Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (01)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (01)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJanuary 3, 2025Updated:January 6, 202522 Comments10 Mins Read9K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Sijui kwako ndoa ina maana gani lakini kwangu Mimi ndoa ilinipotezea Muda wangu, iliniacha na  Maumivu na kilema cha Maisha yangu. 

    Sikuwahi kuwaza chochote kuhusu ndoa wala kuitamani, lakini siku moja nilikua natoka sokoni  Mabibo naelekea nyumbani Magomeni Usalama, niliposhuka kwenye daladala kwa bahati  mbaya niliteleza na kuanguka wakati navuka barabara. Mfuko wenye vitu nilivyonunua sokoni  uliangukia pembeni. 

    Nilihisi aibu sana siku ile na kibaya zaidi mvua ilikua imenyesha majira ya asubuhi, lilijaa tope  lililoniharibia Baibui langu. Eneo nililoangukia palikua na kijiwe cha Bodaboda. Kama  uwajuavyo walianza kushangilia anguko langu kitu kilichozidi kunipa hasira lakini sikuwa na la  kufanya zaidi ya kujiokotanisha pale. 

    “Pole sana Dada” niliisikia sauti hii nikiwa nasimama, aliyenipa pole alinipatia na mfuko wangu  akiwa ameokotanisha vitu vyangu. Alikua kijana mzuri mtanashati sana, nilijikuta nikiwa na  kigugumizi kumjibu 

    “Unaelekea wapi?”  

    “Nyuma ya sheli, usijali” nilisema nikiwa najipangusa tope kutoka kwenye Baibui langu jeusi,  akanipa mkono wake 

    “Naitwa Salehe Mwinyimkuu” Alijitambulisha kwangu, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha  nilimjibu 

    “Naitwa Saida” 

    “Nimefurahi kukufahamu, wacha nikusogeze” alisema, kwa msaada alionipa isingelikuwa hisani  kukataa alichokiomba. Taratibu tuliikanyaga ardhi kuelekea karibu na nyumbani kwetu. Kwa  muda mchache nilihisi kumjua kidogo, niligundua ni mpole, mwemye hekima na busara tele  licha ya kuniambia ana Miaka 27 tu. 

    “Mimi nina Miaka 23” nilijitanbulisha kwake huku nikianza kunogewa na mazungumzo yake.  Tuliongea mengi hadi kubadilishana namba za simu kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwa Mtu  nisiyemjua.

    Tulizidi kuwasiliana kwa zaidi ya mwezi mzima huku tukiwa marafiki wa kawaida tu lakini  baadaye Salehe alinitongoza.  

    Nisiwe mwongo wala mnafiki hata kabla ya kunitongoza nilianza kumpenda hivyo kunitongoza  alikua anatimiza wajibu wake kama Mwanaume kwani nisingeliweza kumwambia Nampenda  isitoshe Mimi nilikua Bikra kwa wakati ule.  

    Tulianza mahusiano ya Kimapenzi lakini nilimwambia Salehe kuwa Mimi nimelelewa kwenye  familia ya Dini sana, Baba yangu ni msaidizi wa Shekh Mkuu wa Msikiti wa Magomeni hivyo  kama ananipenda kweli basi awaone wazazi wangu kwanza. Sijui tuseme alikua na kiu sana au  alikua anahitaji Mke sana maana alilifanya hilo siku tatu tu baada ya kumwambia 

    Baba yangu alifurahi sana, Mama pia alifurahi zaidi akaniambia 

    “Mwanangu ndoa ni Nusu ya Dini, sisi Wazazi wako tunakutakia kila lililo jema, Mungu  akuongoze” Daima Mama yangu alikua Mtu wa karibu sana kwangu, alisimama na Mimi  kwenye kila jambo hata ambalo Baba yangu alipingana na Mimi. 

    Salehe hakutaka kuchelewesha alilipa Mahali siku iliyofuata. 

