Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Mungu Amenisahau Sehemu Ya Saba (07)
    Hadithi

    Mungu Amenisahau Sehemu Ya Saba (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 3, 2024Updated:October 4, 20247 Comments9 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mungu Amenisahau
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishiaย 

    “Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifunguaย  mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingiaย  nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu yaย  kuulizaย 

    “Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha nilionaย  kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti yaย  kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni,ย  nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipikiย  ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwaย  nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimuย  wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Endeleaย 

    SEHEMU YA SABA

    Nilizinduka nikiwa Amana Hospital, daktari alikuwa kandoย  yangu akiangalia jinsi nilivyokuwa nikiamka kutoka katikaย  Usingizi mzito wa ile ajali, nilikuwa na maumivu makali yaย  Mgongoย 

    “Tulia utakuwa sawa” Alisema Daktari huyo ambaye alianzaย  kukagua macho yangu kisha aliniulizaย 

    “Unaitwa Nani?”ย 

    “Naitwa Jojo” nilijibu kwa maumivu makali sana.ย 

    “Unaishi wapi?” Aliniuliza, nilitikisa kichwa ishara ya kuwaย  nilikuwa sina makaziย 

    “Ndugu zako wapo wapi?”ย 

    “Sina ndugu hapa, wapo Tabora…..aliyenileta hapa yupoย  wapi?” Nilimuulizia yule Msaniiย 

    “Umeletwa hapa na wasamalia wema tu hata hivyo wameondokaย  zao”ย 

    “Msanii hajafika hapa?”ย 

    “Hakuna aliyekuja kukuona” Alijibu yule Daktari kishaย  aliniambiaย 

    “Unapaswa kwenda soba kwanza ili kukuondoa kwenye matumizi yaย  madawa, vipimo vimeonesha damu yako inakiwango kikubwa chaย  madawa ya kulevya” Alisema yule Daktari kisha alisemaย 

    “Gharama zote zitalipwa na Hospitali”ย 

    “Asante sana” nilisema, nilifurahi kwa upande mmoja sababuย  sikupenda kuwa Mtumwa wa madawa ya kulevya tena.ย 

    Nilipopata unafuu nilipelekewa Soba, nilifundishwa vitu vingiย  mno, nilikutana na wengine ambao walikuwa wameathirika zaidiย  na Madawa ya kulevya, niliishi huko kwa zaidi ya miezi sitaย  hadi nilipopona kabisa na kuacha matumizi ya dawa za kulevya.ย  Baada ya hapo, nilikabidhiwa kwa Mama mmoja ambaye alikuwaย  akiitwa Mama Zahara, alikuwa ni Mama fulani mnene hiviย 

    “Utaenda kuishi kwake sababu huna mahali pa kwenda kuishi,ย  huko mtaani utarudi tena kwenye ulevi” Alisema Mtu wa Soba.ย  Nilifurahia sana kwenda kuishi kwa huyo Mama, niliona naendaย  kufungua ukurasa mpya wa Maisha yangu, ukurasa ambaoย  utatengeneza upya Maisha yangu.

    “Utaishi kwangu kwa Muda kisha utaamuwa kama utaendelea auย  utarudi kwenu Tabora” Alisema Mama Zahara, basi tuliingiaย  kwenye gari yake kisha tulienda nyumbani kwake, alikuwa naย  nyumba nzuri sana kubwa ambayo alikuwa akiishi na Wasichanaย  waliotoka Soba.ย 

    Niliishi hapo kama Mwanafamilia, Maisha yalikuwa mazuri sana,ย  tulipewa kila kitu, hadithi za walio wengi pale walikuwaย  hawana makazi kama Mimi, wengine waliondoka na wengineย  tulibakia.ย 

    Miezi miwili ilikatika nikiwa hapo kwa Mama Zahara, Siku mojaย  Mama Zahara alisafiri, alituaga kuwa anaenda Mombasa Kenya.ย  Alituhasa sana kuendelea kuishi kwa upendo wa hali ya juuย  sana na pia kuishi kwa kujali afya na malengo yetu,ย  alipoondoka kila mmoja aliachiwa pesa yake kwa ajili yaย  kujikimu kidogo maana alikuwa anaenda kukaa huko kwa kipindiย  cha mwezi mmoja.ย 

    Kulikuwa na Mdada aliyeiywa Salome, tulijenga ukaribu sana,ย  alikuwa na hela nyingi kuliko Msichana yeyote pale, nilipataย  shahuku ya kumuulizaย 

