβ alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumiΒ ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.Β
βUsicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hataΒ beseni zima nakua namaliza mapemaβ Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanishaΒ anachoongea, nikasema
βSawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ilaΒ nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mamaβ nilisema nikiwaΒ nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwaΒ nigeuke . Endelea
SEHEMU YA TATUΒ
Alikua ni Baba Mkwe wangu, Basi yule Mama alipomwona Baba Mkwe akafurahi sanaΒ
βAfadhali nimekuona Bosi wangu, siku hizi ndio mmeamua msiniungishe si ndiyo?β aliyatupaΒ maneno kwa Baba MkweΒ
βAh! Mama mboga mboga huyo, basi fanya kama kawaida. Saida hebu leta beseniβ alisemaΒ Baba Mkwe, nilishangaa sana lakini sikutaka kuonesha chochote. Nikaelekea ndani kishaΒ nikarudi na Beseni.Β Β
Huwezi amini yule Mzee alichukua Mchicha wote na nyanya zote ambazo yule Mama alikuaΒ nazo kwenye beseni, nilihisi kama naota vile maaana mchicha wote ule tule wawili? HalafuΒ akatoa pesa yake mfukoni na kulipia kisha yule Mama akaondoka zake, Yule Mzee akabebaΒ Beseni hadi jikoni halafu akaniambiaΒ
βUnapaswa kupika Mchicha wote, ukimaliza nitakuelekeza cha kufanyaβ Uwiii, nilihisiΒ nachanganikiwa. Msomaji unaweza usinielewe lakini Jaribu kununua Mchicha wa Elfu KumiΒ halafu kaa hapo uuchambue na uupike, nakwambia utamaliza usiku mgongo ukiwa unauma, sasaΒ fikiria tupo wawili tu halafu nipike Mchicha wote ule, haki nilihisi yule Mzee ana mapungufuΒ fulani ndani yake.Β Β
βSawa Babaβ jinsi alivyonitazama ilinifanya niitikie tu na siyo vinginevyo ili nisijeΒ nikamkasirisha tena, halafu kwa madoido alielekea sebleni kuendelea kunywa chai, nilibakiΒ nimejishika kiuno. Beseni la Mchicha naanzaje kuchambua Jamani halafu nipike tule wawili tu,Β sikuwahi kusikia kwa Watu kuhusu visa vya Baba Mkwe mara nyingi nilisikia kuhusu MamaΒ Mkwe ila anachofanya Mzee huyu ni zaidi ya Ukatili.Β
Sikutaka kupoteza muda hata hamu ya Chai iliniishia, nilianza kuchambua Mchicha harakaΒ haraka na uzuri Mungu alinipa Mkono mwepesi sana, hilo hata Mama yangu alikua akilisifiaΒ sana. Hata niwe na kazi kubwa kiasi gani nitaifanya kwa muda mfupi sana, sikutaka hataΒ kunyanyua simu na kumpigia Mume wangu Salehe kumweleza anayonifanyia Baba yake sababuΒ sikutaka kuwagombanisha.Β
Tokea saa Nne asubuhi nilimaliza Kuchambua saa kumi kasoro nikiwa nimechoka na hapo badoΒ sijapika, halafu Baba Mkwe alikua akija kunikagua jikoni kama nimemaliza au vipi hukuΒ akinitaka kifanya haraka kupika. Nilijaribu kumwambia kua nimpikie yeye cha Mchana kidogoΒ ili apoze njaa huku mimi nikiwa naandaa huo Mchicha wa Elfu Kumi.Β
Baada ya kumaliza alinionesha sufuria kubwa ambalo hupikiwa kwenye mashuhuli ili nipikieΒ humo, halafu akaniambia
βUkimaliza kupika usiipue sufuria hadi niwepoβ Unafikiri aliongea kimzaa? Hapana alinikaziaΒ sura yake mbayaΒ
