Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Kisasi Changu-03
    Hadithi

    Kisasi Changu-03

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJuly 4, 2024Updated:July 7, 202416 Comments8 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ” Huku kwa Minii muda huo anazidi kupiga hatua kwa pembeni kidogo aliona Kuna garii inaingia alivyotazama vizuri aliona sura iliyofanana na Nick alifanya kutabasamu huku akimpatia ishara ya salamu kupitia macho yake na kudhibitisha tabasamu lake ni kweli ni mzima, lakini alizungumza.

       “Kama upo hapa! Naamini nipo salama.” 

    Endelea 

    SEHEMU YA TATU 

    Hatimae Minii akawa amefika hadi sehemu yenye tukio alifanya kuangaza kwanza sehemu aliyoandaliwa atakaa, ilikuwa ni sehemu yenye seat mbili nakatika seat hizo walifaa kukaa watu wawili lakini hakumuona mtu anaeingia seat ya pili kwa muda huo atakuwa wapi, akiwa Bado kasimama alishangaa mkono wake ukishikwa na kuunganisha pamoja alitazama mtu aliemshika ndipo akaona ni mtu ambae atakaa katika kiti Cha pili kumaanisha ndie mtu walifaa kuambatana nae, alimsikia akizungumza baada tu ya kumshika akimhoji.

       “” Wewe ni nani..!!?”

    Minii alifanya kuuachia kwanza mkono lakini kijana huyo alifanya kuukakamaza mkono akimsihi wapige hatua kuelekea mbele.

    Kelele za shangwe zilisikika eneo hili zikiwakalibisha watu hawa walionekana ni kama wageni rasmi katika sherehe hiyo, Minii hakuisha kuwakinaii kwa kuwatizama watu wote waliozunguka White House akifanya kuwakalili, baadae pembeni yake alisikia kuulizwa na yule kaka alie ambatana nae.

       “” Waitwa nani kwanza…!!?” Maswali ya Kijana yalioneshwa wawili hawa hawafahamiani kabisa.

       “” Kwanini umetaka kunioa…!!? Lilikuwa swali la Minnie kabla hata hajajibu swali lake.

       “” Kwasababu umekuwa ukijiibia kuja White House, kwani wewe ni nani?””

    Muda huo kulisikika sauti ya mshereheshaji akiomba watu wakae attention kumpokea “” White House anaingia”  Huyu Ndie mmiliki wa hii nyumba yeye alifahamika kama MR Danshoo, japo wengi walimuita kwa kumpatia ubini wa hadhi nyumba yake ” Mr White House.”  Minii baada ya kusikia hivyo alitoa macho kitu ambacho kilimstaabisha ni hakuwahi kumuona live MR White House, zaidi ya kumuona kwenye makala jinsi akisifiwa kwa utajili wake mashuhuri, na Leo ndio anamuona mbele ya macho yake, Alitoaje machooo….!!!!

    Hadhara nzima ilikaa kimya huku Kila mtu akitafuta nafasi yake ya kukaa vizuri make wanamjua vizuri huyu white house kifo huwa ni sekunde tu.

       “” Akhaaa!! Kwahiyo huyu ndie miongoni mwa watu waliomuua Mama’ngu! Mhuu…!! Mbona anaogopwa hivi?””

    Minii alijisemea kimya kimya huku akimuona mtu wa kama miraba minne akisogea pale.

     “” Ooh nitakufa Mbona nitafanikiwa kulipa kisasi?, Baba atakuwa salama lakini…?”

       “” Miniii….!!! Huwa unawazaga Nini kwanza kwenye hii kichwa yako?”

    Minii akatulia baada ya kuona anasumbuliwa sana na kijana yule, akaona bora amuulize hata jina.

       “” Wewe hapo unaitwa Nani…!!?”

       “” Alexander…!!”

       “” Mhuu Alex…?”

       “” No, Alexander.”

    Minii ikabidi acheke chini chini kwamba hataki kuitwa kwa kifupi si Alex ila Alexander…?

       “” Wewe waitwa nani…!?”

       “” MINNIER in English, kiswahili ukiishia Minii so mbaya.”

      “” Ahaa…!! Bandit.”

    Minii akashituka kwanza, kwamba yeye aliitwa Bandit inamaana mnyang’au au alionekana kama jambazi kuwa White house au alimfikiliaje kwanza? akafanya kutabasamu tu.

    Huku White House alichukua maiki akiendelea kutoa Utambulisho.

       “” Habari Mabibi na Mabwana! Siku ya Leo tuna hafla fupi ya kumuoza kijana wangu! Tayari kwasasa amekuwa mkubwa na Ndoa imekuwa Ina muungano mzuri wa kibiashara kwa kuunganisha pande mbili namaanisha Mr Denishoo na Mr Mzobe kwasasa watakuwa pamoja kusimamia mradi mpya ulionganisha pande mbili ambao tutaufungua Leo rasmi mara tu baada ya Ndoa hii kukamilika, mradi wetu tumeupatia jina la ALEMI MECHANIC GROUP, Nishati zote zitakuwa zikizalishwa kwenye hii kampuni na kampuni hii itakuwa mkononi kwa Wanandoa wetu wapya ndio watasimamia mradi huu. Basi tuendelee na sherehe yetu.”

