Ilipoishia “Hizi ni risasi zilezile, chukueni maiti hizi na wengineΒ fanyeni msako hapa haraka sana” Ilikuwa ni sauti ya mmoja waΒ Askari waliokuja pale kanisani, bado Mtaalam Sande, MzeeΒ Dawson na vijana wake wakiwa ndani ya Andaki bila kuwa naΒ taarifa kuwa Jesca alikuwa ameuawa na Six, lilipofunguliwa lango kuu la Kanisa ndipo mshituko na Mshangao mkubwaΒ ulipowashika polisi hao, walikuta Miili ya watu ikiwaΒ inatokwa na mvuke kama vile nyama inayochomwa, harufu yaΒ nyama ilitapakaa kanisa zima wakaagiza zima moto kumwaga MajiΒ katika kanisa hilo, muda mchache polisi walifanikiwa kuingiaΒ ndani ya kanisa na kukuta Miili mingi ikiwa imeharibikaΒ vibaya sana.Β
Taarifa ilizagaa kwa haraka sana juu ya shambulio hilo laΒ kutisha ambalo lilitumia silaha ya sumu na risasi, SandeΒ akawashauri akina Mzee Dawson kuwa hawapaswi kutoka kwaΒ wakati huo hadi polisi watakapo maliza msako wao. EndeleaΒ
SEHEMU YA TISA
“Nina mashaka juu ya uhai wa Jesca, yeye ni mmoja wa walinziΒ wa hapa kanisani, sijasikia majibizano ya risasi, huwendaΒ amekufa kifo Baridi” Alisema Mzee Dawson akionekana kushindwaΒ kuzuia chozi lakeΒ
“Una maanisha nini kusema Kifo Baridi?” Alihoji Mtaalam SandeΒ Olise huku akimtazama Dawson kwa jicho lililo kazaΒ
“Kufa bila kujibu mapigo, Walengwa tunaotafutwa katika vitaΒ hii ni sisi. Sitaki makubwa yawakute wasio na hatia” AlinenaΒ DawsonΒ
“Una maaana gani?”Β
“Ni bora nijitokeze kupambana nao ili kunusuru Maisha yaΒ wengi yanayowekwa rehani, ikiwa kufa Mimi au kupona waoΒ ninachotaka ni usawa” Aliongeza DawsonΒ
“Kumbuka Polisi watakuangalia kama muarifu kuanzia hivi sasa,Β hautokuwa huru kufanya chochote kama Mkuu wa Kitengo, vitaΒ hii ni ngumu Mkuu! Vipi kama Rais ataamuwa kukupaka tope?Β Utakuwa salama?” Aliuliza Sande Olise, Mzee Dawson akamezaΒ funda zito la mate kisha akasemaΒ
“Tusipopambana sasa hivi tutakuja kupambana nje ya muda,Β tunapaswa kuwa macho zaidi”Β
“Unashauri tufanye Nini Mkuu tupo tayari kukusaidia katikaΒ vita hii” Alisema Kisko kwa utii Mkubwa, Dawson alikuwa kamaΒ Mzazi kwao, ndiye aliyewachukua kutoka katika kituo chaΒ Watoto yatima na kuwaonesha Mwanga wa Maisha, DawsonΒ akawageukia na kuwaambiaΒ
“Natamani hii vita msipigane sababu mna kila sababu ya kuwaΒ hai ili mje mpigane hapo baadaye sisi tukiwa tumetundikaΒ daruga au tukiwa tumekufa. Niliwaandaa mje kuwa hazina muhimu baadaye” Alisema Dawson kwa sauti ya Baba kwa Watoto wake,Β nyuso za Kisko na Chande zilisinyaa huku macho yao yakitazamaΒ chini.Β
“Babaa!! ” Aliita Chande, Dawson akageuza macho yakeΒ kumtazamaΒ
“Tupo tayari kwa sasa kufa kwa ajili ya Taifa letu, turuhusuΒ tukusaidie hii vita” Dawson alipomaliza kumsikiliza ChandeΒ akarudisha macho yake kwa Sande Olise, WakajikutaΒ wanatazamana huku sura zao zikizungumza KijasusiΒ
“Tuangalie tunatokaje hapa Shimoni, haribuni kila kitu iliΒ kupoteza ushahidi wa kazi za hapa ndani, kila mmoja avae suraΒ bandia haraka sana” Aliagiza Mzee Dawson kwa sauti iliyojaaΒ mamlaka ya Kijeshi, kazi ikaanza rasmi.Β
MSAKOΒ
“Shit!” Ilikuwa ni sauti ya John Brain baada ya kupokeaΒ taarifa usiku huo, hakutegemea kusikia kuwa Dawson na SandeΒ Olise bado wanaendelea kupumua, aliona ni makosa makubwa niΒ sawa na kumjeruhi mnyama Mkali.Β
