Sijui kwako ndoa ina maana gani lakini kwangu Mimi ndoa ilinipotezea Muda wangu, iliniacha naย Maumivu na kilema cha Maisha yangu.ย
Sikuwahi kuwaza chochote kuhusu ndoa wala kuitamani, lakini siku moja nilikua natoka sokoniย Mabibo naelekea nyumbani Magomeni Usalama, niliposhuka kwenye daladala kwa bahatiย mbaya niliteleza na kuanguka wakati navuka barabara. Mfuko wenye vitu nilivyonunua sokoniย uliangukia pembeni.ย
Nilihisi aibu sana siku ile na kibaya zaidi mvua ilikua imenyesha majira ya asubuhi, lilijaa topeย lililoniharibia Baibui langu. Eneo nililoangukia palikua na kijiwe cha Bodaboda. Kamaย uwajuavyo walianza kushangilia anguko langu kitu kilichozidi kunipa hasira lakini sikuwa na laย kufanya zaidi ya kujiokotanisha pale.ย
โPole sana Dadaโ niliisikia sauti hii nikiwa nasimama, aliyenipa pole alinipatia na mfuko wanguย akiwa ameokotanisha vitu vyangu. Alikua kijana mzuri mtanashati sana, nilijikuta nikiwa naย kigugumizi kumjibuย
โUnaelekea wapi?โย ย
โNyuma ya sheli, usijaliโ nilisema nikiwa najipangusa tope kutoka kwenye Baibui langu jeusi,ย akanipa mkono wakeย
โNaitwa Salehe Mwinyimkuuโ Alijitambulisha kwangu, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kishaย nilimjibuย
โNaitwa Saidaโย
โNimefurahi kukufahamu, wacha nikusogezeโ alisema, kwa msaada alionipa isingelikuwa hisaniย kukataa alichokiomba. Taratibu tuliikanyaga ardhi kuelekea karibu na nyumbani kwetu. Kwaย muda mchache nilihisi kumjua kidogo, niligundua ni mpole, mwemye hekima na busara teleย licha ya kuniambia ana Miaka 27 tu.ย
โMimi nina Miaka 23โ nilijitanbulisha kwake huku nikianza kunogewa na mazungumzo yake.ย Tuliongea mengi hadi kubadilishana namba za simu kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwa Mtuย nisiyemjua.
Tulizidi kuwasiliana kwa zaidi ya mwezi mzima huku tukiwa marafiki wa kawaida tu lakiniย baadaye Salehe alinitongoza.ย ย
Nisiwe mwongo wala mnafiki hata kabla ya kunitongoza nilianza kumpenda hivyo kunitongozaย alikua anatimiza wajibu wake kama Mwanaume kwani nisingeliweza kumwambia Nampendaย isitoshe Mimi nilikua Bikra kwa wakati ule.ย ย
Tulianza mahusiano ya Kimapenzi lakini nilimwambia Salehe kuwa Mimi nimelelewa kwenyeย familia ya Dini sana, Baba yangu ni msaidizi wa Shekh Mkuu wa Msikiti wa Magomeni hivyoย kama ananipenda kweli basi awaone wazazi wangu kwanza. Sijui tuseme alikua na kiu sana auย alikua anahitaji Mke sana maana alilifanya hilo siku tatu tu baada ya kumwambiaย
Baba yangu alifurahi sana, Mama pia alifurahi zaidi akaniambiaย
โMwanangu ndoa ni Nusu ya Dini, sisi Wazazi wako tunakutakia kila lililo jema, Munguย akuongozeโ Daima Mama yangu alikua Mtu wa karibu sana kwangu, alisimama na Mimiย kwenye kila jambo hata ambalo Baba yangu alipingana na Mimi.ย
Salehe hakutaka kuchelewesha alilipa Mahali siku iliyofuata.ย
โWewe Kijana ni Mtu wa wapi?โ Baba alimuuliza Salehe wakiwa katika mazungumzo yaย kawaida, kama Mzazi ni lazima ahakikishe usalama wa Binti yakeย
โKwetu Rukwa lakini nipo Hapa Dar Likizoโ alisema Saleheย
โOoh! Unajishughulisha na nini?โย
โNimeajiliwa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Rukwa Mjiniโย
โUtamtunza Binti yangu?โย
Kwanza Salehe alicheka kidogo kisha akamwambia Babaย
โNisipomtunza Mke wangu nitamtunza Nani, wanasema Mbuzi unayemlisha ndiye utakaye mkamua maziwaโ Basi Baba na Salehe wakaishia kuangua vicheko, ilileta raha sana.ย ย
