Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Baada ya Kichapo, Iwobi aahidi Makubwa Timu ya Taifa Nigeria
    Africa | CAF

    Baada ya Kichapo, Iwobi aahidi Makubwa Timu ya Taifa Nigeria

    David MohamedBy David MohamedMarch 31, 2023No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Nigeria, Alex Iwobi amewaahidi mashabiki wa Super Eagles kuwa kikosi hicho, kitarejea katika ubora wake, licha ya kufungwa bao 1-0 na Guinea Bissau siku chache baada ya kumalizika kwa mchezo huo katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka ujao nchini Cote D’ voire.

    Nigeria ambao wanajivunia mshambulizi shupavu kutoka klabu ya Napoli ya Italia, Victor Osimhen walipigiwa upato mkubwa kushinda mechi hiyo, lakini mambo yalikuwa tofauti, baada ya  Mala Balde kuipa Guinea Bissau bao hilo la ushindi.

    Iwobi ambaye anaichezea klabu ya Everton nchini Uingereza, amesema wachezaji wenzake wamekubali aibu na sasa wanaangazia michuano inayofuata.

    “Sisi kama timu ni lazima tuzinduke na kile ambacho tutafanya ni kujiboresha. Kwa mashabiki nitawaomba wasife moyo waendelee kutushangilia kwa sababu tunajitolea kwa hali na mali si kwa ajili yetu binafsi bali kwa taifa kwa ujumla,” amesema Iwobi.

    Kufuatia ushindi wa Guinea Bissau sasa inashikilia uongozi wa kundi A kwa alama saba, Nigeria ni ya pili kwa alama sita, Sierra Leone ya tatu kwa alama mbili na Sao Tome Principe ni ya mwisho wakiwa na alama moja.

    Katika hatua nyingine, baadhi ya wanasoka waliobobea walifanikiwa kufungia timu zao za taifa akiwemo Sadio Mane, Mohammed Salah na Sebastian Haller.

    Sadio Mane ambaye alirejea kwenye kikosi cha Senegal baada ya kukosa kombe la dunia kufuatia jeraha, alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Mozambique jijini Dakar.

    Mo Salah alifunga bao la kwanza na kusaidia kupatikana kwa bao la pili katika ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malawi jijini Cairo na kusonga kutoka nafasi ya mwisho hadi ya kwanza kwenye kundi D.

    Haller ambaye alirejea uwanjani mwezi uliopita baada ya kupata matibabu ya saratani ya tezi dume, alifunga bao la pili la Ivory Coast katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Comoros mjini Bouake.

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.