“Inawezekanaje wasiwepo kanisani wakati mtoa taarifaΒ amehakikisha kuwa Sande aliingia hapo? Endapo Sande na DawsonΒ wakapata muda wa kupanga mipango yao kazi hii itakuwa ngumuΒ kwetu” Alisema tena John Brain huku akizitazama sura za SixΒ na Malaika ambao walikuwa wamenywea.Β
“Nimefanya msako kanisa zima lakini sikupata kuhisi hataΒ harufu zao, huenda walicheza mchezo wa sarafu baada yaΒ kugundua kuwa tunawafuatilia” Alijibu MalaikaΒ
“Watakuwa wapi?” Aliuliza John Brain akionesha kutafakariΒ jambo peke yake, kisha akawaambiaΒ
“Nendeni lakini Mjiandae kwa msako maalum” Malaika na SixΒ wakaondoka, John Brain akampigia simu Rais na kumjulishaΒ taarifa ile ambayo ilionekana kumchanganya sana RaisΒ
“Hivi mnajua mnafanya masihara kwa Watu gani? Hao jamaa wanaΒ medali za ushindi kwenye kila jambo, Dawson ana fahamu siriΒ yetu hivyo hapaswi kuendelea kuishi” Alisema Rais kama MtuΒ aliyeingia kwenye mshituko ni wazi kuwa alitarajia kusikiaΒ kuwa Dawson na Sande wameuawa
“Tunalijuwa hilo na vijana wangu wanalifanyia kazi jambo laΒ muhimu ni kuhakikisha unatupatia Mtu wetu baada ya sikuΒ chache, tutakuwa tumeimaliza kazi hii na kuondoka hapaΒ Nchini”Β
“Msifanye Makosa mengine John , mtajikuta mnawajibishwa!Β Ngoja nijisafishe haraka sana” Rais alikata simu, alionekanaΒ kuwa mwenye msongo wa mawazo huku akionekana kuwa na hofu juuΒ ya mpango wake wa siri juu ya Mauwaji ya Makam wa RaisΒ kujulikana na kuwekwa hadharani, akanyanyua simu na kumpigiaΒ Mkuu wa Idara ya polisi na kumueleza kuwa Dawson ni mharifuΒ anapaswa kusakwa kwa kila njia ili apatikane, Rais aliamuwaΒ kucheza karata mbili.Β
Moja ni kuwatumia Mafia Gang kumfyeka Dawson na nyingine niΒ kutumia Jeshi la polisi kumsaka popote alipo, agizo la RaisΒ lilianza kutekelezwa, Polisi wakaagizwa kuelekea nyumbani kwaΒ Dawson usiku huo huo.Β
Rais alikaa katika kiti chake huku akizidi kujiingizaΒ mawazoni, Nchi ilikuwa imeingia katika Msako, PolisiΒ walivunja nyumba ya Dawson na kufanya msako mkubwa bilaΒ mafanikio, wakati huo Dawson na timu yake wakiwa wanatokaΒ katika shimo kule kanisani, Polisi wachache walikuwepo eneoΒ la tukio kule kanisani usiku huo, Walifanikiwa kuchomoka paleΒ kanisani kimya kimya kisha wakaruka ukuta wa kanisa naΒ kutokomea.Β
Dawson alishajua kuwa polisi wataenda nyumbani kwake hivyoΒ akawaambia wasiende huko badala yake waelekee kwenye makaziΒ ya siri ambayo alikuwa akiishi Inspekta Zola, ilikuwa niΒ safari ya Kilomita kadhaa kutoka pale kanisani hadi kufikaΒ huko, walilazimika kutembea kwa mguu sababu polisi walikuwaΒ wakikagua magari yanayoingia na kutoka kila kona ya jijiΒ hilo, haikuwa salama kwao kutumia usafiri wa gari licha yaΒ kuvaa sura bandia, mwendo wa masaa mawili Walifika kwenyeΒ makazi hayo, Dawson alifahamu namba za siri za kufunguliaΒ milango hiyo ikawa rahisi wao kuingia ndani.Β
Kumbukumbu ya Zola iliendelea kuwatesa baada ya kuingia humo,Β Sande aliiona picha aliyopiga na Zola wakiwa mafunzoni hadiΒ chozi lilimbubujika aligundua kuwa Rafiki yake huyo alikuwaΒ akimpenda na kumkumbuka sana, walikuwa na ndoto ya kuonanaΒ siku moja lakini ndiyo hivyo Sande alichelewa kurudi hadiΒ Zola akauawa, Dawson aliifahamu nyumba hii vizuri sana sababuΒ mpango wa nyumba hii aliusuka mwenyewe ili Zola aitumieΒ nyumba hii kwa kazi zake maalum, akawaonesha chumba ambachoΒ kilikuwa na silaha akawataka kujiandaa kwa ajili ya kazi hiyoΒ kubwa iliyo mbele yao.
