Ilipoishia “Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, Luciaย aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwaoย Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongozaย Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambiaย
“Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe Mimiย siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa.. Endeleaย
SEHEMU YA NANE
“Aaah usijali samahani kwa hilo, tunapita kushoto ili tuwahiย kufika” Alisema Mwanaume huyo kisha alikata kushoto lakiniย Lucia alimuulizaย
“Huko barabara imefungwa kuna ujenzi utapita vipi alafu kunaย pori kubwa huko” Alisema Lucia jamaa alizidi kuongeza giaย kisha alicheka, ndipo Lucia alipomkumbuka Desmond na kauliย yake, basi Lucia akaanza kuhangaika ili ashuke maana alijuwaย hapo ni lazima atafanyiwa kitu kibaya, kumbuka Tayari maagizoย ya kuuawa kwa Lucia yalikuwa yametolewa na Desmond, katikaย pirikapirika gari hiyo ikajikuta ikipoteza uelekeo na kugongaย Mti.ย
Hali zao zilikuwa mbaya mno, Lucia alijitahidi kufunguaย mlango akiwa hoi damu zikiwa zinamtoka, Mwanaume huyo nayeย alikuwa akitokwa na Damu usoni, naye alifungua mlango akaanzaย kumfukuza Lucia aliyekimbilia porini eneo ambalo lilikuwa naย mlima hivi. Akiwa anazidi kukimbia Lucia alimpigia sana simuย Noela lakini simu haikupokelewa, katika kukimbia akajikutaย ameindondosha simu yake.ย
Mwanaume huyo aliiokota simu ya Lucia kisha aliendeleaย kumfukuza, bahati mbaya Lucia alijikwaa akaanguka chini, maraย moja Mwanaume huyo akiwa ana vuja damu alimfikia.ย
“Wewe ni Nani na unataka nini?” aliuliza Lucia akiwa katikaย hali ya hofu sana huku akiwa amechoka.ย
“Unataka kujua mimi ni nani na Nataka nini kwako si ndiyo?ย Mimi ni muuwaji nimekuja kuchukua roho yako Lucia” Alisemaย Mwanaume huyo akionekana kumfahamu vizuri sana Lucia
“Uniuwe kwa kosa gani mbona sikufahamu?” aliuliza Lucia akiwaย katika hali ya hofu huku maumivu ya Mguu yakizidi kumtafuna.ย
“Kosa lako ni Moja tu, kujifanya mjuwaji. Umeonywa mara ngapiย kuhusu Mandy wewe?” aliuliza Mwanaume huyo na kumfanya Luciaย sasa ajuwe kuwa Desmond alishatuma Mtu ili auawe.ย
“Ina maana umetumwa na Desmond si ndiyo? unafikiri ukiniuwaย itakuwa mwisho wa kila kitu? nakuhakikishia kifo changuย hakitofanya siri yenu isitoke, tena itatoka kwa kishindoย kikubwa sana” Alisema Lucia katika hali ya kujiamini sanaย baada ya kujuwa kuwa alitakiwa kufa kwa maagizo ya Desmondย
Yule Mwanaume alimbana vizuri Lucia pale chini akahakikishaย anakosa hewa kwa zaidi ya dakika moja kabla ya kunyongaย shingo ya Lucia, baada ya hapo alipiga simu mahali akasemaย
“Kazi imeisha” Alisema kisha aliubeba mwili wa Lucia akaendaย kuuweka kando ya Barabara hiyo ambayo ilikuwa na giza sanaย kisha akaliwasha gari lake lililobamiza kwenye Mti kishaย aliondoka eneo hilo.ย
Shughuli ilikuwa imepamba moto, Noela hakumuona Lucia akiendaย hapo licha ya kuarikwa, hakujuwa kuwa Lucia alikuwa ameuawaย porini. Desmond alimuuliza Noela alikuwa akifikiria niniย baada ya kumuona akiwa kama Mtu mwenye kutafakari jamboย
“Rafiki yangu Lucia, alisema anakuja hadi sasa hivi, nampigiaย simu hapatikani” Alisema Noelaย
“Atakuja tu, Watu wengine ndio kwanza wanaingia hivyo nayeย ataingia tu” Alisema Desmond huku akijuwa fika kuwa Luciaย alikuwa ameuawa.ย
Muda ulienda bila Lucia kutokea eneo hilo, shughuliย ilifanyika kwa bashasha zote. Desmond akawa mchumba rasmi waย Noela, ilikuwa ni siku yenye furaha sana Kwa Noela na Mamaย yake sababu jambo hilo lilisubiriwa kwa muda mrefu, basiย zikapigwa picha za kutosha, Watu walikula hadi kusaza, Furahaย ilitawala usiku huo. Baada ya kuisha tukio hilo, Desmondย aliaga ili aondoke lakini alimuona Mtu mmoja aliyemfananishaย akiwa ameketi mahali anazungumza na Mwanume mmoja.ย
Desmond alimtazama sana Mwanaume huyo huku akijiulizaย alimuona wapi, akakumbuka alimuona siku ambayo aliliona gariย lake likiwa maegesho ofisini wakati gari hilo alilitumbukizaย baharini, alikuwa hamfahamu Mtu huyo na wala hakumuarika, ilaย hakutaka kulipa uzito jambo hilo maana kama hakuarikwa naย yeye basi atakuwa amearikwa na Mpenzi wake Noela.
