Ilipoishia “Tulienda moja kwa moja anapoishi Shonaa akaniambia kesho yakeย atanipeleka kwa huyo Bosi, nilikuwa nimechoka hivyo sikuwa naย maswali mengi zaidi ya kuhitaji Kupumzika tu, kweliย nilipumzika hadi asubuhi kulivyo pambazuka. Shonaa aliamkaย mapema sana, alikuwa amepangisha chumba kimoja na sebule,ย nilienda hadi sebleni nilimsalimiaย
“Mambo Dada?” Aliacha alichokuwa anakifanya kisha alitabasamuย akanijibuย
“Poa tu umeamka salama?” Aliniulizaย
“Ndiyo nipo sawa! Umedamka hivyo?” Nilimuulizaย
“Si unajuwa tena Maisha ya Mjini ndugu yangu, ukiendekezaย Usingizi utakufa masikini” Alisema kisha tulicheka, nilionaย nimepata Mtu wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali yanguย
“Jana ulisema utanipeleka kwa Bosi asubuhi hii” “Usijali, subiria nimalize kupasi nguo zangu” Alijibu Shonaaย ย
Endeleaย
SEHEMU YA PILI
“Unaitwa Nani?” Nilimuulizaย
“Naitwa Shonaa, wewe ni Jojo Eeh?”ย
“Ndiyo Naitwa Jojo” nilijibu huku nikiwa ninatabasamu.ย
Punde mlango wake uligongwa waliingia wasichana wengineย wawili ambao walikuwa wamelewa, walisema maneno ya hovyoย hovyo kisha walipitiliza hadi chumbani, mmoja alinisukumaย nikaangukia kwenye kochi, kiukweli nilishtuka sana.ย
“Usijali Jojo utazoea, ndiyo Maisha yetu” Alisema Shonaaย nilimsogeleaย
“Ndiyo Maisha yenu? Ina maana mnaishi Watatu hapa?”ย Nilimuuliza Shonaa, alinisogelea akaniambia, Bado watatuย hawajarudiย
“Eeeh?” Nilishangaa Watu sita wanaweza vipi kuishi hapoย
“Wewe ni wa saba Jojo, utazoea tu najuwa inakupa wakati Mgumuย sana. Atakaye wahi kurudi analala Kwenye kitanda, ukichelewaย kwenye kochi, ukichelewa zaidi unalala chini” Alisema Shonaaย kisha aliendelea na kazi yake, kusema ule ukweli nilijilaumuย kwanini nilikuja Dar, niliona ugumu ulio mbele yangu.ย Nilitoka ndani nikampigia Msonjo ili ikiwezekana nirudiย Tabora mara moja, niliona ni bora kulala njaa kuliko Maishaย yaleย
“Jojo tutapata wapi nauli ya wewe kurudi haraka hivyo?ย Vumilia kidogo mbona mapema hivi unakata tamaa jamani?”ย Ilikuwa ni sauti ya Msonjoย
“Sikia Msonjo, yaani siwezi kuvumilia japo kwa sekunde moja,ย wewe haupo ila Maisha yanatisha hivi Watu wa Mjini ndioย wanaishi hivi? Chumba kimoja Watu saba?”ย
“Jojo! Ngoja niongee na Bosi tuone inakuwaje!” Alisema Msonjoย
“Jitahidi nakuomba Msonjo nipo katika nyakati ngumu sana”ย Nilisema kisha salio liliisha kwenye simu yangu, nilipogeukaย nyuma nilimuona Shonaa akitikisa kichwa chake, alikuwaย akisikitika.ย
