Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Tisa 

Siku iliyofuata nilitakiwa kuelezea kilichoendelea baada ya  kuhamishwa kwenye ile nyumba na kupelekwa nyumba nyingine,  niliketi kwenye kiti nikiwa nimezungukwa na wale Mawakili  akiwemo yule aliyeajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwa  akimlea Mtoto wangu kwa sasa. 

“Hujazungumzia Maisha ya Jonas akiwa kwenye mahusiano na Mama  yako?” 

“Vipi kuhusu Anko wako! Alikufa au alikimbia?” 

“Je, uliwezaje kutoka?” Endelea

SEHEMU YA KUMI

Yalikuwa ni maswali machache yaliyoelekezwa kwangu na wale  Mawakili, nilivuta pumzi kisha niliendelea kuwasimulia jinsi  ilivyokuwa.

Nyumba ile ilikuwa nje ya Mji pia, ilikuwa  tulivu na kulikuwa na mlinzi, Anko Sanga alikuwa haishi pale  tofauti na ilivyokuwa mara ya kwanza nilikuwa nikiishi nae  kule kwenye nyumba nyingine, alikuwa akija kutimiza haja zake  za kimapenzi kama kawaida kwani ndio ulikuwa msingi wao wa  kuendelea kuwa Matajiri. 

Upande wa Jonas alikuwa akiishi na Mama, naye alikuwa  akitumika lakini utofauti wa yeye na mimi ni kuwa yeye  alikuwa kama Msukule tu alifanya vitu kwa dawa alizowekewa na  Mama na sio kwa moyo wake, mimi nilikuwa nikifanya kwa  lazima. 

Mlinzi wa pale Nyumbani alikuwa akizunguka huku na kule,  nyumba hii haikuwa ya ghorofa bali ilikuwa ya kawaida tu  lakini ilitegemea pia nitoke kwa kutumia mlango, siku moja  nilimuita yule Mlinzi, hata yeye hakujua ni kwanini nilikuwa  sitakiwi kutoka ndani, alipokuja tulianza kuongea 

“Bosi amesema sipaswi kuongea na wewe, natakiwa nihakikishe  hautoki” Alisema 

“Sasa haujamuuliza kwanini?” 

“Sijamuuliza” 

“Unamzuia Mtu na hujui kwanini?” 

“Natakiwa kuifanya kazi iliyonileta hapa” 

“Sikia, Mimi ni Mke wake ndio maana hataki sababu amegundua  nina mwanaume mwingine” Nilianza kumuongopea ili kutengeneza  ukaribu maana nilijua nikimwambia ukweli ataanza kuniogopa. 

“Oohoo! Wanawake bwana. Sasa unamsaliti Mtu ana hela namna  hii?” 

“Unafikiria pesa ndio kila kitu? hapana Mapenzi yana umuhimu  Mkubwa kuliko hata hiyo pesa unayoiongelea” 

“Ha!ha! usinichekeshe mie, ina maana wewe Mke wa tajiri  unaweza ukatoka kimpenzi na mimi mlinzi eti kisa Mapenzi?”  aliongea akiwa anajipigia debe, sasa nilifanikiwa kuujua  udhahifu wake ulipo

“Anhaa! kumbe kupitia huyu ninaweza kikatoka hapa nikiwa hai  kabisa” Nilijisema nikiwa nimeangusha tabasamu, tulikuwa  tukizungumza kupitia dirisha. 

“Sasa kisichowezekana ni nini? Mnajidanganya wanaume kwa  kuamini pesa ndio inafanya wanawake wakupendeni, au labda  uzuri wa sura ndio humvutia Mwanaume, si unaona kama mimi  napenda mapenzi ya kweli tuu na sio pesa” Yule Mlinzi  alicheka cheka kama Zuzu vile, kwenye mpira wanasema kosa  moja unaadhibiwa kwa kufungwa goli moja, sasa kosa moja  alilolifanya Anko Sanga ni kuweka yule mlinzi pasipo  kumuelekeza mazingira yalivyo. 