**ย
Ndugu wa Salehe walifika tena waliazimia kuwa ndoa ipite kabla likizo ya Salehe haijaisha iliย tuondoke wote kuelekea Rukwa, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitaolewa na kwenda mbaliย kama Rukwa. Kidogo nilipata huzuni, nilimzoea Mama yanguย
โUsijali, hata Mimi niliwaacha Wazazi wangu Morogoro nikaja kuishi na Baba yako Saida. Umriย ukifika hakuna la kukuzuia kuanzisha Familia yakoโ Mama yangu hakuacha kunitia Moyo. Babaย aliachia tabasamu maana tulikuwa wote sebleni
โNgoja niwaache muongee maongezi yenu ya kikeโ alisema Baba akaelekea zake Msikitini,ย zilipita siku kadhaa hadi siku ya ndoa ilipowadia. Ndoa ilipita salama, Siku ya pili tulianza safariย ya kuelekea Rukwa Mimi na Mume wangu Salehe.ย ย
Bado nilikua Bikra wala hakunigusa usiku wa kwanza wa ndoa yetu hotelini kabla ya Kuanzaย safari, kwakua nami nikikua mgeni wala sikudai chochote kile. Tulifika Rukwa Usiku sana tenaย nikiwa ninasinzia, tulichukua Taxi hadi nyumbani kwa Saleheย
โKaribu nyumbani Mke wangu, jisikie uko nyumbani kabisa na hapa ndipo tutakapoishiโ alisemaย tukiwa tunashuka kwenye taxi, tulisimama mbele ya nyumba moja iliyo giza sana, sikushangaaย sababu mwenye nyumba hakuwepo kwa muda mrefu. Nilijiegemeza kwenye bega la Saleheย nikamwambiaย
โMume wangu, ulipo nipo na nitaendelea kuwepo siku zoteโ lile Taxi liliondoka, kazi yaย kuhamishia mabegi ndani ilianza. Salehe alikua ametangulia nami nilibakia nyuma nikikokotaย begi. Sijui ni mawazo yangu au nilisikia kitu halisi kabisa, nilisikia sauti za Watoto wakiombaย Msaadaย
โSubhannahโผโ nilishtuka, sikuisikia tena ile sauti maana mwanzo ilitokea ndani ya ile nyumbaย ambayo tulikua tukielekea. Mapigo ya moyo yalinienda mbio, niliposikiliza vizuri walaย sikuzisikia tena nikajua ni fikra zangu tu. Basi niliendeelea kuvuta begi hadi ndani, taaย zikawashwaย
Palikua kimya sana, uzuri sikua na njaa wala hamu ya kula zaidi ya Kulala kutokana na Uchovuย wa safari. Nilisimama kusuburia Salehe anioneshe chumba chetu, akaufunga mlango kishaย akaniongoza hadi chumbani, nilipofika nilijitupa Kitandani na kujilaza kama pono bila kujaliย kuwa kitandani palikua vumbi tupu.ย
Nililala Usingizi wa nusu kifo hadi mapambazuko, sauti ya jogoo kuwika niliisikia ikiniamsha naย kuniambia ni muda muafaka wa kuanza majukumu ya nyumbani. Macho yalijawa na Ukunguย usio kifani, nilijinyoosha kama Kinda la ndege halafu nikajikuta nikipigwa na Butwaa zito sanaย ambalo kiukweli nilishangazwa mno na nilichokionaย
โNipo wapi hapa?โ Nilijiuliza swali hili, niliipapasa akili yangu inikumbushe jambo lakiniย haikua tayari kufanya hivyo, Salehe hakuwepo Kitandani. Moyo ulinienda hali Jojo,ย nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani.ย
Nitakueleza kwanini nilipigwa na Butwaa la ajabu, kwanza harufu ya Udi wenye harufu mbayaย ilizagaa kote ndani, pili nilisikia sauti ya Mtu akitwanga na kwa hakika alikua akitwangia ndaniย halafu sauti ya Mtoto Mchanga anayelia nilizidi kuisikia. Taratibu nilitaka kujuwa nipo wapiย haswa maana tayari nilianza kupata hofu fulaniย
Nilipiga hatua za taratibu hadi mlango wa kutokea chumbani, ile sauti ilitoweka na palikuaย kimya sana. Moyo wangu haukutulia kabisa licha ya ukimya wa ghafla niliousikia, jua lilikuaย tayari limeshatoka
Nyumba ilikua safi sana. Ilikua na korido ndefu yenye vyumba kadhaa japo kwa wakati huoย sikuhesabu kutokana na hali niliyokua nikiihisi. Basi Mimi Saida nilijiulizaย
