Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mayele apewe Pesa tu! Ataendela Kubaki?
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Mayele apewe Pesa tu! Ataendela Kubaki?

    David MohamedBy David MohamedJune 15, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Baada ya kutetea taji lao la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mabosi wa Yanga wamesema katika uongozi wao wapo tayari kumuuza mchezaji yeyote ambaye watapokea ofa nzuri.

    Yanga ilitetea taji hilo kwa kuifunga Azam FC bao 1-0, fainali iliyochezwa Uwanja wa mkwakwani, jijini Tanga.

    Hivi karibu Yanga wamemuuza kiungo wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeenda Azam FC na kuna tetesi mshambuliaji wao bora Fiston Mayele huenda asiwe miongoni mwa mastaa wa timu hiyo msimu ujao. Fei ameuzwa kwa zaidi ya Sh200 milioni.

    Akizungumza mara baada ya fainali za kombe hilo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Gulamali alisema kama kuna timu inamhitaji Mayele na ikitoa pesa nzuri basi hawana budi kumuuza.

    Mayele

    “Hatuna sababu za kuzuia kumuuza mchezaji kama timu inayomtaka itatoa pesa nzuri, Yanga ni timu yenye wachezaji wazuri na wapo kwenye soko kwasasa na ndio maana tumepata mafanikio kwenye mashindano yote tuliyoshiriki msimu huu,” alisema Gulamali.

    Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said alisema mipango yao ya msimu ujao ni kuboresha kikosi chao zaidi.

    “Kwa sasa tulikuwa tunamalizia michezo yetu na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwa kutetea makombe yetu na tumeweza huku tukifika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika, ni mipango ambayo tulijiweke tangu miaka mitatu nyuma, hivyo nafanikio haya hayajaja kirahisi.

    “Kuhusu usajili wa msimu ujao ni jambo ambalo lipo mbele yetu, ikiwemo kuongeza mikataba wachezaji ambao imemalizika na tunahitaji kuendelea nao,” alisema Hersi.

    Soma hapa kwa taarifa zaidi za usajili.

    Fiston Mayele habari za yanga ligi kuu bara Mayele tetesi za usajili usajili yanga
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.