Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tatu-03)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 28, 202516 Comments9 Mins Read1K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishiaย 

    Kupitia daraja la Kigamboni, Mzee Shayo aliendesha Subaruย  kama yupo kwenye mbio za Magari, wakati huo Barabara zilikuwaย  nyeupe, Watu wengi waliogopa kupoteza uhai wao, walibakiaย  majumbani mwao huku wachache wakiendelea kufanya safari,ย  ilimuwezesha Mzee Shayo kufika Ikulu ya Magogoni haraka sana,ย  alikuta ulinzi umeimarishwa hapo lakini alipowatazama Walinziย  hao alijikuta akikata tamaa, aliona ni ngumu sana kupambanaย  na huyo Mwanaume anayeitwa Chogo. Endelea

    SEHEMU YA PILI

    Aliuliza mahali ambapo Rais wa Nchi alikuwa amehifadhiwa kwaย  ajili ya usalama, ilikuwa ni ndani ya chumba kimoja ambachoย  kilikuwa na milango ya umeme, chumba hicho kilipatikanaย  katikati ya jengo la Ikulu.ย 

    Rais akiwa na waziri Mkuu ndani ya chumba hicho walimuonaย  Mzee Shayo akiingia huku sura yake ikionesha kukosa tumaini,ย  Rais alimdaka Mzee Shayoย 

    “Shayo! Nini kinaendelea?” Aliuliza Rais huyo aliyeitwaย  Martin Bingoย 

    “Ugaidi Mkuu” Alijibu kwa utii Mzee Shayoย 

    “Inakuwaje hadi ugaidi unaingia katika Nchi hii yenye amaniย  kwa zaidi ya Miaka 60 sasa, nyie kama jicho la Taifa mkoย  wapi?” Alihoji Rais akionekana kuchanganikiwaย 

    “Mkuu! Ugaidi huu unaratibiwa na Mtanzania, mkazi wa Jiji laย  Arusha. Mara moja nitatuma timu kuhakikisha anafuatiliwaย  mahali alipozaliwa na kupata taarifa zake, kuanzia hapoย  tutajuwa tunapambana vipi kuhakikisha tunamdhibiti” Alisemaย  Mzee Shayo, maneno yake yalikuwa kama dhihaka kwa Rais Martinย  Bingo, alimtandika kofi Mzee Shayoย 

    “Tayali kambi la Lugalo lipo chini ya huyo Mtu na kundi lakeย  la ESS, anateka kila sehemu nyeti ya Nchi hii, nimepataย  taarifa pia kambi la Jeshi la Majimaji nalo lipo chini yake,ย  Shayo uzembe wa aina yoyote utasababisha damu nyingiย  kumwagika” Alisema kwa hasira huku akimkaripia Mzee Shayoย  ambaye kiumri alikuwa Mkubwa kuliko Rais Martinย 

    “Mkuu! Naomba niende” alisema Mzee Shayoย 

    “Ndani ya masaa manne nipate majibu ya hili jambo Shayo,ย  vinginevyo utahusishwa pia na Ugaidi huu” Alisema Rais, Mzeeย  Shayo aligeuka na kuondoka Ikulu, alipoingia kwenye gari lakeย  chozi lilimbubujika, alipiga usukani kisha aliondoa gari eneoย  hilo.

    Tuachane na habari za Kitengo na hasira za Rais Martin juu yaย  uvamizi huu wa kutisha, Ndani ya Jiji la Nairobi, Uwanja waย  ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata kulikuwa na ujio waย  Msichana mmoja mzuri sana, Mweupe. Alionekana kuwa makiniย  sana pindi alipokanyaga ardhi hiyo, kutokana na Ugaidiย  uliokuwa umetanda ndani ya Ardhi ya Tanzania, Ulinzi ulikuwaย  imara sana ndani ya Uwanja huo, muda mchache baada ya ndegeย  hiyo kutua Taifa la Kenya lilitangaza kusimamisha shughuliย  zote za anga yaani hakuna ndege nyingine kuingia wala kutoka.ย 

