Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (07)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJanuary 12, 2025Updated:January 13, 202516 Comments15 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.Β  Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vileΒ  vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yanguΒ  niteseke.Β 

    Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuonaΒ  Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikuaΒ  nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawaΒ  anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguoΒ  akampa Mzee Mwinyimkuu. Endelea

    SEHEMU YA SABA

    Walionekana kupiga stori za hapa na pale kana kwamba walijuana muda mrefu, nilijua hii ilikuaΒ  ni tabia yake Kaka Hamidu kupenda kuongea sana na Watu tofauti tofauti pasipo kujua kuaΒ  aliyekua anaongea naye alikua katili sana na laiti angelijua hata asingelikanyaga mguu wakeΒ  ndani ya hii nyumba. Taratibu nilirudi ndani nikaingia chumbani, nikafunga mlango huku choziΒ  likinibubujikaΒ Β 

    Hapakuchukua muda mrefu mlango uligongwa, halafu uligongwa taratibu sana na hapo hapoΒ  sauti ya Mzee Mwinyimkuu ikasikika ikiniitaΒ 

    β€œMkwe” yaani nilizidi kukereka lakini kwa kuhofia uhai wa Kaka Hamidu ikanilazimu kuitikiaΒ  japo kwa shingo upandeΒ 

    β€œAbee Baba” nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango, ghafla akanisukumiza hadi ndani kishaΒ  akaufunga mlango na kunishika shingoniΒ 

    β€œNilikuonya lakini unaonekana hutaki kusikia si ndiyo, sasa kwa taarifa yako hakunaΒ  utakachofanya nisikijue. Ulichojaribu kukifanya leo sokoni kinaweza kukugharimu, subiri KakaΒ  yako aondoke nitakuonesha rangi yangu halisi na yule Mtu wako anakufuatilia sasa nayeΒ  arobaini yake imefika” alisema kisha akanitupa pembeni, kwakuwa nilikua mwembamba ikawaΒ  rahisi sana kwake kunisukuma, nikawa nakohoa ila nikawa nimejua kua nilichokusudia kwa yuleΒ  Mwanaume kule Buchani kilifanya kazi ila sasa nikawa naogopa sababu ni lazima atadhurika tu.Β 

    β€œJiandae uje uonane na Kaka yako, kumbuka nilichokwambia ukifanye la sivyo naye ataishiaΒ  humu” alisema kwa sauti yenye mikwaruzo huku akimalizia na ishara ya kuweka mkonoΒ 

    shingoni kuwa atamuuwa. Lugha ya chozi ndiyo Lugha pekee ambayo nilikua naizungumza kilaΒ  wakati, umri wangu na yote ninayoyapitia vilinizidi kabisaΒ 

    Ili kumlinda Kaka Hamidu nililazimika kuigiza kuwa kila kitu kipo sawa, nilifunga vizuriΒ  kitambaa mguu ambao ulikatwa kidole kisha nikavalia na soksi, Nikanawa usoni ili kujipaΒ  utulivu wa sura yangu iliyochoka mateso na manyanyaso ya Mzee Mwinyimkuu. NilisimamaΒ  mbele ya kioo huku kwa mbali nikisikia namna ambavyo Mzee Mwinyimkuu na Kaka HamiduΒ  walivyokuwa wakichekeshanaΒ 

    Nilipohakikisha nimejiweka vizuri, nilitoka chumbani nikaenda sebleni ambapo Kaka HamiduΒ  alikuwepo, niliizima hisia ya majonzi nikaingia sebleni, Kaka Hamidu alifurahi sana sababuΒ  hakuwahi kuhudhuria harusi yangu na pia ilipita kitambo pasipo kuonana, nilimkaribisha kwaΒ  furaha ya kuigiza na kumtaka ajisikie yupo nyumbani kisha nilimuacha na kwenda kumuandaliaΒ  chakula.Β 

    Niliporudi nilimpa chakula akaanza kula huku akinisifia kuwa mapishi yangu hayajabadilika,Β  yeye alionekana kuwa na amani na furaha ya kweli sababu hakuna alichokuwa anakifahamu hadiΒ  muda huo, isipokua mimi niliyejiona nilikua ndani ya shimo refu lililoenea giza zito nisione paΒ  kutokea, tabasamu lilitanda kote usoni pangu ili tu kumlinda Kaka Hamidu, na jinsi mudaΒ  ulivyokuwa umeenda niliogopa sana kama atalala ndani ya nyumba hii ya Kutisha, nilitamaniΒ  aondoke baada ya kumaliza kula tu.Β 