“Baada ya kupambazuka tutakuwa katika hekaheka nzito yenyeΒ maamuzi ya kuondoa uhai wetu au kuturuhusu kuendelea kupumua,Β kama tuna muda wa kufurahi basi huu Usiku uliobaki unawezaΒ kuwa ndio muda pekee wa kufanya hivyo” Alisema Dawson akiwaΒ ana mimina mvinyo kwenye glasi, kila mmoja akanyanyua naΒ kuanza kunywaΒ
“Kwa ajili ya Zola, tusherehekee Maisha yake sababuΒ ameimaliza kazi aliyokula kiapo kuifanya ili kulinda TaifaΒ lake” Yalikuwa ni maneno ya Sande Olise ambaye naye aliunganaΒ na Mzee Dawson wakanywa Glasi moja moja, Chande na KiskoΒ wakaungana pale wote wakapata Mvinyo kama Ishara ya kuyaenziΒ Maisha ya Inspekta Zola ambaye ameuawa ndani ya Ikulu, hadiΒ kufikia muda huo hakukuwa na taarifa iliyotolewa popote kuwaΒ Inspekta Zola alikuwa amekufa, si akina Dawson wala upande waΒ Rais ambao ndio walitekeleza Mauwaji hayo.Β
Asubuhi ya siku iliyofuata iliwakuta Dawson na vijana wakeΒ wakiwa ndani ya jumba la siri hilo alilokuwa akiishi MtaalamΒ Zola, taarifa kuwa Dawson amelisaliti Taifa ilianza kuzagaa,Β akatajwa Dawson kama ndiye Mhusika namba moja wa Mauwaji yaΒ Waumini kule kanisani, taarifa ikafika mbali na kusema anaΒ viashiria kuwa alitaka kuipindua Nchi hiyo kwa kusababishaΒ taharuki ikiwemo Mauwaji ya kutisha yaliyokuwa yakifanyikaΒ pia Mauwaji ya Makam wa Rais, gunzo lilikuwa limetanda, niΒ kama Bundi mweusi alikuwa ameyazunguka Maisha ya Dawson,Β ikatolewa taarifa kuwa Dawson anashirikiana na Askari mmojaΒ wa Usalama wa Taifa aliyeitwa Sande Olise ambaye alikuwaΒ akiishi Botswana.Β
“Huyu Mjinga anajaribu kuharibu taswira niliyoijenga MiakaΒ mingi katika Taifa hili” Alisema Dawson kwa hasira hukuΒ akitafuta rimoti ya TV ili aizime, Sande alimzuiaΒ
“Huna haja ya kupaniki, anachokifanya Rais ni kujaribuΒ kujisafisha na kuyatia doa Maisha yetu. Kwakuwa anajua unaΒ siri zake basi anaitumia hii nafasi kukudidimiza iliΒ usiaminike na yeyote yule” Alisema Sande kisha DawsonΒ akamuulizaΒ
“Mimi ni mzalendo kwa Taifa hili, nimekuwa kwenye nafasi hiiΒ kwa Marais zaidi ya tano, iweje huyu aje kuharibu kila jemaΒ nililopanda kwenye Taifa hili, baada ya kuniulia Rafiki yanguΒ anadiriki kuniita Msaliti wa Taifa hili” Dawson alionekanaΒ kuchukizwa sana na kitendo kile, akapapasa kiuno chake akatoaΒ bastolaΒ