    “Wewe Kijana ni Mtu wa wapi?” Baba alimuuliza Salehe wakiwa katika mazungumzo ya  kawaida, kama Mzazi ni lazima ahakikishe usalama wa Binti yake 

    “Kwetu Rukwa lakini nipo Hapa Dar Likizo” alisema Salehe 

    “Ooh! Unajishughulisha na nini?” 

    “Nimeajiliwa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Rukwa Mjini” 

    “Utamtunza Binti yangu?” 

    Kwanza Salehe alicheka kidogo kisha akamwambia Baba 

    “Nisipomtunza Mke wangu nitamtunza Nani, wanasema Mbuzi unayemlisha ndiye utakaye mkamua maziwa” Basi Baba na Salehe wakaishia kuangua vicheko, ilileta raha sana.  

    ** 

    Ndugu wa Salehe walifika tena waliazimia kuwa ndoa ipite kabla likizo ya Salehe haijaisha ili  tuondoke wote kuelekea Rukwa, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitaolewa na kwenda mbali  kama Rukwa. Kidogo nilipata huzuni, nilimzoea Mama yangu 

    “Usijali, hata Mimi niliwaacha Wazazi wangu Morogoro nikaja kuishi na Baba yako Saida. Umri  ukifika hakuna la kukuzuia kuanzisha Familia yako” Mama yangu hakuacha kunitia Moyo. Baba  aliachia tabasamu maana tulikuwa wote sebleni

    “Ngoja niwaache muongee maongezi yenu ya kike” alisema Baba akaelekea zake Msikitini,  zilipita siku kadhaa hadi siku ya ndoa ilipowadia. Ndoa ilipita salama, Siku ya pili tulianza safari  ya kuelekea Rukwa Mimi na Mume wangu Salehe.  

    Bado nilikua Bikra wala hakunigusa usiku wa kwanza wa ndoa yetu hotelini kabla ya Kuanza  safari, kwakua nami nikikua mgeni wala sikudai chochote kile. Tulifika Rukwa Usiku sana tena  nikiwa ninasinzia, tulichukua Taxi hadi nyumbani kwa Salehe 

    “Karibu nyumbani Mke wangu, jisikie uko nyumbani kabisa na hapa ndipo tutakapoishi” alisema  tukiwa tunashuka kwenye taxi, tulisimama mbele ya nyumba moja iliyo giza sana, sikushangaa  sababu mwenye nyumba hakuwepo kwa muda mrefu. Nilijiegemeza kwenye bega la Salehe  nikamwambia 

    “Mume wangu, ulipo nipo na nitaendelea kuwepo siku zote” lile Taxi liliondoka, kazi ya  kuhamishia mabegi ndani ilianza. Salehe alikua ametangulia nami nilibakia nyuma nikikokota  begi. Sijui ni mawazo yangu au nilisikia kitu halisi kabisa, nilisikia sauti za Watoto wakiomba  Msaada 

    “Subhannah‼” nilishtuka, sikuisikia tena ile sauti maana mwanzo ilitokea ndani ya ile nyumba  ambayo tulikua tukielekea. Mapigo ya moyo yalinienda mbio, niliposikiliza vizuri wala  sikuzisikia tena nikajua ni fikra zangu tu. Basi niliendeelea kuvuta begi hadi ndani, taa  zikawashwa 

    Palikua kimya sana, uzuri sikua na njaa wala hamu ya kula zaidi ya Kulala kutokana na Uchovu  wa safari. Nilisimama kusuburia Salehe anioneshe chumba chetu, akaufunga mlango kisha  akaniongoza hadi chumbani, nilipofika nilijitupa Kitandani na kujilaza kama pono bila kujali  kuwa kitandani palikua vumbi tupu. 

    Nililala Usingizi wa nusu kifo hadi mapambazuko, sauti ya jogoo kuwika niliisikia ikiniamsha na  kuniambia ni muda muafaka wa kuanza majukumu ya nyumbani. Macho yalijawa na Ukungu  usio kifani, nilijinyoosha kama Kinda la ndege halafu nikajikuta nikipigwa na Butwaa zito sana  ambalo kiukweli nilishangazwa mno na nilichokiona 

    “Nipo wapi hapa?” Nilijiuliza swali hili, niliipapasa akili yangu inikumbushe jambo lakini  haikua tayari kufanya hivyo, Salehe hakuwepo Kitandani. Moyo ulinienda hali Jojo,  nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani. 