“Unaitwa nani?” nilimuuliza 

“Joji” 

“Nashukuru kukufahamu Joji” nilisema kisha nilihakikisha  namvuta kwangu ili anisaidie baada ya maongezi aliondoka na  kurudi getini, haikuchelewa sana alikuja Mtu wa pikipiki  akampatia mzigo Joji, Mzigo ulikuwa wangu. 

nilipoufungua nilikuta picha za Mtoto wangu Moyo,  nilifarijika sana kwani nilimuomba Anko Sanga anisaidie hilo  jambo ili niweze kumuona binti yangu japo kwa picha tuu.  Nilimuita Joji na kumuonyesha zile picha kwa kutumia dirisha 

“Hivi Joji si unifungulie tuongee vizuri?” 

“Sina funguo za hapo Dada ningekufungulia angalau uote jua” 

“Anhaa usijali” Nilianza kugundua baadhi ya vitu, na ndicho  nilichokuwa nakihitaji. 

Kilikuwa kipindi cha masika na mvua zilianza kunyesha, Joji  akakimbilia kwenye kibanda chake, nikasema nitahakikisha  ananisaidia ili nitoke pale. Nilivua nguo zangu na tayari  giza lilikuwa limeingia, nilimuona akiwa anapika kwenye  kibanda chake ambacho kilikuwa karibu na geti, nilichukua  sturi nikasimama nikiwa Uchi wa mnyama nikiwa nimewasha taa. 

Nilikuwa karibu na dirisha, nilifungua pazia zote ili tu  kumuonyesha Joji mwili wangu. Sikuuona uthamani wa mwili  wangu ikiwa Anko Sanga alikuwa akiutumia atakavyo. Nilikuwa  nikijishikashika mwilini kama vile mnenguaji wa bendi fulani  kwenye kumbi za starehe. 

Nilifanya hivyo kwa dakika kadhaa kisha nilishuka na kuzima  taa, nilipochungulia dirishani nilimuona Joji akikimbia  kukatiza mvua kurudi kwenye kibanda chake!

“Mtego wa Mwanaume ni ngono” Nilisema nikiwa ninavalia nguo  zangu, kwa ishara ile niliona ni kweli nilifanikiwa kumfanya  Joji kama toi la kuchezea Watoto, sikuwa na nguvu ya kusema  nipambane nae ili nitoke bali niliutumia udhaifu kutafuta  njia ya kutoka pale ndani. 

Asubuhi mapema Joji aligonga dirisha langu, niliposikia sauti  yake nilienda dirishani. 

“Umeamkaje Dada Vero?” 

“Salama sijui wewe kipenzi” Nilivyomuita kipenzi ndio akawa  anacheka cheka 

“Nimeamka poa nikasema nije kukujulia hali yako” “Anhaa! sasa Joji ninashida ya simu” 

“Mbona mimi sina simu? boss amesema sitakiwi kuwa na simu” 

“anhaa kumbe! huwagi na hamu ya kwenda kutafuta mabinti huko  nje au unaogopa kumsaliti Mkeo” 

“Ha!ha!ha! sina Mke mimi, hata hivyo kutoka hapa hadi kwenda  kwenye makazi ya Watu ni zaidi ya Kilomita 90” 

“Unasemaje? kwani hapa ni wapi?” nilikumbuka hata nilipoletwa  pale nilikuwa nimefungwa kitambaa usoni ili nisijue naenda  wapi 

“Msituni karibu na mpaka wa Kenya” Kauli ya Joji ilinivunja  Moyo kabisa niliona ugumu ulio mbeleni 

“Mbona umeshtuka hivyo kwani hakukwambia?” 

“Tuachane na hilo Joji, nataka nikaoge alafu nitakushtua  baadae” Joji aliondoka nami nilienda kuoga kisha nilipika  chakula, kilipokuwa tayari nilimpa Joji 

“Ahsante sana, Boss ameniambia nisichukue kitu kutoka kwako  wala mimi kukupa chochote” 

“Anhaa! sasa Joji, nimekaa huku kwa takribani wiki sasa  natamani sana kuwa na mtu karibu nimevumilia nimeshindwa”  Nilianza kumtega makusudi kabla hajanijibu tulisikia honi ya  gari, haraka Joji alikimbilia geti. 

