Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Jasusi Sehemu Ya Saba (07)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Saba (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaDecember 4, 2024Updated:December 5, 202445 Comments17 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Kama Maisha yangu yatakoma leo Ikulu, Sande uje kufanya hiiย  kazi kuliokoa Taifa mara moja” Alisema Zola kisha choziย  lilimtoka, akakata simu hiyo. Visa vya baadhi ya Askariย  kupotea vilikuwa vingi katika Taifa hilo, Zola baada ya Masaaย  mawili alikuwa akikaguliwa kwa ajili ya kuingia Ikulu,ย  ilikuwa ni mara ya kwanza Zola kuitwa na Rais huyo, si Raisย  huyu Pekee bali Zola hakupata kujulikana na Rais yeyoteย  aliyepita, hii ilimpa shaka sana Zola kwanini Rais ampigieย  simu wakati ambao alikuwa akimbana yule Askari amwambieย  ukweli kuwa Nani anafanya Mauwaji yale.ย  Endeleaย 

    SEHEMU YA SABAย 

    Upande wa Sande Olise, Chozi la Zola lilimkumbusha mbali sanaย  wakati huo Zola alipokuwa akiogopa kwenda kufanya mafunzoย  hayo ya Ujasusi na Upelelezi Nchini Mexico, mafunzo hayoย  yaliambatana na Mafunzo ya Ukomando, Sande ndiyeย  aliyemshawishi Zola kuingia huko laiti kama asingelimshawishiย  basi Zola angekuwa Askari wa kawaida kabisa, Mafunzo hayaย  hufanywa siri sana, kitengo cha siri cha Mzee Dawson ndichoย  kilichokuwa kikifanya uchaguzi wa nani aende na Nani asiendeย  hivyo Dawson alificha sana majina ya Askari wake wa siriย  ambao ndio alikuwa akiwatumia kwenye majukumu mazito ambayoย  Serikali ilimpa, haraka akafungua Kabati lake lililo chumbaniย  kwake akaitoa simu ya Siri ambayo ilitumika kwa ajili yaย  Mawasiliano yao ya Kiaskari, akampigia Mzee Dawson.ย 

    Mzee Dawson ( Google ) aliposikia sauti ya Sande alijuwaย  kulikuwa na tatizo, akameza funda zito la Mate, sauti hiyoย  hakuisikia kwa miaka mingi sana. Licha ya kuwa ni Mmoja waย  vijana wake wa Kitengo lakini Sande alikuwa Botswana kwaย  miaka mingi mno, alipojitambulisha ndio Mzee Dawson akapataย  kujihakikishia zaidiย 

    “Sande! Bado unanikumbuka?” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaaย  wasiwasi sana huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio, maraย  nyingi hakuwa akipokea simu za siri sababu yeye ndiyeย  aliyekuwa akiratibu kazi za Kijasusi hivyo yeye ndiyeย  aliyekuwa Mpigaji mara zote kutafuta vijana wake, leoย  alitafutwa yeye na Sande!!ย 

    “Naam! Mkuu wa Kitengo, Mimi ni P045! Simu ya dharura, narudiย  Nchini kwa kazi maalum, nahitaji Baraka zako!!” Ilikuwa niย  sauti iliyojaa uzalendo na ujasiri wa hali ya juu uliombatanaย 

    ย ย 

    na Utii sababu licha ya Mzee Dawson kuwa Mkubwa kiumri badoย  alikuwa ni Askari mwenye Cheo kikubwa sana! Alikuwa ni kamaย  Baba yao mzazi kwenye kazi za Kijasusi.ย 

    “Zola amewasiliana na wewe?” Aliuliza Dawsonย 

    “Ndio, yupo hatarini. Maisha yake yapo mikononi mwa Raisย  Zagamba, narudi kumkomboa” Alisema Sandeย 

    “Uuuupss!!”ย 

    “Ndio Mkuu! Kwasasa Mkuu wa Nchi anawinda maisha ya Zola, niย  ngumu kujuwa kama atatoka salama sababu yupo njiani anaendaย  Ikulu ameitwa na Rais” Kauli hii ilimpa mshituko Mkubwa sanaย  Mzee Dawson,ย 

    “Tuongee baada ya dakika chache” Alisema Dawson, kishaย  alikata simu hiyo. Mara moja kanyanyua simu yake akampigiaย  Zola ili kuthibitisha alichokisia, Simu ya Zola ilikuwaย  imezimwa.ย 

    “Shit!!” Akasema Dawson kisha akatoka nyumbani kwakeย  akaelekea Ikulu, Sande alikaa kusubiria simu ya Mzee Dawson!!ย 

