Ilipoishia “Joshua naomba tuonane kwenye mgahawa muda huu” Alisema Noelaย kisha alikata simu, Desmond alishusha pumzi zake baada yaย kujiridhisha kuwa Noela hajagundua lolote maana kamaย angedungua asingemuita jina la Joshua bali angemuita Desmond,ย kumbe Noela alishajuwa kila kitu, alikuwa katika upeleleziย wake binafsiย
Desmond alipotoka pale Hotelini moja kwa moja alienda kuonanaย na Mchumba wake Noela kama alivyoambiwa, alimkuta Noela akiwaย amejawa na tabasamu na bashasha kitu ambacho kilimfanyaย Desmond azidi kujiamini kuwa Noela hajafahamu lolote lile,ย waliagiza chakula huku Noela akizidi kumsoma Desmond, akiliย ya Desmond haikutulia kabisa sababu alihitaji kufahamu kamaย Joel alikuwa amefanikiwa kupeleka Hundi ile kwa Mtu wa Tatu. Endelea
SEHEMU YA KUMIย
“Nimetoka Hospitali, unamkumbuka yule rafiki yangu uliyewahiย kuniona naye hapa?” aliuliza Noela makusudi ili kuzidiย kumsoma Desmondย
“Eeeh nakumbuka, anaumwa?” alihoji Desmondย
“Hapana amekutwa ameuawa huko porini, inasikitisha mno alafuย kaacha Mama anayeumwa sana” Alisema Noela huku akiwa makiniย sana na jicho lake la uchunguzi, Desmond alishtuka mno hukuย macho yake yakiwa yamemtoka pima kama Mjusi aliyebanwa naย mlangoย
“Ameuawa…..Nani aliyemuuwa?” alihoji Desmond akiwa katikaย hali ya kuchanganikiwa sana, Noela akagundua kuwa alichokuwaย ametumiwa na marehemu Lucia kilikuwa na ukweli mtupuย
“Haijajulikana, polisi wanafanya uchunguzi. Inasemekana piaย ameacha mgonjwa ambaye yupo mahututi na huyo mgonjwaย inawezekana kuwa chanzo cha kifo cha Lucia” Alisema Noelaย huku jicho lake likiongeza umakini wa kumtambua Desmondย
“Mgonjwa!! aaah Noela, naomba tuachane na hizo stori,ย tumekuja hapa kula Mpenzi” Alisema Desmond kisha alimwambiaย Noelaย
“Naenda chooni mara moja” Desmond alinyanyuka akaelekeaย Chooni bila kujuwa kuwa Noela alikuwa tayari amegundua kuwaย yeye ni Muuuwajiย
Japo moyo ulimuuma sana Noela ila kilichompata Lucia alijionaย ana kila sababu ya kuleta haki, Desmond alipofika chooniย alijiinamia kwenye sinki la kunawia maji akiwa amechoka sana,ย alianza kuhisi ugumu mkubwa sana kwenye Maisha yake,ย alimpigia simu Joel akamuuliza kama amekutana na huyo Mtu waย Tatu.ย
Joel akiwa ndani ya gari hilo aliloelekezwa alipokea simu,ย alionekana kuzungumza kwa kutulia sana huku pembeni yakeย kukiwa na mwanaume mmojaย
“Nimeshampatia” Alisema Joelย
“Haya basi tukutane mara moja pale tunapokutanaga….naonaย mambo magumu, Kifo cha Lucia kimekuja kuharibu kila kitu”ย Alisema Desmond, baada ya simu ya Desmond kukatwa Joelย alimgeukia Mwanaume ambaye yupo ndani ya hiyo gani akamwambiaย
