Chozi lilikuwa likinimwagika, nilikuwa nikimuaga Mama yanguย kwa mara ya Mwisho Mkoani Tabora.ย
“Mama! Umeniacha Mama yangu, nimebaki mwenyewe” Nilisema kwaย sauti iliyowaumiza wengi, alikuja Mama mmoja alinishikaย vizuri akaniambiaย
“Jojo usilie sana utakufuru, Muache Mama yako apumzike kwaย Amani” Alisema kwa sauti iliyojaa maumivu pia sababu alikuwaย ni jirani yetu. Hadi Mama anafariki hakuwahi kunioneshaย mahali ambapo ndugu zake walikuwa wakiishi hata hivyo alikuwaย hapendi kuzungumza kuhusu ukoo wao.ย
Mama yangu alizikwa katika Ardhi ya Tabora, ukawa mwishoย wake, nilikumbuka maneno yake kuwa Kila siku Binadamuย wanakufa, walio hai wanakuwa kwenye hiyo foleni, kila mmojaย ataenda huko ambako Wafu huenda na hawarudi, alisemaย
“Jojo ipo siku tutatengana hatuta onana tena, nikitanguliaย ishi vizuri na Watu, niombee Mama yako” Alisema siku mojaย akiwa anaumwa, japo sikupenda sana kusikiliza kauli za Mamaย ambazo zilikuwa zikiniumiza. Hatimaye maneno yake yalitimia,ย aliniacha nikiwa bado namuhitaji sana.ย
Huzuni ilinijaa, siku mbili zilipita. Nilimkumbuka Mamaย yangu, alikuwa ni ndugu yangu pekee katika hii Dunia, baadaย ya Mama walifuata majirani zangu sababu hata Baba yanguย nilikuwa simjui.ย
“Pole Jojo, Mungu atakurudishia tabasamu lako siku moja”ย Alisema jirani mmoja ambaye alikuwa akichuma mboga katikaย Bustani yake ndogo iliyo kando ya nyumba yetu iliyo Bomokaย upande mmoja. Nilimtazama Mama Rafia, niliangalia nyumba yetuย kisha nilitabasamuย
“Ndio, Mungu hawezi kukusahau Jojo, amekupa kila kitu” Mamenoย ya Mama Rafia yalizidi kunipa tabasamu kidogo, nilikuwaย nimejikunyata nilimfuata alipokuwa anachuma mboga za majani
“Chukua kidogo ikusaidie leo” Alisema tena Mama Rafiaย
“Nashukuru Mama Rafia” Nilisema, Basi nilichuma kiasi kidogoย cha mboga kisha nilirudi ndani, Maisha hayakuwa mazuri paleย nyumbani, sikuwa na kazi yoyote ile.ย
Nilikagua Mkaa haukuwepo, Mafuta wala chumvi vyoteย havikuwepo, niliingia chumbani nilipekuwa kwenye begiย nilikuta pesa kama Shilingi elfu tatu na senti zake. Niliendaย kununua Mkaa wa shilingi Elfu moja na mahitaji mengine madogoย kisha Unga robo ili nisogeze Mchana huo.ย
Wakati narudi nilikutana na Mama Rafia, alikuwa ni Mamaย Mcheshi sana, alikuwa anapenda utani mno. Kila nilipomuonaย nilijihisi kupona maumivu yanguย
Nilipika chakula changu vizuri, nilikula, nilipata muda waย kupumzika na kutafakari nini nifanye. Umri wangu wa miaka 28ย haukunitosha kuhisi naweza nikajikwamua, nilishusha pumziย zangu maana kila nilichokuwa nakifikiria hakikunipa majibuย yenye uhakika, nilijiegesha Kitandani nikiwa natazama matunduย ya paa la bati alafu nilijikuta nikicheka maana ilikuwa kamaย chujio la tui la nazi vile.ย
Mara nilisikia sauti ya Mtu akiniita huko Nje, ilikuwa niย sauti ya Mkaka aliyeitwa Msonjoย
“Abee! Nakuja” Nilisema, nilijikurupusha kisha nilitokaย ndani, alikuwa Mkaka fulani hivi mcheshi na alikuwa maarufuย sana mtaani kwetu, alikuwa akiyajuwa fika Maisha yetu.ย
“Muarabuuu wa Tabora” Alisema Msonjo kwa utani, nilikuwa naย asili ya uarabuย
“Abee!” Niliitika nikiwa nafunga khanga yangu vizuri “Pole kwa kifo cha Mama yako Jojo” Alisema Msonjoย
“Nimeshapoa ndiyo Maisha, wacha apumzike ameumwa sana”ย Nilisema kisha nilifuta choziย
“Sasa Jojo, kwa jinsi ulivyo hupaswi kuishi Tabora, unatakiwaย kwenda kuishi Dar sababu huko ndio kuna Maisha mazuri yaย kuishi wewe na rangi yako” Alisema Msonjo, nilijiweka makiniย kumsikilizaย
“Una maanisha nini?” Nilimuuliza
“Kuna Bosi anatafuta wafanyakazi yupo Dar nikasema siweziย kukuacha ndugu yangu, ni bora ukatafute Maisha huko Mjini”ย Maneno yake yalinifanya nikumbuke nilichokuwa nakiwaza nikiwaย ndani.ย
“Kazi gani hiyo?”ย
“Mmh! Yeye ni tajiri tu sina hakika sana ila anahitajiย Wafanyakazi, utalipwa vizuri Jojo hebu angalia maisha yako,ย Mama hayupo tena unafikiri utaishi Maisha ya dhiki hadi lini”ย Alisema tena Msonjoย
