Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » FUNGATE (Sehemu Ya Kwanza) Fungate-01
    Hadithi

    FUNGATE (Sehemu Ya Kwanza) Fungate-01

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 13, 2024Updated:May 19, 202423 Comments5 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Fungate
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Katika Maisha, kila mmoja anakuwa na ndoto kubwa yenye kumpa furaha Maishani mwake,hata wewe una ndoto ambayo siku moja ikitimia utakuwa ni mwenye kufurahi sana.Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Robson, alisoma, alipata kazi nzuri iliyomuingizia pesa nyingi, alikuwa na muonekano mzuri, mtanashati lakini alikuwa na ndoto ambayo alitamani kuiona siku moja ikitimia, ndoto yake kubwa ilikuwa ni kumuoa  Sylvia.

    Ndoto ya Robson ilitimia, Sylvia aliridhia kuolewa na Robson, maandalizi yote yalienda sawa na ndicho ambacho Robson alikuwa akikitaka, nafsi ya Robson ilikunjuka akawa mwingi wa furaha, si kazini hata nyumbani kwake alikuwa mwingi wa  kutabasamu

    “Hakika Robson unaenda kutimiza ndoto zako za muda mrefu Kaka” Alisema rafiki yake Robson aliyeitwa Mark

    “Zaidi ya Sylvia sijaiona furaha nyingine Mark, kumuoa yeye ni jambo linaloenda kunipa furaha sana” Alisema Robson wakiwa wanapata chakula cha mchana nje ya ofisi yao

    “Mna mpango wa Fungate?” Aliuliza Mark

    “Ndiyo! Nimepanga kumpeleka Kilimanjaro Kaka, tena tukaishi karibu na Mlima kwa wiki mbili za mwanzo kisha tukamalizie Mwanza kula sato” Alisema Robson kisha walicheka kwa pamoja

    “Umetisha sana, Unyama mwingi Rob!!”

    Tukiachana na upande wa Robson, Nyumbani kwao Sylvia hali haikuwa hivyo kabisa, Sylvia hakuhitaji kabisa kuolewa na Robson, alikubali kwasababu Baba yake alimlazimisha kufanya hivyo, Sylvia aliwaambia Wazazi wake kuwa ana Mwanaume anayempenda sana hivyo ataolewa na huyo na siyo Robson

    “Hili linaenda kufanyika Silvia, unaolewa na Robson, Kijana Mtanashati, mchapakazi..” alisema Baba yake Sylvia siku mbili kabla ya ndoa ya Robson na Sylvia, hakukuwa na mjadala tena.

    Usiku wa kuamkia siku ya ndoa, Sylvia alimwambia Mama yake kuwa waliangalie upya jambo walilolitaka yeye alifanye

    “Mama naolewana Mtu ambaye hayupo ndani ya moyo wangu” alisema Sylvia

    “Usiseme hivyo Mwanangu, mbona Robson ni Kijana mpole, mzuri na anaonekana anakupenda sana”

    “Mama, suala siyo Robson kunipenda bali ni Mimi kumpenda yeye, hii itakuwa ndoa ya upande mmoja Mama, naomba tafadhali tusitishe hii ndoa Mama yangu” alisema Sylvia, alimpa wakati mgumu Mama yake wakati mipango yote ilipangwa na maandalizi yalishafanyika

    “Hadi hapa tulipofikia Sylvia hakuna namna tunaweza rudi nyuma, huna budi kuingia kwenye ndoa, nina imani Utampenda Robson” Alisema Mama yake Sylvia kisha aliondoka chumbani na kumuacha Sylvia akilia

    “Kwakuwa mmenilazimisha, nitamfanya Robson ajutie kuniowa”

    Alijisemea Sylvia kwa hasira kubwa sana.Siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku ya ndoa ya Robson na

    Sylvia, Robson alikuwa mwenye kufurahi sana wakati Sylvia akiwa mwenye kuchukizwa lakini mbele za Watu alionesha tabasamu, Sylvia alikumbuka jinsi alivyokutana na Robson kwa mara ya kwanza.

    Alikutana naye chuoni Udom, wote walikuwa wakisomea masuala ya fedha. Walijenga urafiki kwa zaidi ya miaka miwili, Mwaka wa tatu Robson alimueleza Sylvia kuwa anampenda, kutokana na urafiki wao Sylvia alimwambia Robson

    “Siwezi kuwa na mahusiano na wewe sababu sisi ni marafiki, pia unajuwa kuwa nina Mtu wangu Robson” Alisema Sylvia

    “Mtu wako amekutelekeza yupo nje ya Nchi kwa zaidi ya mwaka bila mawasiliano na wewe, unaweza vipi kujihesabu kuwa upo naye? Alafu kuhusu urafiki wetu nina imani tukiwa wapenzi tutazidi kupendana” Alisema Robson

    “Hilo haliwezekani Robson, nakuchukulia kama rafiki yangu, nakupenda kama rafiki na si vinginevyo”

    “Sylvia ninayosema yanatoka ndani ya moyo wangu, tafadhali kubali kuwa wangu” Alisema Robson, Sylvia alimtazama Robson kisha alimuuliza

    “Itakuwaje kama Brahama atarudi Tanzania?”