    Nitakueleza kwanini nilipigwa na Butwaa la ajabu, kwanza harufu ya Udi wenye harufu mbaya  ilizagaa kote ndani, pili nilisikia sauti ya Mtu akitwanga na kwa hakika alikua akitwangia ndani  halafu sauti ya Mtoto Mchanga anayelia nilizidi kuisikia. Taratibu nilitaka kujuwa nipo wapi  haswa maana tayari nilianza kupata hofu fulani 

    Nilipiga hatua za taratibu hadi mlango wa kutokea chumbani, ile sauti ilitoweka na palikua  kimya sana. Moyo wangu haukutulia kabisa licha ya ukimya wa ghafla niliousikia, jua lilikua  tayari limeshatoka

    Nyumba ilikua safi sana. Ilikua na korido ndefu yenye vyumba kadhaa japo kwa wakati huo  sikuhesabu kutokana na hali niliyokua nikiihisi. Basi Mimi Saida nilijiuliza 

    “Ah ni mawazo gani haya Jamani, Ewee Allah niepushie Mbali” nilisema kisha nilirudi  Chumbani kutafuta simu yangu nimpigie Salehe aniambie alipo si unajua maisha ya Ugeni yanavyoanza. Nilikumbuka mara ya mwisho simu niliiweka kwenye mkoba wangu 

    Sikuwa na shaka sana kuhusu simu yangu, niliikuta lakini kwa bahati mbaya ilikua imeisha chaji.  Niliketi kitandani nikiwaza mambo kadhaa lakini niliona ni bora niweke simu chaji niwasiliane  na Salehe 

    Nilipomaliza kuweka chaji na kuhakikisha simu yangu inaingia chaji nilipata nafasi ya  kukiangalia kwa uzuri chumba, kilipangwa vizuri sana hadi nilijikuta nikitabasamu, nilijuwa ni  Mume wangu Salehe alikua ameamka mapema na kuweka mazingira sawa. Nilijiona ni mwenye  Bahati sana kuitwa Mke wa Salehe, nilikua na nguo zangu zilezile nilizokuja nazo hivyo wazo la  kubadilisha nguo lilinijia lakini kabla ya kufanya hivyo nilisikia Mlango wa nje ukigongwa. 

    Sikujua naanzia wapi kuitikia wito huo, nilisogea hadi mlango wa chumba na kusikiliza vizuri.  Mgongaji wa mlango alikua ni Mwanamke na sauti yake ilikua karibu sana hivyo kwa haraka  niliamini anagonga mlango wa Nyumba ya Salehe. Hakuna aliyeitikia ile hodi hadi pale  nilipoamuwa kumkaribisha nikiwa ndani tena kwa sauti ambayo aliisikia vizuri, nilijiangalia  kama nilikua nipo sawa kutoka ndani kisha nilianza safari mara moja kutembea kwenye korido  kuuelekea Mlangoni. 

    Niliufungua mlango wa kwanza kwa kutekenya kitasa tu kisha nikauelekea mlango wa Uwani  ambao ndio mgongaji alikua hapo, nilipoufungua nilikutana na Mama Mmoja aliyebeba tenga la  mboga mboga kichwani, alikua ameshakata tamaa alikua akiondoka nikamwita 

    “Mamaaa‼” alipogeuka alirudi hadi Mlangoni 

    “Shikamoo Mama” nilimsalimia kwa adabu, ndivyo nilivyofundishwa kwetu kwa wazazi wangu,  yule Mama alitabasamu kisha akaniuliza 

    “Hauchukui Mboga leo?” Nilitabasamu maana aliuliza kana kwamba alishawahi kuniuzia mboga  ila nilielewa Lugha ya Kibiashara huwa hivyo mara zote 

