Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kisasi Changu-04
    Hadithi

    Kisasi Changu-04

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJuly 5, 2024Updated:July 7, 202415 Comments7 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Asia akabaki kumtizama tu, bilashaka anakumbuka vitu vingi sana awapo mazingira ya nyumbani. 

    Naomi nae akawa amefika na kumpatia bahasha ndogo iliyokuwa imeandikwa kwa juu “” Kwako Nickson Mzobe “

       “” Twende bhana naona simu zimeanza hapa, nikitulia nitaisoma.”

    Endelea 

    SEHEMU YA NNE 

    Huku upande wa pili kwa Minii pamoja na Alexander walifika pamoja kwenye kampuni inayoenda kufunguliwa, vibosile wengi walikuwepo Minii ndio anaangaza hivi ndio anamuona Baba’ke ikabidi asogee karibu yake, Baba alifanya kumshika mkono kichwani ni kama anambariki baadae aliongea kwa chini chini.

       “” Usisahau Ndoa yako na Alexander ni kwaajili ya kisasi tu.”

    Minii alitabasamu tu baada ya kumuona Alexander kafika isingekuwa rahisi kumjibu.

       “” Baba baadae tutaonana naona tunahitajika huko mbele.”

       “” Sawa, ” Alexander……!! Baba Alimuita kwanza Mume wa Miniii. Akageuka.

      “” Mwangalie sana Binti yangu awe salama .”

      “” Sawa Baba kumlinda ni jukumu langu.”

    Muda huo Minii alikuwa kapiga hatua Hadi mbele akimsubili Alexander afike.

       “” Ufunguzi umekamilika nyie hapa kwasasa ni wamiliki halali wa ALEMI MECHANIC GROUP na kampuni hii Ina muungano wa majina yenu namaanisha ALEMI ni ALEx na MInii ” Basi njoeni msaini hapa.

    Ni Mwanasheria mmoja aliongea akiwapatia mkataba wasaini.

    Ilikuwa ni Majira ya usiku Minii alikuwa yupo kwenye chumba kikubwa kilichokuwa kimepambwa vizuri ni kama kiliandaliwa kwa Wanandoa, Minii hakuacha pirika pirika ya kuzunguka chumba hicho mara Mlango ulifunguliwa alikuwa ni Alexander alifika.

       “” Ooh Mwalii..!!! mbona unahaha tenaa, ulifikili siku nzima itaishia mchana tu?”

    Minii hakutaka kumjibu zaidi ya kujilaza kwenye sofa huku akikunja nne.

       “” Bwana Alex…!!! Hivi unafikili Mimi nafaa kuwa mkeo?”

    Alexander ikabidi amfuate mpaka kwenye sofa akafanya kukaa karibu na kichwa chake, Minii akafanya kuinuka akisimama kuelekea kunako dirisha huku akichungulia nje akitazama mazingira ya White House alibaki kuongea kimya kimya.

       “” Mtu mmoja anamiliki eneo kubwa namna hii si unyanyasaji tu, watu wanakosa viwanja vya kununua mpaka wanatupiwa bondeni huko kiasi kwamba mvua zikizidi wanasombwa na maporomoko.””

    Muda huo Alexander aliingia bafuni kuoga baadae alivaa mavazi ya kulalia na kuchukua laptop ya Minii Kuna kazi alitaka kuifanya wakati huo.

       “” Miniii,,, nitolee password hapa.”

    Minii ndio anageuka akaduwaa kwanza Ani kwenye laptop yake ndio alifaa kumtolea password mbona Kuna mambo mengi ya Siri na hakupaswa kuyafahamu au kuyaona kabisa? ikabidi asogee.

       “”” Weee Alex wewee si unayo ya kwako jamaniii na Mimi na kazi nayo sahiii….!!”

    Alexander alifanya kumkata jicho Kisha akamshika mkono kwanza.

    “” Mimi si mumeo hapa…!!? Halafu niite Alexander ” 

    Alexander aliongea kwa ukali kidogo mpaka Minii akarudi nyuma anafikiria kumbe tayari ni mke na alifaa kumsikiliza Bwana Alexander, mbona alihisi ni kama Kuna kitu kimepungua katika maisha yake yaani atakuwa akimtii kwa Kila kitu.”

    Alisogea mpaka kitandani akakaa kwanza akizidi kutafakari maneno ya Alexander, wakati muda huo Alexander alikuwa akicheka chini chini akajua kamtikisa Miniii, bahati mbaya Ile anacheka Minii akawa ameona akichezesha mabega ndo akagundua kumbe alicheza na akili yake, akasimama kumfuata,, nae akafanya kumsogelea Kisha akasogea karibu yake akifanya kumkaba shingoni mpaka Alexander akashituka.