    Alipofika Ikulu, Dawson alikaguliwa kabla ya kuruhusiwa, mojaย  kwa moja akaelekea ofisini kwa Rais, akamsimamia Rais naย  kumpigia Saluti kisha akaketi kwa heshimaย 

    “Dawson!! Kwanini umekuja kama Mkimbizi kutoka Somalia?”ย  Alihoji kwa dhihaka huku akiwa anaandika kituย 

    Dawson alimtazama Rais Jacob Zagamba huku akili yakeย  ikipingana na mawazo yake juu ya kuuliza kuhusu Inspektaย  Zola, hakutaka ijulikane kuwa Zola ni Askari wake wa siri waย  Kitengoย 

    “Nimekuja tuongee kuhusu Hii kesi”ย 

    “Umefikia wapi Dawson?”ย 

    “Bado uchunguzi unaendelea lakini nimefikia mahali pazuriย  sana na siku si nyingi nitakupa mrejesho kuhusu Kundi laย  Mafia Gang” Alisema Dawson huku macho yake yakionesha kuwaย  sicho kilichompeleka pale.ย 

    “Dawson nahitaji hili jambo ulimalize ndio maana nikaliletaย  katika Meza yako, ninachotaka kusikia siku moja ni kuwaย  umeuwa Wahusika wote na kuileta miili hapa, hao Watuย  hawatakiwi kuishi kabisa” Alisema Rais na kumpa maswaliย  Dawson, kwanini Rais atake Watu hao Wauawe?

    “Nitawakamata kisha watahukumiwa kufungwa kifungo cha Maisha,ย  hiyo ni ahadi yangu kwako Mkuu” Rais akamtazama Dawson kwaย  hasira kisha akagonga mezaย 

    “Nimesema nahitaji Miili yao, fyeka kundi hilo haramu naย  mazalia yake hapa Nchini, Dawson narudia tena nahitaji miiliย  yao, hawana kesi ya kujibu….hili jambo linapaswa kufanywaย  siri, kinachotakiwa ni kuwa Watu hao wakifa basi vifoย  vitakoma, hakuna atakayeuliza wako wapi, haya ni maagizoย  yangu” Alisistiza Rais, muda huo akaingia Jamaa mmoja mweusiย  aliyepanda Hewani, alionekana kuwa ni Usalama wa Taifa, Raisย  akamuuliza Mtu huyoย 

    “Safari inaanza?”ย 

    “Ndio Mkuu” Alijibu kwa Utii, kisha Rais akachukua funguo yaย  gari akampatia jamaa huyo, Dawson hakuelewa kilichoendeleaย  pale japo hakujuwa Zola yupo wapi.ย 

    Baada ya jamaa huyo kuondoka Dawson akaaga ili aweze kuondokaย 

    Alipofika karibu na Lango kuu la Ikulu alikutana na walinziย  wawili ambao ni dhahiri walikuwa wakimsubiria yeye ili wamtoeย  nje, alipowafikia walimpa ishara kuwa wao walikuwaย  wanamsubiria, Dawson akatupa macho yake huku na kule, Milangoย  mingi ilikuwa imefungwa, walinzi hao ambao walivalia sutiย  nyeusi waliongozana na macho makali ya Dawson ili kujuwaย  alikuwa akiangalia nini, basi wakampa tena ishara kuwaย  aongozane nao, wakati anatoka pale mlangoni macho yakeย  yalitupa uangavu kuelekea kwenye maegesho ya Magari ya Ikulu,ย  ndipo alipomuona Jamaa aliyetoka kuzungumza na Rais akiwaย  amebeba begi kubwa lililomzidi uzito, Dawson alijikutaย  akiingiwa na shahuku ya kutaka Kujuwa jamaa huyo alikuwaย  akifanya safari gani. Akawageukia walinzi akawaambiaย 

    “Asanteni! Nitafika” Alikuwa na nia ya kuwatoroka ili afanyeย  upelelezi wake sababu bado kichwa chake kilikuwa kinaliaย  alamu kuwa Zola yupo matatizoni,ย 

    “Ni wajibu wetu kukufikisha lilipo gari lako” Alisema mmojaย  wa walinzi hao tena akiwa anatabasamu, walimjuwa vyema Dawsonย  kuwa ni mmoja wa Askari waliotegemewa sana na Kila Raisย  aliyepita, alikuwa na cheo kikubwa mno, pale pale Zolaย  akapata akili, akakohoa na kutoa damu kitu ambachoย  kiliwashtua wale Walinzi wakiamini anaumwa, ni kweli Dawsonย  alikuwa anaumwa mapafu yake kutokana na uvutaji wa sigara ilaย  hapa aliamuwa kucheza na akili za Walinzi hao ili awatoroke,ย  taharuki ikazuka pale huku mmoja akijaribu kuita gari yaย  wagonjwa