“Ngoma imeanza kuchezwa, Hii Hundi hakikisha unachukua pesaย na kuziweka kwenye akaunti nyeusi, ni lazima tumtumie Desmondย kuvuna pesa alafu kila kitu kitamuangukia mwenyewe” Aliagizaย Mwanasheria Joel, kumbe mwanasheria Joel ambaye niย mwanasheria wa Mandy ndiye Mtu wa tatu ambaye alikuwaย akijifanya kuzunguka kwenye suala lililojificha ili apateย pesa kutoka kwa Desmond kwa kujifanya anajuwa siri zaย Desmond, Mwanaume aliye pembeni yake ndiye yule ambayeย Desmond alikuwa akimtilia shaka na ndiye aliyekuwa akifanyaย michezo mingi michafu na ndiye aliyelitoa lile gari kuleย Baharini kisha akaliweka gari lingine kisha akawapigia simuย polisiย
Basi, Baada ya kumaliza kuongea na Joel akifikiria ni Mtuย mzuri anayeshirikiana naye alirudi kwa Noela ambayeย alijifanya yupo bize akipata chakula, angalau baada ya kutokaย Chooni alionekana kuwa sawa japo Noela alikuwa ameshamgunduaย muda mrefu, walipata chakula ndipo Noela alipomchomekeaย Desmondย
“Nasikia Mgonjwa wa Marehemu Lucia ameamka leo, ingekuwaย faraja sana kwa Lucia kumuona mgonjwa aliyemhudumia kwa mudaย mrefu akiamka” Alisema kwa mtego Mkubwa sana na Desmondย akaingia mtegoni, alishtuka akaulizaย
“Unamaanisha Mandy?” alihoji akiwa ameamka kutoka kitini,ย ndipo sasa akawa amemdhihirishia wazi Noela kuwa ana Mke piaย ni Muuwajiย
Noela naye akaamka akijifanya kushangaaย
“Heee kumbe unamjuwa?” Alihoji Noelaย
“Hapana….Hapana simjui, Noela tutaonana baadaye” Alisemaย Desmond kisha aliondoka mbio kuelelekea Hospitalini bilaย kujuwa kuwa alikuwa ametegwa, Haraka Noela alimfuata kwaย nyuma kisha naye aliingia kwenye gari yake akawa anamfuatiliaย Desmond kwa nyuma, Safari hii ilifika hadi kwenye Hospitaliย aliyolazwa Mandyย
Akiwa amepaki gari eneo lingine la Hospitali tofauti naย alipopaki Desmond, Noela alipokea ujumbe kuwa Mgonjwa Mandyย amerudisha fahamu, huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Daktariย Mkuu wa Hospitali sababu alimuachia maagizo kuwa akiamkaย Mandy apewe taarifa na pia alipewa agizo moja kubwa sana,ย Noela akakumbuka alichomwambia Daktariย
Alimwambia kuwa anafanya uchunguzi wa kifo cha Lucia naย huwenda mgonjwa huyo akawa ndiyo chanzo cha kifo cha Luciaย hivyo atakapoamka pengine kuna siri anaifahamu hivyo kitu chaย kwanza ahakikishe anamuweka sawa kiakili ili Desmondย asishtuke mapema hadi pale watakapopata ushahidi wa kutosha
Akiwa mbio mbio, Desmond alifunga breki miguuni mwa Daktariย Mkuu aliyekuwa akitoka wodini kwa Mandyย
“Dokta nimesikia Mke wangu ameamka” Alisema Desmond akiwaย katika hali ya haraka na hofu mnoย
“Ndiyo Mkeo ameamka ila bado hana nguvu, unaweza ukamuona ilaย usimkumbushe chochote” Alisema Dokta, Basi Desmond aliufunguaย mlango wa wodi hiyo, kweli alimuona Mandy akiangaza huku naย kule kama Mtu aliyekuwa akijiuliza yupo wapiย