“Nimekuelewa Msonjo ila nahitaji muda kupona kwanza kutokanaย na maumivu ya kumpoteza Mama kisha nikiwa tayari nitakuambia”ย Nilisemaย
“Mh! Haya…Maamuzi ni yako wewe! Ukiwa tayari utasema, alafuย upo na nani?”ย
“Hahaah! Msonjo hebu niache sitaki kucheka” Nilisema kishaย niliingia ndaniย
“Jojo mimi sina Mke kwahiyo kama ukiona vipi wewe niambie tu”ย Alisema kwa utani akiwa anaondoka, nilishamzoea kwa utaniย wake.ย
Nilipofika chumbani nilikaa kitandani nikatafakariย alichokisema Msonjo, ni kweli sikuwa na kazi na sikuwa naย tumaini lolote Tabora, kuhusu uzuri ni kweli nilikuwa mzuriย mno ila sasa uzuri ndio uwe kigezo cha Mimi kuishi Maishaย mazuri na kupata kazi? Nilicheka kidogo.ย
Siku zilienda, Maisha yalizidi kunichapa Tabora, nililalaย njaa, nilikula mlo usio na shibe, Mwezi mzima ulikatika.ย Nilimtafuta Msonjo kuhusu masuala ya kazi huko Dar.ย Alinieleza kazi yenyewe hadi mwili ulichoka yaani, ilikuwa niย kazi ya kuwa Baamediย
“Hiyo siwezi Msonjo nina shida lakini hiyo kazi hapana”ย Nilimwambia Msonjo huku nikiwa ninakaa juu ya Tofaliย
“Sasa kipi bora ulale njaa hapa Tabora au ukale Maisha Dar?ย Wewe kule unaenda kwa mipango na malengo yako, hauendi kuishiย Maisha ya Kibaamedi” Alisema Msonjoย
“Mh lakini Msonjo hakuna kazi nyingine?”ย
“Jojo, Mchagua jembe siyo Mkulima” Alisema Msonjo akawaย anaondoka, nilifikiria nikaona ni bora nikubali
“Msonjo” nilimuita, alisimama kisha alisogea nilipo “Nakusikiliza” Alisemaย
“Nipo tayari” nilisemaย
“Hayo ndiyo Maneno niliyotaka kusikia kutoka kwako Jojo, hapoย umenifurahisha ngoja nimpigie huyo Bosi” Alimpigia huyo Bosi,ย ilitumwa nauli muda huo huo, nilipaswa kujiandaa ili keshoย yake nianze safari kutoka Tabora kwenda Darย
Nilirudi nyumbani, nilimpa taarifa Mama Rafia, alinitafutiaย Mtu wa kuishi pale kwa kipindi chote ambacho nitakuwa Dar,ย Nilijiandaa, Usiku Msonjo alinieletea Tiketi ya Basi kishaย alinipa kiasi cha pesa kwa ajili ya matumizi nikiwa safarini,ย moyo ulikuwa ukinienda mbio, sikuwahi kwenda Dar ilikuwaย ndiyo mara yangu ya kwanza.ย
Alinipa namba ya huyo Bosi wa kazi, alikuwa ni Mwanaume, kwaย jinsi alivyonielekeza Msonjo Bosi alikuwa ni Mmiliki waย migodi huko kusini mwa Tanzania katika Mkoa wa Lindi.ย
Alfajiri safari ya kuelekea Dar ilianza. Ilikuwa ni safariย iliyojaa mawazo, nitaishi vipi, hiyo kazi sijui kamaย nitaiweza. Tulipofika Dar, nilikuja kupokelewa na Mdada mmojaย ambaye alijitambulisha kwangu kama Shonaa, alikuwa na umriย sawa na Mimi, ulikuwa ni usiku.ย
Tulienda moja kwa moja anapoishi Shonaa akaniambia kesho yakeย atanipeleka kwa huyo Bosi, nilikuwa nimechoka hivyo sikuwa naย maswali mengi zaidi ya kuhitaji Kupumzika tu, kweliย nilipumzika hadi asubuhi kulivyo pambazuka. Shonaa aliamkaย mapema sana, alikuwa amepangisha chumba kimoja na sebule,ย nilienda hadi sebleni nilimsalimiaย
“Mambo Dada?” Aliacha alichokuwa anakifanya kisha alitabasamuย akanijibuย
“Poa tu umeamka salama?” Aliniulizaย
“Ndiyo nipo sawa! Umedamka hivyo?” Nilimuulizaย
“Si unajuwa tena Maisha ya Mjini ndugu yangu, ukiendekezaย Usingizi utakufa masikini” Alisema kisha tulicheka, nilionaย nimepata Mtu wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali yanguย
“Jana ulisema utanipeleka kwa Bosi asubuhi hii” “Usijali, subiria nimalize kupasi nguo zangu” Alijibu Shonaaย
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILI ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx
13 Comments
Imeanza vzr sana
inaonekana ina mambo mazuri huko mbele
Iko vizuri na inaonekana ni yakuzunisha
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐
Vizur๐
Asantee adim
Hii story itakuwa tamu acha niendelee kuifatilia
Ni moto๐ฅ next please mwandishi๐
Kubal xan ๐
Nangoja muendelezo nahisi unakuwa na na visanga
Nmeipenda ila nlikua na wazo (ushauri)
Unajua kuandika mwandishi big up
zfaszw