“Unaenda wapi?” Alihoji Sande
“Ikulu kuondoa uhai wa hayawani yule, hastahili kuishi pale,Β anastahili kuwa Kaburini au Jela kwa yote aliyoyafanya”Β
“Hebu tulia, kumbuka John Brain ni Mtu mwenye akili sana. HuuΒ ni mtego na lengo ni kukufanya uchukie, Rais anakujua vizuriΒ hupendi mchezo na uzushi, ukitoka hapa hata hufiki mbaliΒ wanakuuwa” Alisema Sande huku akimsistiza Dawson atulie,Β chozi lilikuwa likimbubujika Mzee Dawson, akajitupa kitiniΒ kama Mtu aliyekata tamaa.Β
“Huna haja ya kukurupuka, Tumetajwa kuwa Wauwaji na wasaliti,Β tukikamatwa huko nje hatutokaa kuonekana tena, tutaliachaΒ Taifa hili katika giza kama ambavyo Zola ameliacha. NimekujaΒ hapa kwa ajili ya kazi hii, nitazame Mimi kwa sasa kamaΒ ambavyo ulikuwa ukimtazama Zola na kumuamini, hamisha kilaΒ kitu kutoka kwake kisha kiweke kwangu, Mimi ni Zola niliyeΒ katika Umbo la Sande, hakuna kitakacho haribika” Yalikuwa niΒ maneno ya Kikomandoo kutoka kwa Sande Olise, alisema akiwaΒ amefanikiwa kumpokonya Bastola Dawson.Β
Akampatia ile Bastola Kisko akamwmbiaΒ
“Ukiitumia vibaya itakupeleka pabaya, tuliza akili ndipoΒ uitume ifanye kazi yake” Alimkabidhi kisha AkasemaΒ
“Baada ya miaka mingi narudi kazini kupambana na John Brain,Β kivuli chake kitaendelea kuitesa hii Nchi, huyu Rais MpumbavuΒ siku zake za kuwa madarkani zinahesabika” Alisema kishaΒ akaelekea kwenye moja ya vyumba vya siri vya jengo hiloΒ ambavyo vilikuwa vimeshafunguliwa na Mzee Dawon.Β
Akakuta Ramani ya mpango wa Zola ikiwa ukutani, akaangaliaΒ namna Zola alivyopanga mambo yake pale akajikuta akitabasamuΒ kwani kila jambo alikuwa ameliandika katika Ramani hiyo.Β
Nyuma ya Sande alikuja kusimama Mzee Dawson huku akimtazamaΒ Sande namna alivyokuwa makini kutazama Ramani ya ZolaΒ
“Ulikuwa na askari shujaa sana ambaye hasahau mbinu zako”Β Alisema Sande Olise kisha aligeuka na kumtazama Mzee DawsonΒ aliyekuwa akifuta chozi lake, kifo cha Zola kilimuumiza sana.Β
“Nina uhakika kama utawatunza vijana hawa wawili wanawezaΒ kuwa Sande na Zola wa baadaye, kwasasa Mzee Dawson pumzika.Β Afya yako haikuruhusu kuendelea na vita hii, nitapambana MimiΒ na hawa vijana, utabakia hapa” Aliongeza Sande, ni kweli afyaΒ ya Dawson haikuwa nzuri kutokana na pombe na sigara.