    “Hivi Salome hizo pesa unatoa wapi?” Kwanza alicheka kishaย  alinijibuย 

    “Nazitafuta Jojo, unafikiria pesa inaokotwa?”ย 

    “Sijamaanisha kuwa inaokotwa ila nimeuliza ili nijuwe”ย 

    “Jibu zuri ni matendo, kesho ni Jumamosi, usiku tutoke”ย  Alisema Salome, alikuwa ni Mdada fulani mnene kiasi mweusi,ย  macho yake yalikuwa makubwaย 

    “Usiku tena?”ย 

    “Ndiyo, hofu yako ndiyo umasikini wako, ni lazima Jojoย  ujifunze kutengeneza pesa kwa ajili ya Maisha yako,ย  unafikiria siku ukiondoka hapa kwa Mama Zahara utapewa pesaย  ya kuanzia Maisha? Utapewa nauli tu, sasa utaishi vipi hukoย  kwenu?” Alisema Salome, maneno yake yalikuwa na mashikoย  kwenye ufahamu wangu, alichokisema niliona kina ukweliย 

    “Sawa tutaenda” Nilimkubalia bila kujuwa alikuwa anatakaย  kunipeleka wapi, wakati huo ule uzuri wangu ulikuwa umerejeaย  tena kwa kasi sana sababu nilikuwa naishi vizuri sana paleย  kwa Mama Zahara.

    Siku iliyofuata Usiku tulitoka tukiwa tumevalia vinguoย  vifupi, japo nilimuuliza tulikuwa tunaenda wapi ilaย  aliniambia nitaona, nilimuamini sababu alikuwa ndiye rafikiย  yangu pale kwa Mama Zahara.ย 

    Tulichukua Taxi hadi Magomeni, ilikuwa mishale ya usiku waย  saa tano, tulipofika aliniambia tusubirie. Tulisimamaย  barabarani tu, baridi lilikuwa kali sana pale kiasi nilikuwaย  najikunyata.ย 

    “Tutasimama hadi saa ngapi Salome? Mimi nimechoka” nilisema,ย  kiukweli tulisimama kwa zaidi ya nusu saa, alikuwaย  akisimamisha magari binafsi ya Watu lakini yalikuwaย  hayasimamiย 

    “Salome nimechoka mwenzio” Nilisema huku hasira ikianzaย  kunishikaย 

    “Unataka kuharibu sasa si ndiyo?”ย 

    “Salome hii ni Biashara ya Ngono unaifanya si ndiyo? Sasa siย  bora ungeniambia kule nyumbani unafikiri ningekuja huku Mimi?ย  Yaani sijui mimi nakuwaje Aisee huwa naingizwa kwenye mamboย  yasiyofaa kirahisi sana” Nilisema kwa kujilaumu, Salomeย  alirudi kuendelea kusimamisha gariย 

    Nilikaa pembeni, Idadi ya Wanawake hapo ilianza kuongezeka,ย  walivalia kama sisi tulivyovaa na wengine walikuwa wakivutaย  sigara, niliyachukia Maisha yale kabisa, nilimfuata tenaย  Salomeย 

    “Kama huwezi kuondoka na Mimi basi nitaondoka mwenyeweย  Salome” Nilisemaย 

    “Nipe dakika tano tu nakuomba Jojo kisha tutaondoka” Alisemaย  Salomeย 

    “Sawa ni dakika tano tu baada ya hapo sitakuwa na muda waย  kuendelea kukusubiria” Nilisema kisha nilirudi kuketi kandoย  kidogo ya waliposimama waoย 

    Baadaye niliona gari ikisimama, Salome alianza kuzungumza naย  Mtu wa kwenye gari japo sikusikia walichokiwa anakizungumzaย  ila nilihisi itakuwa amepata Mtejaย 

    Alikuja akaniambiaย 

    “Si ulikuwa unataka kwenda nyumbani? Basi wewe nenda mimiย  nitarudi asubuhi” Alisema Salome

    “Sasa ulichoniletea huku ni nini Salome? Aaah” nilisema kwaย  kuchukia sanaย 

    “Nenda Jojo tutaongea nyumbani ila usimwambie Mtu yeyote”ย  Alisema Salome kisha alikimbilia kwenye gari akapanda kishaย  gari iliondoka. Nilichukia mno istoshe kiatu kilikuwaย  kinanibana sana mguu wa kushoto, niliamuwa kukivua iliย  nisizidi kuumia.ย 

    Nilisimama pembezoni mwa waliposimama wale wanawakeย  wanaojiuza, nilikuwa nasubiria gari ya kurudi nyumbani.ย  Ghafla nilisikia purukushani, nilipogeuka niliona waleย  wanawake wakikimbia huku na kule huku wakipiga mayowe.ย  Nilihamaki, nilihitaji kujuwa wamepatwa na nini, pundeย  niliona Watu waliovalia sare za polisi.ย 

