Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Tatu
“Ndio ishakuwa hiyo hairudi nyuma, akitaka unampa atakavyo”
Tulicheka kwa pamoja kuashiria tulikuwa tumefurahi wote kwa kilichotokea. Nikawa nahisi raha ile ya kusex na Jonas hata nikiwa darasani nililoa kila nilipomtazama, naye alihisi hilo. Endelea
SEHEMU YA NNE
Nilipotoka darasani alinifuata na kunipa mate na kunipapasa lakini hofu yangu ikawa kwenye kukeketwa, nikasema sitampa mapenzi Jonas hadi tulewe.
Ikawa ndio mchezo, tunapiga pombe kwanza ndio tunaenda kusex akawa ananipa pesa za matumizi mara mbili ya mwanzo, nikawa namtumia Mama zimsaidie hata hivyo baadae alizikataa huku akiniambia kuwa hakuwa na shida ya pesa.
Nilihisi ni vile aliona aibu tu kupokea zile pesa, nikawa nazitumia tu, hata zile Elfu 50 alizonipa Anko Sanga nilizitumbua chuoni mpaka marafiki zangu walishangaa, nilianza kuipenda pombe maana nilikuwa nikiitegemea kwenye kusex.
“Siku hizi Veronica yupo vizuri anapiga maji hatari, anatupita hata sisi wazoefu” yalikuwa ni maneno ya Sofia akimwambia Konzo.
Nilianza kuhisi nina ujauzito, nilitapika hovyo hata Wanachuo wengine walishtuka na minong’ono ikawa mingi kuwa nina mimba
“Chuo kizima wanajua una mimba Veronica, hukuwa muangalifu” “Wanasema nina mimba?”
“Ndio, tena taarifa zipo kila kona. Sijui kama Jonas hazijamfikia”
“Unasema sikuwa mwangalifu hivi nasex nikiwa nimelewa huo uangalifu unatokea wapi?”
“Itabidi umueleze mapema Jonas au unataka kuitoa juu juu?” “Kutoa mimba naogopa Konzo, ngoja niongee na Jonas kwanza”
Nilimtafuta Jonas na niliongea nae akaniuliza ninawaza nini kuhusu ujauzito,nilimueleza kuwa sikufikiria kuhusu kuitoa ile mimba maana nilikuwa muoga, alifurahi kisha akaniambia atailea
“Kuhusu kusoma Jonas?”
“Utasomaje na mimba my love?”
“Itakuwaje Naogopa Mama akijua nina mimba jonas”
“Twende kwenu kwa Mama yako mengine niachie mimi” Alisema, na kunihakikishia kuwa haitakuwa tatizo, nilimjua jinsi Mama yangu alivyonisihi kusoma.
Kila nilipo ongea nae aliniuliza jinsi masomo yalivyokuwa yakiendelea, nilimuhakikishia kuwa nitatimiza ndoto zangu na za kwake, sasa akisikia nina mimba sijui itakuwaje.
Nilianza kuwaza, sikuwa tena na muda wa kufuatilia masomo, Jonas alinichukua nikawa naishi kwake, alikuwa na nyumba aliyojengewa na Baba yake! Wazazi wake walikuwa huko Tabora baada ya kustaafu kazi ya Kuitumikia nchi kwenye vitengo nyeti vya Serikali, wakamjengea nyumba na kumpa uhuru wa kubakia Dar.
“Nyumba yenu ni nzuri Jonas, wazazi wako wakijua unakaa na Mwanamke watakuelewa?”
“Achana na hofu zisizo na msingi Veronica, nimeamua kuwa na wewe hivyo hakuna atakaye nipinga kwenye maamuzi yangu!” Jonas alikuwa ni Mwanaume mwenye misimamo yake, alitaka niwe huru kwenye kila jambo!
“Kuanzia leo sitaki unywe pombe, Utaharibu ujauzito” Alisema, nikaacha kabisa kunywa pombe, bado hofu yangu ya kukeketwa ilinitesa sana hadi nikamwambia Mama kuwa najihisi niko tofauti na Wanawake wengine, Mama akaniambia Wao ndio wako tofauti na mimi kwasababu mimi nipo kamili.
Kumbe nyakati zote hizi, Mama na Anko Sanga walikuwa wamekamilisha mambo yao, ile shuka yenye damu ilikuwa kama sadaka ya mambo ya Anko Sanga kufanikiwa, aliipeleka ile shuka kwa mganga wakapata pesa na akabadirisha Maisha ya Mama hata wakati namwambia nimtumie pesa zimsaidie hakuzihitaji sababu alikuwa nazo tena za kutosha tuu!
Tulipanga safari ya kwenda Arusha, Ili kumtambulisha Jonas kwa Mama yangu Mzazi,
Tulipofika Arusha nilijuwa naenda kwenye Uwanja wa vita ya pili ya Dunia, ningefanyaje na nina mimba? ilikuwa ni lazima nimueleze Mama, aliponiona alifurahi kuniona lakini ujio wangu ulimtatanisha baada ya Kumuona Jonas
“Huyu ni nani?” aliniuliza kwa Kilugha cha kwetu, lengo lake Jonas asijue ameuliza nini
“Ni mgeni Mama nitakutambulisha nyumbani”
“Veronica! Veronica! haya” Alisema, Mama huku tukiongoza kuelekea nyumbani, Mama alihisi tu kuwa niliyekuja nae hakuwa mgeni wa kawaida.