    “Msijali nahitaji Kitambaa” Alisema Zola kwa sauti yenyeย  kikohozi, Walinzi hawakuwa na kitambaa, mmoja akatoka kwendaย  kuchukua tishu ili imsaidie Dawson, ulikuwa mtego. Harakaย  Dawson akajikunjua na kumpiga ngumi kali sehemu ya shingo naย  kufanikisha kumzimisha pale pale, akamburuza hadi maegesho yaย  magari yaliyo karibu, Wakati huo yule Jamaa akiwa analipakizaย  lile begi ndani ya buti.ย 

    Akamficha mlinzi yule kwenye maegesho, akaingia kwenye gariย  yake na taratibu akaanza kulifuata gari hilo ambalo lilikuwaย  likianza kutoka taratibu kuelekea getini, Naam!! Dawsonย  aliliangalia gari hilo kwa taswira yenye mashaka sana hukuย  akitilia mashaka lile begi, hakuacha hata hatua moja alikaaย  nyuma ya gari hilo lililokuwa likiingia barabara kuuย  iliyokuwa ikitoka Mjini, Gari hiyo ilibadilisha uelekeo naย  kuelekea eneo la Bahari ambako ni nadra sana kuona Magariย  yakiongoza huko, Dawson alisogea kwa spidi sawa na gari hiloย  kisha mbele aliona gari hilo likiwa limesimama kando ya Mitiย  ya Mikoko, Dawson akalipita gari hilo makusudi iliย  kumuaminisha jamaa huyo kuwa yupo peke yake.ย 

    Alipofika mbele Dawson alisimama kisha akashuka ndani ya gariย  akawa anarudi Taratibu liliposimama gari lile alilokuwaย  akilifuatilia, walikuwa mbali zaidi ya Kilomita 15 kutokaย  Ikulu, eneo hilo gari chache sana zilikuwa zikipita. Yuleย  jamaa akafungua buti na kulitoa begi kisha akalitelekeza eneoย  lile, Dawson alikuwa amejificha mahali, jamaa alipoondokaย  Dawson alisogea na kulifungua.ย 

    Alijikuta akianguka kwa Mshituko huku macho yake yakishindwaย  kuamini alichokiona ndani ya begi hilo, chozi lilianzaย  kumbubujika Dawson, aliuwona mwili wa Inspketa Zola ukiwaย  ndani ya begi hilo, Dawson alijikuta akiwa amepoteza mmoja waย  Maaskari wake wa siri ndani ya Kitengo hicho, alilia kwaย  uchungu sana! Maisha ya Inspekta Zola yalikuwa yametamatishwaย  ndani ya Ikulu, mwili wake ulikuwa na vidonda na matundu yaย  risasi, Dawson akalifunga begi hilo kisha akalivuta hadiย  kwenye gari yake akaliweka kwenye buti akaondoka na mwiliย  huo.ย 

    Akiwa barabarani alionekana kuwa na hofu, nyuma yake kulikuwaย  na lile gari lililotoka Ikulu lilikuwa likimfuatilia kwaย  nyuma, Dawson aligundua hilo haraka akafanya ujanja iliย  kulipoteza lakini gari hilo lilikuwa bado nyuma ya Dawson kwaย  zaidi ya kilometa 35 kutoka usawa wa Bahari ambako aliuokotaย  mwili huo ndani ya begi, Dawson alichofanya ni kutembea kwaย  mwendo wa kawaida ili apambane na Mtu aliye ndani ya gariย  hilo baada ya kuhisi kuwa hakukuwa na usalama wa Maisha yake,ย  alisogea kwa umbali ndipo akaona kuna uzio wa Polisiย waliokuwa wakifanya msako barabarani, Dawson akagundua kuwaย  kuna mchezo umechezwa ili yeye apotee, haraka akabadilishaย  uelekeo na kuingia Barabara ya pili ambayo ilikuwa ya vumbiย  kisha akaenda kutoka barabara nyingine, muda huo gari lileย  lilikuwa nyuma yake.ย 

    Dawson alikuwa na sifa kubwa juu ya ujuzi wa kuendeshaย  magari, sifa ambayo Zola aliwahi kuishuhudia siku mojaย  alipotembelewa na Dawson, Naam! Akaongeza spidi kwa harakaย  akachomoka kama ndege ya kivita, alifanya hivi makusudi iliย  kulipoteza gari lile lililotoka Ikulu, dakika chache alikuwaย  amesha lipoteza, akasogea hadi karibu na jengo moja chakavuย  sana, Dawson aliona sasa Maisha yake yanaweza kuingia dosari,ย  aliona kuna kila dalili kuwa Rais alikuwa na lengo laย  kumpoteza baada ya kufanikisha kumfyeka Zola pale Ikulu, japoย  alikuwa Mzee lakini nyakati hizi mbaya alijitahidi kulibebaย  begi lenye mwili wa Zola akapanda nalo juu ya jengo hilo laย  ghorofa ambalo lilikuwa halijaisha.ย 

