Ilipoishia “Hizi ni risasi zilezile, chukueni maiti hizi na wengineย fanyeni msako hapa haraka sana” Ilikuwa ni sauti ya mmoja waย Askari waliokuja pale kanisani, bado Mtaalam Sande, Mzeeย Dawson na vijana wake wakiwa ndani ya Andaki bila kuwa naย taarifa kuwa Jesca alikuwa ameuawa na Six, lilipofunguliwa lango kuu la Kanisa ndipo mshituko na Mshangao mkubwaย ulipowashika polisi hao, walikuta Miili ya watu ikiwaย inatokwa na mvuke kama vile nyama inayochomwa, harufu yaย nyama ilitapakaa kanisa zima wakaagiza zima moto kumwaga Majiย katika kanisa hilo, muda mchache polisi walifanikiwa kuingiaย ndani ya kanisa na kukuta Miili mingi ikiwa imeharibikaย vibaya sana.ย
Taarifa ilizagaa kwa haraka sana juu ya shambulio hilo laย kutisha ambalo lilitumia silaha ya sumu na risasi, Sandeย akawashauri akina Mzee Dawson kuwa hawapaswi kutoka kwaย wakati huo hadi polisi watakapo maliza msako wao. Endeleaย
SEHEMU YA TISA
“Nina mashaka juu ya uhai wa Jesca, yeye ni mmoja wa walinziย wa hapa kanisani, sijasikia majibizano ya risasi, huwendaย amekufa kifo Baridi” Alisema Mzee Dawson akionekana kushindwaย kuzuia chozi lakeย
“Una maanisha nini kusema Kifo Baridi?” Alihoji Mtaalam Sandeย Olise huku akimtazama Dawson kwa jicho lililo kazaย
“Kufa bila kujibu mapigo, Walengwa tunaotafutwa katika vitaย hii ni sisi. Sitaki makubwa yawakute wasio na hatia” Alinenaย Dawsonย
“Una maaana gani?”ย
“Ni bora nijitokeze kupambana nao ili kunusuru Maisha yaย wengi yanayowekwa rehani, ikiwa kufa Mimi au kupona waoย ninachotaka ni usawa” Aliongeza Dawsonย
“Kumbuka Polisi watakuangalia kama muarifu kuanzia hivi sasa,ย hautokuwa huru kufanya chochote kama Mkuu wa Kitengo, vitaย hii ni ngumu Mkuu! Vipi kama Rais ataamuwa kukupaka tope?ย Utakuwa salama?” Aliuliza Sande Olise, Mzee Dawson akamezaย funda zito la mate kisha akasemaย
“Tusipopambana sasa hivi tutakuja kupambana nje ya muda,ย tunapaswa kuwa macho zaidi”ย
“Unashauri tufanye Nini Mkuu tupo tayari kukusaidia katikaย vita hii” Alisema Kisko kwa utii Mkubwa, Dawson alikuwa kamaย Mzazi kwao, ndiye aliyewachukua kutoka katika kituo chaย Watoto yatima na kuwaonesha Mwanga wa Maisha, Dawsonย akawageukia na kuwaambiaย
“Natamani hii vita msipigane sababu mna kila sababu ya kuwaย hai ili mje mpigane hapo baadaye sisi tukiwa tumetundikaย daruga au tukiwa tumekufa. Niliwaandaa mje kuwa hazina muhimu baadaye” Alisema Dawson kwa sauti ya Baba kwa Watoto wake,ย nyuso za Kisko na Chande zilisinyaa huku macho yao yakitazamaย chini.ย
“Babaa!! ” Aliita Chande, Dawson akageuza macho yakeย kumtazamaย
“Tupo tayari kwa sasa kufa kwa ajili ya Taifa letu, turuhusuย tukusaidie hii vita” Dawson alipomaliza kumsikiliza Chandeย akarudisha macho yake kwa Sande Olise, Wakajikutaย wanatazamana huku sura zao zikizungumza Kijasusiย
“Tuangalie tunatokaje hapa Shimoni, haribuni kila kitu iliย kupoteza ushahidi wa kazi za hapa ndani, kila mmoja avae suraย bandia haraka sana” Aliagiza Mzee Dawson kwa sauti iliyojaaย mamlaka ya Kijeshi, kazi ikaanza rasmi.ย
MSAKOย
“Shit!” Ilikuwa ni sauti ya John Brain baada ya kupokeaย taarifa usiku huo, hakutegemea kusikia kuwa Dawson na Sandeย Olise bado wanaendelea kupumua, aliona ni makosa makubwa niย sawa na kumjeruhi mnyama Mkali.ย
