Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mungu Amenisahau Sehemu Ya Sita (06)
    Hadithi

    Mungu Amenisahau Sehemu Ya Sita (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 1, 2024Updated:October 2, 202411 Comments10 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mungu Amenisahau
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko,  kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada ya  kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayo  Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwa  kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza unga  pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadi  hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20  kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutuliza  kiu yangu. 

    “Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlango  ukifunguliwa 

    “‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisi  ili kusiwe na maswali. Endelea 

    SEHEMU YA SITA

    “Haya namalizia kupika kikiwa tayari nitakuja kukuita”  alisema Mama Nesha kwa sauti ya mbali akiwa Jikoni nami  nilimjibu 

    “Sawa Mama” Basi nilipitiliza hadi Chumbani kwangu huku ile  kiu ikizidi kuongezeka hadi nilisahau kufunga mlango, nguvu  zilianza kuniisha nikawa nafungua kete huku nikiwa  natetemeka, nilikuwa nimekaa chini, nilifanikiwa kufungua  kisha nilianza kuvuta madawa kwa pupa sana, kwakuwa nilikuwa  nimeshazoea wala hayakunipa shida sana. 

    Nilivuta kwa nusu saa hadi niliona akili ikisizi kama vile  nilikuwa nataka kuingia usingizini, kumbe Mama Nesha alikuja  Chumbani kuniambia kuwa chakula kipo tayari, aliniona nikiwa  ninavuta madawa sababu mlango ulikuwa wazi 

    “Jojo” alisema Mama Nesha kwa mshituko Mkubwa 

    “Unatumia madawa ya kulevya Jojo?” Aliuliza kwa mshituko  akiwa amenisogelea, alinikata hamu zote nikamtazama kama  mwizi aliyefumwa akiiba, sikutaka Mtu yeyote ajuwe kuwa  nilikuwa natumia madawa ya kulevya 

    “Kumbe ndiyo maana ulipoteza fahamu kwa siku mbili ni sababu  unatumia madawa ya kulevya, hii taarifa nampa Baba Nesha  kisha naenda polisi sitaki uje utuletee matatizo” Alisema  Kisha alianza kuondoka kwa haraka pale chumbani, kiukweli  madawa yaliniondoa utu wangu kabisa, nilibadilika kutokana na  Maisha niliyoishi mwote nilimopita, nilifikiria kumuuwa Mama  Nesha

    Haraka nilimkimbilia Mama Nesha hata kabla hajafika chumbani  kwake, nilimkaba shingo yake kwa nguvu sana sababu madawa  yalikuwa yakinipa nguvu, nilihakikisha namuuwa Mama Nesha  bila huruma huku madawa yakishinikiza kufanya hivyo. 

    “Jooo Joo, unanii…uwaa” Alisema Mama Nesha lakini sikujali  hata mateso aliyokuwa akiyapata, sikutaka kuingia matatizoni  kabisa. Niliendelea kukaba shingo yake hadi hatua ya mwisho  ambapo alilegea kabisa na kufariki. Nilipomuuwa Mama Nesha  ndipo akili yangu ya kawaida iliporejea, niliwaza kukimbia  msala huo. 

    Haraka nilirudi chumbani kwangu, nilichukua begi na vitu  vyangu vyote kisha niliondoka, nilikimbilia stendi nilipanda  gari ya kurudi Dar. Nilikuwa nimechanganikiwa kabisa, uzuri  ni kuwa Baba Nesha alikuwa amesafiri 

    “Dada futa pua yako kuna uchafu” Alisema Mkaka aliyekaa siti  moja na Mimi, aliuwona ule unga eneo la pua yangu ila  hakujuwa kama ulikuwa ni Unga wa madawa ya Kulevya 

    “Asante sana” Nilijibu kisha nilijifuta haraka sana, ilikuwa  ni mishale ya saa 9 Mchana, nilifika Dar saa 1 Usiku.  Sikujuwa niingilie wapi usiku ule, pesa iliyobakia ilikuwa  chache sana. Usiku ule niliona ni bora nitafute Gesti nilale 

    Nilipata gesti maeneo ya Temeke Mwisho kule kwa nyuma,  nililala hapo Usiku huo hata sikukumbuka kula. Asubuhi  niliona taarifa ya habari ikielezea juu ya Mauwaji  niliyoyafanya ila uzuri ni kuwa hakuna aliyekuwa na picha  yangu ila tu jina la Jojo ndilo lililo tajwa, nilimuona pia  Baba Nesha akisema kwa uchungu na maumivu makali sana,  alielezea jinsi alivyoniokota Shambani kwake na kunifanyia  wema, yalikutwa madawa ya kulevya kwenye kile chumba ambacho  nilikuwa nikiishi. Roho iliniuma sana ila sikuwa na jinsi  sababu tayari nilishaamuwa kukimbiza Maisha yangu vinginevyo  ningekamatwa na polisi. 