βSawa Babaβ nilimjibu kwa sauti ya chini iliyojaa hofu kubwa, sikutaka kupoteza muda nilianzaΒ kuupika ule mchicha mwingi huku nikitamani kucheka na kulia kwa wakati Mmoja, ni vileΒ niliambiwa mambo ya kwenye ndoa ni siri ya ndoa siyo vizuri kuyatoa nje ila nilitamani nipigeΒ picha niwatumie rafiki zangu waone kichekesho nilichokutana nacho Rukwa.Β
Nilipiga moyo konde nikawa napika hadi ulipoiva, nilihakikisha chumvi iko sawa kishaΒ nilimwita Baba Mkwe ili kabla sijaondoa sufuria jikoni aone. Alipofika aliniambiaΒ
βTia hiiβ alinipa karatasi yenye Unga mweusi ninyunyize kwenye mchicha, sikusita nilifanyaΒ hivyo halafu akaniambia baada ya dakika Kumi epua kisha acha upoe halafu kapumzike.Β Alisema akiwa anatabasamu hadi nikajiulizaΒ Β
βHuyu Mzee ni Mzima kweli, sekunde kumi ananuna sekunde kumi anachekaβ Sikummaliza,Β nilimtazama hadi alipozama chumbani kwake. Basi nilipomaliza niliepua kisha nilifanya kamaΒ alivyonielekeza kisha nikaenda zangu chumbani kulala maana nilikua nimechoka sana yaani hataΒ njaa iliacha kuuma.Β
**Β
Niliamka kama saa moja na Nusu hivi Usiku, kitu cha kwanza kilikua kuangalia simu yanguΒ kama Mume wangu amenitafuta. Hapakua na ujumbe wala Missed Call yake, nikajaribuΒ kumpigia lakini nikaambiwa simu yake haipatikani niache Ujumbe wa Sauti, nikaitupa simuΒ pembeni kisha nikausikilizia mwili wangu namna unavyowaka moto kwa maumivuΒ
Pale pale nikaanza kujisikia hali ya kutapika, nikaelekea Bafuni nikatapika vitu vya Kijani mfanoΒ wa mlenda hivi. Baada ya kutapika nilianza kujisikia vizuri kiasi, nikahisi huwenda labdaΒ nilibadili mazingira. Sasa wakati namalizia kunawa mdomoni nikaona kitu kama hirizi nyekunduΒ imeangukia chini, nilishtuka sana maana siku zote hirizi ni ishara ya Uchawi.Β
Nusura nipige kelele lakini nilijizuia, nikafikiria nifanyaje nimwambie yule Mzee lakiniΒ nikahofia anaweza sema mimi Mchawi, pia nikafikiria nimuulize Mume wangu Salehe atakapoΒ rudi ila nikahisi hivyo hivyo, sikujua nifanye nini na ile hirizi. Nikaisukuma kwa mguu naΒ kuisweka nyuma ya bomba mahali ambapo siyo rahisi kwa Mtu yeyte kujua kuwa kuna hirizi iliΒ nione ni ya Nani na kwanini ipo Bafuni.Β
Kama ni ya Mume wangu basi ataitafuta na kama ni ya yule Mtu niliyefanya naye mapenziΒ Usiku halafu akatoweka katika mazingira ya kutatanisha ni lazima atarudi tena, nilijiona kamaΒ askari aliye vitani.Β
Muda huo njaa ilianza kuniuma, nikaiwaza chai yangu jikoni, basi nikavaa dera na kuelekeaΒ jikoni. Hapo giza lilikua tayari limeingia, nilitafuta zile chapati lakini sikuziona popote paleΒ nikahisi huwenda Baba Mkwe alizichukua na kuzila. Nikawaza nipike ili nile, lakini nikapataΒ
wazo la kumuuliza Baba Mkwe atakula nini, nilimuita sana lakini hakuitika, nikamtazama koteΒ bila mafanikio yoyote yaleΒ
Wakati wazo la kwamba atakua ametoka liliponijia ndipo nilipoanza kusikia sauti fulani ya ajabuΒ sana ikitokea chumba kimoja kilicho katikati, kama vile palikua na mnyama anayekula nyamaΒ ndani ya hicho chumba.Β Β