โAh ni mawazo gani haya Jamani, Ewee Allah niepushie Mbaliโ nilisema kisha nilirudiย Chumbani kutafuta simu yangu nimpigie Salehe aniambie alipo si unajua maisha ya Ugeni yanavyoanza. Nilikumbuka mara ya mwisho simu niliiweka kwenye mkoba wanguย
Sikuwa na shaka sana kuhusu simu yangu, niliikuta lakini kwa bahati mbaya ilikua imeisha chaji.ย Niliketi kitandani nikiwaza mambo kadhaa lakini niliona ni bora niweke simu chaji niwasilianeย na Saleheย
Nilipomaliza kuweka chaji na kuhakikisha simu yangu inaingia chaji nilipata nafasi yaย kukiangalia kwa uzuri chumba, kilipangwa vizuri sana hadi nilijikuta nikitabasamu, nilijuwa niย Mume wangu Salehe alikua ameamka mapema na kuweka mazingira sawa. Nilijiona ni mwenyeย Bahati sana kuitwa Mke wa Salehe, nilikua na nguo zangu zilezile nilizokuja nazo hivyo wazo laย kubadilisha nguo lilinijia lakini kabla ya kufanya hivyo nilisikia Mlango wa nje ukigongwa.ย
Sikujua naanzia wapi kuitikia wito huo, nilisogea hadi mlango wa chumba na kusikiliza vizuri.ย Mgongaji wa mlango alikua ni Mwanamke na sauti yake ilikua karibu sana hivyo kwa harakaย niliamini anagonga mlango wa Nyumba ya Salehe. Hakuna aliyeitikia ile hodi hadi paleย nilipoamuwa kumkaribisha nikiwa ndani tena kwa sauti ambayo aliisikia vizuri, nilijiangaliaย kama nilikua nipo sawa kutoka ndani kisha nilianza safari mara moja kutembea kwenye koridoย kuuelekea Mlangoni.ย
Niliufungua mlango wa kwanza kwa kutekenya kitasa tu kisha nikauelekea mlango wa Uwaniย ambao ndio mgongaji alikua hapo, nilipoufungua nilikutana na Mama Mmoja aliyebeba tenga laย mboga mboga kichwani, alikua ameshakata tamaa alikua akiondoka nikamwitaย
โMamaaaโผโ alipogeuka alirudi hadi Mlangoniย
โShikamoo Mamaโ nilimsalimia kwa adabu, ndivyo nilivyofundishwa kwetu kwa wazazi wangu,ย yule Mama alitabasamu kisha akaniulizaย
โHauchukui Mboga leo?โ Nilitabasamu maana aliuliza kana kwamba alishawahi kuniuzia mbogaย ila nilielewa Lugha ya Kibiashara huwa hivyo mara zoteย
โMimi ni mgeni hapa Mama, labda kesho nikiwa nimeyafahamu vizuri mazingira nawezaย kuchukua. Usiache kupitishaโ nilisema kisha yule Mama aliondoka huku akiitikiaย
โNapita kila siku Mtaa huu, Wahiiii mboga mbogaโ alienda mbele zaidi kisha alitokomeaย machoni pangu. Kuzungumza na yule Mama ni kama kulinisahaulisha kuhusu Salehe lakiniย alipoondoka nilijiulizaย
โSalehe ameenda wapi mbona hajaniaga?โ Niliufunga mlango kisha nilirudi ndani, Nyumbaย ilikua kubwa ya Kisasa lakini ilikua kimya sana sikusikia hata sauti ya ndege kuruka. Uwaniย
palikua na sehemu ya kukaa nikaona ni bora nikae hapo kwanza nipate upepo, nilijikutaย nikipitiwa na Usingizi wa ghafla tu.ย
Ndoto za hapa na pale zilinifuata usingizini na kunipa hekaheka hadi nikashtuka. Niliposhtukaย nilikutana na sura mbili, moja ilikua ya Salehe na nyingine ni ya Mzee mmoja mweusi aliyevaliaย Baraghashia nyeupe na kanzu nyeupe. Macho yao yalikua kwanguย
โEeeh imekuaje umelala hapo Mke wangu?โ aliniuliza Salehe, nilijitabasamisha kidogo kamaย Mtu anayezuga ili asinione kuwa mvivuย ย
โHewa ya hapa inavutia, kaupepo nikajikuta nasinzia tuโย
โSawa, huyu ni Baba yangu anaitwa Mzee MwinyiMkuu. Ni Baba yangu Mzaziโ alisema Salehe,ย nilimsalimia yule Mzee kwa heshima sana hata naye alifurahia na kuona ni namna gani ninaย heshima.ย
โMarhaba Mkwe wangu mzuri, hakika Mwanangu hakukoseaโโ akasema kwa Utani tukajikutaย tukicheka kidogoย