Tuliongea mambo machache kabla ya kuniuliza kuhusu chuo, bado nilimsistiza kuwa tutaongea nyumbani. Tulipofika nyumbani nilishangaa mazingira jinsi yalivyo badirika, Nyumba ilifanyiwa ukarabati, ilikuwa imeng’ara sana, sikutaka kumuuliza Mama japo kulikuwa na mabadiriko mengi sana.
“Karibu Jonas!” Nilimkaribisha kipenzi changu, Mama alinitazama kwa jicho la husuda hadi nikajiuliza mara mbilimbili.
“Mh! sio kwa mabadiliko haya Mama”
Hakunijibu, nafikiri alisubiria kuona utambulisho wa Jonas, nilianza kumtambulisha yule Mwanaume kwa Mama, alinisikiliza nilipomaliza aliniita nje
“Umesema yule ni nani?” Aliniuliza Mama baada ya kuniita nje, ni kama hakufurahishwa na utambulisho ule. Alionekana kuwa na hasira
“Ni mume wangu mtarajiwa Mama” nilisema kwa kutimiza wajibu tu wa kumjibu Mama yangu lakini alikuwa kwenye hasira
“Veronica nilikupeleka chuo ukasome na sio kuhangaika na wanaume, kwahiyo hakuna chuo tena?”
“Ndio Mama, sasa ni Mjamzito?”
“Unasemaje? Mja nini? Gharama zote ni kazi bure” aliongea Mama kisha alinivuta nywele
“Mama unaniumiza Aaaah”
“Mjinga wewe! Veronica umefanya nini”
Alinisema sana yaani hadi nilijisikia hovyo nikaanza kutapika, Jonas alivyosikia natapika alinifuata ili kunihudumia, Mama akampiga kikumbo wakati wanapishana Mlangoni, Jonas akamuomba msamaha Mama kwa kitendo kile lakini Mama hakujibu aliingia ndani.
“Upo salama Veronica?” alinishika huku nikiendelea kutapika, uwepo wa Jonas ulinifanya nijisikie vizuri kila nilipomtazama nilijihisi ni mwenye bahati, alikuwa akijua jinsi ya kumjali Mwanamke.
Alikaa na mimi hadi nilipomaliza kutapika, alinipeleka sebleni kisha akanilaza kwenye kochi, akaelekea Jikoni ambako alisikia purukushani, alipofika alimkuta Mama yangu
“Samahani Mama, naweza kupata Uji na limao?” alimuuliza Mama kwa heshima zote
“Uji na Limao? ulipokuwa unampachika ujauzito uliniomba ruhusa?” Mama alijibu kwa jaziba sana nilikuwa nikisikia maongezi yao, sikuwa na nguvu ya kuongea kabisa, nilimjua Mama yangu jinsi alivyo Mkaksi
“Hapana Mama, Veronica hajisikii vizuri ndio maana nimekuuliza hivyo. Nisamehe kama nimekukwaza hata hivyo ninaweza nikatengeneza mwenyewe”
“Hivi ndivyo ambavyo watoto wajeuri huongea, utengeneze uji kwenye nyumba za watu ndio adabu uliyofundishwa? Huyu Veronica anakupa jeuri sana sasa tutaona Kama kuna kitakachoendelea”
“Unamaanisha nini Mama?”
“Utanielewa taratibu” Mama aliondoka, Jonas alibakia akiwa haelewi yale Maneno ya Mama yalitokana na nini, basi alipoangaza aliona jiko la gesi akaliwasha na kuweka Maji, akatafuta unga akaweka kwenye Maji kisha akaanza mapishi yake.
Akaenda kununua Limao gengeni akaweka kwenye uji kisha akaniletea, nilimuonea huruma jinsi alivyonijali, alikuwa akivuja jasho, rangi yake nyeupe iligeuka kuwa nyekundu.
“Hujazoea haya Maisha Jonas?” Nilimuuliza baada ya kupata nguvu, uji ulinisaidia maana nilitapika sana na kupoteza maji na chakula nilichokuwa nimekula.
“Hata kama sijazoea napaswa kuzoea sababu ndio mazingira niliyopo Veronica”
“Unateseka kisa mimi Jonas?”
“Sio wewe tu, bali na Mtoto aliye tumboni” Tulijikuta tukicheka na kufurahi hadi usiku ulipoingia, Umeme ulizimika usiku kukawa na giza, Mama alikuwa amejifungia chumbani kwake.
“Hatuwezi kulala hapa na mbu hivi Veronica, utaugua Malari na Mama mjamzito hapaswi kung’atwa na Mbu” alisema Jonas huku akinishauri nikagonge kwenye mlango wa Mama
“Unapenda kusikia maneno yake ya kukera?”