Sauti ya kuunguruma kabisa kama vile simba anakula nyama, nilishtuka sana halafu mapigo yaΒ moyo yakaanza kunienda mbio huku nikiwa ninatetemeka, nilijiuliza ni nini kinaendelea ndaniΒ ya nyumba ya Mume wangu Salehe maana tokea nimefika ni mauzauza tu, shahuku ya kutakaΒ kujuwa kuna nini ilinianza.Β
Palikua kimya hapakuwa na dalili ya Mtu yeyote kuingia ndani isipokua sauti ya ajabu yaΒ kutafuna na kuunguruma humo ndani, pumzi za nguvu zilinitoka huku kifua changu kikipataΒ shida ya kuzisukuma pumzi hizo zilizojaa hofu sana. Nikapata wazo jipya la kuchungulia badalaΒ ya kuufungua mlango huo, basi nilimwomba Mungu kwanza kabla ya kulianza zoezi hilo.Β Β
Taratibu nilipeleka jicho langu kubwa kwenye tundu la kitasa cha Mlango, ile sauti badoΒ ilikuwamo lakini kilichonishtua ni kuliona lile sufuria la Mchicha likiwa tupu ndani ya kileΒ chumba. WeeeβΌ nilishtuka hadi nikaacha kuchungulia, kimbelembele chote kiliniisha harakaΒ sana.Β
Nikanyanyua miguu yangu kuelekea jikoni kuangalia kama lile sufuria lipo, nilipofika sikulionaΒ hivyo nikawa na Uhakika kabisa kuwa Sufuria lipo ndani ya kile chumba, lakini limeendaΒ kufanya nini na ule Mchicha unaliwa na Nani, ile sauti ni ya Nani?Β Β
Sikupata jibu lolote lile, hofu ilizidi kunizonga huku mwili ukiniisha nguvu, nikakimbiliaΒ chumbani ili nimpigie simu Salehe. Kiukweli woga mkubwa ulioambatana na kukosa nguvuΒ ulinishika sana, niliichukua simu haraka sana na kumpigia Salehe huku nikiomba simuΒ ipokelewe. Bahati nzuri safari hii simu ya Mume wangu iliitaΒ
βSalehe Pokea simu tafadhaliβ nilisema huku sauti ikinijia ya kutaka kulia, kabla hataΒ haijapokelewa mara mlango ulianza kugongwa. Huo mshituko nilioupata ulinifanya nidondosheΒ simu yangu ikaangukia chini na kupasuka kioo kabisa. Sikujali kuhusu simu nilijali kuhusu niΒ Nani anaugonga mlango wa chumba changu.Β
βSaidaβ niliisikia sauti ya Baba Mkwe wangu, jinsi nilivyokua namwogopa yule nilizidiΒ kutetemeka, akaita mara ya pili na tatu huku akizidi kukaza sauti yake ikabidi niitike kama MtuΒ aliyeamshwa UsingiziniΒ
βNjooβ alisema halafu nikasikia kama kaondoka pale mlangoni, nilishusha pumzi nzitoΒ sana,pumzi ambayo kama pangelikua na karatasi basi ingelipeperukia mbali kutokana naΒ mshindo wa pumzi yangu. Nikaiokota simu, cha ajabu ni kuwa muda wote Salehe alikua anaitikaΒ
ile simu yaani alikua akiongea na kuniuliza mbona siongei, wakati naiweka sikioni akakata simu.Β Nikajaribu kumpigia lakini bahati mbaya nyingine simu ilikua haina uwezo wa kugusika naΒ kufanya kazi zaidi ya kuiangalia tu.Β
Nusura chozi linibubujike lakini sikuacha kujipa moyo, nikajikaza ili Yule Mzee asigundue chochote kuhusu Mimi, papo hapo nikaelekea kufungua mlango huku nikiigiza kanakwambaΒ ndiyo nimetoka kuamka, sikujua yule Mzee ananiita wapi ikabidi Mimi ndiyo niite ili nijuweΒ alipo. Ulikua usiku mgumu sana kwanguβ¦β¦TuendeleeeeβΌΒ