โSamahani, najua umenitafuta ila nilienda kumpokea Baba maana aliniambia nikirudi tu atakujaย kwa ajili ya kukusalimia wewe Mke wanguโ alijielezea Salehe, ni kweli Mzee MwinyiMkuu alikuja na begi dogo la Mgongoni lililochakaa sana.ย ย
โAaaah! Nimefurahi sana kumuona Baba yako Salehe, karibu Baba.โ Nilisema kisha nilisimamaย na kulishika begi la Mzee MwinyiMkuu ambalo lilikua sakafuni, kabla sijaliinua yule Mzeeย alinishika mkono kwa nguvu sana hadi nilishtuka, nikamtazama Usoni alikua amenikazia suraย yakeย ย
โHili begi halishikwi na kila Mtu, Salehe unajua pa kulipelekaโ alisema Mzee MwinyiMkuu,ย nilihemwa maana sikutegemea lakini hata kama ningelichukua ningelipeleka wapi wakati naย Mimi ni Mgeni pale. Nilishusha pumzi, kilinishuka nikarudi kukaa, Salehe akaniambiaย
โMzoee Baba yangu ana utani sana Saida, wacha nikaweke begi lake nakujaโ Mara mojaย alipomaliza kusema alinyanyuka Salehe na kuelekea ndani, yule Mzee hakuacha kunitazama kwaย jicho kali kama vile kuna kitu nimeharibu hadi nilianza kumwogopa, ikanilazimu kumwombaย Msamahaย
โSamahani Baba sikujuaโย
โSiku nyingine uwe unauliza, umeelewa?โย
โNdiyo Babaโ Nilipomjibu alinikata jicho fulani la husda kisha akatoa mguno fulani wa kichekoย cha dhihaka halafu akanyanyuka na kuiburuza kanzu yake akaingia zake ndani,nilishusha pumziย zote kama Mgonjwa wa Pumu. Niliusikia moyo wangu namna ulivyoamka nakuanza kudundaย tena, hata koo ilianza kupitisha mate kwa kasi. Yaani sijui nikueleze vipi unielewe namnaย nilivyokua nimeshikwa na woga kupitiliza, sura ya yule Mzee niliyona imekaa kikatili sana
Wakati naendelea kujiuliza mara Mume wanu Salehe alirudi kutoka ndani, akaketi mahaliย alipokua ameketi Baba yakeย
โBaba yako ni Mkali sana Salehe hadi nimeogopa. Nimefanya kipi kibaya, kumsaidia Begi niย vibaya eti?โ Nilimuuliza Mume wangu, yeye akanishika bega akaniambiaย
โUtamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizoย kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaaย hapa.ย ย
โIna maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?โย
โNdiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?โ Basi kuzungumza naย Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Saleheย akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo hukuย dimpozi zangu zikionekanaย ย
Comments ziwe nyingi apa LEO kwa Kaka Mkubwa
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILI YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx


22 Comments
Heri ya Mwaka Mpya 2025
Riwaya nzuri sana, Asante sana kwa utunzi mzuri ubarikiwe
Unyama uendelee
Japo jasusi hamkuimalizia
Hii balaa ๐ฅ๐ฅmwanzo tu linaonekana big up kaka mkubwa
Uhakika ni hatariii mwendelezo please
Iko poa xna
MAUZA UZA
Saida kaolewa na Msukule๐
Baba mkwe Msukule
Asante Admin โค๏ธ baada ya kimya kirefu saivi tunaburudika tena na
KAKA MAKUBWA more Love from Zanzibar โค๏ธโค๏ธ
Kaka MKUBWA โค๏ธโค๏ธโค๏ธ
Duuuh kitu usicho kujua ni sawasawa na usiku wa giza
๐โโ๏ธ๐๐kumeanza kuchangamkaa
Atajua ajui ngoja mda wa kwenda kulima usiku ufike ,kwenye begi bado ajasemaaaa
Eeh hapoo uhakikaa kaka mkubwa ongeza kitu
Familia ya kichawi iyo
Mhh
[email protected]
Umetisha
Ulituacha mbali kidogo tungesahau
Ubaya ubwela
Familia ya kichawi iyo
Mhh
Ya pili please
Aisee Mwanzo Ni wamoto ,Pameanza na Mushkeli๐
Riwaya nzuri jaman nmechelewa kuianza
Nice