    Mzee Mwinyimkuu alikua ameketi anasikiliza maongezi yetu, akawa ananikumbusha stori zaΒ  zamani na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa nilipokua mdogo nilikua na tabia ya kulialia,Β  kwake alichukulia kama ni sehemu ya mazungumzo mazuri lakini kwangu niliona anapotezaΒ  muda badala ya kula akamaliza mapema aondoke, baadaye akaniuliza kama naweza kupokeaΒ  simu kutoka kwakeΒ 

    Huwezi amini alininunulia simu ndogo ili nisikae bila simu kwa wakati ambao nilimwambiaΒ  Mama kuwa namsubiria Mume wangu Salehe akirudi aninunulie simu mpya. Niliitaka sana ileΒ  simu lakini jicho alilonikata Mzee Mwinyimkuu nikajikuta nikimwambiaΒ 

    β€œAsante Kaka, muda siyo mrefu Salehe atarudi atanunua simu ni wajibu wake. Hiyo kampe WifiΒ  yangu” nilisema kanakwamba nilikua kwenye utani lakini moyoni nilitamani angenipa kisiri ileΒ  simu ila sasa alikua hajui kuwa napitia mateso makali sana na vitisho vya kila aina. MzeeΒ  Mwinyimkuu akajikoholesha, jasiri haachi asili yake nikashtuka lakini nikajishtukia na kurudiΒ  kwenye hali ya kawaidaΒ 

    β€œSaida, Muandalie mgeni sehemu ya kulala. Apumzike akimaliza kula maana anaonekanaΒ  amechoka” alisema Mzee Mwinyimkuu, nilishtuka sana sikutaka Kaka Hamidu asikie vitimbiΒ  vya Usiku vya hii nyumba, nikaitikia kwa wasiwasi sanaΒ 

    β€œNjoo Mama” akasema Mzee Mwinyimkuu, mbele ya Mtu mwingine hujionesha ni Mtu mzuriΒ  lakini tukiwa wawili ananitendea unyama na ukatili wa kutisha sana. Nilitabasamu nikiwaΒ 

    namtazama Kaka Hamidu ambaye naye alikua akitabasamu huku akinitazama, ndani ya moyoΒ  wake aliiamini hii picha ya nje kuwa nina amani na furaha lakini niliamini kama atalala hapaΒ  basi ataiona picha ya ndani ya Maisha yangu kitu ambacho kitahatarisha Maisha yake.Β 

    Niliongozana na Mzee Mwinyimkuu hadi kwenye korido, akairudisha ile sura yake ya MbuziΒ  ambayo niliizoea japo inatisha, kwa sauti ya chini nzito akaniambiaΒ 

    β€œChumba cha mwisho kushoto, muandalie mazingira ya kulala.” Alisema, sijui kwanini alisistiza Kaka Hamidu alale wakati alikuja bila begi lolote lile akionekana amekuja Mara moja tu, lichaΒ  ya yote sikutaka alale pale ila sikujua nawezaje kumshawishi aondoke.Β 

    β€œSawa” hakunipa onyo lolote lile baada ya kuitikia aliondoka na kurejea sebleni, nilienda mojaΒ  kwa moja kwenye chumba nilichoelekezwa ambacho Kaka Hamidu atalala. SikuwahiΒ  kukifungua kile chumba wala kukisogelea, ilikua ndiyo mara ya kwanza nakifunguaΒ 

    Nilipoingia ndani nilianza kuona vitu vilivyoniacha mdomo wazi, huyu Mzee alitaka makusudiΒ  nione pia. Palijengwa kitu kama kaburi katikati ya kile chumba, halafu palikua na mifupa mingiΒ  sana ya Binadamu, mafuvu ukutani, halafu nikasikia sauti ya kutisha ikisemaΒ 

    β€œHiki ni Chumba cha Hamidu” sauti hiyo ilinipa kiwewe nikajikuta nikipiga yowe nikakimbiaΒ  kuelekea sebleni, Kaka Hamidu akawa Mtu wa kwanza kunidaka na kuniuliza kuna nini. HapoΒ  akili ikanikaa sawa kuwa sikupaswa kupiga kelele namna ile, nikajitahidi kujikaza lakini tayariΒ Β 

    nilikua nimezua taharuki halafu cha ajabu Mzee Mwinyimkuu alikua akitabasamu tu kituΒ  ambacho kilizidi kunipa maswali yasiyo na majibu.Β 