    Mr Denishoo alimaliza kwa kuhitimisha huku akiwakalibisha watu wote wafurahie lakini yeye aliamua kutoka na Bodyguards wakielekea kwenye kampuni itakayoenda kufunguliwa hivi karibuni.

    Huku taratibu zote za Ndoa ziliendelea mpaka zikakamilika na kutangazwa kuwa ni Wanandoa lakini Wanandoa hawa hawakuonesha kujali kitu kilichoendelea pale zaidi ya Kila mtu kuielekeza akili yake kuwaza Mambo yake, kwa Minii alikuwa akiuona ushindi ndani yake anajua kwa hio hatua aliyopiga ni rahisi kulipa kisasi Cha Mama’ke ” 

     Baadae tutajua kwanini Minii nafsi yake inamuwia kulipa KISASI, ilikuwaje Mama’ke akapoteza maisha tutajua mbele ya safari

    Baada ya Ndoa kukamilika Minii alienda kubadilisha mavazi na kuvaa mavazi ya kazi, alipo ndani alikitazama kidole chake Cha chanda aliona kinae Pete ya Ndoa, Pete Ile ilimkumbusha kabisa muda si mrefu katangazwa kuwa mke wa mtu tena yeye hapo ni mke wa Alexander na sio Alex alihisi kucheka tu huku akitupia koti lake na kutoka hadi nje waelekee kwenye ufunguzi wa kampuni.

     

    KAMBI YA JESHI KWA NICK.

    Nick kipindi hicho alikuwa tayari ni kijana mkubwa tu mwenye mwili uliojengeka vizuri na mazoezi, muda huo alikuwa kajiegesha nje kidogo na Kambi kulikuwa kunae jiwe kubwa aliamua kujilaza Chali huku akiwa anakumbuka mambo mengi yaliyohusu familia yake, ni miaka mingi Sasa Dada’ke atoweke nyumbani siku hiyo alimpazia sauti sana akisema waliomuua Mama’ke lazima wangelipa, mawazo yalikuwa mengi sana ikabidi ainuke baada ya kusikia mchakato ni kama Kuna mtu anakuja pale.

       “” Ooh Eliud, Vipi Leo hakuna Lindo hata la kutoka nje ya Kambi? make nimekumbuka nyumbani Leo.”

    [ Eliud huyu ndie alikuwa rafiki yake na Nick alimshuhudia siku Ile Minii akimpazia sauti nae alibahatika kujiunga na jeshi]

    Wakati wanazidi kuongea mazungumzo yao yaliingiliwa alikuwa ni Amri akiwa na wenzake watatu, kwa kumbukumbu ya mwisho hawa ndio wanajeshi walioonana na Minii siku ya mwisho porini.

       “” Nimesikia umekumbuka nyumbani, Halafu Yule Dada’ako mzuri mzuri alienda wapi? Make mara ya mwisho tulimuona porini akiwinda ndege au alitoroshwa?

    Nick ikabidi asimame kwanza akimkaribia Amri.

       “” Hapana mdogo wangu hawezi kutoroshwa namna hiyo, sielewi kipi kiliwakuta yeye na Baba’ngu ila watakuwa hai.””

       ” Mhuu sawa, lakini mara ya mwisho alienda kuwinda.”

    Nick akaona awaache maana ni kama walimchanganya tu, ilibidi asimame na kuwaacha pale, lakini Amri alimsogelea karibu.

       “” Leo nilitakiwa kuongozana na wenzangu kuhemea chakula Cha Kambi nitakuachia nafasi hii ufike kwenu.”

    Amri aliamua kumfanyia fare Nick alihisi kabisa Kuna muda anakuwa mood less huenda kwenda kwake nyumbani itamfanya awe sawa, Nick hakusita kumpatia mkono kama ahsante.

    Nick alipata muda wa kupita nyumbani na hii ni mara baada ya kuagana na wenzake akiwaacha sokoni, Alifika Hadi nyumbani kwao nyumba ilikuwa kimya sana akawa anafikilia Kuna watu aliwapangisha pale inamaana walihama au walilala, ikabidi azidi kuingia ndani akifanya kugonga mlango.

       “” Hii nyumba watakuwa wapi teenaa…!!?”

    Ukimya ulivyozidi aliamua kuingia kwenye Moja ya chumba chake alichokuwa akikitumia, alichukua file Moja lilokuwa na vitu vingi vyenye ukumbusho wa familia yake lakini ndani yake aliona album ya picha nakuamua kuipitia Kila picha iliyokuwa mle. Alikutana na picha ya Mama’ke alifanya kuitazama mpaka machozi yakitiririka.

       “” Bila Mama kupoteza maisha, Mdogo wangu,, Baba’ngu wote wangekuwepo,,, Leo wote wamekimbia kwenda kulipa kisasi Cha kifo chako,,, Sijui hata wako wapi lakini walipaswa hata kunijulisha sehemu walipo.”

       “” Nickson….!!!