    Hadi anafika juu alikuwa hoi, akajikuta akianguka chini kishaย  akatoa simu yake yenye mkonga kutoka katika mfuko wakeย  akapiga mahali.ย 

    “Sande! Zola ameuawa Ikulu muda mchache uliopita” Alisemaย  Dawson huku akijifuta jasho, jioni ilikuwa ikiingiaย 

    “Unasemaje?” Ilisikika sauti ya Sande upande wa piliย 

    “Ndio hivyo, mwili wa Zola nipo nao hapa lakini hata Maishaย  yangu yapo hatarini, huyu Rais ni Mtu hatari kulikoย  inavyodhaniwa” Ilikuwa ni sauti iliyotoka kikomavu sana,ย  Ghafla akasikia mchakacho, Dawson akakimbilia sehemu yenyeย  uwazi kwa ajili ya kuchungulia chini, akaliona lile gariย  jeusi lililotoka Ikulu, ni wazi kuwa Rais alituma Mtu kwaย  ajili ya kumfuatilia Zolaย 

    “Mkuu mbona Kimya?” Aliuliza Sande Olise baada ya kuonaย  ukimya umetawalaย 

    “Nacheza sarafu ya Kifo Sande!” Akakata simu mara moja baadaย  ya kuwa ameshamuelekeza Sande, mara moja akatafuta sehemu yaย  kujificha, begi lile lilikuwa katikati ya chumba kimoja.ย 

    Hakuwa Mtu mmoja bali walikuwa wawili wakiwa ndani ya sutiย  nyeusi, mmoja akiwa amevalia miwani nyeusi na mwingine akiwaย  na macho makavu sana, sura zao zilimtambulisha Dawson kuwaย  Watu hao walitoka Kitengo cha Usalama wa Taifa Ikulu, Dawsonย  alishazoea Maisha ya kuwindana akavuta pumzi zake mara mojaย  kisha akajikunja mithiri ya nyani Mzee huku Mgongo wake ukiwa umevunjika vilivyo, masikio ya Dawson yalikuwa makini sanaย  kusikiliza hatua za Wataalam hao ambao wazi walikuwa naย  mafunzo maalum na walijuwa wanamtafuta Mtu wa namna gani,ย  jinsi walivyokuwa wakipishana huku wakilindana ilimfanyaย  Dawson afunge kiwambo cha kuzuia sauti ya Risasi kusikika.ย 

    Hata kabla Dawson hajafyatua Risasi, alisikia mlio wa gari yaย  polisi, kisha hatua za jamaa wale kukimbia zilisikika, Harakaย  Dawson akaenda kuchungulia akawaona jamaa hao jinsiย  walivyokuwa wakidanda kushuka chini kama nyani, akashushaย  pumzi zake kisha akili ya kujuwa afanye nini ili polisiย  wasiukute mwili wa Zola ilimjia, kando yake kulikuwa naย  dirisha lililokuwa na mabomba mawili yaliyoshuka hadi chini,ย  akajivuta haraka akalibeba begi na kuteleza nalo hadi chiniย  kisha akajificha nyuma ya kichaka kwa umakini zaidi sababuย  alijuwa maadui zake walikuwa eneo hilo, akanyata huku akiwaย  amelibeba begi akakatiza mtaro wa maji machafu akaendaย  kutokezea Barabarani akasimamisha Bajaji na kutokomea zake,ย  Jamaa wale walipofika hawakujuwa Dawson aliondoka vipi pale,ย  mmoja akavuta simu na kupiga mahaliย 

    “Mkuu!! Dawson ameyeyuka” Alisema kwa utii huku mkono wakeย  uliobeba simu ukiwa na misuli na Glove!ย 

    “Mnamjuwa huyo Mtu vizuri, hakikisheni hachomoki” Ilikuwa niย  sauti ya Rais Zagamba ikisikika katika sikio la Jamaa huyoย 

    “Sawa Mkuu!” Aliitikia kisha alikata simu.ย 

    MSAKO GIZANIย 

    Malaika, Six na John Brain baada ya kuona imekuwa ngumu kwaoย  kumpata Mtu wao ambaye walihangaika Nchi nzima katika vituoย  vyote vya polisi bila mafanikio, waliuwa Maafisa wengi waย  polisi ili kumtisha Rais aamuru kuachiwa kwa Mtu waoย  ilishindikana. John Brain akaja na Mpango wa kutaka kusambazaย  Ugonjwa hatari wa Ebola, Kabla ya kuanza kwa mpango huo Johnย  Brain alimpigia simu Rais ili kumtaka amuache Mtu wao harakaย  sana.ย 