    “Kama atarudi nipo tayari kukuacha uendelee naye Sylvia”

    Alisema Robson, kutokana na sharti hilo Sylvia alikubali kuwa na Robson, Mapenzi yao yalikuwa ya kuvutana sana sababu bado Sylvia alikuwa akimuwaza sana Brahama ambaye alikuwa ndiye Mwanaume wake wa kwanza.

    Zilikuwa ni kumbukumbu za Sylvia akiwa anajiandaa kuelekea kanisani, alishika simu yake akajaribu kuipiga namba ya Brahama lakini haikupatikana, kisha akamtumia meseji Robson akamuuliza

    “Tunaenda kuwa Mke na Mume, unaikumbuka ahadi yako?” Baada ya kutuma ujumbe, Sylvia aliendelea kuvalia gauni la harusi, mara ujumbe uliingia

    “Nakumbuka si kuhusu Brahama?”

    “Ndiyo, kama atarudi kwa ajili yangu itakuwaje utakubali Matokeo?” Aliuliza Sylvia lakini ujumbe wake haukujibiwa na Robson hadi muda ambao alikuwa tayari amemaliza kujiandaa

    Gari lilipofika waliingia kwenye gari, familia ya Sylvia ilienda kanisani Magomeni, muda wote Sylvia alikuwa akijaribu kumpigia Brahama lakini simu haikupatikana, Mama yake Sylvia aligundua kuwa Mwanaye hana furaha kabisa, alimshika na kumwambia

    “Tuliza akili yako Sylvia kwani unaenda kupiga hatua kubwa sana katika Maisha yako” Alisema Mama yake Sylvia baada ya kugundua Mwanaye hayupo sawa , Robson na familia yake walikuwa wa kwanza kufika kanisani, hakika alipendeza sana kwa nje lakini ndani ya moyo wake alianza kuwa na mashaka kutokana na zile meseji ambazo alitumiwa na Sylvia muda mchache kabla ya kuingia kanisani.

    Shangwe na vigeregere viliibuka kanisani baada ya Familia ya Sylvia kuingia kanisani, waliopiga vigeregere hawakujuwa mioyo ya Sylvia na Robson ilikuwa kwenye msuguano mzito sana, wao walifurahia kuona Robson anamuowa Sylvia, taratibu zilifanyika kikamilifu.

    Ndoa ilifungwa? Nini kilitokea? Gusa Hapa Kusoma Sehemu Ya Pili

     

    Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

    Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii [email protected]  

    Fungate Kijiweni Riwaya ya Fungate stori ya kusisimua

    23 Comments

    1. Stuart on May 13, 2024 9:09 pm

      Nzuri

      Reply
      • Trinity on May 14, 2024 2:27 pm

        Kitu Fungate tunasubr sehem ya pil saa 11 jion plz Adimin

        Reply
        • David on January 17, 2025 6:11 pm

          Nzuri sanaaa mkuu

          Reply
      • Mubarak on May 14, 2024 2:38 pm

        😎

        Reply
    2. Moderich on May 13, 2024 9:14 pm

      Patamu hpo

      Reply
      • Massay on May 14, 2024 3:17 am

        Nzuri sana

        Reply
    3. Candy on May 13, 2024 10:14 pm

      Umeipotezea KOTI JEUSI umeshatuchanganya sana au ndo iliishia pale?

      Reply
      • Rumbyambya Jr on May 14, 2024 6:59 am

        Iliisha ile mbona si uliona Adela kawa Tajiri mtoto

        Reply
      • Lizzy on May 14, 2024 7:33 am

        Nadhani iliishia pale kwasababu watu walishamjua muuwaji mkuu ni Martha

        Reply
    4. Egon on May 13, 2024 10:59 pm

      Ipo unyama sana

      Reply
    5. Precious on May 13, 2024 11:12 pm

      Nice

      Reply
    6. Emmanuel Ngoma on May 14, 2024 12:16 am

      Itakuwa nzuri

      Reply
    7. Juma Pazy on May 14, 2024 5:55 am

      imeanza vzr ngoja tuone mbele

      Reply
    8. Zacharia john on May 14, 2024 9:00 am

      Forced marriage hiyo robson kitamkuta kitu

      Reply
    9. Mkobo jr on May 14, 2024 11:03 am

      Yan hii yakujenga urafki kwanz kumbe unamtaka daah inatuumiza sanaaa

      Reply
    10. Rhino on May 14, 2024 6:09 pm

      Weka sehem ya pili admin

      Reply
    11. Mugabo on May 14, 2024 8:14 pm

      It’s nice

      Reply
    12. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Tatu) Fungate-03 - Kijiweni

    13. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04 - Kijiweni

    14. Hamisi halidi on May 17, 2024 3:25 pm

      Mbn stor tamu inabidi uwe na group maalumu jamani mana

      Reply
    15. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Tano) Fungate-05 - Kijiweni

    16. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Sita) Fungate-06 - Kijiweni

    17. Yuster on January 27, 2025 1:02 pm

      Mambo yamenoga 🔥

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.