    β€œEti Babu huyu ana nini?” akauliza Kaka Hamidu akiwa amenishika bega huku macho yakeΒ  akiyapeleka kwa Mwinyimkuu aliyeketi bila hata kujitingishaΒ 

    β€œSaida Bwana, sasa nini kinakufanya unamshtua Kaka yako, hadi leo hujaizoea hii nyumba tu?”  Aliniuliza Mzee Mwinyimkuu lakini swali lake lilijaa dhihaka sana kitu ambacho sikukipendaΒ  kabisa wakati alijuwa alichokua amekifanya. Bumbuwazi niliyonayo ilinifanya nishindwe kujibuΒ  swali lolote lileΒ 

    β€œHamidu hebu twende ukaone kilichomshitua huyu” akasema Mzee Mwinyimkuu, MoyoΒ  ulifanya kama unataka kusimama hivi kwa namna nilivyoshituka, nikajiuliza kama Kaka HamiduΒ  ataenda kule atakiona kile chumba cha kutisha chenye kaburi ndani na hapo kizaa zaa kitaanzaΒ  kwake, nikajitahidi nimzuie nikamwitaΒ 

    β€œKaka Hamidu…” alikua tayari ameongozana na Mzee Mwinyimkuu, walikuwa wameshafikaΒ  kwenye korido wakiwa wamebakisha hatua chache sana kukifikia kile chumba cha kutisha,Β  macho yalinitoka nikiwaangalia walivyokuwa wakienda kisha walisimama mlangoniΒ  wakatazamana kwa mshangaoΒ 

    Halafu Kaka Hamidu akaangua kicheko huku akigeuka na kunitazama nikiwa nimesimamaΒ  mlango wa kuingilia sebleni, alicheka kama Mtu aliyepandwa na wendawazimu, hapo hapoΒ 

    nikaisikia simu yake ikiita maana aliiacha kwenye kochi, nikatamani kurudi niipokee ili nitoeΒ  taarifa kusudi akipotea kila Mtu ajue pa kuanzia lakini sikupata hata hiyo nguvu mara akaniitaΒ 

    β€œSaida hebu njoo” aliniita Kaka Hamidu, alikua tayari ameacha kucheka. Akaniita tena kwaΒ  kunisitiza kuwa niende, nikajikuta bila kujiuliza mara mbili naanza kupiga hatua kama Mgonjwa,Β  kumbuka hapo nna maumivu ya Uchi wangu pia kidole kilichokatwa halafu nilishakata tamaaΒ Β 

    Nilisogea taratibu huku nahesabu hatua zangu kama mwendawazimu, nilijua naenda kuona niniΒ  sababu nilichokiona mwanzo ni kile kile. Nilipofika nilishangaa sana, Jamani eti kile chumbaΒ  chenye kaburi na mafuvu na mifupa ya Binadamu kilikua hakina chochote zaidi ya kitanda kizuriΒ  kilochotandikwa shuka safi sana na zaidi kilikua kinanukia ila chini palikua na paka aliyetuliaΒ  zake.Β 

    Kaka Hamidu akanishika bega akaniulizaΒ 

    β€œNi lini utaacha kuogopa paka Mdogo wangu? Wewe ni Mtu mzima sasa pia ni Mke na huwendaΒ  ukawa Mama baadaye, unaogopa Paka kweli?” aliniuliza, haikuwa siri ni kweli nilikua naogopaΒ  paka lakini nilichokiona mwanzo wala hakuwa paka, sasa nikajiuliza ni mawazo yangu tu auΒ  nilichokuwa nimekiona kilikua halisi na hiki tunachokiona ni kiini macho tu.Β 

    Nilihema mfululizo kama vile moyo ulishusha pumzi na kuamua kurejea kwenye mapigo yaΒ  kawaida, basi nilikaa kimya sikusema chochote kile.Β 

    β€œUtalala hapa, si ulisema kesho asubuhi unarudi Mbeya?” aliuliza Mzee MwinyimkuuΒ 