Alimfungulia geti Anko Sanga, hapana shaka alikuwa anataka  penzi maana ndicho ambacho huwa kinamleta, lakini alikuwa na mizigo ya chakula. Joji alimsaidia kuingiza ndani, ikawa ndio  mara ya kwanza kwa Joji kuingia ndani. 

Nilimuonesha sura ya kikauzu ili asilete mazoea mbele ya Anko  Sanga, aliketi akaniambia kuwa Jonas ana hali mbaya  amepelekwa hospitali 

“Anaumwa nini?” 

“Amepata ajali ya gari” 

“Nilijua mnanitaka mimi tu, kumbe hata Jonas pia?” 

“Nitolee upuuzi wako hapa, nimeamua tu kukupa taarifa  vinginevyo usingejua chochote, heshimu hilo” 

“Tafadhari naomba nimuone japo mara moja tu, najua hawezi  kupona hadi unakuja kuniambia hapa, ikishindikaana mimi  kumuona basi hata binti yake amuone Baba yake japo kidogo,  amjue kama ndio Baba yake” Tulikuwa tukiongea chumbani wakati  huo Joji akiwa ameondoka. 

Hakunijibu sababu hakupenda sana kujibu masuala mengi  niliyomuuliza hasa yaliyohusu familia yangu. Badala yake  nilimuona akivua nguo zake na kupaka dude lake mafuta,  alilichezea hadi likasimama na jinsi lilivyo refu, alinifuata  na kunilaza chali kisha aliniondoa chupi, Nilishazoea haya  maisha lakini kipaumbele changu kilikuwa ni kutoroka siku  moja. 

Aliniingiza dude lake hadi lilipozama lote akawa ananifanya,  nikaanza kupiga kelele za mahaba ili tu Joji asikie kuwa  nikilikuwa nikiliwa, lengo langu ni kumhamasisha ili nione  atatumia akili gani ya kiume kuingia ndani wakati ambao Anko  sanga atakuwa ameondoka. 

Alinifanya kwa dakika 15 tu kisha alivalia suruali yake na  kuwasha gari, akaondoka zake. Nikaenda dirishani kumuangalia  Joji akiwa anafunga geti, akaja hadi dirishani kuniita maana  alishaanza kupenda kupiga stori na mimi. 

“Mbona unatabasamu hivyo jamni Joji” 

“Hapana nimefurahishwa tuu” 

“umefurahi na nini?” 

“Kukuona tu Dada Vero” 

“Njoo Basi ndani Joji ukate kiu yako

“Kiu? yanini” 

“Kuniona alafu nikupe kitu kitamu zaidi” 

“Sasa nitaweza vipi kuingia ndani jamani wakati mlango  umefungwa na geti la nje pia?” 

“We mwanaume Bwana unashindwa hata kutumia mawazo machache  uliyonayo, sio kila kizuri huliwa kwa sheria vingine huliwa  kwa kuvunja sheria” Niliongea kwa kurembua sana, nililazimika  kufanya hivi sio kwa Mapenzi yangu bali nipate kutoka mle  ndani. 

Nilimuona Joji akiwaza jambo, nilimtazama kisha aliniambia “Ngoja nizunguke huku nyuma niangalie cha kufanya” 

“Sawa mpenzi nakusubiria wewe tu” Kweli Joji alizunguka nyuma  ya nyumba kisha nilimsikia akiniita kutokea chooni alinitaka  nimfungulie mlango, nilikimbilia Chooni nilimuona akiwa  anapenya kwenye dirisha dogo la juu kabisa mwa ile choo,  alikuwa akipita kwa kujilazimisha sana nilimuona jinsi  alivyokuwa akiumia hadi akafanikiwa kuingia ndani tena kwa  kuanguka, nilimsikia akilalamika 

“Oooh! Mkonoooo” 

“Pole jamani Kidume, pole sana” nilisema kisha tulielekea  chumbani, akaenda pale dirishani kuchungulia 

“Anhaa! kumbe huwa unaniona kwa staili hii Dada Vero?” 