       “” Wewee unataka kuniua Miniii… Niache basi, sitapenda haya matani yako.”

       “” Kwanini unacheza na akili zangu! Leta laptop yangu haraka.””

    “” Sio ugomvi chukua bhana.”

    Minii ndio akamuachia huku akichukua Laptop yake na kwenda kukaa kwenye sofa Kisha alianza kuitumia Kuna kitu alikuwa akikifatilia kupitia laptop yake, Kuna picha alikuwa akizifungua moja baada ya nyingine zilimuonesha ni White House akiwa amezungukwa na watoto watatu akawa anafikilia kati ya wale watoto watatu mbona anaemuona kwenye hiyo nyumba ni Alexander tu. Vipi kuhusu huyu wa kike na wakiume wao wapo wapi?” Alifanya kumtizama Kwanza Alexander alimuona kalala tayari ikabidi na yeye aweke laptop pembeni angalau apate usingizi hata hivyo muda ulienda sana.

    Ni Asubuhi kunapambazuka Alexander alikuwa wa kwanza kuamka Minii akawa ameshituka akimtizama jinsi anavyotafuta nguo kwenye kabati baadae alibeba na kuingia nazo bafuni, baada ya muda alitoka akiwa kavaa alimtizama Minii kwanza akaona kalala bado hakutaka kumuamsha zaidi ya kutoka nje, Ile ametoka tu Minii nae akawa ameamka na kujiandaa chap Kisha nae akatoka nje, alianza kutembea akizungumza jumba hilo lililokuwa na vyumba vingi mwisho kabisa alifika kwenye Mlango mmoja uliokuwa wazi kwa kuangalia tu ilionesha ni jikoni kulikuwa kunawapishi wakiandaa chai nae akawa ameingia mle, wapishi waliokuwa mle ilikuwa ni ngumu kumtambua Miniii kuwa ndie Mwali wa nyumba hiyo na jana tu ndio waliungamanishwa pamoja na alikuwa Bibi harusi?

    Wapishi hawa waliendelea na stori zao huku wakiendelea kuteta mambo mengi, Kuna mpishi mmoja alitambulisha kwa umbile lake akiitwa tolu kwani alikuwa kapanda hewani sana na alikuwa mwembamba pia.

       “Awee sikia tolu, Sema Alexander kaoa mwanamke mrembo kweli kuliko hata Alex,, lakini najiuliza huyu Binti alifahamiana vipi na huyu au ni kazini?””

    Minii baada ya kusikia hivyo ikabidi asimamishe masikio vizuri, lakini akasitushwa na sauti ikimuuliza.

       “” Wewe ni nani…? Haupo kwenye hii sekta labda uliagizwa..!?”

    Minii akahisi kuchanganyikiwa make wote wakamsogelea karibu. Ni tolu ndio alimshitukia.

       “” Hamchelewagi kutia sumu kwenye vyakula mkahatalisha vibarua vyetu.” Tolu akazidi kuongea huku akimshika mkono akimkazia macho.

       “” Achaaa,,, Ni Mimi niliemuagiza.”

    Wote wakageuka kumtizama alieongea, wakamuona ni  Bwana Alexander ikabidi wote wainamishe kichwa chini kuomba msamaha. “” Tusamehe Boss hatukujua.”

    Minii ndio akasogea taratibu akimfuata Alexander huku kichwa chake akiwa kainamisha chini kwa unyenyekevu kabisa, Alexander hakuzungumza chochote mpaka walifika kwenye chumba Chao anafika anashangaa kukuta meza imejaa vyakula, akawa amekaa na kutulia huku akisubili Alexander aongee kitu, lakini alimpatia maji ya kunawa kwanza.

       “” Kama utakaa sehemu moja ukatulia wewe hapo hautakuwa Minii…!!?”

    Ni swali alilomuuliza Minii mara tu ya kuinua kikombe Cha maziwa anywe, Miniii akawa ameishia njiani na kukishusha kikombe kile.

       “” Samahani Alex, Nisamehe sitarudia, Nilikukosa chumbani nikawa nakuangaza nje ndio nikatokea jikoni.”

    “” Sawa,, kingine niite Alexander,, huyo Alex ni mtu mwingine kabisa,, utamuita wakati mwingine.”