    “Mimi ni mgeni hapa Mama, labda kesho nikiwa nimeyafahamu vizuri mazingira naweza  kuchukua. Usiache kupitisha” nilisema kisha yule Mama aliondoka huku akiitikia 

    “Napita kila siku Mtaa huu, Wahiiii mboga mboga” alienda mbele zaidi kisha alitokomea  machoni pangu. Kuzungumza na yule Mama ni kama kulinisahaulisha kuhusu Salehe lakini  alipoondoka nilijiuliza 

    “Salehe ameenda wapi mbona hajaniaga?” Niliufunga mlango kisha nilirudi ndani, Nyumba  ilikua kubwa ya Kisasa lakini ilikua kimya sana sikusikia hata sauti ya ndege kuruka. Uwani 

    palikua na sehemu ya kukaa nikaona ni bora nikae hapo kwanza nipate upepo, nilijikuta  nikipitiwa na Usingizi wa ghafla tu. 

    Ndoto za hapa na pale zilinifuata usingizini na kunipa hekaheka hadi nikashtuka. Niliposhtuka  nilikutana na sura mbili, moja ilikua ya Salehe na nyingine ni ya Mzee mmoja mweusi aliyevalia  Baraghashia nyeupe na kanzu nyeupe. Macho yao yalikua kwangu 

    “Eeeh imekuaje umelala hapo Mke wangu?” aliniuliza Salehe, nilijitabasamisha kidogo kama  Mtu anayezuga ili asinione kuwa mvivu  

    “Hewa ya hapa inavutia, kaupepo nikajikuta nasinzia tu” 

    “Sawa, huyu ni Baba yangu anaitwa Mzee MwinyiMkuu. Ni Baba yangu Mzazi” alisema Salehe,  nilimsalimia yule Mzee kwa heshima sana hata naye alifurahia na kuona ni namna gani nina  heshima. 

    “Marhaba Mkwe wangu mzuri, hakika Mwanangu hakukosea’’ akasema kwa Utani tukajikuta  tukicheka kidogo 

    “Samahani, najua umenitafuta ila nilienda kumpokea Baba maana aliniambia nikirudi tu atakuja  kwa ajili ya kukusalimia wewe Mke wangu” alijielezea Salehe, ni kweli Mzee MwinyiMkuu alikuja na begi dogo la Mgongoni lililochakaa sana.  

    “Aaaah! Nimefurahi sana kumuona Baba yako Salehe, karibu Baba.” Nilisema kisha nilisimama  na kulishika begi la Mzee MwinyiMkuu ambalo lilikua sakafuni, kabla sijaliinua yule Mzee  alinishika mkono kwa nguvu sana hadi nilishtuka, nikamtazama Usoni alikua amenikazia sura  yake  

    “Hili begi halishikwi na kila Mtu, Salehe unajua pa kulipeleka” alisema Mzee MwinyiMkuu,  nilihemwa maana sikutegemea lakini hata kama ningelichukua ningelipeleka wapi wakati na  Mimi ni Mgeni pale. Nilishusha pumzi, kilinishuka nikarudi kukaa, Salehe akaniambia 

    “Mzoee Baba yangu ana utani sana Saida, wacha nikaweke begi lake nakuja” Mara moja  alipomaliza kusema alinyanyuka Salehe na kuelekea ndani, yule Mzee hakuacha kunitazama kwa  jicho kali kama vile kuna kitu nimeharibu hadi nilianza kumwogopa, ikanilazimu kumwomba  Msamaha 

    “Samahani Baba sikujua” 

    “Siku nyingine uwe unauliza, umeelewa?” 