    Kilichowafanya Mafia Gang kuendelea kuwepo Nchini ni Mtu waoย  ambaye alikamatwa, kesi iliyokuwa ikimkabili Mtu huyo ilikuwaย  ni kesi ya Mauwaji ya Makam wa Rais. Muda huo Rais alikuwaย  nyumbani kwake Ikulu akitafakari nini cha kufanya baada yaย  kumkosa Dawson ambaye sasa alikuwa ameshaupata mwili wa Zolaย  na kwa vyovyote Dawson atakuwa ameifahamu siri ya Mauwajiย  yanayoendelea kutokea, mezani alikuwa na kikombe kidogo chaย Kahawa ambacho kilikuwa kikitoka mvuke kuashiria kuwa Kahawaย  ilikuwa ya moto sana.ย 

    Simu ilipoita ilikuwa imemzindua kutoka Mawazoni, akaangaliaย  ni nani aliyekuwa akipiga akaona ni John Brain. Akalambaย  midomo yake kabla ya kupokea huku akiwa anaelekea Chooni.ย 

    “Kazi yako imeshaisha, tumekutoa katika kesi ya wizi naย  ufisadi ambayo ushaidi alikuwa nao Makam wa Rais,ย  kilichobakia kilikuwa ni kutupa Pesa zetu lakini cha ajabuย  unamshikilia Mtu wetu hadi hivi leo, tumekupa taarifa kupitiaย  vifo vingi tulivyovisababisha lakini inaonekana hujatakaย  kuelewa”ย 

    “Brain! Tukae mezani tulizungumze hilo”ย 

    “Michezo ya kitoto isiwepo tafadhali, kama utashindwaย  kukubaliana na sisi basi tutahakikisha unang’oka madarakani”ย  Alisema John Brainย 

    “Usijali Brain, hakuna kitakacho haribika” Rais alipotokaย  Chooni alisimama kando ya mlango, Mlinzi wake alisogea naย  kumuuliza kama yupo sawa!ย 

    “Hakikisheni Dawson anauawa haraka iwezekanavyo” Yalikuwaย  ndio maagizo pekee aliyoyatoa Rais kisha akarudi ofisiniย  kwake.ย 

    Mzee Dawson, akiwa ndani ya Bajaji alitafakari mambo mengiย  aliyoyafanya na Rais huyo, jinsi alivyotumika kwa ajili yaย  Taifa, hakuwahi kufikiria kama Rais angelikuwa ndiye tatizo.ย  Alijikuta chozi likimdondoka baada ya kulitazama begi hiloย  ambalo lilikuwa na mwili wa mmoja wa Askari wake wa siriย  sana, akapiga simu sehemu kisha akatoa maagizo fulani ya siriย  ambayo ni lazima uwe kwenye mfumo wake ili uweze kuelewa,ย  hata dereva bajaji aliachwa njia panda, kisha akageuza naย  kumpigia simu Sande Olise.ย 

    “Sande ni lazima urejee Haraka sana” Alisema Dawson kishaย  alikata simu bila kusikiliza jibu la Sande Oliseย 

    “Hapo kunja kushoto! Ukiona kibao cha kanisa simama”ย  Alielekeza Dawson, mara moja Bajaji lilifuata maagizo kishaย  likasimama.ย 

    “Pesa yako hii hapa” Dawson alitoa noti ya Elfu kumi naย  kumpatia dereva kisha akamwambiaย 

    “Chenji itakusaidia”

    “Asante sana Kaka!!” Dereva alisema kisha akaondoka zake,ย  Dawson alikuwa amesimama mbele ya geti la kanisa hilo. Wakajaย  Vijana wawili ambao walikuwa wamevalia nguo za kitawaย  wakalibeba begi hilo huku Dawson akiwa anatokwa na machozi,ย  akawafuata huku vijana hao wakionekana kujuwa nini chaย  kufanya.ย 