    β€œEeeh asubuhi narudi ili nijiandae halafu kesho kutwa niende Dar” alijibu Kaka Hamidu,Β  akanishika mkono tukarudi sebleni nikiwa kimya. Nilimhurumia sana Kaka Hamidu maanaΒ  nilianza kuwa na wasiwasi kuwa Mzee Mwinyimkuu kuna mpango fulani ameupanga dhidiΒ  yake. Muda huo huo Mzee Mwinyimkuu akapokea simu halafu akatuacha pale akaelekea njeΒ  kuzungumza ikionekana kama kuna Mtu aliyemtarajia alikua amefika nje.Β 

    Nilipanga kumshawishi Kaka Hamidu asilale ndani ya ile nyumba lakini sikujua naanzia wapiΒ  Mimi. Nikiwa natafakari Kaka Hamidu akaniulizaΒ 

    β€œHuonekani kuwa sawa Saida, kuna tatizo gani hapa?” aliuliza kama Mtu aliyeanza kuoneshaΒ  wasiwasi wa ghafla japo muda wote huo alikua akionesha kutokuwa na wasiwasi kabisa.Β  Kwakuwa alionesha kuwa na wasiwasi nikaona ni bora nimueleze ili aokoe uhai wake sababuΒ  uhai wa Wazazi wangu ulikua mikononi mwangu.Β 

    Nilisogea na kupiga magoti mbele yake nikashika na miguu yake huku chozi likinibubujika.Β 

    β€œKaka Hamidu, usilale ndani ya hii nyumba na kama utafanya hivyo basi kifo chako kitakuwaΒ  karibu zaidi na wewe” nilimwambia chozi likizidi kunibubujika, hata sauti iliyonitokaΒ  iliambatana na kilio kisicho na sauti KubwaΒ 

    β€œUnamaanisha nini?” 

    Nikavua soksi na kmwonesha Kaka Hamidu nilivyokatwa kidole ili ayaamini kwa harakaΒ  maneno nitakayo mwambia, alishtuka sana.Β 

    β€œHuyu Mzee siyo Mtu mzuri Kaka yangu, okoa Maisha yako bado una muda wa kufanya hivyo.Β  Hii nyumba imejaa uchawi na mateso makali, hata kile chumba unachoambiwa ulale ni chumbaΒ  chenye kaburi ndiyo maana nilishtuka. Ondoka bado una muda” Nilimueleza Kaka Hamidu,Β  haikuhitaji elimu ya chuo kikuu kujua kua Kaka Hamidu alikua ameshanielewa.Β 

    Akajawa na taharuki na hasira sababu alikua ananipenda sana na isitoshe hakuna nduguΒ  anayeweza kumuacha ndugu yake kwenye shida kiasi kile.Β Β 

    β€œSaida siwezi kukuacha hapa, nitamfundisha adabu huyu Mshenzi” akasema Kaka Hamidu,Β  kimwili Kaka Hamidu alikua amejazia jazia hivyo kama utamuweka mizani moja na MzeeΒ  Mwinyimkuu basi yeye ndiye atazidi. Akanishika mkono kwa nguvu akasemaΒ 

    β€œTunaondoka wote”  

    β€œKaka nenda wewe tu, mimi niache hapa ili Wazazi wangu wawe salama” nilisema, sasa KakaΒ  Hamidu akaanza kupaza sauti kitu ambacho sikukitaka kabisa. Nilichotaka ni siasa zaidi ili KakaΒ  Hamidu aondoke pasipo Mzee Mwinyimkuu kujuwa chochote kile.Β 

    Mara tukasikia mlango ukifungwa tena siyo kufungwa kawaida ni kule kufungwa kwa kufuriΒ  kabisa halafu ni Mlango wa kuingilia nyumba kubwa, Kaka Hamidu akanipa ishara ya kukaaΒ  kimya. Alidhamilia kuomdoka na Mimi, nami niliona ni bora niondoke naye kuliko kubaki tenaΒ  kwa Mzee MwinyimkuuΒ Β 

    Akaingia Mzee Mwinyimkuu pale sebleni, alikua amevalia suruali, singlendi na BalaghashiaΒ  kama kawaida yake, hakututazama kabisa akalisogelea kabati na kuiweka funguo kwenye drooΒ  kwa mbwembwe sana huku akiwa anapiga zake mluzi.Β 

    Ilikuwa ndiyo nafasi pekee ambayo Kaka Hamidu alikua ameipata, akachukua jagi la kioo lenyeΒ  maji kisha akasogea taratibu hadi nyuma kwa Mzee Mwinyimkuu, akampiga na lile jagi kisogoniΒ  kwa nguvu hadi Mzee Mwinyimkuu akagugumia kwa maumivu na damu zikaanza kutokaΒ  alipopigwa akaanguka chini huku akionekana kutaka kusema jambo lakini alikua akishindwa.Β Β 