“Inawezekanaje wasiwepo kanisani wakati mtoa taarifaย amehakikisha kuwa Sande aliingia hapo? Endapo Sande na Dawsonย wakapata muda wa kupanga mipango yao kazi hii itakuwa ngumuย kwetu” Alisema tena John Brain huku akizitazama sura za Sixย na Malaika ambao walikuwa wamenywea.ย
“Nimefanya msako kanisa zima lakini sikupata kuhisi hataย harufu zao, huenda walicheza mchezo wa sarafu baada yaย kugundua kuwa tunawafuatilia” Alijibu Malaikaย
“Watakuwa wapi?” Aliuliza John Brain akionesha kutafakariย jambo peke yake, kisha akawaambiaย
“Nendeni lakini Mjiandae kwa msako maalum” Malaika na Sixย wakaondoka, John Brain akampigia simu Rais na kumjulishaย taarifa ile ambayo ilionekana kumchanganya sana Raisย
“Hivi mnajua mnafanya masihara kwa Watu gani? Hao jamaa wanaย medali za ushindi kwenye kila jambo, Dawson ana fahamu siriย yetu hivyo hapaswi kuendelea kuishi” Alisema Rais kama Mtuย aliyeingia kwenye mshituko ni wazi kuwa alitarajia kusikiaย kuwa Dawson na Sande wameuawa
“Tunalijuwa hilo na vijana wangu wanalifanyia kazi jambo laย muhimu ni kuhakikisha unatupatia Mtu wetu baada ya sikuย chache, tutakuwa tumeimaliza kazi hii na kuondoka hapaย Nchini”ย
“Msifanye Makosa mengine John , mtajikuta mnawajibishwa!ย Ngoja nijisafishe haraka sana” Rais alikata simu, alionekanaย kuwa mwenye msongo wa mawazo huku akionekana kuwa na hofu juuย ya mpango wake wa siri juu ya Mauwaji ya Makam wa Raisย kujulikana na kuwekwa hadharani, akanyanyua simu na kumpigiaย Mkuu wa Idara ya polisi na kumueleza kuwa Dawson ni mharifuย anapaswa kusakwa kwa kila njia ili apatikane, Rais aliamuwaย kucheza karata mbili.ย
Moja ni kuwatumia Mafia Gang kumfyeka Dawson na nyingine niย kutumia Jeshi la polisi kumsaka popote alipo, agizo la Raisย lilianza kutekelezwa, Polisi wakaagizwa kuelekea nyumbani kwaย Dawson usiku huo huo.ย
Rais alikaa katika kiti chake huku akizidi kujiingizaย mawazoni, Nchi ilikuwa imeingia katika Msako, Polisiย walivunja nyumba ya Dawson na kufanya msako mkubwa bilaย mafanikio, wakati huo Dawson na timu yake wakiwa wanatokaย katika shimo kule kanisani, Polisi wachache walikuwepo eneoย la tukio kule kanisani usiku huo, Walifanikiwa kuchomoka paleย kanisani kimya kimya kisha wakaruka ukuta wa kanisa naย kutokomea.ย
Dawson alishajua kuwa polisi wataenda nyumbani kwake hivyoย akawaambia wasiende huko badala yake waelekee kwenye makaziย ya siri ambayo alikuwa akiishi Inspekta Zola, ilikuwa niย safari ya Kilomita kadhaa kutoka pale kanisani hadi kufikaย huko, walilazimika kutembea kwa mguu sababu polisi walikuwaย wakikagua magari yanayoingia na kutoka kila kona ya jijiย hilo, haikuwa salama kwao kutumia usafiri wa gari licha yaย kuvaa sura bandia, mwendo wa masaa mawili Walifika kwenyeย makazi hayo, Dawson alifahamu namba za siri za kufunguliaย milango hiyo ikawa rahisi wao kuingia ndani.ย
Kumbukumbu ya Zola iliendelea kuwatesa baada ya kuingia humo,ย Sande aliiona picha aliyopiga na Zola wakiwa mafunzoni hadiย chozi lilimbubujika aligundua kuwa Rafiki yake huyo alikuwaย akimpenda na kumkumbuka sana, walikuwa na ndoto ya kuonanaย siku moja lakini ndiyo hivyo Sande alichelewa kurudi hadiย Zola akauawa, Dawson aliifahamu nyumba hii vizuri sana sababuย mpango wa nyumba hii aliusuka mwenyewe ili Zola aitumieย nyumba hii kwa kazi zake maalum, akawaonesha chumba ambachoย kilikuwa na silaha akawataka kujiandaa kwa ajili ya kazi hiyoย kubwa iliyo mbele yao.