Hofu ilimjaa sana Desmond kisha alimsogelea Mandy taratibuย huku akiwa mwenye maswali mazito sana ya kuwa Mandy amemjuwaย Desmond kuwa ni Muuwaji wa Mama ake, Mandy alipomuona Desmondย alionekana wazi kuwa na maumivu makali moyoni, alimtazamaย Desmond huku chozi likimbubujika, yule Daktari Mkuu alisimamaย mlangoni akichungulia tuย
Mandy alikumbuka siku ya tukio la yeye kupigizwa ukutani naย Desmond, siku hiyo ilikuwa hivi, aliiyona cheni ya Mama yakeย kwenye koti la suti la Desmond, cheni ambayo Desmond aliivuaย kwenye shingo ya Mama Mandy baada ya kumuuwa kisha akaiwekaย kwenye koti lake, Mandy alipoiyona ile cheni ndipoย alipogundua kuwa Desmond ni Muuwaji, wakati anapiga Simuย Desmond alitokea ndipo vurugu za kufukuzana zilipoanzaย
Tuendelee, Basi Desmond alisogea na kumshika mikono Mandyย akamwambiaย
“Umeamka Mama?” alihoji Desmondย
“Wewe ni Nani?” aliuliza Mandy, Desmond alishtuka sana kishaย akajiuliza ina maana Mandy amepoteza kumbukumbu zake,ย alijikuta akitabasamu maana kama amepoteza kumbukumbuย hatoweza kumtaja kama Muuwaji wa Mama yake.ย
“Pole kwa maumivu sawa Eeh!! Mimi ni Mume wako Desmond”ย Desmond alijitambulisha pale, Daktari alielekea moja kwa mojaย kwenye maegesho ya Magari akamwambia Noela kuwa Mandyย amefanya kama alivyoagizwa yaani kujifanya amepotezaย kumbukumbu.ย
“Safi sana, Desmond ni mchumba wangu na hii pete amenivishaย jana tu” Alisema Noela kisha aliivua pete hiyoย
“Sistahili kuwa na pete yake sababu ni Mume wa Mtu piaย Muuwaji, kwakuwa ameshajulikana ndiye Muuwaji basi kaziย iliyobakia niachie Mimi”ย
“Sawa!!” Noela aliondoka Hospitalini hapo.
Desmond alibakia Hospitali kwa ajili ya kuangalia kama kunaย chochote Mandy anaweza akakumbuka, hii ilimfanya yule Daktariย ashindwe kumpa taarifa muhimu Noela.ย
Jioni ilipoingia ilimkuta Noela akiwa nyumbani kwao akiwaย kwenye tafakari nzito kuhusu Desmond ambaye alimdanganya jinaย kama Joshua, alikumbuka vingi ikiwemo walipotoka, alijikutaย akiangusha chozi lenye maumivu makali sana, mapenzi aliyompaย Desmond yalikuwa ya dhati sana kwa kipindi chote, kugunduaย kuwa Desmond alikuwa Muuwaji na Muongo kulimliza sana Noela.ย
Alijikuta kwenye wakati mgumu sana, ndiyo alimpenda sanaย Desmond hadi kufikia hatua ya kuvishwa pete lakini angefanyaย nini wakati Mwanaume huyo alikuwa Muongo na Muuwaji.ย
Jioni hiyo alitoka akarudi kule Hospitali, Desmond alikuwaย wodini kwa kipindi chote akiwa na mawazo kuwa huwenda Mkeย wake atarudisha kumbukumbu muda wowote ule, ili kumtoa paleย Noela alimtumia meseji Desmond akimwambiaย
“Mpenzi naelekea kwenye pori ambalo Lucia aliuawa, kunaย taarifa kuwa alipotoka nyumbani kwao alitoka na kitabu chenyeย siri pengine nacho kilikuwa ni sababu ya kifo chake,ย inasemekana kilipotea porini” Alipotuma meseji hiyo alijuwaย wazi kuwa Desmond ataenda huko porini ili kuhakikishaย alichoambiwa, kweli muda huo huo Desmond alikurupuka kutokaย pale wodini akaingia kwenye gari kisha akatoka.ย