    Msichana huyo alikaguliwa kisha aliambiwa avue miwani. “Unaitwa Faudhia?” Aliuliza mmoja wa Askari wa Ukaguziย 

    “Ndiyo!!” Alijibu Msichana huyo ambaye alifahamika kamaย  Faudhia, askari alimtazama sana Faudhia kabla ya kumruhusuย  aweze kuondoka Uwanjani hapo, Faudhia aliporuhusiwa baada yaย  kuwa amekamirisha taratibu zote aliita Taxiย 

    “Nipeleke Nairobi Hotel” alisema Faudhiaย 

    “Nairobi Hotel, ni KSH 500” alisema dereva huyo ambayeย  alikuwa ni Mwanamke, Faudhia alikuwa siti ya nyuma akamwambiaย 

    “Muhimu nifike hapo kwa wakati” alisema Faudhia huku Mwanamkeย  huyo akiondoa gari lake katika eneo hilo.ย 

    “Unaonekana upo makini sana, nini kimekuleta hapa Kenya?”ย  Aliuliza Mdada huyo ambaye sura yake haikupata kuonekana kwaย  Faudhia, lilikuwa ni swali la mtego ambalo Faudhia alilikwepaย  haraka sanaย 

    “Hiyo Hotel ina huduma zote muhimu ee? Nimepata sifa zake”ย  Alisema Faudhiaย 

    “Kenya hakuna Hotel hoi hai, hiyo uliyoitaja ndiyo Hoteliย  bora sana hapa Nairobi” Alijibu Mdada huyo ambaye hakupataย  kutambulika alikuwa anaitwa nani, hakumuuliza tena kituย  kingine Faudhia hadi pale walipofika katika Hoteli ya Nairobiย  ambayo ilikuwa mbali kutokea ulipo Uwanja wa Jomo Kenyata.ย 

    “Here we goo ( tumeshafika ) ” alisema Mdada huyo huku akiwaย  amesimamisha gari mbele ya Hoteli hiyo ambayo kwa muda huoย  ilikuwa imefungwa kutokana na tahadhali ambazo Taifa la Kenyaย  liliamuwa kuchukua.ย 

    Yule Mdada aliondoka zake, Faudhia alilitazama Tax hadiย  lilipozama kisha alisogea getini akatoa kitambulisho maalumย  kuwa alishafanya booking ya Chumba Hoteli hiyo, alikaguliwaย  na kuruhusiwa kuingia Hotelini.

    Akiwa ndani ya chumba chake alipokea simu ya Mtuย  aliyemkusudia ndani ya Hoteli hiyo, jamaa huyo aliitwa Khalidย  Bangala, alikuwa dalali maarufu sana ndani ya ukanda waย  Afrika Mashariki, alikuwa ni miongoni mwa wachache ambaoย  walikuwa wakiwindwa sana na Serikali zote kutokana naย  Biashara yake ya kusafirisha mizigo, na biashara haramu yaย  usafirishaji wa Binadamu wakiwemo wana mgambo wa kundi laย  Kigaidi la ESS ambalo lipo Tanzania.ย 

    Haraka Faudhia alimfungulia mlango jamaa huyo ambaye alikujaย  na Watu watatu ndani ya Chumba hichoย 

    “Mna uhakika nitaingia Tanzania Kabla ya mipaka kufungwa?”ย  Aliuliza Faudhia akiwa makini kumtazama Khalid Bangala, jamaaย  huyo alicheka kisha akajibu kwa kujimwambafaiย 

    “Itakuwa ni Biashara yangu ya kwanza kukwama kwenye maishaย  yangu, sijawahi kukwamisha biashara yangu” Alisema kishaย  Faudhia alishusha pumzi zake, ilikuwa ni majira ya jioni.ย 