“Baada ya kupambazuka tutakuwa katika hekaheka nzito yenyeย maamuzi ya kuondoa uhai wetu au kuturuhusu kuendelea kupumua,ย kama tuna muda wa kufurahi basi huu Usiku uliobaki unawezaย kuwa ndio muda pekee wa kufanya hivyo” Alisema Dawson akiwaย ana mimina mvinyo kwenye glasi, kila mmoja akanyanyua naย kuanza kunywaย
“Kwa ajili ya Zola, tusherehekee Maisha yake sababuย ameimaliza kazi aliyokula kiapo kuifanya ili kulinda Taifaย lake” Yalikuwa ni maneno ya Sande Olise ambaye naye aliunganaย na Mzee Dawson wakanywa Glasi moja moja, Chande na Kiskoย wakaungana pale wote wakapata Mvinyo kama Ishara ya kuyaenziย Maisha ya Inspekta Zola ambaye ameuawa ndani ya Ikulu, hadiย kufikia muda huo hakukuwa na taarifa iliyotolewa popote kuwaย Inspekta Zola alikuwa amekufa, si akina Dawson wala upande waย Rais ambao ndio walitekeleza Mauwaji hayo.ย
Asubuhi ya siku iliyofuata iliwakuta Dawson na vijana wakeย wakiwa ndani ya jumba la siri hilo alilokuwa akiishi Mtaalamย Zola, taarifa kuwa Dawson amelisaliti Taifa ilianza kuzagaa,ย akatajwa Dawson kama ndiye Mhusika namba moja wa Mauwaji yaย Waumini kule kanisani, taarifa ikafika mbali na kusema anaย viashiria kuwa alitaka kuipindua Nchi hiyo kwa kusababishaย taharuki ikiwemo Mauwaji ya kutisha yaliyokuwa yakifanyikaย pia Mauwaji ya Makam wa Rais, gunzo lilikuwa limetanda, niย kama Bundi mweusi alikuwa ameyazunguka Maisha ya Dawson,ย ikatolewa taarifa kuwa Dawson anashirikiana na Askari mmojaย wa Usalama wa Taifa aliyeitwa Sande Olise ambaye alikuwaย akiishi Botswana.ย
“Huyu Mjinga anajaribu kuharibu taswira niliyoijenga Miakaย mingi katika Taifa hili” Alisema Dawson kwa hasira hukuย akitafuta rimoti ya TV ili aizime, Sande alimzuiaย
“Huna haja ya kupaniki, anachokifanya Rais ni kujaribuย kujisafisha na kuyatia doa Maisha yetu. Kwakuwa anajua unaย siri zake basi anaitumia hii nafasi kukudidimiza iliย usiaminike na yeyote yule” Alisema Sande kisha Dawsonย akamuulizaย
“Mimi ni mzalendo kwa Taifa hili, nimekuwa kwenye nafasi hiiย kwa Marais zaidi ya tano, iweje huyu aje kuharibu kila jemaย nililopanda kwenye Taifa hili, baada ya kuniulia Rafiki yanguย anadiriki kuniita Msaliti wa Taifa hili” Dawson alionekanaย kuchukizwa sana na kitendo kile, akapapasa kiuno chake akatoaย bastolaย
“Unaenda wapi?” Alihoji Sande
“Ikulu kuondoa uhai wa hayawani yule, hastahili kuishi pale,ย anastahili kuwa Kaburini au Jela kwa yote aliyoyafanya”ย
“Hebu tulia, kumbuka John Brain ni Mtu mwenye akili sana. Huuย ni mtego na lengo ni kukufanya uchukie, Rais anakujua vizuriย hupendi mchezo na uzushi, ukitoka hapa hata hufiki mbaliย wanakuuwa” Alisema Sande huku akimsistiza Dawson atulie,ย chozi lilikuwa likimbubujika Mzee Dawson, akajitupa kitiniย kama Mtu aliyekata tamaa.ย
“Huna haja ya kukurupuka, Tumetajwa kuwa Wauwaji na wasaliti,ย tukikamatwa huko nje hatutokaa kuonekana tena, tutaliachaย Taifa hili katika giza kama ambavyo Zola ameliacha. Nimekujaย hapa kwa ajili ya kazi hii, nitazame Mimi kwa sasa kamaย ambavyo ulikuwa ukimtazama Zola na kumuamini, hamisha kilaย kitu kutoka kwake kisha kiweke kwangu, Mimi ni Zola niliyeย katika Umbo la Sande, hakuna kitakacho haribika” Yalikuwa niย maneno ya Kikomandoo kutoka kwa Sande Olise, alisema akiwaย amefanikiwa kumpokonya Bastola Dawson.ย
Akampatia ile Bastola Kisko akamwmbiaย