“Hata kama ana maneno kiasi gani, ni lazima ulale ndani ya chandarua. Kama itawezekana ukalale nae alafu mimi nitalala hapa”
“Oooooh Mungu wangu” nilinyanyuka na kuelekea kugonga Mlango, vyumba vingine vilikuwa vimefungwa.
Nilimgongea Mama zaidi ya mara tatu, mara ya nne alifungua mlango
“Unasemaje?” aliuliza kwa kisirani hadi nikaogopa. “Mama naomba funguo ya chumba kimoja ili nilale na Jonas”
“Ulale na Jonas? hivi una akili wewe? nyumba yangu ulale na Mwanaume?” Nilikaa kimya kumsikiliza maana ningemjibu angeweza hata kutufukuza. Alipomaliza kuongea aliingia chumbani kwake, nilisimama hadi nikakata tamaa ila wakati naondoka nilisikia mlango ukifunguliwa na ufunguo ukatupwa chini kisha Mlango ukafungwa tena.
Niliwasha tochi ya simu na kuuokota bila kujua utakuwa unafungua mlango gani kati ya Milango ile minne, Jonas alinisaidia kujaribu hadi tulipopata chumba husika.
Mle kulikuwa na kitanda nilichokuwa nakilalia zamani, vitu vingi vilikuwa ni vile nilivyo viacha. Kulikuwa na vumbi, tulifanya usafi mdogo usiku uleule, tulipomaliza tukawa hoi tumechoka.
“Inabidi tukaoge” Alisema Jonas, ni kweli maana jasho lilikuwa limetutapakaa mno
“Sasa inabidi nikaanze ndipo ukaoge wewe maana Mama akitusikia itakuwa shida”
“Sawa nakusubiria” Nilianza kwenda kuoga, niliporudi naye alielekea kuoga. Kutokana na uchovu wa safari na ile mimba nilijikuta nikizama usingizini, Jonas hakurudi kabisa hadi majira ya saa 8 usiku niliposhtuka.
Nilipoangaza sikumuona kabisa Jonas, nilipapasa bahati nzuri umeme ulikuwa umerudi niliamka na kuwasha taa.
Sikupata kumuona wala kumsikia, nilichanganikiwa, ikabidi nikamuangalie sebleni, nilimkuta akiwa amelala sebleni. Nilimuamsha kisha tulielekea Chumbani
“Unalala pale na mbu wale Jonas?”
“sijui hata nimewezaje kulala pale Veronica, nakumbuka mara ya mwisho nilienda bafuni kuoga, nilijikuta nikipata kizunguzungu tu sikujua kilichoendelea hadi nimekuta pale”
“Mh! kutoka bafuni hadi Sebleni?” kiukweli ilichekesha Mtu atoke Bafuni ambapo ilikuwa ikitazamana na chumba chetu aelekee Sebleni ambako ni mbali
“Usinichekeshe Usiku huu” Nilisema
“Ni kweli Veronica sijui nimefikaje kule” ilikuwa kama hadithi iliyosadikiwa tu huku ukweli wa tukio ukibakia kuwa wa kuchekesha.
Basi tulilala hadi asubuhi kulipo pambazuka, mimi niliamka kwasababu nililala vizuri lakini Jonas nilimuacha akiwa bado amelala, nilimgongea Mama mara kadhaa lakini sikusikia majibu kutoka kwake, ndipo nikaelekea nje. Kulikuwa na jirani mmoja alikuwa akifanya usafi nje, alikuwa akinifahamu maana nimeishi pale kwa miaka mingi sana. Aliponiona alifurahi alafu akanisalimia kwa mbwembwe zote.
“Nimekusikia ukimuita Mama yako!”
“Ndio, lakini sipati majibu”
“Ametoka mapema sana, gari ndogo imemchukua Alfajiri” “Eeh! ameenda wapi tena?”
“Ina maana ametoka bila kukuaga binti yake?” Nilipoona ananiuliza maswali ya kimbea nilimuaga na kuelekea ndani.
Niliandaa chai ili Jonas akiamka ale maana tulilala bila kula alafu nilikuwa nikihisi njaa sana, nilipomuangalia nilimkuta akiwa amelala sikutaka kumuamsha, alipoamka alinikuta sebleni nikiwa nimekaa. Tulijumuika kunywa chai pamoja baada ya kumaliza tulirudi chumbani kwetu, hatukumuona Mama kwa zaidi ya siku saba pasipo kujua alienda wapi, hakutaka kabisa kupokea simu
“Ni mtu mzima huyo anajua anachokifanya” Alisema Jonas “Sikatai lakini ni maisha gani haya? tuondoke basi”
“Lengo la kuja huku ni kumpa taarifa Mama lakini hatuwezi kuondoka bila yeye kiridhia, Veronica mpenzi tuvumilie tu hadi pale hasira zake zitakapoisha”
“Kwanini Mama ananifanyia hivi mimi, kama hakunizaa yeye?” nilijiuliza baada ya kukumbuka tukio la kubakwa na Anko Sanga ambapo Kwa maelezo ya Mama ilionesha kuwa alikuwa akijua kila kitu .
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
3 Comments
Fupii
Nzuri Ila fupi
Ya leo Ni Fupi Saana