Lakini wakati anatoka Desmond, yule Mwanaume anayetumwa kaziย na Mwanasheria Joel alikuwa pale ndani akamuona Desmondย akitoka kisha Noela aliingia wodini, yule Mwanaume alimpigiaย simu Joel haraka sana akamwambia alichokiona, basi harakaย Joel alimpigia simu Desmond na kumueleza kuwa kulikuwa naย mchezo uliokuwa ukichezwa hapo na kwamba mpenzi wake Noelaย alikuwa hapo Hospitalini na baada ya yeye kutoka Mpenzi wakeย huyo aliingia wodini kwa Mke wake Mandy.ย
Desmond alisitisha safari ya kwenda eneo ambalo Lucia aliuawaย baada ya kuambiwa kuwa kuna mchezo mchafu Hospitalini, harakaย aligeuza gari akarudi kule Hospitalini, akiwa hoi haiย aliingia wodini na kumkuta Mandy akiwa amelala huku chumbaย hicho kikiwa kimya sana, Desmond alishangaa sana wakatiย aliambiwa na Joel kuwa mpenzi wake alikuwa hapo, akaamuwaย kumpigia simu ili ajihakikishie alichoambiwa, simuย ilipopokelewa ilionesha wazi kuwa Noela alikuwa barabaraniย hivyo alishindwa kuthibitisha alichoambiwa, alimpigia simuย Joel na kumwambia alichokiona lakini Joel alimtaka Desmondย kuwa makini sana maana Mpenzi wake alikuwa hapo Hospitaliniย na huwenda anafahamu kuhusu Mandy.
Alienda kukutana na Mwanasheria Joel ambaye alikuwaย akimchezea Mchezo mchafu, Joel alimuonesha video Desmondย iliyomuonesha Noela akiingia na kutoka pale wodini, ndipoย alipopata picha kamili kuwa Noela alikuwa amefanikiwaย kumfahamu, Joel alimuulizaย
“Huyo ameshajuwa siri kuwa wewe ni Muuwaji, kibaya zaidi huyoย ni mpenzi wako alafu mpelelezi utafanya nini?” Desmond alikaaย kimya baada ya sekunde kadhaa akamwambiaย
“Nitajuwa cha kufanya” Desmond alitoka kuonana na Joel,ย alionekana kuwa mwenye mawazo sana ya nini afanye, alimpigiaย simu Noela akamuuliza kama alifanikiwa kukipata hicho kitabu,ย alifanya hivyo makusudi ili kumfanya Noela afahamu kuwa badoย Desmond hajajuwa chochote.ย
Noela alimwambia kuwa hawakufanikiwa kukipata kitabu ilaย uchunguzi bado unaendelea, Desmond alipata wazo la harakaย nalo ni kuondoa uhai wa Noela maana Mke wake hakumbukiย chochote hivyo kwa vyovyote Mtu anayeweza kusema ukweli niย Noela.ย
Alimtunia ujumbe wakutane nyumbani kwake usiku wa siku hiyo,ย baada ya kuupata ujumbe Noela aliwataarifu polisi aliokuwaย akifanya nao kazi maana alihisi huwenda Desmond alishafahamuย kuwa anaijuwa ile siri ya Mauwaji. Usiku ulipofika Noelaย alienda nyumbani kwa Desmond, alimkuta akiwa ameketi mahaliย anapata biaย
Noela aliketi naye akapata chupa ya Bia bila hata kumsemeshaย Desmond, waligida kidogo kisha Desmond alimuuliza Noelaย
“Umemuaga Mama?”ย
“Ndiyo!!” Alijibu Noelaย
“Siku moja ya uchumba wetu umeshavua pete ya uchumba” Alisemaย Desmond ndipo Noela aliposhtuka sasa kuwa Desmond alikuwaย ameshafahamu.ย