“Ukiitumia vibaya itakupeleka pabaya, tuliza akili ndipoย uitume ifanye kazi yake” Alimkabidhi kisha Akasemaย
“Baada ya miaka mingi narudi kazini kupambana na John Brain,ย kivuli chake kitaendelea kuitesa hii Nchi, huyu Rais Mpumbavuย siku zake za kuwa madarkani zinahesabika” Alisema kishaย akaelekea kwenye moja ya vyumba vya siri vya jengo hiloย ambavyo vilikuwa vimeshafunguliwa na Mzee Dawon.ย
Akakuta Ramani ya mpango wa Zola ikiwa ukutani, akaangaliaย namna Zola alivyopanga mambo yake pale akajikuta akitabasamuย kwani kila jambo alikuwa ameliandika katika Ramani hiyo.ย
Nyuma ya Sande alikuja kusimama Mzee Dawson huku akimtazamaย Sande namna alivyokuwa makini kutazama Ramani ya Zolaย
“Ulikuwa na askari shujaa sana ambaye hasahau mbinu zako”ย Alisema Sande Olise kisha aligeuka na kumtazama Mzee Dawsonย aliyekuwa akifuta chozi lake, kifo cha Zola kilimuumiza sana.ย
“Nina uhakika kama utawatunza vijana hawa wawili wanawezaย kuwa Sande na Zola wa baadaye, kwasasa Mzee Dawson pumzika.ย Afya yako haikuruhusu kuendelea na vita hii, nitapambana Mimiย na hawa vijana, utabakia hapa” Aliongeza Sande, ni kweli afyaย ya Dawson haikuwa nzuri kutokana na pombe na sigara.
Wakapanga mipango ya kumuondoa Rais Madarakani kisha kuanikaย uchafu na madudu yake yote, Dawson alitakiwa kubakia paleย kwenye jumba la siri wakati ambao Sande na vijana wawili waย Dawson watakapokuwa wanaondoka, wakapewa sura bandia iliย watakapotoka nje wasijulikane.ย
Muda huo Magari mawili meusi yalikuwa yakiingia Ikulu,ย alikuwa ni John Brain, Six na Malaika, utatu ambaoย ulilisumbua Taifa kwa muda mrefu, waliitwa na Rais huyoย Mshenzi. Waliingia wakiwa kama wageni wakiwa ndani ya suraย bandia ili wasitambulike sababu Vyombo vingi vya habari hasaย vya nje vilikuwa vikiripoti taarifa zao za Mauwaji na jinsiย ambavyo walikuwa wakitafutwa, Waliongoza hadi ofisini kwaย Rais huyo bila Ulinzi wowote kutokana na maagizo ya Rais.ย
Rais alipowaona alinyanyuka na kusogea karibu na John Brainย kisha akamuulizaย
“Mnataka niwape nini ili Dawson na Sande wauawe? Mnapaswaย kujuwa kuwa Dawson ni nyati aliyejeruhiwa akitoka hukoย mafichoni hatutokuwa salama” Alisema huku akionekanaย kuchanganikiwa, jasho lilikuwa likimvujaย
“Tatizo umechanganya vitu viwili kwa wakati mmoja, Polisiย wanahangaika kuwatafuta na sisi tunahangaika kuwapata. Kilaย tunapopiga hatua polisi wanakuwa eneo la tukio, au unatakaย tusamabratishe na polisi wako?”ย
“Kama hilo ni tatizo nitawaingiza katika mfumo wa usalama waย Taifa mkiwa katika sura hizo, John utakaa pembeni sababu yaย rangi yako ila Malaika na Six wataingia na kufanya kazi maraย moja, watakuwa na amri kwa askari pindi wanapokutana katikaย jukumu la kuwawinda Sande na Dawson,watapewa vitambulishoย maalum”ย
Rais akawaingiza Six na Malaika katika mfumo wa idara yaย Usalama wa Taifa, wakapewa na Vitambulishoย ย
vilivyowatambulisha kama Watu wa Usalama, ikawa rahisi kwaoย kuwa huru kufanya kazi ya kuwasaka Dawson na Sande Oliseย ambao walikuwa kizingiti kikubwa kwa Rais na John Brainย kumpata kijana wake aliyekuwa akishikiliwa na Rais.ย
Polisi wakatawanywa kila kona ya Jiji kuhakikisha Dawson naย Sande hawapigi hata hatua moja, kazi ya polisi ilikuwaย kuwakamata lakini kazi ya Six na Malaika ni kuwauwa, wakiwaย ndani ya Sura bandia walirudi pale Kanisani ambakoย walisababisha Mauwaji ya kutisha ya Waumini na Askari mmojaย wa siri wa Mzee Dawson, walirudi kama Watu wa Usalama,ย wakahitaji kuchunguza eneo hilo huku akili zao zikiwaambia kuwa pengine Dawson na Sande bado wapp eneo hilo, walimjuaย vizuri Dawson jinsi alivyo na akili nyingi.ย
