Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Ligi Kuu Inakaribia Hivi Ndivyo Wazawa Wanatakiwa Kufanya
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Ligi Kuu Inakaribia Hivi Ndivyo Wazawa Wanatakiwa Kufanya

    Living ShayoBy Living ShayoJuly 26, 2024Updated:July 26, 20244 Comments3 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mchezaji wa Ligi Kuu Feisal Salum
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ni mashariki mwa Afrika sehemu ambayo Bahari ya Hindi imepita, nchi ambayo imefunikwa na maeneo makubwa yenye mito na maziwa, ardhi yenye udongo wenye rutuba na vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na safu za milima na mabonde.

    Tanzania nchi yangu, hii ndiyo fahari yetu sote, tunajivunia nawe kwenye pande zote za duniani, na ndiyo maana halisi ya Soka la nyumbani limenoga, tumeungana watu wa rika tofauti kuitazama burudani hii ya Kabumbu popote pale nchini, wazawa na wageni kwenye Ligi yetu wanatupa Ladha ya Ligi kuu pamoja na Championship.
    Wacha leo niwaambie nikiwa kwenye ardhi ya Chief Mkwavinyika Mwinyigumba, naamini hata watoto na wajukuu wa Kinjekitile Bokero Ngwale wataisikia, msimu ujao unatarajiwa kuwa mgumu sana kila timu inahitaji kufanya vizuri usajili umefanyika na timu zote kambini maandalizi ya msimu mpya.

    Zaidi ya miaka minne sasa wageni wamekuwa Lulu nchini, sifa mbwembwe wamekuwa wakipewa wao, ni wakati sasa na sisi wazawa kuonyesha ubora wetu, uwezo Ufundi na vipaji tunavyo vya kutosha, kwa sasa hatuhutaji kupendelewa Bali wazawa wanahitajika kupambana zama zinakwenda sana muda unasonga mbele, uwekezaji umeongezeka watu wanaweka hela.

    Vituo mbalimbali vinafunguliwa vijana wanafundishwa na vipaji mitaani vinaonekana, hakuna haja ya kupunguza idadi ya wageni 12 wanatosha sana na Wala siyo wengi, kilichobora ni kupambana na kujituma ukionyesha uwezo jitihada hakuna Kocha atakunyima nafasi kosa kuna wageni.

    Mara ngapi tumeshuhudia wageni wakiwekwa benchi na wazawa, mara ngapi vijana wamepambana mbele ya wageni na wakatoboa na kuwa na nafasi ya uhakika ya kucheza mbele ya wageni? Vijana wangapi wamekwenda kucheza Soka la kulipwa kupitia Ligi ya nyumbani. Ni wakati sasa wa kuendelea kupambana Feisal Salum, Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathiri Yahya Pascal Msindo ni baadhi ya wazawa wanaopata nafasi kwa kuwaweka wageni kwenye mbao ndefu.

    Nikukumbushe kuwa Saimon Msuva, Himid Mao walipata nafasi ya kucheza nje ya nchi kupitia Ligi ya nyumbani, hakuhitaji kutafutiwa nafasi ya lazima ili wazawa wacheze. Mnaocheza Ligi kuu sasa Academy ni nyingi sana nchini vijana wanawaangalia nyie kama kioo chao, wanawatazama kama watu wenye ushawishi mkubwa sana kwao na kuwafanya kuwa na matamanio makubwa kupitia nyie.

    Ni wakati sasa kuwaonyesha kuwa wazawa wanaweza hakuna haja ya kuonekana wanatafutiwa nafasi maana wana ubora wa kushindana na wageni.

    Wageni wamefanya Ligi yetu kama daraja kwao kufika mbali Kimataifa tena kwenda kwenye vilabu vikubwa barani Afrika na Mfano halisi Upo Kipre Junior, Luis Miquisone, Fiston Mayele wamekwenda vilabu hivyo baada ya kuonyesha uwezo wakiwa nchini sasa kwanini isiwezekane kwetu?
    Mimi sina mengi sana Wacha niwaache na hayo machache tu ila Imani yangu ni kuwa wazawa wana uwezo tu mkubwa na ilo kadri miaka inakwenda taratibu wanadhihirisha ilo.

    SOMA ZAIDI: Baada Ya Usajili Tuitegemee Yanga Ya Namna Gani Msimu Huu?

    ligi kuu NBC Premier League ngao ya jamii 2024/2025 simba vs yanga

    4 Comments

    1. Pingback: Misingi Sahihi Ya Wachezaji Vijana Ni Elimu Ya Makocha

    2. Sensible on July 26, 2024 2:15 pm

      Wafate nyayo za Fei toto. Zanzibar finest huyu ni balaaa kwa washambuliani wote wamuige Fei. Ila kwa beki pia Kuna kijana kutoka kwenye vikosi SI mengine ni Ibra Bacca huy ni beki Bora sana kwa Sasa kakita viunga vya NBCPL. Wasimsahau dogo mmoja matata kutoka azam anakichafua sana katika ENEO la kiungo. Ni kiungo halisi kabisa jina nimemsahau kidog ila hachafuki Wala hana fujo uwanjani ila kazi yake usipme ni noma (bitegeko)

      Reply
    3. Pingback: Hatukatai Umefanya Vingi Ila Hili Ni Deni Kubwa Sana Kwako

    4. Johnson on July 26, 2024 2:36 pm

      Kaka hapo si wazawa tatizo viongozi, pili wazawa washajiona watawa especially hao wanaojiita wakongwe kongole kwa simba kwa kuvua ndaga na kuwaachaa kambale wenye ndevu

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.