“Ha!ha! Usiniite Dada, niite jina langu” Niliongea huku  nikimpiga busu, palepale nikaona jinsi dudu lake  lilivyosisimka, alikuwa akiniangalia kwa uchu sana, nilijua  tu alikuwa amekaa kitambo bila kufanya mapenzi. 

Nilimvua shati kisha nilimwambia anisubiri kidogo nakuja,  alikubali nilitoka pale chumbani, nilienda hadi kwenye begi  langu nikatoa Picha ya Mtoto wangu, nikaipeleka chooni, kisha  nilichukua vidonge vya usingizi nikaviponda na kuvitia kwenye  juisi, nilikuwa nikivitumia vidonge hivi kwasababu nilikuwa  nakosa usingizi kabisa. Niliogopa kutia vidonge vingi  angeweza kushtuka hivyo nilimtilia kidogo tu, nilitaka  kuondoka Siku hiyo maana nilijua kama nitamwambia Joji  ingechukua siku nyingine kutoka pale na sikuwa tayari kumpa  Uchi wangu!

“Samahani kwa kuchelewa” niliongea baada ya kuwa nimekwisha  ingia chumbani, nilimuona akiwa ameshavua nguo zote  amejifunika taulo tu, yaani alikuwa amejiandaa kwa mchezo. 

Nilimpa ile juisi kisha nilimwambia anywe apunguze presha,  kwa jinsi alivyo na papara aliinywa yote kisha nilimfuata na  kuanza kumchezea, nilimchezea hadi nilipohakikisha ana anza  kulegea, hadi alipopitiwa na usingizi. 

Haraka nilivalia nguo zangu, nikaenda chooni nikaichukua ile  picha na kuiweka kwenye mfuko wa suruali niliyoivaa.  Nilipoangalia pale alipopitia Joji palikuwa juu sana nikaenda  kuchukua Viti nikavibebanisha kisha nikapanda, wakati  nahangaika pale nilijikuta nikitereza kutoka juu ya kiti hadi  nikaangukia chini kama mzigo, nikahisi maumivu ya mguu lakini  nikasema nitajitahidi hadi nitakapo fanikiwa kuondoka zangu,  nilifanya jaribio la kupanda tena juu ya vile viti. 

Nilishika bomba la maji ambalo lilinisogeza hadi kwenye lile  dirisha dogo nikapitisha kichwa changu, nilijikuta natokwa na  machozi baada ya kupigwa na kaupepo, nilivuka nikajirusha  hadi nje. Kwanza nilimshukuru Mungu kwa ile hatua niliyofikia  maana ndio ilikuwa nafasi pekee ya kutoka pale. 

Japo nilikuwa na maumivu ya Mguu, ndipo niliposikia sauti ya  Joji ikiniita, hata kabla sijapiga hatua nilisikia honi ya  gari pale getini, ni wazi kuwa kulikuwa na gari iliyokuwa  ikitaka kuingia, nilijua tu atakuwa ni Anko Sanga maana  alikuwa na machale sana. 

Nilijibanza pale pale, Joji aliposikia ile honi akataka atoke  haraka akafungue geti ili ionekane hakuniona nikiwa  ninatoroka, 

“Veronica najua unanisikia, usifanye jaribio la kuondoka  tafadhari” Aliongea Joji akiwa anapanda atokee kwenye lile  dirisha, nikasema liwalo na liwe pembeni kulikuwa na kipande  cha mti uliokauka niliuchukua na kukaa makini nikitazama pale  ambapo angetokea, Honi ilipigwa zaidi ya mara saba hatimaye  ukimya ulitawala. 

Joji alipotokeza kichwa chake nilimpiga na kile kipande cha  Mti, nilimpiga tena na tena akiwa hawezi hata kurudi nyuma,  nilihakikisha nampiga hadi azimie na ndicho kilichotokea  nilimpiga hadi nikamuaribu ile sura yake, damu zikawa  zinamtoka kama bomba la maji lililo pasuka, kwakuwa ilikuwa  ni nyuma ya nyumba hakukuwa na shida yoyote, nilimuacha akiwa  juu ananing’inia. 

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA KUMI NA MOJA

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

6 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version