βNjooβ aliniita baada ya kusikia sauti yangu, aliniita kwenye chumba kile kile ambacho nilisikiaΒ sauti ya ajabu na kuona lile sufuria la Mchicha.Β Β
Taratibu na kwa hofu niliufungua mlango huku nikimwomba Mungu nisikutane na chochoteΒ kibaya. Nilipofika nilimkuta akiwa amesimama. Chumba kilikua na sufuria chini lakiniΒ nilipoingia niliusikia mwili wangu ukiwa unasisimka sana kitu ambacho kilinifanya nihisiΒ hapakuwa sehemu salamaΒ
βAbeehβΌβΒ
βOndoa halafu ujeβ aliongea kwa sauti kavu, huku kidole chake akikionesha kuelekea kwenyeΒ sufuri lililo tupu halafu funiko lake likiwa pembeni, chini palikua na chembe chembe za MchichaΒ kama vile kuna waliokuwa wanakula kwa Pupa sana, niliinama haraka ili nitoke pale chumbani.Β Nilitoka haraka hadi nikajigonga mlangoni lakini sikusikia maumivu yoyote yale. NilipofikaΒ Jikoni nilijikuta chozi likinitoka, nilitamani kumpigia simu Mama niweze kuondoka maanaΒ niliona yule Mzee alikua na mambo yasiyoeleweka, Mume wangu naye sikujua kwaniniΒ aliniacha na Baba yake.Β
Nilijikaza kikike hadi nikarudi tena chumbani mle na kufanya usafi kisha yule Mzee akaniambiaΒ
βHalafu ujeβ nilihisi nitakuwa nimemaliza kumbe ndiyo kwanza alinihitaji tena, kibaya zaidiΒ alikua amevalia msuli mwekundu na Singlendi nyeupe iliyochanika, juu alikua na balaghashiaΒ nyeusi ndogo.Β
βSawa Babaβ nilisema kisha nilienda kuweka ule uchafu kwenye mfuko wa taka jikoni, moyoΒ uliniuma sana. Siku ya pili ya ndoa yangu lakini sikuwahi kujuwa maana ya hiyo ndoa ni nini.Β Basi, nilirudi ndani ya kile chumba, yule Mzee akaniambiaΒ
βUlikumbuka kuja na gauni ulilofungia ndoa?β ilinichukua sekunde kadhaa kulijibu swali hiliΒ maana sikujua anamaanisha nini.Β Β
βNdiyoβ¦βΌβΒ
βKalivae uje, kuna mila za kwetu kwa Mwanamke aliyeolewaβ alisema yule Mzee, niliitikia kwaΒ kichwa safari hii, halafu niliondoka taratibu hadi chumbani kwangu. Maswali hayakuisha.Β Nikaufunga kwanza mlango kisha nikajaribu kuwasha ile simu nione kama itafanya kaziΒ niwapigie wazazi wangu. Nilihitaji msaada zaidi na moyo wangu uliniambia hivyo
Simu iliwaka lakini haikukubali kubinyika , lakini muda huo huo simu iliita. Salehe alikuaΒ akinipigia, nilihangaika kuipokea lakini haikukubali hadi ilipokata, mara baada ya kukata simuΒ ukaingia ujumbe, niliweza kuusoma kidogo sana lakini haukumalizika sababu simu ilikuaΒ imelockΒ
βSaida nisamehe Mimi, yote ni Makosa yangu. Baba yanguβ¦β Ujumbe uliishia hivyo, sikuelewaΒ alitaka kusema nini kuhusu Baba yake. Nikiwa natafakari mara mlango uligongwa na sauti yaΒ yuke Mzee niliisikia ikisema βNakusubiri wewe muda unaenda huuβΒ Β
βNakuja Baba namaliziaβ nilisema kwa sauti isiyo na shaka kwake halafu nikaitafuta ile gauni,Β sikuwa na budi bali kuivaa tu ili nione atasema nini yule Mzee. Nilipata hisia mbaya dhidi yake. Nilivalia lile gauni haraka haraka kisha niliificha simu yangu ndani ya gauni, sijui kwaniniΒ nililipata wazo hili la kwenda na simu japo haifanyi kazi.Β
Nilipoingia ndani ya kile chumba, Baba Mkwe aliniambiaΒ Β