    Walitembea na kuingia kanisani, wakasogea hadi kwenyeย  maegesho ya magari, wakaweka begi chini kisha, mmoja akaingiaย  kwenye gari moja iliyokuwa hapo maegesho, akalisogeza mbeleย  kidogo alafu akashuka, Kijana aliyebakia akafunua kitambaaย  cheusi ambacho kilikuwa chakavu sana, pakaonekana kuwa naย  andaki fulani, akafungua mlango mdogo uliokuwa na hadhi yaย  mlango wa kisima cha maji, pakaonekana kuwa na ngazi yaย  kushuka chini, kisha mmoja akaingia na begi hilo huko chini,ย  mwingine akafuatia kisha Dawson akamalizia, walipofanikiwaย  kuingia humo, akaja Mwanamke mmoja ambaye naye alikuwaย  amevalia nguo za Kitawa kisha akafunga ule mlango, akawekaย  kile kitambaa chakavu na kusali, alipomaliza akaingia kwenyeย  gari na kulirudisha pale lilipokuwa mwanzo, huwezi kugunduaย  kuwa kulikuwa na watu waliozama Ardhini.ย 

    Walipofika chini, waliwasha taa ndani ya andaki hilo ambaloย  Mzee Dawson alikuwa akilitumia kwa ajili ya kazi zake zaย  siri, vijana hao walikuwa ni wanafunzi wake. Mmoja aliitwaย  Chande na mwingine Kisko, walikuwa ni vijana ambao alitumiaย  gharama zake Binfsi kuwasomesha na kuwapeleka mafunzoniย  Nchini Korea, walijiingiza Katika kanisa hilo ili wawezeย  kufanya kazi na Mzee Dawson.ย 

    Andaki hilo lilichimbwa muda mrefu kabla ya Mzee Dawsonย  kufadhili ujenzi wa kanisa hilo. Ilikuwa ni siri kubwa sanaย  na Watu wengi hawakujua kama kanisani kulikuwa na andakiย  lililotumika kufanyia kazi za Kijeshi, Mwanamke aliyekujaย  kuziba pale juu alikuwa ni miongoni mwa Watoto ambaoย  walipoteza Wazazi wao kutokana na visa mbali mbali,ย  aliwachukua na kuwafundisha kazi za Kijeshi, Mwanamke yuleย  aliitwa Jesca. Huyo ndiyo Mzee Dawson.ย 

    Huzuni ilikuwa imetanda ndani ya andaki hilo, Chande na kiskoย  walimpa pole Dwson kwa kumpoteza rafiki yake Kipenzi naย  Askari wake wa Siri aliyefanya naye kazi kwa muda mrefu, Zolaย  alijulikana kama Polisi wa kawaida lakini nje alikuwa niย  komando mwenye mafunzo ya Kijeshi na kijasusi.ย 

    Saa ya Dawson ilikuwa ikilia kushiria kuwa eneo hilo lilikuwaย  kimya sana, Chande akaenda kufungua mlango mmoja ambaoย  ulionekana kufungwa muda mrefu sana, wakaingia huko wakiwa naย  begi, ndani ya chumba hicho kulikuwa na Makaburi matatuย lakini kulikuwa na mashimo mengine mawili ambayo yalionekanaย  kuchimbwa muda mrefuย 

    Dawson akatoa amri ya kufunguliwa kwa begi hilo, hata akinaย  Chande walijawa na maumivu ndani ya mioyo yao, Zola alikuwaย  amekufa, wakamzika kwemye moja ya mashimo yale lakiniย  lilikuwa limebakia shimo moja, Kisko akaulizaย 

    “Mkuu Mashimo manne yamepokea Watu, bado moja. Kwaniniย  ulichimba matano?” Dawson alicheka kwa maumivu kisha akamjibuย  Kiskoย 

    “Marafiki hukaa pamoja, hawa ni marafiki zangu pekeeย  niliokuwa nawategemea katika Maisha yangu, wote wameniacha,ย  hilo shimo moja ni kaburi langu mwenyewe” Chande na Kiskoย  walimtazama Mzee Dawson kwa jicho lililojaa huzuni sana kishaย  akawaambiaย 

    “Muda wangu ukifika mtanifukia hapo kisha mtaharibu kila kituย  hapa, hamtaishi tena kanisani, mtakuwa huru kuyatumikiaย  Maisha yenu, mna muda mchache sana wa kuendelea kuwa pmoja naย  Mimi, nifuateni” Dawson alikaza sura yake kisha akaelekeaย  mahali huku vijana wake wakimfuata huko.ย 

    Akafika mahali akasimama akawaambiaย 

    “Mwisho wa mtawala katili umefika, nawapa kazi ya kumfutaย  haraka sana”ย 

    “Mtawala gani huyo?” Dawson akafunua Shuka sehemu ambakoย  kulikonekana kuwa na mitambo mingi sana, akawasha Projektaย  kisha akawaonesha picha ya Rais wa Nchiย 

    Vijana wake wakashtuka sana sababu Kwa muda mrefu Dawsonย  alikuwa pamoja na Rais huyo, Chande akaulizaย 

    “Tumfute Mkuu wa Nchi?”ย 

    “Hafai kupewa hicho cheo, yeye ndiye chanzo cha Mauwajiย  yanayoendeelea kutokea hapa Nchini, anapaswa kulipa kwa damuย  alizomwaga, anapaswa kulipa kwa Kifo cha Zola, kama sio Ujuziย  wangu basi nami ningekufa kama Zola” Wakashusha Pumzi zaoย  kisha mmoja akaulizaย 

    “Tutaweza vipi kumfuta Mtu mwenye Ulinzi mkali, Mtu ambayeย  anaishi Ikulu, Mtu mwenye jeshi?”ย 

    “Yupo atakayewasaidia”ย 

    “Nani huyo?”