    “Nimekuwaje Mimi Jojo?” Nilisema kwa maumivu makali sana  ndani ya moyo wangu, sikutegemea kabisa kama ningefikia hatua  ya kuwa Muuwaji. Nilifikiria sana niliona ni bora nitafute  pesa nirudi nyumbani kwetu ila sikuwa na kazi. Nilibakiwa na  shilingi Elfu 10 tu ambayo ilikuwa ndiyo pesa pekee  niliyonayo, niliiangalia huku nikitafakari 

    Ghafla mlango uligongwa, nilishtuka sana, nilihisi ni polisi  maana kesi ya kuuwa ni kubwa mno, niliuliza 

    “Nani?”

    “Nahitaji kufanya Usafi” nilisikia sauti, nilijuwa tu atakuwa  ni Mtu wa Usafi wa ile Gest, niliangalia saa ya ukutani  niliona ni saa 3 asubuhi, muda wa Mimi kuondoka pale Gest  uliwadia, nilienda kumfungulia kisha aliniuliza 

    “Unalipia tena au unaondoka?” 

    “Naondoka, ila nitarudi, naomba nikuachie Begi langu  tafadhali” 

    “Mh! Labda ukamuombe yule Mkaka wa mapokezi maana mimi  sihusiki kabisa na hayo, muombe atakukubalia tu ilimradi kuwe  na usalama” 

    “Usalama upo Dada yangu” Basi, kwakuwa nilikuwa  nimeshajiandaa, nilikuwa nimevalia suruali nyeusi na raba  nyeusi, juu shati jeupe nilielekea Mapokezi kumuomba Mkaka wa  Mapokezi anihifadhie begi langu 

    “Habari Kaka yangu” 

    “Salama” alinijibu akionesha sio Mtu wa Stori nyingi 

    “Samahani Kaka yangu naomba unihifadhie Begi langu kuna  mihangaiko nikaifanye nikirudi nitalichukua” Nilisema kwa  kujiamini kama vile mfanyabiashara aliyetokea mkoani kuja Dar  kununua bidhaa, yule Mkaka kwa umakini sana kisha aliniuliza 

    “Kuna usalama?” Nilijichekesha kidogo kisha nilimjibu “Ndiyo Kaka yangu” 

    “Fungua tuone kuna nini!” Alisema akiwa ananikodolea macho  kama Askari wa Barabarani 

    Nilijiamini sababu sikuwa na chochote cha kushangaza,  nilifungua begi nikatoa nguo zote 

    “Ni nguo zangu tu Kaka yangu” 

    “Sawa liache ila hakikisha unalirejea leo leo” Alinisistiza  kwa ishara ya Kidole, nilimuaminisha kuwa nitalifuata japo  sikuwa na uhakika maana hata sehemu ya kwenda kuliweka lile  begi sikuwa nayo, nilirejesha nguo kwenye begi haraka sana  kisha nilimpatia lile begi 

    “Asante Kaka yangu jioni nitarudi Baada ya Mizunguko”

    Basi niliondoka pale, hadi kituo cha magari ya kuelekea  Mjini. Niliona Magari ya Kariakoo, Tabata, Ubungo, niliona ni  bora nielekee Ubungo maana jina hilo halikuwa ngeni kwangu  kuliko Kariakoo na Tabata. 

    Nilikuwa mwingi wa kuwaza, nilitoa ile Elfu 10 kisha kondakta  aliniambia hana Chenji atanipatia mbele, basi nikatulia  zangu. Nakumbuka ndani ya gari waliweka redio ya Clouds  kipindi cha Leo tena ikawa inasikika ile habari ya Mimi  kumuuwa Mama Nesha. 