Akaendelea kuaga Watu kwa ajili ya kuondoka eneo hilo, ghaflaย aliguswa begani na Msichana mmoja ambaye alikuwa akihudumiaย Watu vinywaji, msichana huyo alimpa Desmond ujumbe waย karatsi, Desmond akamuuliza Msichana huyoย
“Ametoa Nani?”ย
“Mkaka yule…” Msichana huyo alipoonyesha alipokaa Mtuย aliyetoa ujumbe huo hakuwepo hapo, akaanza kumtafuta kwaย macho lakini hakumuona ila Desmond alimuona mwanzo Mtuย aliyekaa hapo, alikuwa ni yule Mwanaume aliyemuona ofisiniย kwakeย
“Haya sawa asante” Alisema Desmond, kisha alisogea pembeniย akafungua ujumbe huo akakuta maneno yaliyosomekaย
“LUCIA AMEKUFA LAKINI SIYO MWISHO, TUKUTANE JUMATATU KATIKAย HOTELI YA HAVANA SAA 7 MCHANA!! CHUMBA NAMBA 43, NINAย USHAHIDI WA ULIYOYAFANYA”ย
Desmond alishtuka sana, alimtafuta Mwanaume huyo bilaย mafanikio, alitoka nje kabisa lakini hakufanikiwa hataย kumuona Mtu huyo alijikuta akichoka mwili na akili, Mtu waย tatu bado aliendelea kumtesa lakini bahati nzuri aliifahamuย sura yake, alimuita Mwanasheria Joel kisha waliondoka hapoย kwa ajili ya kujadili ni jinsi gani watamkabili Mtu huyo.ย
Noela alilala fofo baada ya kunywa pombe vya kutosha, aliamkaย siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni Jumatatu, akili yakeย ikamwambia kuwa siku hiyo hawezi kufanya chochote zaidi yaย kupumzika tu, lakini baadaye alifikiria kuhusu Lucia,ย alijaribu tena kupiga simu ya Lucia lakini haikuita kabisa.ย
Alianza kupata mashaka pengine amepata tatizo ila hakuwa naย Mtu wa kumuuliza, aliwasha Tv ili aangalie habari za hapa naย pale, ndipo alipokutana na taarifa ya kifo cha nesi Luciaย aliyeuawa kwa kunyongwa shingo hadi kufa, Roho ilimripukaย sana Noelaย
Alishtuka sana kusikia taarifa hiyo na kibaya zaidi ni kuwaย aliacha Mama ambaye ni mgonjwa sana, mara moja Noela alivaliaย nguo zake akamuaga Mama yake kisha akaelekea mahali ambapoย maiti ya Lucia ilikuwa imehifadhiwa, ni katika ile ileย Hospitali ambayo Lucia alikuwa akifanyia kazi, alikutana naย Daktari Mkuu wa hiyo Hospitali akawa anazungumza naye.ย
Mkuu huyo alimuelezea Lucia kwa jinsi alivyoweza mbele yaย Noela, kikubwa zaidi Noela alikufa akiwa masikini, piliย alikuwa na ndoto za kuja kuwa Nesi bora zaidi katikaย Hospitali hiyo na tatu aliacha Mgonjwa aliye katika haliย mbaya sana.ย
“Mgonjwa aliye katika hali mbaya?” Alihoji Noelaย
“Ndiyo! alikuwa akimuhudumia kwa kipindi chote, alikuwa naย ndoto ya kumuona Mgonjwa huyo anakuwa mzima tena lakini ndotoย ya Lucia imezimika ghafla kama Mshumaa” Alieleza kisha choziย lilimtoka akalifuta, Noela alipelekwa hadi kwenye chumbaย ambacho Mgonjwa wa Lucia alikuwa amelazwa, hakuwa mwingineย bali ni Mandy Mke wa Desmond.ย