Walitumia vyema macho yao ya Kijasusi na mafunzo waliyoyapataย kutoka kwa John Brain wakagundua kuwa kuna andaki eneo laย maegesho ya Magariย
Six na Malaika wakapeana ishara, haraka bastola zao zikawaย zinatazmaa eneo hilo ili kama kuna Mtu atatokea basiย wamdhibiti haraka sana.ย
Wakalisukuma gari na kuona mlango wa kuingia ndani, harakaย wakiwa makini sana wakafungua na kuanza kuingia humo taratibuย huku masikio yao yakiwa makini kusikiliza ndani ya andakiย hilo lenye giza sana.ย
Walipofika chini wakawasha tochi ya simu kisha wakaona mahaliย ambapo wangewasha taa, walipowasha wakaona vitu vikiwaย vimeharibiwa pale, wakakagua kila kona lakini hakukuwa naย Watu, tayari Mzee Dawson na vijana wake walishaondoka paleย muda mrefu sana kisha wakaharibu vitu ndani ya andaki hilo,ย elimu yao ya kijasusi haikuwafanya wao kukata tamaa ya kutakaย kujuwa andaki hilo lilihusiana na niniย
“Kwa vyovyote haya yalikuwa makazi ya siri ya Dawson! Huendaย ameishi hapa kwa kitambo sana” Alisema Sixย
“Hata awe makini vipi ni lazima ataacha alama humu, tutajuaย kama ni yeye na ameenda wapi” Alisema Malaika, msakoย uliendelea ndani ya andaki hilo lililoonekana kuwa makazi yaย kutulia sana, katika upekuzi wao waliona Makaburi manneย ambayo yalikuwa ndani ya chumba kimoja.ย
Walipoangalia vizuri waliona namba za siri ambazo Mzee Dawsonย aliwapa vijana wake kama majina na alama zao, namba hiziย zilikuwa za siri sana, ilikuwa ngumu kugundua chochote lakiniย alizitambua kisha akampigia simu John Brain na kumuelezaย kuhusu Makaburi hayo manne yenye namba za siri, John Brainย alikuwa na mtandao mkubwa sana na alizijua siri nyingi zaย Mataifa mbalimbaliย
“Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupoย hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola,ย fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliaminiย Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake.ย
Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwaย bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenyeย kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwaย likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuiaย kufanya kazi yao,
Comments ziwe nyingi apa wikiendi itoke EPISODE NDEFU YA 10ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxย
ย ย
22 Comments
unyama
Kazi kazi
Toa hata tatu mzee baba
Weeknd usitubanie asee
Kila unaesima naomba ucoment please
Too hot๐
Ya motoo
.wendelzo jmn pia zilishwe hata tano kwa siku ๐ฅฐ๐ฅฐ
Simulizi ya ๐ฅ
Mtunzi wa Simulizi hii anitafute kuna Zawadi yakeโฅ๏ธโฅ๏ธโฅ๏ธ
Daah imefka penyew mkuu uwe unatoa hata mbili basi mkuu
Stor iko poa sana
Hatar iyooรณoo
Nzuri sana
Shusha chuma mkuu ๐คด
Weeee
Kesho tuwahishie Basi pia ilefushe hata kidogo maana siku za mpira hua unabana Sana
Jmn huyu malaika na six. Si sande wawauwe fasta wasijeniulia Mzee wangu Dowson jmn
Admin story Kali sn ni km vile mtu unaangalia movie
Hili ni bomu la kutegwa ardhini kilo mia moja haponi mtu hapo ni mbele kwa mbele ๐คธ๐คธ๐คธ๐ก
๐ฅ
Natamani ingekuwa movie kbs yani uwii admin upewe maua yako โบ๏ธ
Kazi nzuri admin una jitahidi
3exvik