    Kaka Hamidu alikua akimuangalia Mzee Mwinyimkuu alivyokua anatapa tapa, kwa sekundeΒ  kadha tu zilitosha kumnyamazisha akawa ametulia tuli pale chini kama maji ya Mtungi, ikawa niΒ  nafasi ya dhahabu sana kuondoka ndani ya ile nyumba.Β Β 

    β€œTwende” akasema kaka Hamidu akiwa amenishikilia mkono kwa nguvu tukawa tunaelekeaΒ  mlangoni ili tuondoke. Tulipofika Mlangoni tukapata akili ya ile funguo, ndiyo! Palikua naΒ  kufuri mlangoni, funguo aliiweka kwenye droo kule sebleni,.Β 

    Hapakuwa na ujanja isipokua Kaka Hamidu kurudi sebleni kuchukua funguo, alipofika SebleniΒ  hakumuona tena Mzee Mwinyimkuu pale sakafuni wala sebleni kote, ni kama aliyayuka mithiriΒ 

    ya Barafu juani. Akaniita, nikakimbilia sebleni nami nikawa shuhuda wa kutoweka kwa MzeeΒ  Mwinyimkuu, tulitazama kwa mshangao mkubwa.Β 

    Tusingeweza kurudi nyuma tena, Kaka Hamidu akafungua droo na kuikuta funguo, akaichukuaΒ  kisha akaniambia tuondoke. Cha kushangaza ambacho kilitufanya tugande kama Barafu niΒ  kuukuta ule mlango tuliohangaika kuchukua funguo ukiwa wazi kabisa, halafu nje tukisikia sautiΒ  ya Mtu kama akichakata kuni hivi.Β Β 

    Sote tukawa na hofu sana, Nani ameufungua ule mlango bila kusikila sauti yoyote? HakunaΒ  aliyekua na jibu la moja kwa moja, Kaka Hamidu akaona ni bora apige simu ili aombe msaada,Β  alishaona siyo rahisi kuondoka ndani ya ile nyumba ya kutisha, halafu ilikua mishale ya usikuΒ  mchanga kama saa 3 hivi lakini matukio yaliyotokea na ukimya uliokuwa umetanda na gizaΒ  ilionesha kama vile ni Usiku mnene.Β 

    Akajipapasa na kukumbuka simu aliiacha Kwenye kochi, kabla hata hajapiga hatua kurudiΒ  sebleni, pale pale taa zote zikazima. Pakawa giza tupu hata nuru moja isionekane, pakawa kimyaΒ  kabisa, sikumsikia tena Kaka Hamidu isipokua sauti ya kugugumia ambayo aliitoa kwa nguvu,Β  papo hapo nikasikia kitu kikianguka kama Mzigo β€˜Puuh’ 

    β€œAaaaah‼” niligumia kwa hofu lakini ghafla nikabanwa mdomo wangu halafu sauti ya MzeeΒ  Mwinyimkuu ikagonga ngoma za Masikio yangu, nilishtuka sana.Β Β 

    β€œShiiiiiβ€Ό!” akanitaka nikae kimya. Nilikuwa nahema juu juu, mara papo hapo taa zikawaka.Β  Nilichokiona jamani sitakuja kusahau Maisha yangu yote, nilihisi uchizi, nilihisi wendawazimu.Β  Mwili ulipoa kama nimemwagiwa maji ya Baridi. Kaka Hamidu alikua sakafuni, damu nzitoΒ  ilikua imetapakaa kila mahali.Β Β 

    Alitenganishwa kichwa na kiwiliwili chake, damu zilikua zinaruka kwenye shingo yake. HataΒ  Mzee Mwinyimkuu aliponiachilia sikua na nguvu nilianguka chini nikakalia damu.Β 

    β€œNilikuonya hukusikia” akasema Mzee Mwinyimkuu, alisema. Mkononi alikua ameshikilia kisuΒ  kikubwa chenye damu. Niliishia kudondosha chozi tu, mara akaingia Mwanaume mmoja naΒ  kuanza kuuvuta mwili wa Kaka Hamidu kuelekea nje, Mze Mwinyimkuu akakichukua kichwaΒ  cha Kaka Hamidu na kukipeleka kwenye kile chumba alichokua amekiandaa kwa ajili ya kulalaΒ  Kaka Hamidu.Β 

