Ilipoishia “Basi Maisha ndani ya Gereza yaliendelea, siku moja baada yaΒ kazi ilikuwa ni majira ya saa 7 Mchana, ulikuwa ni muda waΒ kupata Chakula. Tulikuwa tukipanga mistari miwili kwa ajiliΒ ya kupata Chakula, msitari wa kwanza nilikuwepo Mimi, sasaΒ katika tazama tazama nilistaajabu nilimuona Sarafina, yuleΒ Mdada ambaye alifukuzwa na Shonaa kisa Mimi, nilitamaniΒ kumuita ila nilikumbuka kuwa alikuwa na hasira na Mimi,Β nilimgeukia Isabela nikamuulizaΒ
“Yule yupo hapa kwa muda gani?” Nilimuonesha kidole SarafinaΒ
“Nimemkuta hapa, anaonekana kahukumiwa muda mrefu ilaΒ inasemekana aliiba pesa kwa tajiri mmoja”Β
“Vipi unamjuwa?”Β
“Ndio namjuwa” Basi baada ya kuwa tumeshachukua chakulaΒ tulienda kula, Isabela aliniulizaΒ
“Unamjua vipi yule”Β EndeleaΒ
SEHEMU YA NANE
“Wakati nakuja hapa Dar ndio nilionana naye ila tuliachanaΒ kwa shari, aliniona mbaya akidai nimesababisha amefukuzwaΒ pale alipokuwa anaishi” NilisemaΒ
“Mh! Sasa itabidi ujiadhari maana yule ana kundi lake hapaΒ gerezani ambalo linaendesha ubabe mwingi, akijuwa kama upoΒ hapa utaishi kwa shida sana” Alisema Isabela.Β
“Ni kweli lakini nitamkwepa vipi wakati tunaishi kwa uwaziΒ hivi, ikiwa mimi nimemuona nina imani na yeye ataniona tu.”Β
“Cha msingi ni kumkwepa vinginevyo utateseka sana hapa Jojo”Β
“Mh! Tutaona itakavyokuwa” Tulipomaliza kula tulirudiΒ kuendelea na kazi za Shamba, jioni tulihesabiwa kishaΒ tulikula na kurudishwa kwenye vyumba kwa ajili ya kulala,Β kila chumba kilikuwa na wafungwa 8 ambao tulikuwa tukilalaΒ humo. Bahati nzuri chumba chetu hakikuwa na muhuni hataΒ mmoja, kumbe taarifa ya Mimi kuwepo Gerezani alikuwa nayoΒ Sarafina, kama Isabela alivyoniambia kuwa Sarafina alikuwa naΒ kundi la ubabe pale gerezani.Β
Usiku tukiwa tumelala tena fofofo maana kazi za pale GerezaniΒ zilikuwa ngumu mno hivyo Mtu akilala anakuwa kama amekufa.Β Nilishtuka geti la chumba chetu lilikuwa likifunguliwa alafuΒ tochi ilinimulika Usoni, aliingia mdada mmoja ambaye hakuwaΒ Askari, aliniambia nimfuate.Β
Niliamka kisha nilimfuata, niliingizwa kwenye chumba kimojaΒ kisha kilifungwa, kilikuwa ni chumba chenye giza mno kiasiΒ kwamba sikuweza kuona chochote kileΒ
“Nipo wapi?” Nilijiulza kwa sauti ya chini huku nikipapasiaΒ
“Dada yangu kwanini umenileta huku?” Niliuliza, sautiΒ ilijirudia tu katika kile chumba, sikujibiwa. Mara taaΒ iliwashwa, nilikutana na macho ya SarafinaΒ
“Sarafina” Niliita kwa mshituko maana sikutegemea kamaΒ ningekutana naye katika Mazingira yale, kwa vyovyote vileΒ aliyenileta alijuwa nini anafanya.Β
“Karibu Jojo, Mungu wangu alinisikia kilio changu, hatimayeΒ nimekutana na wewe” Alisema Sarafina akipiga hatua ndogoΒ ndogo kusogea nilipokuwa nimesimama.Β
“Sarafina sikufanya chochote kibaya dhidi yako, sikutegemeaΒ kama ingekuwa vile. Nisamehe tafadhali, tuyamalize”
“Pengine umesahau Jojo, nilikuokoa yule Mwanaume asikubake,Β nilimpiga mbele yako kukuonesha kuwa sikupenda alichokifanya.Β Wema wangu kwako ndiyo uliozaa matunda yale, sikuwa na paΒ kwenda, nilikuacha pale lakini nilisema ipo sikuΒ nitakuonesha. Siwezi kuwa na haraka na wewe sababu upo kwenyeΒ himaya yangu” Alisema Sarafina akiwa anazunguka huku na kuleΒ