    Nilishtuka sana nikahisi kama nimegundulika kuwa ndiye  niliyeuwa maana niliona kama watu wananiangalia kumbe hata  haikuwa hivyo bali ni wenge langu tu 

    “Konda nashuka” Nilisema huku nikiwa kwenye hekaheka za  kupishana na watu kwa nguvu ili nishuke 

    “We Dada si ushuke taratibu” Alisema Mdada mmoja, wala  sikujali nilisukuma Watu hadi nilipofika mlangoni, hata  sikukumbuka chenji yangu nilishuka kisha niliingia mtaani,  niliona kabisa nilikuwa nimechanganikiwa kabisa. Kila  niliyekutana naye niliona ni Polisi na anakuja kunikamata,  nikawa kama Chizi jumlisha na madawa ya kulevya amabyo  nilikuwa nikiyatumia. Ilikuwa ni maeneo ya Buguruni Sheli,  niliongoza njia ya kuelekea Vingunguti kupitia kwa Mnyamani. 

    Nilitembea kwa umbali mrefu sana bila hata kuhisi kuchoka  hadi nilipofika Machinjio ya Vingunguti, nilishuka na ile  barabara ya kuelekea Barakuda, nilipofika Kwenye Daraja  nilituliza wenge langu. Nilikuwa wa hovyo sana kuliko hata  ninavyoweza kuelezea hapa 

    Nilitembea taratibu, njaa ilianza kunichapa huku ile hamu ya  kuhitaji madawa ya kulevya ikizidi kuniingia. Kila  aliyenitazama aligundua haraka kuwa nilipoteza uwezo wa  kujiamini, rangi na asili yangu ya uarabu ilifunikwa na  mawazo nikawa kama Muarabu aliyefirisika. Ilifika mahali hata  viatu niliviona vizito, nilivivua na kuvishika mkononi,  nilitafuta sehemu nikakaa 

    Mwili ulijaa arosto ya Madawa ya kulevya mno, nilijilaza  chini ya Mti nikiwa nimejikunyata. Niliwaza nikutane na  Shonaa anisaidie lakini sikujuwa alikuwa akiishi wapi, sikuwa  na simu wala nilikuwa simfahamu Mtu yeyote ndani ya Jiji la  Dar-es-salaam. 

    Nilikuja kushtuka giza lilikuwa limeingia, mwili ulikuwa  hauna nguvu kabisa. Kumbe pale nilipokuwa nimelala palikuwa ni maskani ya wavuta bangi, moshi wa Bangi ulipopita kwenye  pua zangu nilijikuta nikisisimka sana, nilimuomba jamaa  aliyekuwa anavuta akanipa 

    Niliivuta haraka haraka kama vile Mtu mwenye njaa kali  anapopata chakula katika mazingira asiyoyategemea. 

    Wahuni wote walinishangaa sana kisha ukimya ukawa umetawala,  hata sikuchukua dakika moja nilikuwa nimeumaliza ule msokoto,  basi liliibuka shangwe kutoka kwao wakinisifu kuwa Mimi ni  jembe. Nilicheka pia maana nguvu ilikuwa imeshaniingia  mwilini, wahuni walikuwa ndiyo wanangu. 

    Basi tulikaa pale wakiwa wanapiga stori zao, kulikuwa na  ubaridi fulani hivi ambao kila nilipovuta Bangi nilihisi joto  la kutisha lenye raha ndani yake. Kadhaa waliondoka akabakia  Jamaa mmoja tu ambaye alianza kuniuliza maswali ya hapa na  pale 

    “Unaitwa Nani mrembo?” Aliuliza akiwa anacheka cheka, alikuwa  teja 

    “Jojo” 

    “Oh Jojo jijooo…Hahaha! Naitwa Domingo, mimi ndiye  niliyepiga kampeni zote za CCM mwaka 1890 Nchini Japani”  Alisema, zilikuwa ni stori za kuchekesha sana ambazo kwa muda  huo niliona zilikuwa kweli kwasababu nilikuwa muathirika wa  madawa hivyo akili yangu ilijaa uteja mno 

    “Ha!ha!ha! Wewe ni noma” nilisema nikiwa ninafurahi 

    “Sema nini Jojoo…twenzetu mageto tukale raha au unasemaje?”  Aliuliza Domingo 

    “Poaa” Nilijibu hata sikufikiria Chochote, Tuliondoka tukiwa  tunapiga Stori za ajabu ajabu zilizotokana na bangi 

    Gheto lenyewe lilikuwa ni kiota kilichojengwa kwa mifuko  kando ya Mto msimbazi. 