    Ni sauti alisikia masikioni mwake na kuamua kufunika Ile Album, ni aliitambua vyema kabisa mtu huyo alimuita kwa kirefu ikabidi ageuke huku akimuita jina lake.

       “” Asia, kwanini upo hapa…!!?”

    Dada yule alietambulishwa kwa Majina ya Asia alimsogelea na kumkumbatia tu.

       “” Najua unavyojisikia, lakini Kila kitu kitakaa sawa tu.””

    Nick alifanya kuinuka huku akirudisha Kila kitu mahali pake.

       “” Vipi mmemaliza mahemezi..!? Wakati mwingine usinifuate tenaa.”

    Asia alimtizama Kisha akacheka tu na kumkumbatia zaidi.

       “” Wakati mwingine pia Mimi sitazuia hisia zangu pale nitapoona unaumia, Siwezi vumilia Nickson.”

       “” Sawa nimekuelewa, ila umeniita kama Mama kabisa mpaka nimehisi uwepo wake.”

       “” Basi, hata hivyo nafaa kurudisha Mapenzi ya Mama na Mimi ni Mama pia, natakiwa nilee mtoto wangu kwa Mapenzi mazuri.””

    Nick hakusita kumpatia busu mrembo huyu kwani wao walikuwa tayari wapo kwenye Huba zito japo Huba lao lilikuwa la kujificha pindi wawapo kazini wengi waliwafahamu ni kama Marafiki tu na kingine wote walikuwa kwenye kitengo kimoja.

       “” Hivi…, Mama Naomi katoka? Akimuulizia Mama aliekuwa kapangishwa pale.””

      “” Nimefika hapa naona makufuri labda wapo sokoni. Tuondoke tu.”

    Wanafika mlangoni ndio wanamuona Binti wa Mama Naomi ambae ni Naomi akifika Toka shule.

       “”” Ooh Kaka… Leo umetukumbuka, ni siku nyingi huonekani..!?”

       “” Huwa naja lakini unakuwa shule.”

      “” Hata Mama asiseme..?”

    Nick akatabasamu tu Kisha alitoa noti ya elfu kumi akimpatia.

      “” Utanunua madaftari, Mama akirudi mwambie nilikuepo nitakuja siku nyingine teena.””

       “” Sawa Kaka, Nimekumbuka kitu kwanza nisubilieni hapoo,, Mama alisema nikupe nikikuona.”

    Naomi akawa amekimbia ndani, Nick akabaki kumtizama tu.

       “” Kamekua Sasa, umri aliokuja nao nyumbani hapa nikimwangalia sahii kaongezeka kweli, nawaza alivoongezeka hapa Minii sijui kaongezekaje huko aliko.”

    Asia akabaki kumtizama tu, bilashaka anakumbuka vitu vingi sana awapo mazingira ya nyumbani. 

    Naomi nae akawa amefika na kumpatia bahasha ndogo iliyokuwa imeandikwa kwa juu “” Kwako Nickson Mzobe “

       “” Twende bhana naona simu zimeanza hapa, nikitulia nitaisoma.”” 

    Nini Kitaendelea? Minnie amekubali kuolewa akalipe kisasi? Vipi kuhusu Nick? Atapambana nae kulipa kisasi? Wewe Ungelipaje KISASI? Usikose SEHEMU YA NNE

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

     

     

    Kisasi Changu Riwaya Ya Kisasi Changu

    16 Comments

    1. Zacharia on July 4, 2024 6:14 pm

      Admini apewe maji kwanza jamn riwaya zake nzuri ebu tumpooze koo kidogo

      Reply
    2. Dimess on July 4, 2024 6:27 pm

      Fupi kali
      Ndefu kali itapendeza zaidi

      Reply
    3. Mabadiliko on July 4, 2024 6:29 pm

      Good job kiongoz nakupenda sana

      Reply
    4. Alhaji on July 4, 2024 6:36 pm

      Kitu ya moto moto

      Reply
      • Fawziya Hassan on July 5, 2024 7:35 am

        Asante kaka kwa Hadithi nzuri n yenye kuvutia 💕
        More ❤️

        Reply
    5. Hamisi on July 4, 2024 6:38 pm

      Nice sana

      Reply
    6. Rosemary Edward on July 4, 2024 7:40 pm

      Nice job I like it

      Reply
    7. Ramadhani on July 4, 2024 7:56 pm

      Nzuli kabisaa

      Reply
    8. Calvin paul on July 4, 2024 8:06 pm

      😋😋😋😋

      Reply
    9. Fatma on July 4, 2024 10:25 pm

      🔥🔥🔥

      Reply
    10. Saruuh on July 5, 2024 12:47 am

      🤩😘

      Reply
    11. Tinner Rober on July 5, 2024 9:27 am

      Makini sana ❤❤❤

      Reply
    12. Shuu on July 5, 2024 3:07 pm

      Stori nzuri

      Reply
    13. Alice simbeye on July 5, 2024 4:08 pm

      Ooh hongera

      Reply
    14. Veronica William on July 7, 2024 5:35 pm

      Upewe maua yako kaka

      Reply
    15. Habiba on July 7, 2024 11:21 pm

      Riwaya nzuri saaan admin kazi nzuri

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.