“Sarafina tafadhali sana, nisamehe hujui ni mambo mangapiΒ magumu nimekutana nayo, nimeishi Maisha magumu sana, hukumuΒ niliyopewa ni adhabu tosha kwangu…” Nilisema kwa uchunguΒ sanaΒ
“Lakini sio adhabu yangu, yangu itakuwa zaidi ya hiyo hukumuΒ uliyopewa, wema wangu ukageuka kuwa udhalilishaji, siri yaΒ ugonjwa wangu iliwekwa wazi, namjuwa Sana Shonaa kulikoΒ unavyomjuwa wewe ni lazima alinianika kwenye kila jambo”Β Alisema Sarafina akiwa amefika karibu zaidi na MimiΒ
Nilipiga goti nikamuomba Sarafina asinifanye chochote kibayaΒ maana kama aliweza kupata funguo ya chumba chetu maana yakeΒ alikuwa na uwezo hata wa kuniuwa na hakuna ambaye angesemaΒ chochote kile.Β
“Magret” Aliita, yule Mdada aliyekuja kunichukua alikujaΒ ndaniΒ
“Mrudishe, nitamalizana naye” Alisema Sarafina kishaΒ nilirudishwa kwenye chumba chetu cha gereza.Β
Nilikuta Watu wa Chumba chetu wakiwa macho ni dhahiri kuwaΒ walisikia Wakati Mimi ninaondolewa pale gerezani. Mtu waΒ kwanza kuniuliza alikuwa ni IsabelaΒ
“Ulienda wapi Jojo?” Nilivuta pumzi nikamueleza nilipokuwaΒ
“Itabidi uwe makini sana Maana Sarafina ni Mtu mkorofi mnoΒ hapa gerezani, ipo namna anaweza akafanya maisha yako yakawaΒ si kitu hapa gerezani” Alisema Isabela akadakia MwanamkeΒ mwingine akasemaΒ
“Wakati anafika aliwahi kupigana na askari Watatu naΒ akawadhibiti vizuri sana, tokea siku hiyo amekuwa na urafikiΒ na Mkuu wa Gereza hili, mara kadhaa amekuwa akitoka na kurudiΒ haijajulikana wana ajenda gani, hivyo unapaswa kuwa makiniΒ sana Jojo vinginevyo hata sisi tutakuwa hatarini. Ana kundiΒ lake hapa na linatambulika na Mkuu wa Gereza, wao hawafanyiΒ kazi yoyote ile zaidi ya kutoka na kurudi” Yalikuwa ndiyoΒ maelezo yake kuhusu Sarafina, hilo la kupiga AskariΒ halikunitisha sana maana nilikumbuka aliwahi kumpiga yuleΒ Mwanaume aliyetaka kunibaka.
“Ina maana anaishi humu gerezani kwa uhuru bila kubugudhiwaΒ na chochote?”Β
“Ndiyo! Ni Mtu hatari sana, anaendesha biashara ya kuuzaΒ Bangi na Unga hapa Gerezani, anachumba maalumu cha kulala naΒ anapewa mahitaji yote ayatakayo” alielezea huyo MwanamkeΒ mwingine, kiukweli nilijawa na woga sana, nilipitia kote ilaΒ niliona dhahiri Maisha yangu yataishia ndani ya gereza,Β nilimuuliza IsabelaΒ
“Ndugu zako wanakuja kukuona?”Β
“Hapana nahisi hawajaambiwa chochote na Mume wangu”Β Alinijibu, lengo langu lilikuwa kama wanafika niwape maelezoΒ waende nyumbani kwetu Tabora wakauze kibanda chetu ili wajeΒ kunikomboa pale gerezani, nilichoka sana.Β
Wao walilala maana ulikuwa ni usiku mwingi, ila Mimi nilikuwaΒ macho hadi Alfajiri ambapo tuliamshwa kwa ajili ya kazi, sikuΒ zote nilikuwa napewa kazi nafanya na wenzangu ila siku hiyoΒ ilikuwa tofauti sana, kwanza nilipelekwa kwenye kuvunja maweΒ adhabu ambayo hupewa Wafungwa waliofungwa kwa kosa laΒ Mauwaji. Pili niliambiwa natakiwa kuwa peke yangu, basiΒ nilipelekwa huko na Askari mmoja, kulikuwa ni eneo lenye MaweΒ yaliyochimbuliwa, nilipewa nyundo kubwa nilianza kazi yaΒ kuvunja mawe, Mchana ulipoingia nilisikia kengele kwa ajiliΒ ya kwenda kupata Chakula lakini yule askari alinizuiaΒ akaniambia siruhusiwi kula kwa siku hiyo.Β
