Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    Baraka JohanessBy Baraka JohanessJune 27, 2024Updated:July 22, 202426 Comments3 Mins Read14K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Baadhi ya tetesi zinadai kuwa huenda kiungo wa Zambia na mchezaji wa Simba Clatous Chota Chama anaweza kujiunga na klabu ya Yanga akitokea Simba. Klabu ya Simba haijafanya juhudi zozote za kumuongezea mkataba mchezaji huyo na tetesi nyingi zikidai tayari klabu ya Yanga imeshaweka donge nono mezani kwajili ya usajili wa kiungo huyo

    Kama Chama atajiunga na miamba hiyo yaani mabigwa wa kombe la NBC Premier League (Yanga) ataongeza upana wa kikosi na kufanya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Miguel Gamondi kuwa na wachezaji watatu wa kariba moja na wenye uwezo wa kucheza namba 10 uwanjani kwa ufasaha.

    Swali ni je kama Yanga watamnasa Chama ipi ni hatima ya Aziz ki na Pacome kama watalazimika kubaki muundo wa uchezaji wa Yanga utakuwaje nani atapata nafasi ya kucheza nafasi ya namba 10 yani kiungo mshambuliaji nyuma ya striker namba 9 namba ambayo wachezaji wote watatu wanakuwa huru sana wakiicheza.

    Kwanza pichani hapo juu ni muonekano wa eneo la kati hadi mbele litakavokuwa kama chama atafanikiwa kujiunga na yanga sasa tudadavue msitari wa Chama, Aziz Ki na Pacome utachezaje

    Kwanza nikuhakikishie kuwa wachezaji wote hao watatu wanaweza kucheza katika nafasi ya namba 10 ndani ya mechi moja kwa lugha ya kisoka inaitwa (Triple ten) au (3 10’s) tujue ili kucheza namba kumi watatu unahitaji nini.

    Kitu cha muhimu ni kuwa unahitaji namba kumi wawili wenye uwezo wa kucheza maeneo ya pembeni na kufanya mikimbio kwenye eneo la kati kwajili ya kutengeneza idadi ya namba kumi 3 nikukumbushe Chama na Saido walicheza kama namba 10 wawili Simba msimu jana Saido akisimama kama namba kumi asilia na Chama akitokea eneo la namba 7 na mikimbio kuelekea namba 10

    Pia nikukumbushe Pacome na Aziz Ki wamewahi kucheza kama namba kumi wawili Pacome akitokea eneo la namba saba au kumi na moja hivyo wachezaji wote hao watatu wanauwezo wa kufanya ivoo kucheza pembeni kisha wakakimbilia kati kutengeneza namba 10 3 tazama

    Hivi ndivyo Yanga watacheza kama wakiamua kutumia namba kumi watatu (Lomalisa na Yaoyao watatumika kama mawinga muda wa kushambulia muda ambao Pacome na Max wataingia katikati ) Swali kwa kocha Je kikosi kitakuwa na uwiano mzuri muda wa kushambuliwa yaani wakiwa hawana mpira hii nitaelezea kwenye andiko lijalo itakuwa mada pana ya Yanga akiwa na mpira na bila ya mpira muundo wao wa kiuchezaji

    Swali ni Je Nani anafaa kuanza nafasi ya namba kumi kwa maoni yako Chama, Pacome au Aziz Ki?Β Β 

    SOMA ZAIDI:Β  Je Simba Wana Mradi Mpya Au Wanataka Kurudisha Wa Zamani?

    chama na pacome usajili wa chama yanga

    26 Comments

    1. Jjb-hsnf-fdk on June 27, 2024 10:31 am

      Mie naona hapo anaefaa kuanza namba 10 ni Aziz k wengine pemben

      Lakn kueka kikosi cha yanga na kutumia jezi nyekundu πŸ˜‚sjapenda hio hali ,rangi ya jez ya yanga itumike

      Reply
      • Aloyce masele on June 27, 2024 12:33 pm

        🀣🀣

        Reply
      • Muddy on July 2, 2024 9:39 am

        Nikweli huwezi kupanga kikosi cha machampion ilafu uweje jez nyekundu umetukosea sana

        Reply
    2. MAGANGA on June 27, 2024 10:46 am

      Pacome anastahili namba 10 azizi ki atokee pembeni

      Reply
    3. Blackdevis on June 27, 2024 10:54 am

      Jaman Apo ndy unyama pacome,ki, Aziz,na chama tunaua ila haijapendeza kwahyo jez wapewe uzi wao wa wananch