    Nami nilianza kukimbia, polisi wawili wakawa wananikimbiza,ย  walinikamata mita chache tu kabla hata sijafika mbali.ย 

    “Naomba mniache tafadhali” nilisema wakiwa wananipelekaย  kwenye gari ya polisiย 

    “Wanawake wa Siku hizi bwana, Mwanamke mzuri kama weweย  ujiingize kwenye biashara ya ukahaba, twende tukakufundisheย  kazi huku” Alisema Askari mmojaย 

    “Mimi siyo kahaba nilikuwa nasubiria gari nirudi nyumbani,ย  sijawahi kuuza mwili katika Maisha yangu” Nilijaribuย  kujitetea kidogo ili niachwe.ย 

    “Twende utajuwa huko huko kama ulikuwa ukiifanya hiyoย  biashara au ulikuwa hauifanyi” Alinijibu yule askariย 

    “Kweli mimi sijafanya kama mnataka nimpigie ndugu yanguย  ambaye nilikuja naye huku” Nilisema tenaย 

    “Ndugu yako atakuja kituoni kutoa maelezo huu siyo muda waย  maelezo” Alinijibu Polisi mwingine, tayari tulikuwaย  tumeshafika kwenye gari. Waliniingiza kwenye gari ya Polisi,ย  Wale makahaba nao walikuwa wamekamatwa pia.ย 

    Tulipelekwa kituo cha Polisi, tulitupwa Mahabusu. Sikuย  iliyofuata niliitwa na Polisi nikaambiwa niwapigie nduguย  zangu ila kibaya sikuwa na simu wala namba ya Mtu kichwani,ย  angalau ningempigia Salome au hata Mama Zahra lakini hataย  hivyo Mama Zahra alikuwa nje ya Nchi ningempata vipi?ย 

    “Afande siijui namba ya Ndugu yangu hata mmoja ila naombaย  nipo chini ya Miguu yako twende nyumbani kwetu,ย 

    watakuthibitishia kuwa Mimi sijiuzi kabisa” Nilisema, yuleย  Polisi alicheka akasemaย 

    “Hayo ndiyo maneno yenu, nakusikitikia sana Ndugu yanguย  sababu Rais ametoa maagizo makali sana kuhusu Biasharaย  mnayofanya, siku tatu zijazo mtafikishwa mahakamani naย  mtahukumiwa kufungwa Miaka mitatu au Faini isiyopunguaย  Milioni 6” Alisema yule Polisiย 

    “Kaka yangu wewe una ndugu au hata Dada kama Mimi, naombaย  usimame kama Kaka kwangu niangalie Mdogo wako ninavyoteseka”ย  Nilisemaย 

    “Nikisema nisimame kama Kaka nitasimama kwa wangapi?ย  Tutakomesha hii Biashara kweli? Nenda ukafunzwe na Walimwenguย  huko uendako” Alisema kisha nilirudishwa Mahabusu. Ni Mimiย  peke yangu ndiye niliyekuwa nikilia ndani ya Mahabusu sababuย  sikuzoea maisha yale kabisa.ย 

    Nilionekana kero kwa wale mahabusu wengine wakawa wananisemaย  sana nijikaze sababu Biashara ile ndiyo kila kitu, nilijaribuย  kuwaambia kuwa Mimi siyo kahaba ila hawakutaka kunielewaย  kabisa wakasema kama siyo kahaba nilifikaje pale? Naย  nilijuana vipi na Salome wakati Salome ni kahaba wa mudaย  mrefu?ย 

    Sikuwa na utetezi kabisa, niliishia kulia tu. Ukurasa wanguย  mzuri wa Maisha ambao ulifunguka na kunipa furaha sanaย  ulianza kuchanika, nilijikuta nikirudi kwenye Maishaย  yaliyojaa giza tena, niliishi hapo kwa hizo siku mbili naย  hakuna aliyekuja kunitafuta.ย 

    Siku ya tatu tulipelekwa Mahakamani, Polisi walisimama kamaย  Mashahidi, nililia sana Mahakamani ili niachiwe lakiniย  haikusaidia. Hakuna hata mmoja kati yetu aliyekuwa na kiasiย  cha Shilingi Milioni 6 ili asifungwe, sote tulihukumiwaย  kifungo cha miaka mitatu.ย 

    Tulipelekwa gerezani, siku tunavalishwa sare za Gerezani naย  kukatwa nywele zetu ndipo nilipoamini kuwa nilikuwaย  nimetumbukia kwenye shimo lenye giza, nilifikiria Miakaย  mitatu ilivyokuwa Mingi nitaweza kuishi gerezani kweli? Kamaย  kulia nililia sana hadi mwili ulishika moto lakini hakunaย  kilichosaidia, kilio changu na machozi yangu yaligeuka kuwaย  chozi la samaki lisombwalo na maji, hakuna aliyenisikia walaย  kuthamini chozi langu, kila Mtu alikuwa na matatizo yakeย  ndani ya Gereza hivyo isingelikuwa rahisi kusikilizwa.