Alimtazama Mandy kisha alisemaย
“Hakika Lucia amekufa na ndoto zake” Alisema Noela hukuย akifuta chozi lake, alikumbuka mara ya mwisho alipewa kazi naย Lucia, haraka alitoka wodini ili alekee nyumbani kwakeย kuangalia zile nyaraka alizopewa na Lucia.ย
Wakati anatoka Desmond alikuwa akiingia Hospitalini hapo,ย wawili hao hawakuonana. Haraka akiwa na gari yake Noelaย alifika nyumbani kwao, alimkuta Mama yake akiwa ameketiย sebleni, alitaka kumpita ila Mama yake alisemaย
“Amekuja Mtu uliyemuagiza amechukua sanduku” Alisema Mamaย Noela na kumfanya Noela ashangae ni Nani alikuja kuchukuaย Sandukuย
“Mama unasemaje, sanduku la chumbani kwangu?”ย
“Ndiyo kwani hukumtuma Mwanaume mweusi hivi?” aliuliza Mamaย Noelaย
“Mamaaaaaaa!!” aligumia Noela kisha alielekea chumbani kwakeย haraka, kweli Sanduku liliondolewa chumbani hapoย
Haraka alirudi Sebleni akamuuliza Mama yakeย
“Mtu huyo amekuja saa ngapi?”ย
“muda siyo mrefu sana alikuja na gari akasema umemuagiza naย alikuwa akijuwa hadi lilipokaa nikamiami, ina maana hukumtunaย Mtu?” aliuliza Mama Noela kwa mshangao, Noela hakujibuย alitoka akapanda gari kisha akaanza kumtafuta huyo Mtu,ย alipita mitaa mbali mbali bila mafanikio yoyote yale hadiย alichoka.ย
Aliamuwa kurudi nyumbani, ndipo alipogundua huwenda kulikuwaย na jambo zito lilifanya Lucia auawe, akafikiria atapata vipiย kujuwa alichokuwa anatakiwa kufanya.
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TISA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย 
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Painย
 
		
 
									 
					
19 Comments
Jamani
Duh ubaya ubwelaa
Mm naumiaaa sana ..unatoaje kitu akat hujaambiwaaa
Alafu na wewe ni luciy๐๐
Lucia jamni nlijua ndo star wa move
Qmanina
Ina uma kishenzi๐ฅฒ๐ฅฒ๐ค
Nimeumia mno
Bad news lucia hayupo
Doh๐ฅ
Hadi nimechoka
Jamani Lucia amenyongwa
Inauma sana
Lucia asinge kufa hadithi ingekuwa fupi!!!! Masikini Mandy—-๐ก
Hii Dunia Fanya yanayokuhusu, mengine waachie. Lucia umekufa sasa
kinachoniuma zaid admin anatoa tu si akitaka hii Riwaya tunaomba kila siku tupate au tupe Ratiba nimeisubir sana na nimeumia sana kuona imetoka kipande kimoja
Yeah
..ni kwel hata m nliisubir sana,,,had nkachoka yan…
Mambo vipi Mwana Kijiweni? Kukiwa na mechi mambo yanakua mengi
Sisi tunaomba mbili zetu zilizobaki tusije kukushtaki watu tunatembea na stress utasema sisi ndo Noela ๐ญ
Zaidi ya hatar
SIMULIZI Nani atalifuta chozi langu
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/720
https://maishakitaaonlinetz.blogspot.com/2024/11/simulizisiri-za-giza-sehemu-ya-pili.html
Gonga emoj MOJA kama ukotayari kwa sehemu ya Tatu ya Simulizi hii.
ff8mpa