      Reply
      • chalse chalse on June 27, 2024 11:14 am

        mmoja lazima asubiri hapo hawawezi kuacheza wote

        Reply
    4. Roy Creation on June 27, 2024 11:33 am

      Pacome na Chama wana uwezo mkubwa wa kukaa pembeni coz wanafaida ya kutumia miguu yote na speed ukitofautisha na aziz Ki so Chama na Pacome watokee pembeni then Aziz abaki kama True No 10 wajaze pasi nyingi kati Dube akipoteza Aziz yupo Nyuma anaachia Kombora bila kusahau Pacome au Chama wakipoa kuna kibelenge Maxi anakuja kucover Timu ikishambuliwa Chama sio mzuri kukaba atabaki juu na Dube kwa ajili ya Counter-attack wakat Aziz Pacome na Maxi bila kumsahau Aucho wanarud kukaba timu inakua imebalance ila toa rangi nyekundu kweny kikosi cha yanga apo

      Reply
    5. Pangapanga Msisili on June 27, 2024 11:35 am

      Mpangilio ni mzuri ila jezi haijanipendeza

      Reply
    6. Julius putin on June 27, 2024 11:38 am

      Shida sio watachezaji ,usisahau kama pacome ni namba 8 kiasili na max ni winger kiasili .Na pia mfumo wa yanga wa uchezaji ni kwamba huwa wanabadilishana nafasi, mara 10 awe winger winger awe 10 . Winger awe 8 na 8 awe winger. Kutokana na mfumo huo yanga haina shida kwamba nani atacheza miongoni mwa hao watatu wanaoaobadilishana namba.
      27ALIENπŸ‘ŒπŸ‡

      Reply
    7. Chrispin on June 27, 2024 12:01 pm

      Kutokan na xabi alonso wa bongo tawachezesha pacome atacheza nane(8) chama 10 na azizi ki atatokea winger 11 alf max atatokea winger 7 kati tisa dube imeeisha hiy aucho in defensive middle

      Reply
    8. Mamboleo Africa on June 27, 2024 2:00 pm

      Pacome na chama mawinga, Azizi ki 10 kwasabab azizi ana power shoot nzur kwaiy akiwa anacheza karibu na box itakuwa na faida sana

      Reply
    9. Mamboleo Africa 🌍 on June 27, 2024 2:05 pm

      Pia watakuw wanabadilishana kutokana na mfumo wa mwalim kwa mechi husika

      Reply
    10. Sencha bacsem on June 27, 2024 2:10 pm

      Me Sina shaka hata wote wakawa mabeki bado tabu Iko palepale

      Reply
    11. @Mamboleo_Africa 🌍 on June 27, 2024 4:53 pm

      Pacome na chama wacheze kama mawinga, Azizi ki acheze 10 kwasabab ana power shoot nzur kwaiy akiwa anacheza karibu na box itakuwa na faida sana.

      Reply
    12. @Mamboleo_Africa 🌍 on June 29, 2024 9:57 am

      Ukiona unataka uonekane mzuri kwa kila mtu, ujue umeanza maisha ya kinafikiπŸ“Œ

      Reply
    13. Zzlayd on June 30, 2024 9:39 pm

      Akun wakushinda namsimuu uuh kama sio mtuu kufa golii 10 sijuii

      Reply
    14. Mkangala on July 1, 2024 9:28 pm

      Wakicheza ivo wakikutana na team inayoshambulia mda wote watapigwa nyingi sana maana hapo mkabaji ni aucho tuh wengine kushambulia tuh kukaba aaaah

      Reply
    15. @Mamboleo_Africa 🌍 on July 2, 2024 4:58 pm

      Na jitahid sana kweny mahusiano yako ukae upande wa I LOVE YOU TOO

      Reply
    16. @Mamboleo_Africa 🌍 on July 3, 2024 6:37 am

      Dua ni ileile “Eeh M/Mungu Nipe Mimi Wape Na Wao Pia” 🀲

      Reply
    17. @Mamboleo_Africa 🌍 on July 6, 2024 8:54 am

      Alhamdulillah for everything🀲

      Reply
    18. Pingback: Muda Utatuonesha Tofauti Kati Ya TIMU Na MASTAA

    19. @Mamboleo_ Africa 🌍 on August 1, 2024 9:49 am

      Kaburini utasindikizwa na wengi, lakin mwishon watakuacha peke yako. Hivyo jitahidi kuishi maisha ya kumridhisha muumbaji na wala sio sisi wasindikizaji.

      Reply
    20. @Mamboleo_ Africa 🌍 on August 7, 2024 10:08 am

      CHIZI ANACHEKESHA IKIWA HATOKEI KATIKA FAMILIA YENU

      Reply
    21. @Mamboleo_ Africa 🌍 on August 12, 2024 9:55 am

      Maybe Not today! But Only one thing is true
      I will be Champion one dei. πŸ“Œ

      Reply
    22. @Mamboleo_ Africa 🌍 on August 19, 2024 11:40 pm

      Inspiration
      Then when you have taken a decision, put your trust in Allah.
      ~Surah al imran/v.159

      Reply
    23. Chacha_Matiti on January 20, 2025 2:15 pm

      Siku hizi wamepanuka

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.