    “Hili ndiyo ghorofa langu Jojo, nimekuelewa sana ujuwe”  Alisema Domingo, Bangi zilinifanya nione ni kweli ghorofa,  basi tulilala na kufanya mapenzi hapo bila hata kujuwa afya  ya Domingo, Maisha yangu Mimi Jojo yalizidi kuharibika 

    Asubuhi, Bangi ilikuwa imeondoka. Nilijishangaa mahali  nilipokuwa nimelala, huyo Domingo nilimtazama mara mbili,  alikuwa amejawa na chawa kwenye mwili wake, alikuwa na ukurutu wa kutosha alafu nywele zake zilibadili rangi na kuwa  za dhahabu kutokana na uchafu 

    “Nini hiki Jojo?” Nilijiuliza, nilitema Mate, japo nilikuwa  teja lakini sikufikia hatua ya kuwa Mchafu. Haraka nilitafuta  viatu nikaondoka zangu pale nikamuacha Domingo akiwa amelala.  Watu walioniona nikiwa ninatoka Pale walinishangaa kutokana  na uzuri nilionao 

    Basi nilirudi kule Buguruni kwa kufuata ile barabara  niliyokuja nayo Barakuda. Nilipoteza muelekeo wa Maisha  kabisa, Jojo hali yangu ilikuwa mbaya sikula Tokea nilipokula  kule Rufiji, niliona Vijana waliokuwa wakiomba omba kwenye  magari yaliyo kwenye foleni, nilijiangalia nikaona ni bora  nami nikaombe msaada mana kuna Wakati nilikuwa najitambua  kabisa na kujuwa kuwa sipaswi kuyaishi maisha ya Uteja 

    Niliomba kwenye gari moja badala ya Jingine, wengine  walinikebehi, wengine hawakutaka kunisikiliza kabisa, gari ya  mwisho nilimkuta Msanii mkubwa sana wa kike hapa Tanzania  ambaye siwezi kumtaja jina lake, alikuwa ndani ya gari nzuri  sana akiwa naye anasubiria gari zianze kuondoka, niligonga  kioo chake, alipofungua ndipo nilipomuona kwa uzuri,  alinifanya nitabasamu sababu sikuwahi kumuona ana kwa ana 

    “Nikusaidie nini?” Aliuliza huyo Msanii maana nilikuwa  namkodolea macho tu hata kusema nilikuwa siwezi 

    “Naomba msaada Dada yangu sina pa kuishi, sina kazi, nahitaji  kurudi kwetu Tabora” Nilisema, aliniangalia kwa muda mrefu  bila kusema chochote kisha alimgeukia Mwanaume aliyekuwa naye  kwenye gari nahisi alimuuliza kwa ishara kama anisaidie au  aniache, yule Mwanaume alinitazama juu chini kisha akamwambia 

    “Mchukue” 

    “Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifungua  mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingia  nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu ya  kuuliza 

    “Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha niliona  kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti ya  kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni,  nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipiki  ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa  nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimu  wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Nini Kitaendeea?  Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST? 

    Usikose SEHEMU YA SABA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

     Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx  Mungu Amenisahau xx 

     

      

    Mungu Amenisahau

    11 Comments

    1. Stella on October 1, 2024 2:16 pm

      Awesome thanks
      😍😍😍

      Reply
      • Daniel on October 1, 2024 4:28 pm

        Daah imenoga atar kiongoz

        Reply
    2. Ibrahimu on October 1, 2024 4:20 pm

      Daaaah

      Reply
      • Lucas George on October 1, 2024 5:24 pm

        Unge onganisha ya saba tu maana umetuacha na alosto

        Reply
      • Fatma on October 2, 2024 2:39 pm

        Lahaulaa

        Reply
    3. Daniel on October 1, 2024 4:28 pm

      Daah imenoga atar kiongoz

      Reply
    4. Ignasi on October 1, 2024 5:01 pm

      Nimeipenda pia nimefunzwa kitu

      Reply
    5. Farnoush on October 1, 2024 7:06 pm

      Jojo jijooo😂😂😂 ila mateja bana

      Reply
    6. G shirima on October 1, 2024 8:10 pm

      Sijui kwanini nakua n arosto ya hii kama Jojo na dawa zake

      Reply
    7. yuzzo sailor official on October 2, 2024 3:13 pm

      sehemu ya saba please

      Reply
    8. Patrick paul on October 3, 2024 1:16 am

      Mzigo hatari unazidi kuelekea pazuri keep it up…..

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.