“Nafikiri ni kitu cha kawaida, inakuwaje kwa Mtu akawa naย majina mawili, la uhalisia analificha na kutumia jina feki?”ย Alisema Noela, hakukuwa na siri tena sababu kila jamboย lilikuwa waziย
“Noela umekuwa kikwazo kwangu, ili niwe salama ni lazimaย nikutangulize” Alisema Desmond kisha alitoa bastola akawaย anaifutafuta
“Kwa mpelelezi ambaye amefanya kazi nyingi hawezi kuogopaย kufanya kazi hata kama ni hatari kiasi gani au inamgusaย ampendaye, Desmond….kumbe una Mke tena ni Mke ambayeย ulitaka kuutoa uhai wake kisa pesa, unakumbuka kuhusu Mamaย Mandy?” aliuliza Noela, Desmond alijawa na hasiraย akamnyooshea Noelaย
“Kabla hujaniuwa Desmond, nataka nikwambie kitu kimoja. Pesaย haiwezi kukupa kila kitu katika Maisha yako, ila Maishaย yanaweza kukupa kila kitu ikiwemo na pesa, waliochagua kuishiย walifanikiwa lakini wewe ulichagua pesa ili uishi”ย
“Ishia hapo hapo Noela” Alisema Desmond kisha alifyatuaย risasi iliyowashtua polisi aliokuja nao Noelaย
Haraka waliingia na kumkuta Noela akiwa chini anauguliaย maumivu ya bega, bastola ikawa udhibiti kwa Desmond,ย alikamatwa na wale polisi. Taarifa ya kukamatwa kwa Desmondย ilimfikia Joel, akapata wazo la kuikimbia Nchi maanaย alishajuwa kuwa atatajwa na kukamatwa, Naam!! alitajwa naย Desmond, Joel alienda kukamatwa Uwanja wa ndege….ย
Taarifa ya kukamatwa kwa Joel na Desmond ilimfanya Mandy alieย kwa uchungu mkubwa, baada ya kupona kwa Noela, Desmond naย Joel walifikishwa Mahakamani kwa makosa ya Mauwaji, Mandyย alisimama kama Shahidi namba moja, Hatimaye Desmond na Joelย walifungwa kifungo cha Maisha jela, Mandy alimshukuru sanaย Noela kwa msaada huo hadi kukamatwa kwa Wauwajiย
Noela aliishia maisha ya majuto sana sababu aliamini kamaย angelifanyia kazi mapema bahasha aliyopewa na Lucia basiย rafiki yake huyo asingeliuaawaย
MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย 
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Painย
ย ย
 
		
 
									 
					
15 Comments
Mapenzi na Maumivu โโ
Mapenzi ni Maumivu โ
Na Pesa sio kitu
Utu ndio kila kitu.
Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na mazingatio katik maisha yetu ya kila siku hususan maisha yetu ya saiv.
Asanteni.
Mtunzi na Adminโค๏ธ
Asant adimin
Mapenzi na pesa
Uki ambatanisha na jua
Oyaa oyaa oyaa
๐๐๐๐๐
๐๐
Mhmmmmmmmm admin punguza uvivu
Imeisha ghafula ๐ฅบ
Upendo na maumivu
.pesa SI Kila kitu. ??
.Kila kitu ni pesa??
๐ฅบ๐ฅบ๐ฅบ๐ฅบ
Duh
apo safi bora imeisha imenisubirisha sana hii admin siku nyingine tuwekee ratiba mambo ya mpira yakiwa mengi
Hakika pesa sio kila kitu bali maisha ndiyo kila kitu. Naam nimeyaona maumivu ya mapenzi kwa Noela……… Lucia โฎ๏ธ shujaa wetu!!!!!!
Maumivu maumivu ya mapenzi ๐ฅน๐ฅน๐ฅน
Aisee pesa inanguvu kwenye mapenzi tu lkn siyo kwenye sheria
Mapenzi yanaumiza jamani
9ooa0q
u6f037