    “Ndiyo Baba” Nilipomjibu alinikata jicho fulani la husda kisha akatoa mguno fulani wa kicheko  cha dhihaka halafu akanyanyuka na kuiburuza kanzu yake akaingia zake ndani,nilishusha pumzi  zote kama Mgonjwa wa Pumu. Niliusikia moyo wangu namna ulivyoamka nakuanza kudunda  tena, hata koo ilianza kupitisha mate kwa kasi. Yaani sijui nikueleze vipi unielewe namna  nilivyokua nimeshikwa na woga kupitiliza, sura ya yule Mzee niliyona imekaa kikatili sana

    Wakati naendelea kujiuliza mara Mume wanu Salehe alirudi kutoka ndani, akaketi mahali  alipokua ameketi Baba yake 

    “Baba yako ni Mkali sana Salehe hadi nimeogopa. Nimefanya kipi kibaya, kumsaidia Begi ni  vibaya eti?” Nilimuuliza Mume wangu, yeye akanishika bega akaniambia 

    “Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo  kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa  hapa.  

    “Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?” 

    “Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na  Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe  akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku  dimpozi zangu zikionekana  

    Comments ziwe nyingi apa LEO kwa Kaka Mkubwa

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILI YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    22 Comments

    1. Massay on January 3, 2025 2:10 pm

      Heri ya Mwaka Mpya 2025
      Riwaya nzuri sana, Asante sana kwa utunzi mzuri ubarikiwe

      Reply
      • Shabani matimba on January 3, 2025 2:48 pm

        Unyama uendelee

        Reply
      • Hamisa Joseph on January 4, 2025 10:02 am

        Japo jasusi hamkuimalizia

        Reply
    2. Hope on January 3, 2025 2:16 pm

      Hii balaa 🔥🔥mwanzo tu linaonekana big up kaka mkubwa

      Reply
    3. Salkhan on January 3, 2025 2:17 pm

      Uhakika ni hatariii mwendelezo please

      Reply
      • HAJI RAMADHAN KISENDI on January 3, 2025 6:32 pm

        Iko poa xna

        Reply
    4. Fawziya Hassan on January 3, 2025 2:22 pm

      MAUZA UZA
      Saida kaolewa na Msukule😁
      Baba mkwe Msukule
      Asante Admin ❤️ baada ya kimya kirefu saivi tunaburudika tena na
      KAKA MAKUBWA more Love from Zanzibar ❤️❤️

      Reply
      • Fawziya Hassan on January 3, 2025 3:59 pm

        Kaka MKUBWA ❤️❤️❤️

        Reply
      • Amani shonde on January 3, 2025 9:10 pm

        Duuuh kitu usicho kujua ni sawasawa na usiku wa giza

        Reply
    5. Charz jr😎 on January 3, 2025 2:22 pm

      🏃‍♂️🏃🏃kumeanza kuchangamkaa

      Reply
    6. Ahmed on January 3, 2025 2:58 pm

      Atajua ajui ngoja mda wa kwenda kulima usiku ufike ,kwenye begi bado ajasemaaaa

      Reply
    7. Allen on January 3, 2025 3:27 pm

      Eeh hapoo uhakikaa kaka mkubwa ongeza kitu

      Reply
      • Sharo love malkx 💖 on January 6, 2025 10:37 am

        Familia ya kichawi iyo
        Mhh

        Reply
    8. Abdalaman on January 3, 2025 8:08 pm

      [email protected]

      Reply
    9. Halinga1 on January 3, 2025 9:34 pm

      Umetisha

      Reply
    10. Calvin paul on January 3, 2025 10:37 pm

      Ulituacha mbali kidogo tungesahau

      Reply
    11. mwanah on January 4, 2025 12:57 am

      Ubaya ubwela

      Reply
    12. Sharo love malkx 💖 on January 6, 2025 10:35 am

      Familia ya kichawi iyo
      Mhh

      Reply
    13. Mahdiya on January 6, 2025 1:15 pm

      Ya pili please

      Reply
    14. Michaelkhan on January 7, 2025 10:17 am

      Aisee Mwanzo Ni wamoto ,Pameanza na Mushkeli😃

      Reply
    15. Doricas semu on January 11, 2025 4:47 pm

      Riwaya nzuri jaman nmechelewa kuianza

      Reply
    16. Dickson on January 13, 2025 6:53 pm

      Nice

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.