    Sijui kilichoendelea baada ya hapo nilijikuta nikizidi kuishiwa nguvu, giza zito likatanda nikahisiΒ  usingizi wa ajabu. Nikapoteza uwezo wa kujitambua.Β 

    **Β 

    β€œSaida,Mdogo wangu amka Unisaidie” ilikua ni sauti ya Kaka Hamidu, alikua amesimamaΒ  mbele yangu nikiwa nimekaa kitandani, alikua akivuja damu kila sehemu. Alikua ametisha kiasiΒ  kwamba niligugumia hadi nikapaza sauti yangu kwa hofu. Hivyo ndivyo nilivyoamka kutokaΒ  Usingizi wa kifoΒ 

    Nilikua na maumivu makali sana mguuni, ndoto hii mbaya iliniamsha. Eneo lile lile nililokatwaΒ  kidole lilikua na maumivu makali sana. Niliusogeza vizuri Mguu wangu na kuangalia kidondaΒ  kinaendeleaje, nilipoangalia niliona vidole viwili vikiwa vimeondolewa. Yaani jumla ya vidoleΒ  vitatu vinavyofuatana kuanzia cha mwisho vilikuwa havipo.Β 

    Maumivu yalikua makali, ni bora uyasome kwenye hii hadithi lakini yasikukute, mwili woteΒ  ulipandisha homa ya ghafla, kichwa kilikua kinauma sana. Safari hii sikuwa na uhakika kamaΒ  ninaweza hata kutembea, eneo lenyewe nililopatia ufahamu sikulijua kabisa.Β 

    Nilikua sakafuni, chumba kilikua kitupu isipokuwa mimi tu na maumivu yangu. Nilipiga sakafuΒ  kwa uchovu nikasemaΒ 

    β€œKama uliniumba niteseke hadi nife basi nitakufa na kama huu ni mpango wa shetani basiΒ  hawezi kukuzidi maarifa” nilipomaliza kusema hivi nilijikunyata, Nililia sana. Nilikua tayariΒ  nimempoteza Kaka Hamidu na sijui walimpeleka wapiΒ 

    Eneo lile lilikuwa kimya sana tofauti kabisa na nilivyozoea, sikusikia sauti za Pikipiki walaΒ  mazungumzo yoyote yale. Niliona ni bora nilikague eneo lile, nilichungulia dirishani, nililionaΒ  Pori la Kubwa, nilishtuka. Nikagundua nilikua nimehamishwa kutoka kwenye nyumba ya MzeeΒ  Mwinyimkuu. Nililia sana maana safari hii siwezi kukutana na yeyote yule nikapata msaada,Β  Mzee Mwinyimkuu alishagundua kuwa kama ataniacha huru naweza kutoroka, ilifika hatuaΒ  nilikua mkali nikajisemeaΒ 

    β€œKama kuokoa uhai wangu kutafanya wazazi wangu wafe ni sawa, napaswa kukwepa hayaΒ  mateso Makali. Mungu atapigana kwa ajili ya Wazazi wangu” hayo ndiyo yalikua maamuziΒ  yangu.Β 

    Niliveshwa kaniki pekee halafu nilikua na alama fulani kwenye paja langu, ilikua alama ya ajabuΒ  iliyochorwa kwa moto, palikua na maneno ya ajabu. Huu ndiyo wakati mgumu zaidi kuwahiΒ  kuupitia katika Maisha yangu yote, haukuwa wakati rahisi kwangu, ulikuwa wakati ambaoΒ  nilipoteza tumaini la Maisha yangu lakini sikuweza kufanya chochote isipokua kuuguliaΒ  maumivu na kulia.Β 

    Kilipita kitambo kirefu cha Ukimya, sijui ilikua ni saa ngapi, siku gani au lile eneo ni wapi.Β  Nilichojua ni kuwa bado naendelea kupumua, niliusikia Mlio wa pikipiki. Nikajivuta naΒ  kuchungulia dirishani, niliiona pikipiki ikiwa imesimama kando kidogo kama mita chache tu hiviΒ  kisha Mtu mmoja alisogea mbele kuelekea nyumba niliyopoΒ 