Shonaa alirudi ndani bila kusema chochote ila alikuwaย amesikia mazungumzo yangu, nilipofika ndani aliniambiaย
“Jiandae tuondoke” basi nilielekea chumbani, yaani nilikutaย mazingira ya hovyo sana, jinsi walivyolala wamewekeana Miguu,ย
mwingine alikuwa ametapika karibu na begi langu, kichefuchefuย kilinizonga. Nilijikaza tu hivyo hivyo nilibadilisha nguo,ย kisha nilitoka.ย
“Ndio unavaa hivyo?” Aliniuliza Shonaaย
“Ndiyo kwni kuna tatizo?” Nilimuulizaย
“Mmh! Haya twende” Alisema Shonaa kama vile kuna jamboย alitaka kusema. Tulipanda daladala hadi Sinza kwa Remi,ย kulikuwa na kumbi kubwa mpya ya Starehe iliyoitwa Dar Cityย ndiyo ilikuwa ikimilikiwa na huyo Bosi aliyeitwa Muntaza.ย
Tulienda hapo kwenye huo ukumbi, palikuwa pameshachangamkaย asubuhi asubuhi, Watu walikuwa wakipiga mitungi kama hawanaย akili nzuri, tena ilionesha walikuwa wamekesha hapo hapo,ย ilikuwa ni siku ya Jumamosi.ย
“Shonaa upo na mrembo” Alisema mmoja wa walevi kishaย alimshika shonaa titi, alafu Shonaa hakuonesha kuchukia ndioย kwanza alikuwa akicheka, nguvu ziliniishaย
“Kama kawaida si unanijuwa Mimi” Alisema Shonaa kishaย tuliingia kwenye chemba mojaย
“Shonaa haya Maisha sitoyaweza” Nilisemaย
“Jojo bado hujayaona Maisha tayari unasema hutoweza, sasaย unaweza kurudi kwenu Tabora na huna pesa hata ya kula? Achaย ujinga, fanya kazi hata mwezi mmoja kisha ndioย uondoke…..unakata tamaa mapema, inabidi upambaneย kuhakikisha unapata pesa, hapa Mjini kila kitu ni pesa”ย Alisema Shonaa akiwa amenikazia jicho, kisha aliongoza mbeleย nami nilimfuata. Nilikuwa sijala ila Maisha niliyoyaonaย yalinifanya nishibe, hebu fikiria Mtu anashikwa Titi mbele zaย Watu alafu anacheka wakati Tabora Mtu umshike bega tu bilaย ridhaa yake anakupiga kofi, nilitikisa kichwa changuย
Tuliingia kwenye chumba kimoja ambacho alikuwemo huyoย Muntaza, kilikuwa ni chumba kinachonuka sigara na pombe,ย alikuwa na wasichana wawili makamo yangu. Aliwaondoa baada yaย sisi kuwa tumeshaingia na kuketi kwenye sofa jirani naย alipoketi yeye, nilijikuta naanza kukohoa kutokana na uleย moshi. Muntaza alikuwa ni pande la Mtu, alikuwa na cheniย nyingi na pete, alafu alikuwa na kitambi, umri wake ulioneshaย alikuwa zaidi ya miaka 50ย
Basi Shonaa alimsogelea na kumpiga busu huyo Muntaza,ย nilitazama pembeni nikiwa ninakohoa.