Nilikubaliana na hali halisi, nilifanya kazi kwa bidii sanaΒ bila hata kutegea sababu nilijuwa yalikuwa ni maelekezo yaΒ Sarafina, Jioni nilipelekwa kulala kwenye chumba cha pekeΒ yangu, chumba hakikuwa na taa wala sehemu ya kulalia,Β palikuwa pamemwagwa maji kwenye sakafu. Basi niliketi, japoΒ nililoa lakini ilinilazimu kwani nisingeliweza kusimama kwaΒ muda woteΒ
Kweli aliyesema Maisha ni popote, msemo ulikuwa na maanaΒ kubwa sana, licha ya kutokula chochote lakini nililala kwenyeΒ sakafu yenye maji, niliuchapa Usingizi kutokana na zile kaziΒ ngumu. Usingizi ulinipitiliza hadi asubuhi sana, jua lilikuwaΒ limeshatoka nilipata kuushuhudia mwanga wake kupitiaΒ kidirisha kidogo ambacho kilikuwa juu pale kwenye kileΒ chumba, mazingira ya chumba yalikuwa maalum, kilionekana kuwaΒ ni chumba spesho.Β
Tofauti na vyumba vingine, chumba hicho kilikuwa na getiΒ lisiloonyesha nje, kilikuwa na michoro ukutani na harufu kaliΒ sana ya uchafu, wadudu walikuwa wakitembea kwenye ukuta,Β nilijiinua na kuketi pembeni nikiwa nimeegemea ukuta,Β nilijiuliza kwanini sikuamshwa siku hiyo, masaa yalisogeaΒ njaa ilizidi kuniuma, kiu ilizidi kunishika maana tokeaΒ nilivyokula na kunywa maji siku iliyopita sikula wala kunywaΒ maji tena.Β
Siku iliisha bila geti langu kufunguliwa, giza liliingia, KiuΒ ilinibana sana na njaa ilizidi kuniuma, niligonga nifunguliweΒ lakini hakuna aliyefungua mlango na hakukuwa na daliliΒ iliyoonesha kuwa kulikuwa na Watu karibu. Siku hiyo iliisha,Β Usiku uliingia, nilijaribu kuutafuta Usingizi lakiniΒ sikuupata, nilikaa macho hadi kulipopambazuka, mwili ulikuwaΒ na alama za kung’atwa na Wadudu na mbu.Β
“Mnifungulie nitakufa jamani” Nilisema kwa sauti isiyo naΒ nguvu kabisa, siku mbili bila kula tena nikitoka kufanya kaziΒ haikuwa rahisi kwangu kukabiliana na hali ile, haikusikikaΒ sauti yoyote upande ule, niligumia kwa muda mrefu hadiΒ nilikata tamaa ya Mtu kunisikia, nilirudi nikakaa chiniΒ nikaegemea ukuta nikiwa nimechoka sanaΒ
Baadaye kidogo nilisikia sauti ya geti langu kufunguliwa,Β niliamka haraka, ilitupwa bakuli moja kisha palifungwa,Β nilikimbilia kwanza getini kisha nilisemaΒ
“Mnitoe humu nitakufa, kwanini mnakuwa wakatili kiasi hicho,Β mnanitendea hivi kama nimeuwa?” Nilisema kwa sauti ya juu,Β sauti ya Mtu kutembea ilikoma kisha ukimya ulisikika,Β niligeuza macho yangu kwenye ile bakuliΒ
Nilisogea kuangalia kulikuwa kuna nini, niliifungua kishaΒ niliona Mchuzi mwepesi sana na kipande kidogo cha MuhogoΒ kilicho pikwa. Nililishika lile bakuri huku moyo ukiniumaΒ sana, yaani kukaa siku mbili bila kula alafu niletewe mchuziΒ na kipande kidogo cha muhogo? Nilitamani nimwage tu maanaΒ sikuona kama nilistahili, ila nilipokumbuka kuwa nipo JelaΒ nilifakamia mchuzi huo kisha nilikula muhogo.Β
Angalau kidogo nilikuwa nimekata kiu lakini njaa ilibakiaΒ pale pale. Sekunde chache nilikuwa nimemaliza kula kishaΒ nilikaa chini, Muda ulizidi kwenda, siku zilienda nikiwaΒ ndani ya chumba hicho cha Mateso.Β
Macho yangu yakazoea giza, Uchafu ukatawala mwili wangu,Β nilikojoa humo humo na kujisaidia haja kubwa humo humo, njaaΒ iliponizidi nilikula kinyesi changu sababu nilikuwaΒ nikiletewa supu kila baada ya siku mbili, nilianza kukonda naΒ kudhohofika, sura yangu ilinyauka kutokana na kukosa chakula.