    “Anaitwa SANDE OLISE”ย 

    “Ndio Nani huyo?”ย 

    “Nalazimika kuvunja kanuni nilizowawekea, sikuruhusu Maย  Ajenti kufahamiana lakini imenibidi, huyo ni P045 Olise”ย 

    “Familia inaungana” Alisema Kisko kisha wakampa salutiย  Dawson, aliwatengeneza vijana wake kujuwa kuwa Ajenti wake niย  Familia yao.ย 

    Jioni ya siku hiyo, katika Ukumbi wa Maktaba maarufu yaย  vitabu iliyopo katikati ya Jiji, Rais alikutana na John Brainย  kwa ajili ya mazungumzo, walitazamana kwa sura mbili hukuย  kila mmoja akiwa na silaha inayomlinda, John Brain alikuwaย  ameongozana na Malaika wakati huo Six akiwa kwenye moja yaย  majengo akiwa ameweka Ulinzi kwa kutumbia Bunduki, alikuwa naย  sifa nzuri sana ya Ulengaji wa shabaha kitu ambacho kilikuwaย  kikimpa sifa na Umaarufu Mkubwa kwa John Brain, taa nyekunduย  iliyoashiria kuwa Rais alikuwa akilengwa na Bunduki iligongaย  kwenye kifua, huku John Brain akiwa ana tabasamu, walinzi waย  Rais walipogundua hilo wakataka kuingia kazini lakini Raisย  aliwazuia sababu alihitaji zaidi kuzungumza na John Brain.ย 

    Akaamuru Walinzi wake watoke nje kisha Kamwambia John Brainย 

    “Haina haja ya kuwindana, sisi ni marafiki John, badoย  nahitaji kufanya kazi na nyie” Alisema Rais kisha akatoaย  picha kutoka katika mfuko wake wa koti jeusi lililomshikaย  vizuri,ย 

    “Huyo anaitwa Dawson! Ni mmoja wa Askari wa kutumainiwa zaidiย  hapa Nchini, nahitaji mumpoteze sababu kuendelea kuishi niย  sawa na Kuyaweka Maisha yangu rehani” Akasema Rais, Johnย  Brain akaivuta picha hiyoย 

    “Namjuwa huyu nimewahi kumuona” Akasema Malaika kisha woteย  wakamtazamaย 

    “Kama siyo huyu basi Zola alikuwa anakufa kwa mikono yangu”ย 

    “Hata hivyo Zola ameshakufa, aliyebakia ni huyo Mtu,ย  anahitajika kumfuata Zola alipo haraka iwezekanavyo”ย  Aliongeza Rais kisha picha ya Dawson ikarejeshwa mikononiย  mwakeย 

    “Malipo kwanza kisha umuachie Mtu wangu ndipo kazi yakoย  itafanyika, vinginevyo Nchi yako itatangaza Mlipuko waย  Ugonjwa wa Ebola ndani ya wiki moja, Raia Watakufa kama Kuku, utakuwa ndio mwisho wa utawala wako” Akasema John Brain akiwaย  amemtumbulia macho Raisย  Comments zikiwa 100 naachia ya 8 leoleo