    “Ulisema ni kiasi gani?” Aliuliza Faudhia baada yaย  kuhakikishiwa kuwa angesafiri kutoka Kenya hadi Tanzania bilaย  tatizo lolote lileย 

    “Milioni 10 za Kitanzania, hali si shwari huko mpakani,ย  Watanzania walio jirani wanakinzana na askari kuihama Nchi”ย  Alisema Khalid Bangalaย 

    “Sawa, nitalipa hiyo fedha yote nikifika Tanzania” Alisemaย  Faudhia, Khalid Bangala alimsogelea na kumuuliza kwaย  kumdadisiย 

    “Nchi ambayo Watu wanaanza kuikimbia wewe unatoa Milioni 10ย  kuingia huko, una ajenda gani?” Alihoji Khalid Bangalaย 

    “Nafikiri tuifanye Biashara yetu kwanza Bosi” Alijibu Faudhiaย 

    “Haya! Utalazimika kuingia ndani ya Sanduku” alisema Khalidย  Bangalaย 

    “Una maanisha Jeneza? Nasafiri nikiwa mfu?” Alihoji Faudhiaย 

    “Hapana!! Tunachokifanya kitakusaidia kuingia Tanzania,ย  vinginevyo itakuwa ngumu kwako” Ilikuwa ni Mtihani mgumu kwaย  Faudhia kukubali sharti hilo, haraka alikumbuka jambo fulaniย 

    Kilichomtoa Mexico kilikuwa ni simu ya dharura kutoka kwaย  Mkuu Wa kitengo cha Usalama wa Taifa Mzee Shayo juu ya Ugaidiย  Nchini Tanzania. Alishusha pumzi zake akasema

    “Safari itaanza saa ngapi?”ย 

    “Sasa hivi” Alisema Khalid Bangala, mara moja vijana wakeย  waliingiza sanduku ndani ya Hoteli hiyo kupitia Mlango waย  nyuma wakiwa na mavazi ya waangalizi wa maiti kuhakikishaย  Faudhia anaingia Tanzania, jeneza hilo lilikuwa na matunduย ย 

    madogo madogo ya kuhakikisha hewa inaingia humo ndani.ย 

    Faudhia aliingia ndani ya sanduku akiwa na kibegi chakeย  kidogo sana, safari ilianza. Walipofika nje ya Hoteli Khalidย  aliwatakia vijana wake safari njema, mara moja sandukuย  liliingizwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser yenyeย  nembo ya Hospitali ya Nairobi. Safari ilianza ya kuutafutaย  mpaka wa Namanga ambapo Faudhia ataachwa hapoย 

    Gari hiyo ilianza safari kwa mwendo wa taratibu ili kutokaย  Mjini, ilikuwa ni safari ya hatari sana lakini kwa Khalidย  Bangala na vijana wake ilikuwa ni kazi waliyoizoea, gari hiloย  lilitambuliwa kama gari ya kubeba maiti zinazoenda masafa yaย  mbali. Walipofika kwenye kizuizi cha kutoka na kuingiaย  Nairobi, polisi walianza kulikagua gari hilo ilaย  walipojiridhisha kuwa gari hilo lilikuwa na maiti walilipaย  ruhusa ya kuendelea na safari.ย 

    Safari ilikuwa ndefu sana iliyogubikwa na giza, usikuย  uliingia huku wakizidi kukata miji na vijiji kuutafuta Mpakaย  wa Namanga ambao ulikuwa ndio mpaka salama hadi kufikia mudaย  huo, mara kadhaa Faudhia akiwa ndani ya Sanduku hiloย  aliwasiliana na Mzee Shayo kutoka kitengo kwa njia ya ujumbeย  mfupi wa simu, alimueleza nini anatakiwa kufanya, alitakiwaย  kuelekea Kwenye pori dogo lililopo wilaya ya Longido, hapoย  atakutana na gari kisha ataelekea Jijini Arusha kwa ajili yaย  kuanza safari ya kuelekea Dar.ย 