Usiku mmoja nilikuja kuchukuliwa nikiwa hoi bin taabani, haliΒ yangu ilikuwa mbaya kupita maelezo, nilikuwa nimelegea sanaΒ hata kuongea siwezi, nilichokuwa nasubiria ni ujio wa MalaikaΒ mtoa roho pekee aje anichukue maana sikuwa na tumaini tena laΒ kuendelea kuishi.Β
Nilipelekwa kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa na taa,Β mbele yangu kulikuwa na meza iliyokuwa na chakula chaΒ kutosha, niliambiwa nile nishibe. Taratibu nilianza kulaΒ chakula kile ambacho kilikuwa cha moto hivyo kilinipa nguvuΒ sana.Β
Angalau nilipata unafuu sana, mwili uliingia nguvu hadiΒ nilipata uwezo wa kumuuliza Mdada aliyekuja kunichukua kuleΒ kwenye chumna chenye matesoΒ
“Kwanini mlitaka kuniuwa?” Nilimuuliza kwa sauti ya uchovuΒ kiasiΒ
“Majibu utayapata muda siyo mrefu” Alisema, niliendelea kulaΒ huku nikisubiria hayo majibu. Punde aliingia SarafinaΒ
“Jojo” Alisema kisha aliketi kwenye kiti, alichukua chakulaΒ kidogo akala kabla ya kusema chochote kile, nilimtazama sanaΒ SarafinaΒ
“Kwanini ulitaka kuniuwa Sarafina, ni kosa gani ambaloΒ halisameheki hadi kufikia hatua ya kutaka kuondoa uhaiΒ wangu?” Nilimuuliza Sarafina huku chozi likianzaΒ kunibubujika.Β
“Kiukweli sikutegemea baada ya muda huo uliokaa kule ungetokaΒ ukiwa hai Jojo, hakika wewe ni miongoni mwa wachache wenyeΒ roho ngumu sana, wengi walifia mle ila wewe umetoka, Hongera”Β Alinipongeza Sarafina, ila niliona kama ananikaidisha tuΒ
“Unanipongeza kwa lipi ikiwa ulitaka nife? Wewe ni mnyamaΒ Sarafina…hadithi ya Maisha yangu imebadilika ghafla sana”Β Nilisema huku nikiwa ninafuta chozi languΒ
“Sarafina, kama kifo changu kitakuwa furaha kwako usisiteΒ kunimaliza ili nipumzike hii mitihani mizito ambayo imekuwaΒ ikiniandama baada ya Mama yangu kufa, sitaki kuingia kwenyeΒ mtihani mwingine, imetosha, nimeteseka sana Mimi Sarafina,Β ona nimedhohofika sina hata nguvu” Nilisema kwa uchungu sanaΒ huku nikiwa ninabubujikwa mchozi.Β
Sarafina alifuta chozi lake lililokuwa linaanza kumtoka,Β stori yangu ilimfanya alie kidogo japo baadaye alijifanyaΒ haijamuumiza
“Sikia Jojo, ukiishi kwa kuhitaji huruma ya wengine utaishiaΒ kuishi Maisha ya hovyo sana. Lengo la kukutoa mle ni kutakaΒ kufanya na wewe baadhi ya Majukumu kisha utaachiliwa huru”Β Nilishtuka sana kusikia kuna majukumu nataka kupewa, nilifutaΒ chozi kisha nilimuulizaΒ
“Majukumu?”Β
“Ndiyo! Kwasasa angalia Afya yako kwa mwezi mzima kishaΒ utakapokuwa sawa nitakuchukua tena” Hakunipa hata nafasi yaΒ kumuuliza chochote kile, aliondoka zake. Yule Mdada mwingineΒ alisogea akaniambiaΒ
“Unapaswa kwenda Hospitali” Alininyanyua kisha alinitoa pale,Β Ulikuwa ni usiku mwingi sana, nilipelekwa Kwenye hospitali yaΒ pale pale Magereza.Β Β
Nini Kitaendeea?Β Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?Β
Usikose SEHEMU YA TISA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xxΒ
8 Comments
Nomaaaa
Kazi nzuriπͺπ₯π₯
Kaz nzuri πͺπ₯π₯
Nyie mnafikiri ni majukumu gani anapewa
Dah hii ya leo mpaka machoz
Dah pole Sana sarafina
Napenda tahalifa za kijiwen
f4lc82