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxย 

    jasusi riwaya za kijasusi

    45 Comments

    1. daredajr on December 4, 2024 3:05 pm

      Zola amekufa daaah..๐Ÿ˜ข

      Reply
      • Kenned Ulirk on December 5, 2024 1:02 am

        Unyama sana vita ya akil ila daah rip kamanda zola

        Reply
    2. Wilbert on December 4, 2024 3:07 pm

      Dah inaumiza na inasismua sana

      Reply
    3. G shirima on December 4, 2024 3:11 pm

      Inshallah zitafika 100

      Reply
    4. Deo on December 4, 2024 3:13 pm

      Let’s continue

      Reply
      • Cesilia Nkunga on December 4, 2024 8:01 pm

        Zolaaa ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

        Reply
    5. Angel on December 4, 2024 3:22 pm

      Jaman mambo ni mazito kwelikweli

      Reply
    6. Egibeth on December 4, 2024 3:35 pm

      Mfumo wa viongozi wengi ndo ulivyo dash hakika ni hatarii

      Reply
    7. Amiry imamu on December 4, 2024 3:41 pm

      โœ…

      Reply
    8. Neema on December 4, 2024 3:56 pm

      ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญzola

      Reply
    9. DIzzoh on December 4, 2024 4:03 pm

      Lete kazi tajiri

      Reply
    10. Bonmot on December 4, 2024 4:09 pm

      Bado tu hazjafika comment 100

      Reply
    11. Deogratias on December 4, 2024 4:11 pm

      Zola ameishia dah

      Reply
    12. David on December 4, 2024 4:24 pm

      Pameanza kuchangamka sasa

      Reply
    13. David on December 4, 2024 4:26 pm

      Ndugu admini utengwe siyo kwa weredi huu wa kuteka akili zetu

      Reply
    14. Culture on December 4, 2024 4:26 pm

      Ya mia hii๐Ÿ˜‚

      Reply
      • Fawziya Hassan on December 6, 2024 12:53 pm

        Maskini Zola,๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

        Reply
    15. Lucy on December 4, 2024 5:09 pm

      Zola kaenda du

      Reply
    16. JOSEPH NICHOLAUS KASULI on December 4, 2024 5:09 pm

      Congratualuons admin

      Reply
    17. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 4, 2024 5:09 pm

      Noma sana

      Reply
    18. Charz jr๐Ÿ˜Ž on December 4, 2024 5:10 pm

      Ya 99 hii hapa๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ

      Reply
    19. JOSEPH NICHOLAUS KASULI on December 4, 2024 5:10 pm

      Congratulations admin your are so talented

      Reply
    20. Josephat on December 4, 2024 5:17 pm

      Olise is coming

      Reply
    21. Aretas on December 4, 2024 5:43 pm

      Hatar ila Zola jaman

      Reply
    22. Mussa mabula dumbila on December 4, 2024 6:06 pm

      Duuuh

      Reply
    23. Mussa on December 4, 2024 6:07 pm

      Mmmmmmh hatari

      Reply
      • Dinner on December 4, 2024 7:12 pm

        Jmn mbona Zola kafa kama utani vile๐Ÿฅน๐Ÿฅบ

        Reply
    24. Tyseem on December 4, 2024 7:04 pm

      Mpka chozi limenitoka
      RIP kamanda ZOLA
      ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

      Reply
    25. Joven on December 4, 2024 7:11 pm

      Oyaaaaaa n ebiatar

      Reply
    26. Daurd on December 4, 2024 7:14 pm

      Kimeniuma Zola kufa jamanii

      Reply
    27. Minzo on December 4, 2024 7:22 pm

      Story moja tamu sana…ila zola daa ameondoka mapema sana

      Reply
    28. sylvia on December 4, 2024 7:44 pm

      Zola why dah

      Reply
    29. Hamisa Joseph on December 4, 2024 7:55 pm

      Zola mbna naumia kama ukweli vile

      Reply
    30. wittie on December 4, 2024 7:57 pm

      Nzuri

      Reply
    31. [email protected] on December 4, 2024 7:59 pm

      Dah! Zola umeondoka hivi tunakuona jmn . Haya Sasa .sande njoo ingiaa kzn

      Reply
    32. Dyner on December 4, 2024 8:00 pm

      Zola ameniuma๐Ÿ˜ญ

      Reply
    33. [email protected] on December 4, 2024 8:01 pm

      Admin hongera sn unaweza alafu unaweza TN .Dah isiishe jmn

      Reply
    34. Elizabeth on December 4, 2024 8:17 pm

      Ameniuma san zola๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

      Reply
    35. Debora george on December 4, 2024 9:14 pm

      Jaman Zola sikuegemea Kama mwisho wake utakuwa hvyo ๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข

      Reply
    36. Linah on December 4, 2024 9:20 pm

      ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญSasa Zola amekufaje jamani

      Reply
    37. DAUD DEOGRATIAS on December 4, 2024 10:36 pm

      Zola kafa mtu shupavu ,nasubiri mziki wa Sande Olise na vijana wa Dawson

      Reply
    38. Pray on December 4, 2024 10:49 pm

      Daah

      Reply
    39. Hamza Abdallah Mwalyawa on December 5, 2024 12:40 am

      Sasa picha ndio kwanza inaanza mzee Dawson fungua ukurasa mpya karibu sande olise

      Reply
      • Ahmed Samir on December 5, 2024 11:55 am

        Daaaaah,aiseee kali xna hii simulizi

        Reply
    40. * * * Unlock Free Spins Today * * * hs=d3dd870fa46aeb4c5c04dd67189a84f2* ั…ั…ั…* on June 19, 2025 1:44 am

      pta25q

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.