    Miji mingi ilianza kutekwa na Magaidi hao wa kundi la ESSย  pasipo kuwekwa wazi sababu ya wao kufanya hivyo hukuย  ikifahamika wazi kuwa anayekiongoza kikundi hicho anafahamikaย  kama Martin Gimbo maarufu kama Chogo.ย 

    “Ukifika Arusha utapewa kazi ya kufanya huko kwa muda fulani”ย  Ulikuwa ni ujumbe wa mwisho wa Mzee Shayo, kazi hii ilikuwaย  ndiyo kazi ya Kwanza kwa Faudhia baada ya kuhitimu mafunzoย  huko Mexico, akiwa ndani ya sanduku alitoa picha ya rafikiย  yake aliyeitwa Diana ambaye naye alihusishwa katika ugaidiย  huo, alikumbuka maisha ya nyuma walipokuwa wakisoma woteย  shule ya Majengo huko Mkoani Mbeya, roho ilimuuma sana lakiniย  lilikuwa ndiyo jukumu lake. Aliiweka picha hiyo mfukoni kishaย  alipaza sauti akawauliza vijana wa Khalidi Bangalaย 

    “Tupo wapi?” Aliuliza huku akigonga sanduku hilo

    “Tupo Kilomita chache kufika” Alisema mmoja wa vijana hao,ย  masaa yalizidi kukimbia usiku ulizidi kuwa mwingi sana,ย  Faudhia aliamua kujipumzisha kidogo.ย 

    Tuachane na safari ya Faudhia, ndani ya Jiji la Nairobi,ย  baada ya kupata kazi itakayo muingizia fedha nyingi Khalidย  Bangala. Alikuwa amejipumzisha kwenye moja ya Hoteli, ghaflaย  simu yake iliingia ujumbe mfupi, aliichukua simu na kuanzaย  kuusomaย 

    “Khalid, najuwa una msafirisha Mwanamke kuelekea Tanzania,ย  mnapitia mpaka upi? Namuhitaji huyo Mwanamke” Khalid Bangalaย  baada ya kuusoma ujumbe huo alijawa na mshangao ni naniย  alikuwa amemtumia ujumbe huo na alijuwaje kuwa usiku huoย  alikuwa akimsafirisha mwanamke kuelekea Tanzania, alibonyezaย  kitufe cha kupiga kisha akapiga simu kwenye namba hiyoย 

    “Khalid” ilisikika sauti ya kiumeย 

    “Nani wewe na umejuwaje?” Aliuliza kwa umakini sana Khalidย  Bangala kisha alishusha pumzi zakeย 

    “Kwasasa siyo muhimu sana kunifahamu, itabidi uchague kimoja,ย  kunipatia msichana nikulipe mara mbili au kunipa Kichwaย  chako” Ilisikika tena sauti ya Mwanaume huyo na kumfanyaย  Khalid aone jambo hilo lilikuwa siriazi kiasi gani, alikaaย  kimya bila kutoa jibu loloteย 

    “Kuna kiasi kikubwa cha fedha kwenye gari yako hapo chini,ย  chukua kisha niambie Msichana anapitia Mpaka upi” Alisemaย  tena Mwanaume huyo kisha simu ilikatika, haraka Khalidiย  alishuka chini ya Hoteli mahali ambapo gari lake lilikuwaย  limesimama, alifungua mlango wa mbele hakuona kitu, akafunguaย  mlango wa nyuma ndipo alipokutana n begi dogo, alipolifunguaย  begi hilo lilikuwa limejaa noti nyingi, alijikuta akitabasamuย  Khalid Bangala kwasababu atakuwa ameingiza kiasi kikubwa chaย  fedha, alitoa simu mfukoni kisha alimpigia huyo Mwanaumeย  asiye mfahamuย 