“Wow!” Alisema Muntazaย
“Bosi huyu ni Jojo uliyeniagiza kumpokea” Alisema Shonaa,ย nilijichekesha kidogo ila kiukweli moyo ulikuwa ukiniendaย mbio sana.ย
“Hukumuelekeza mavazi ya kuyavaa?” Alihoji Muntaza “Ndio Mwanzo Bosi nitaongea naye vizuri”ย
“Ok! Muelekeze majukumu yake” Alisema Muntaza kisha aliondokaย hata bila ya kunisemesha chochote.ย
Alpoondoka Muntaza nilizidi kukohoa, nilikuwa nimevaa gauniย na mtandio kichwani.ย
“Jojo ukitaka kuishi hapa vziri kubali hali halisi ilaย ukileta misimamo isiyo na maana utajikuta Mji unakushindaย huu. Hapa ndiyo ofisini kwako, kwangu na kwa wale wadadaย wengine tuliowaacha kule nyumbani, mavazi ya hapa ni kamaย yangu” Alivyosema hivyo nilimtazama alivyovaa, yaani alivaaย kikomdomu tu na vest, chini rabaย
“Ukizubaa unapotea, kuwa mjanja”ย
“Lakini kusema ule ukweli Shonaa haya Maisha sina uhakika waย kuyaweza kabisa, najilaumu sana kuja huku Dar ilaย aliyenitafutia kazi nimemuomba anisaidie kuongea na Bosi iliย anipe nauli nirudi kwetu” Nilisema.ย
“Usijidanganye kuhusu kupewa nauli, hata Mimi nilikuja kamaย wewe miaka miwili iliyopita, nilikuwa muoga nilikuwa nikiliaย nirudi nyumbani lakini ilishindikana”ย
“Lakini Shonaa mimi nimefiwa na Mama yangu mwezi uliopita,ย nahisi nitakuwa namkosea sana kufanya kazi ya hivi, alinileaย katika mazingira bora sana” nilisemaย
“Sawa alikulea katika mazingira bora ila hakuacha msingiย wowote, laiti kama angelikuachia msingi basi usingekuja hukuย kutafuta Maisha, hata Mimi Mama yangu nimemzika mieziย michache iliyopita huko Kilimanjaro, nimerudi sababu hii niย kazi inayoendesha Maisha yangu”ย
Maneno ya Shonaa yalinikata sana kauli, niliona napaswaย kukubaliana na hali halisi japo bado tumaini langu lilikuwaย kwa Msonjo aliyenileta Dar. Kulikuwa na nguo zikizokuwa mleย kwenye chumba alinipatia nizivae, nilijitahidi kukataa lakiniย aliniambia hakukuwa na sababu ya kutoka Tabora kuja Dar niย bora ningebaki Tabora. Basi nilizichukua nikabadilisha,ย sikujiangalia mara mbili, yaani chupi ilikuwa ikionekana,ย nguo zilibana na kushika mwili wangu, kila kiungoย kilijichonga. Kibaya zaidi aliniambia nisivae sidiriaย
“Shonaa hivi siwezi kusema ukweli nitaweza vipi kutembeaย jamani mbona unanipa wakati mgumu hivi” nilisema, Shonaaย alicheka sana. Kabla hata hajaongea chochote aliingia Muntazaย
“Yupo tayari?” Aliulizaย
“Ndiyo Bosi”ย
“Haya akaanze kazi” Alisema kisha alijitupa kwenye Sofa akiwaย anakohoa. Ningefanyaje unafikiri? Nilitoka na Shonaa bilaย ubishi wowote ila nilikuwa navuta vuta nguo zangu iliย zisinichonge hapa mbele kwa Bibi.ย
Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza katika Maishaย yangu kufanya kazi ya Ubaamedi, nilikutana na vikwazo vingiย ikiwemo kushikwa shikwa lakini nilijitahidi kukwepa kadiliย nilivyoweza. Saa 12 walikuja wengine, Mimi na Shonaa tulirudiย nyumbani kupumzika. Nilipewa elfu 10 kama pesa ya siku yaย kazi, niliiweka pembeni ili ikitimia pesa ya Nauli niondokeย zangu.ย
“Umeionaje siku yako ya kwanza kazini?” Aliniuliza Shonaaย
“Nzuri tu” Nilisema kisha nilitoa tabasamu feki, sikutakaย tena kujionesha kuwa kazi hiyo nilikuwa siitaki, kwakuwaย niliona naweza pewa kila siku elfu 10 hivyo ningeweza kurudiย Tabora haraka sana.ย
“Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwaย kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,ย sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi”ย
Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwaย akinikagua, nilionesha lile tabasamu fekiย
“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibanaย kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononiย
“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamuย lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamuย lililotoka moyoniย
“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengineย walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx
ย ย


9 Comments
Fupi sana admin ila tamu โ
Asantee admini
Duh Jamani jojo
Maisha hayo jamani
Jamani
Nzuri sanaaa
Daah Jojo jaman
Mbona sehemu ya Tatu ina chelewa? Au ni mimi sijaona
sehemu ya tatu admin