βKaa katikati ya Chumba kisha jifunike huo mtandio hadi nitakaposema ujifunueβ wakatiΒ anasema alikua akiwasha udi, nikaikumbuka harufu ya Udi. Niliusikia kwa mara ya kwanza sikuΒ ya kwanza naamka ndani ya nyumba hiiΒ
Hakuishia hapo akaweka Udi ule kila pembe ya chumba kisha akaufunga mlango wa chumba naΒ kunikumbushaΒ
βnimekwambia ujifunike huo mtandio na ubugaze macho yako hadi pale nitakapokueleza niniΒ cha Kufanyaβ alisema kwa mkazo kidogo, kwakuwa tayari nilikua na woga basi nikafanya hivyoΒ mara moja. Zikapita dakika kadhaa pakiwa kimya kisha dakika iliyofwata akaniambiaΒ
βOndoa mtandio na ufumbue macho yakoβ aliposema hivyo nilipata hisia ya kuwa kuna jamboΒ nitaliona ndio sababu ya kunitaka niyafumbe macho yangu. Mwili ulizidi kusisimka Jamani..Β
Nilipofunbua macho sasa nilitamani nikimbie lakini haikuwezekana, nilitamani nife lakiniΒ wakati ulikua haujafika, nikatamani ardhi ipasuke niingie lakini hiyo siyo rahisi na mwishoΒ nilitamni ingelikua ndoto niamke nikaendelee na shughuli zangu. Ilikua ni kweli nilizungungwaΒ na Wanaume walio Uchi wa Mnyama, wanaume hao walikua wamepaka vitu kama ungaΒ mweupe usoni na mwili mzima halafu walikua wameinamisha vichwa vyaoΒ
Nilikua natetemeka kwa hofu huku sura yangu ikizidi kuwa yenye kutaka kulia, Baba MkweΒ alikua ameshikilia kisu mkononi akinitazama kwa jicho kali. Yaani jinsi walivyonizungukaΒ wakiwa wamekaa ilinizuia kurudi nyuma wala kwenda mbele bali kutetemeka tu. SijawahiΒ kupata woga kama ambao niliupata siku hii, moyo ulidunda kwa mapigo ya juu sana kiasiΒ kwamba niliyasikia mapigo kama vile mdundo wa Muziki kwenye redio kubwa (Sabufa).Β
βShiiiβΌβ Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisuΒ kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia
βLeo utajuwa ni kwanini uliolewa Bintiβ Alisema halafu akayaongea maneno fulaniΒ nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lughaΒ nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaendaΒ kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi.Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNE YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
14 Comments
Admin kunywa soda naja kulipa
Hii ni hatari
Mambo ni moTo
Duh kah naona vile
Round hii hatapata hata sare Maana Tumeanza Na plan Bπ₯π
Jamani Saida π°
Apo kwenye MISUKULE ningekufa kabisa
Watu Wachawi dunia hii.
Mungu anidumishe kwenye Maombi jamani niolewe na Mtu ninae mjuπSio kwa Misuko suko hii
Amen
Duh mbona kama iih kali sna kuliko zote
Wanao fatilia muvis ΕΊa kibongo kibongo iih imataka kufnana na ile ya famili ya mzee kicheche sema adimini una baya
MUNGU wng . Hukumbuki ht kuswali jmn . Taja ht jina la YESU tu mbona wangesambaratika wote na hapo ungejua mume ni yupi
Haka kazee ndo maana kaliwaka Ile siku Saida anampokelea mkoba kupeleka ndani
Au labda ao watu ndo walikua wanapokezana kumtoa bikra Ile usiku
Mhh wame potelea kwenye kona bana mhh
π€π€π€π€
Ni noma wote wanataka wale mali hap