    “Mpaka wa Namanga, baada ya masaa mawili watakuwa hapo”ย  Alisema Khalid kisha simu ilikatwa na Mwanaume huyo bila hataย  kujibu chochote, fedha zilimuacha Khalid Bangala akiwa mwenyeย  tabasamu zito sana, alijulikana kuwa ni mpenda pesa ndioย  maana alikuwa akifanya kazi za kuhatarisha maisha yake ili tuย  apate pesa.ย 

    Akiwa anaendelea kutabasamu na kufurahi ghafla alihisi ujioย  wa Mtu nyuma yake, alipogeuka tu alikutana na risasi mojaย  kichwani, Habari za Khalid Bangala ziliishia hapo, aliyempiga risasi Khalid alikuwa ni mwanamke mmoja aliyefunga nyweleย  zake vizuri, alikuwa ndani ya Koti jeusi na suruali nyeusi,ย  Huwezi amini Mwanamke huyo ndiye aliyemuendesha Faudhiaย  kutoka Uwanja wa ndege hadi Hotelini, alikuwa ni Diana rafikiย  wa zamani wa Faudhia, alikuwa ametumwa kuchukua pesa ambazoย  waliziweka ndani ya gari ya Khalid Bangalaย 

    “Kazi imeisha!” Alisema Diana kwa njia ya simuย 

    “Waoo Good Girl ( Vizuri Msichana mzuri ) ” ilisikika sautiย  nzito ya kizeeย 

    “Rudi Tanzania” Alimalizia kusema Mwanaume huyo kwa njia yaย  simu, simu hiyo ilikatika, tayali polisi walishafika nje yaย  Hoteli hiyo, Diana alichofanya ni kuingia kwenye chemba yaย  maji machafu akaenda kutokea mbali na eneo hilo.ย ย 

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TATU

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    riwaya za kijasusi

    16 Comments

    1. Verena on May 28, 2025 3:37 pm

      Hatar sana

      Reply
    2. guy on May 28, 2025 5:18 pm

      Next plz

      Reply
    3. Cathbert on May 28, 2025 6:50 pm

      Iko poa xnaa

      Reply
    4. KingzJeelay on May 28, 2025 8:39 pm

      Huyo Diana na faudhia wapo upande wa serikali au magaidi๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿฅฑ๐Ÿฅฑ๐Ÿฅฑ

      Reply
      • Masoudy on May 31, 2025 12:35 pm

        Faudhia ndo star wa picha

        Reply
    5. Adam on May 28, 2025 8:50 pm

      Nzuri

      Reply
    6. Harvey875 on May 29, 2025 1:35 am

      https://shorturl.fm/N6nl1

      Reply
    7. Katherine2713 on May 29, 2025 2:19 am

      https://shorturl.fm/a0B2m

      Reply
    8. Jay3701 on May 29, 2025 3:42 am

      https://shorturl.fm/9fnIC

      Reply
    9. Sam2353 on May 30, 2025 11:12 am

      https://shorturl.fm/6539m

      Reply
    10. Ronald4025 on May 30, 2025 11:45 am

      https://shorturl.fm/68Y8V

      Reply
    11. Katelyn459 on May 30, 2025 1:27 pm

      https://shorturl.fm/j3kEj

      Reply
    12. Veronica2162 on May 31, 2025 6:05 pm

      https://shorturl.fm/hevfE

      Reply
    13. Edmund3277 on June 1, 2025 1:23 am

      https://shorturl.fm/fSv4z

      Reply
    14. Makayla4193 on June 1, 2025 3:12 am

      https://shorturl.fm/xlGWd

      Reply
    15. Freddie3601 on June 1, 2025 5:09 am

      https://shorturl.fm/LdPUr

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Kombe la Dunia May 31, 2025

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Hii hapa ratiba ya mechi za Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025 ambapo…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tatu-03)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Pili-02)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.