    Minii akawa hamuelewi kabisa anakumbuka hata wale wapishi walimzungumzia Alex ni kama walitofautisha kutoka kwenye Alexander Hadi kuwa Alex Sasa anajiuliza ni nani huyo?”

       “” Minii… baada ya kifungua kinywa itabidi tuongozane pamoja na wewe make nikitoka peke yangu White House ataniuliza, lakini naweza nikamkwepa asijue nimetoka ila shida ipo kwako hautoweza kutulia ndani lazima ungetoka tu, watumishi wangekuona Sina namna zaidi ya kuambatana na wewe.”

    Minii akatulia akifikilia akaona njia nzuri ni yeye kubaki Kuna kitu alifaa kukifatilia awapo peke yake akaona hii ndio nafasi nzuri kwake.

       “” Hapana kama unatoka wewe toka tu, Mimi nitakuwa ndani muda wote naahidi sitatoka Alexander.””

       “” Mhuu kweli..!!? kama nitatoka muda wote macho yangu yatakuwa yakikuangaza wewe.””

    “” Nakuhakikishia tafadhari.”

    Alexander alimalizia kunywa chai akimuacha Minii mezani Kisha alichukua mkoti uliokuwa kitandani na kuondoka lakini alipofika mlangoni alimrudia tenaa.

    “” Miniii tafadhari usitoke humu, kama atakuja mtu kuniulizia waambie nimelala, sawa? Usiruhusu mtu aingie ndani.””

    Aliitikia ishara ya kichwa tu, Ile ametoka tu Minii akawahi kufunga Mlango huku akiangalia mazingira ya mle ndani, aliwahi kushika simu yake na kumpigia simu Baba’ke haraka.

       “” Baba, tayari Alexander katoka kipi natakiwa kukifanya sahii…?”

       “” Kakuachia maelekezo Gani?”

       “” Nisitoke humu ndani.”

       “” Sawa, na usitoke kweli, White House imejaa Camera sehemu zote isipokuwa kwenye chumba chenu lakini vyumba vya watumishi vyote vimejaa Camera, hapo inatakiwa uwe makini kwanza make hatua ya kwanza ndio tumeianza ni wewe kuolewa na kijana wa white house, hatua nyingine nakutumia kwenye email hapo, utaipitia kama hutoelewa niulize nikueleweshe tafadhari.”

    Nini Kitaendelea?  Vipi kuhusu Nick? Atapambana nae kulipa kisasi? Wewe Ungelipaje KISASI? Usikose SEHEMU YA TANO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]   

    KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU XX KISASI CHANGU

     

     

    Kisasi Changu Riwaya Ya Kisasi Changu

    15 Comments

    1. Alice simbeye on July 5, 2024 4:19 pm

      I like it

      Reply
    2. Colly_tz on July 5, 2024 4:20 pm

      Ni hatari story ipi🔥

      Reply
    3. Pauline on July 5, 2024 4:30 pm

      Duuuuh

      Reply
      • Fahe on July 5, 2024 8:42 pm

        Admin we fundi bhna 👍👍 add some more plz

        Reply
    4. Tinner Rober on July 5, 2024 4:45 pm

      ❤❤❤❤

      Reply
    5. Tumpe on July 5, 2024 4:49 pm

      Aaah😄

      Reply
    6. Raster de’ ndaturu on July 5, 2024 5:10 pm

      Wow!!

      Reply
    7. Anneth on July 5, 2024 6:31 pm

      👍

      Reply
    8. Freeman on July 5, 2024 7:02 pm

      Duh ni noumaaaa🔥🔥🔥🔥🔥

      Reply
    9. Calvin paul on July 5, 2024 7:56 pm

      Fupi boss adimin

      Reply
    10. Fahe on July 5, 2024 8:43 pm

      Admin we fundi bhna 👍 add some more plz

      Reply
    11. Sadick on July 5, 2024 11:26 pm

      Aseee admin chukua maua yako 🌹🌹🌹 huna baya tajiri ishi sana

      Reply
    12. Rumbyambya Jr on July 6, 2024 7:58 am

      Nikimaliza UE Nitakuja na bonge moja la story lenye Kusisimuwa ni kali mnoo balaaa kisa flani hivi cha Mapenzi And it’s based on True Story Admin
      0688749474/ 0744-119475

      Reply
    13. Maige on July 6, 2024 11:59 am

      Mimi sijaielewa huyo baba yake minii alikuwa mfanya kazi wa hapo au

      Reply
    14. Emmy on July 16, 2024 8:25 pm

      nice

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.