    Nilikubaliana na hali halisi, niliyaanza Maisha mapya ndaniย  ya gereza. Maisha yaliyojaa ubabe, uonevu, utata, manyanyasoย  na kazi ngumu sana. Tulifanya kazi ngumu na kupewa chakulaย  kidogo tena hicho kidogo anakuja Mtu anakuchukulia kwa ubabeย  wake na hakuna cha kumfanya.ย 

    Nilimpata rafiki ndani ya gereza, aliyeitwa Isabela nayeย  alikuwa Mtu wa Tabora hivyo tulikuwa na memgi ya kuzungumza.ย  Yeye alihukumiwa kwa kosa la kumkata Mkono kimada wa Mumeย  wake, japo tulikuwa katika nyakati ngumu sana ila tuliishiaย  kucheka tuu maana hakukuwa na njia nyingine zaidi kutumikiaย  adhabu, Mume wake hakuwahi kuja kumuangalia Gerezani kwaย  miezi zaidi ya mitatu. Isabela alihukumiwa kifungo cha miakaย  miwili tuย 

    “Ukishamaliza kifungo una mpango gani?” Nilimuuliza Isabelaย  tukiwa shambani tunalimaย 

    “Kurudi Tabora tu maana nimegundua Mume wangu hanipendiย  kabisa licha ya kumzalia Mtoto mmoja, angekuja kunionaย  angalau ningekuwa na tumaini. Ila najutia sana hasira zangu,ย  ona nateseka mwenyewe kwa ajili ya mtu ambaye hajali chochoteย  kuhusu Mimi” Alisema, niliona jinsi alivyokuwa na maumivuย  moyoni, ghafla nilijiona sina matatizo kabisa.ย 

    “Pole sana Isabela, yataisha tu. Ukifika Tabora nendaย  nilipokuelekeza waambie nipo Gerezani” Nilisema.ย 

    Basi Maisha ndani ya Gereza yaliendelea, siku moja baada yaย  kazi ilikuwa ni majira ya saa 7 Mchana, ulikuwa ni muda waย  kupata Chakula. Tulikuwa tukipanga mistari miwili kwa ajiliย  ya kupata Chakula, msitari wa kwanza nilikuwepo Mimi, sasaย  katika tazama tazama nilistaajabu nilimuona Sarafina, yuleย  Mdada ambaye alifukuzwa na Shonaa kisa Mimi, nilitamaniย  kumuita ila nilikumbuka kuwa alikuwa na hasira na Mimi,ย  nilimgeukia Isabela nikamuulizaย 

    “Yule yupo hapa kwa muda gani?” Nilimuonesha kidole Sarafinaย 

    “Nimemkuta hapa, anaonekana kahukumiwa muda mrefu ilaย  inasemekana aliiba pesa kwa tajiri mmoja”ย 

    “Vipi unamjuwa?”ย 

    “Ndio namjuwa” Basi baada ya kuwa tumeshachukua chakulaย  tulienda kula, Isabela aliniulizaย 

    “Unamjua vipi yule”ย 

    Nini Kitaendeea?ย  Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?ย 

    Usikose SEHEMU YA NANE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย 

     

    ย ย 

    Mungu Amenisahau

    7 Comments

    1. Lus twaxie on October 3, 2024 4:22 pm

      Aiseee huyo dada nae kama chizi

      Reply
    2. Deo on October 3, 2024 4:27 pm

      Kila siku ni ukurasa mpya maishani

      Reply
    3. Sir yowas on October 3, 2024 4:47 pm

      Asante

      Reply
    4. Brath on October 3, 2024 8:13 pm

      Looh jamani Jojooo anakuwa zuzu

      Reply
    5. yuzzo sailor official on October 4, 2024 1:40 am

      sehemu ya nane please

      Reply
    6. Husna khalfan on October 4, 2024 3:25 am

      Ndivyo mungu anatupitisha magumu ili kujifunza na kuwa bora zaidi

      Reply
    7. ๐Ÿ“ฃ + 1.584571 BTC.GET - https://yandex.com/poll/enter/47uYv1jDg9Q2bCy1CSWpTp?hs=61c78ad60e4ed8bb4229bf301c1daf7d& ๐Ÿ“ฃ on June 18, 2025 5:30 pm

      jv1556

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.