    Kumbuka hapo ni Porini, tokea nimezinduka sikuwahi kumuona yeyote yule isipokua sauti zaΒ  ndege zilizopita kwenye ngoma za masikio yangu yaliyochoka kusikia sauti za kutisha. NilikuaΒ  nimekonda ghafla sana Mimi SaidaΒ 

    Basi, yule Mtu sikuiona sura yake kwa haraka sababu hata nguvu ya kusimama kwa muda mrefuΒ  ilianza kuniisha nikajikuta nikianguka chini, maumivu yalikua makubwa halafu nilikua na njaaΒ 

    sana. Nilisikia tu akifungua mlango ulioonekana kuwa na komeo nyingi, akaingia hadi chumbaΒ  nilichopoΒ 

    Yule Mtu nilimkumbuka kwa haraka sana, alikua ni yule Bodaboda aliyenipeleka sokoni siku ileΒ  ambayo nilikutana na Abuu. Nilikua na wenge zito lakini sikuacha kumtazama kwa makini hadiΒ  nikamtambua. Alikuwa amebeba chakula kwenye Hot-potΒ 

    Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.Β 

    β€œKunywa Maji” alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikuaΒ  ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuulizaΒ 

    β€œMnanimalizia lini nikapumzike?” Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chacheΒ  nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambiaΒ 

    β€œKifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwaje” alisema kisha akanipa maji, sikuwaΒ  na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe haiΒ 

    Comments zikiwa nyingi naachia ya NANE leoleo hapa

    Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA NANE YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxΒ 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    16 Comments

    1. Otchou jr on January 12, 2025 4:52 pm

      Simulizi tamu Sana haichoshi na haiishi hamu kuifuatilia.
      Mola mlezi akubariki mwandishi, aturudhuku neema tuzidi kuwa pamoja Hadi tamati.

      Reply
      • Hamisa Joseph on January 12, 2025 6:14 pm

        Leo nitaota haki mwenyew Nina machungu afu nasoma hii story inatishaa

        Reply
      • Lus twaxie on January 12, 2025 6:18 pm

        Jamaniii. Huyo dada akimbieee …

        Reply
    2. Gyakiee on January 12, 2025 4:53 pm

      Mpka machozii ilaa naaminii Mungu atamfanyiaa njiaa

      Reply
    3. Abdul on January 12, 2025 5:01 pm

      Dah inasikitish san πŸ’”πŸ₯Ί

      Reply
    4. Egibeth on January 12, 2025 5:20 pm

      Duj umeupiga mwingii sanaa admin

      Reply
    5. Patricia Lizzy on January 12, 2025 5:24 pm

      Duh….

      Reply
    6. Fawziya Hassan on January 12, 2025 6:09 pm

      Simulizi inanitoa machozi jamani 😭😭ya Ajabu sana
      Sijawahi kusoma hadithi mfano wake.
      Maskini Saida.
      Vidole vyake nasikia ganzi jamani
      Kaka Hamidu kaenda jamani
      😭😭

      Reply
    7. Fawziya Hassan on January 12, 2025 6:13 pm

      Mzee MwinyiMkuu na Salehe wanafaa kuitwa Nguruwe kwa matendo yao.
      E Mwenyezi Mungu
      Waangamize Wachawi wote Jehannam.
      Ameen.

      Reply
    8. G shirima on January 12, 2025 6:14 pm

      πŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ˜₯πŸ˜₯😭😭

      Reply
    9. Doricas paul on January 12, 2025 6:52 pm

      Sehemu ya nane ata leo hadithi inavutia kusoma inasisimua inahuzunishaa pia

      Reply
    10. Massay on January 12, 2025 7:11 pm

      Duh hatari sana hii

      Reply
    11. HAJI RAMADHAN KISENDI on January 13, 2025 2:30 am

      Inauma sana binadam sis n wabaya sana

      Reply
    12. Ahmed Ruta on January 13, 2025 8:17 am

      Angekua ni mtoto wa 2000 angekua teal amekatwa vidole vyote maana awa wa kizazi iki ni wakaidi balaa

      Reply
    13. Emma komba on January 13, 2025 2:16 pm

      Looh Kisa kinasisimua km nipo ndani yake

      Reply
    14. πŸ“Œ πŸ“Š Balance Update - +1.8 BTC added. Check now β†’ https://graph.org/GRAB-FREE-BTC-07-23?hs=a69fa4876beecdd2ec589e81373fc8ab& πŸ“Œ on August 18, 2025 1:04 am

      i6kjs2

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE β€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.