Wakapanga mipango ya kumuondoa Rais Madarakani kisha kuanikaΒ uchafu na madudu yake yote, Dawson alitakiwa kubakia paleΒ kwenye jumba la siri wakati ambao Sande na vijana wawili waΒ Dawson watakapokuwa wanaondoka, wakapewa sura bandia iliΒ watakapotoka nje wasijulikane.Β
Muda huo Magari mawili meusi yalikuwa yakiingia Ikulu,Β alikuwa ni John Brain, Six na Malaika, utatu ambaoΒ ulilisumbua Taifa kwa muda mrefu, waliitwa na Rais huyoΒ Mshenzi. Waliingia wakiwa kama wageni wakiwa ndani ya suraΒ bandia ili wasitambulike sababu Vyombo vingi vya habari hasaΒ vya nje vilikuwa vikiripoti taarifa zao za Mauwaji na jinsiΒ ambavyo walikuwa wakitafutwa, Waliongoza hadi ofisini kwaΒ Rais huyo bila Ulinzi wowote kutokana na maagizo ya Rais.Β
Rais alipowaona alinyanyuka na kusogea karibu na John BrainΒ kisha akamuulizaΒ
“Mnataka niwape nini ili Dawson na Sande wauawe? MnapaswaΒ kujuwa kuwa Dawson ni nyati aliyejeruhiwa akitoka hukoΒ mafichoni hatutokuwa salama” Alisema huku akionekanaΒ kuchanganikiwa, jasho lilikuwa likimvujaΒ
“Tatizo umechanganya vitu viwili kwa wakati mmoja, PolisiΒ wanahangaika kuwatafuta na sisi tunahangaika kuwapata. KilaΒ tunapopiga hatua polisi wanakuwa eneo la tukio, au unatakaΒ tusamabratishe na polisi wako?”Β
“Kama hilo ni tatizo nitawaingiza katika mfumo wa usalama waΒ Taifa mkiwa katika sura hizo, John utakaa pembeni sababu yaΒ rangi yako ila Malaika na Six wataingia na kufanya kazi maraΒ moja, watakuwa na amri kwa askari pindi wanapokutana katikaΒ jukumu la kuwawinda Sande na Dawson,watapewa vitambulishoΒ maalum”Β
Rais akawaingiza Six na Malaika katika mfumo wa idara yaΒ Usalama wa Taifa, wakapewa na VitambulishoΒ Β
vilivyowatambulisha kama Watu wa Usalama, ikawa rahisi kwaoΒ kuwa huru kufanya kazi ya kuwasaka Dawson na Sande OliseΒ ambao walikuwa kizingiti kikubwa kwa Rais na John BrainΒ kumpata kijana wake aliyekuwa akishikiliwa na Rais.Β
Polisi wakatawanywa kila kona ya Jiji kuhakikisha Dawson naΒ Sande hawapigi hata hatua moja, kazi ya polisi ilikuwaΒ kuwakamata lakini kazi ya Six na Malaika ni kuwauwa, wakiwaΒ ndani ya Sura bandia walirudi pale Kanisani ambakoΒ walisababisha Mauwaji ya kutisha ya Waumini na Askari mmojaΒ wa siri wa Mzee Dawson, walirudi kama Watu wa Usalama,Β wakahitaji kuchunguza eneo hilo huku akili zao zikiwaambia kuwa pengine Dawson na Sande bado wapp eneo hilo, walimjuaΒ vizuri Dawson jinsi alivyo na akili nyingi.Β
Walitumia vyema macho yao ya Kijasusi na mafunzo waliyoyapataΒ kutoka kwa John Brain wakagundua kuwa kuna andaki eneo laΒ maegesho ya MagariΒ
Six na Malaika wakapeana ishara, haraka bastola zao zikawaΒ zinatazmaa eneo hilo ili kama kuna Mtu atatokea basiΒ wamdhibiti haraka sana.Β
Wakalisukuma gari na kuona mlango wa kuingia ndani, harakaΒ wakiwa makini sana wakafungua na kuanza kuingia humo taratibuΒ huku masikio yao yakiwa makini kusikiliza ndani ya andakiΒ hilo lenye giza sana.Β
Walipofika chini wakawasha tochi ya simu kisha wakaona mahaliΒ ambapo wangewasha taa, walipowasha wakaona vitu vikiwaΒ vimeharibiwa pale, wakakagua kila kona lakini hakukuwa naΒ Watu, tayari Mzee Dawson na vijana wake walishaondoka paleΒ muda mrefu sana kisha wakaharibu vitu ndani ya andaki hilo,Β elimu yao ya kijasusi haikuwafanya wao kukata tamaa ya kutakaΒ kujuwa andaki hilo lilihusiana na niniΒ
“Kwa vyovyote haya yalikuwa makazi ya siri ya Dawson! HuendaΒ ameishi hapa kwa kitambo sana” Alisema SixΒ
“Hata awe makini vipi ni lazima ataacha alama humu, tutajuaΒ kama ni yeye na ameenda wapi” Alisema Malaika, msakoΒ uliendelea ndani ya andaki hilo lililoonekana kuwa makazi yaΒ kutulia sana, katika upekuzi wao waliona Makaburi manneΒ ambayo yalikuwa ndani ya chumba kimoja.Β
Walipoangalia vizuri waliona namba za siri ambazo Mzee DawsonΒ aliwapa vijana wake kama majina na alama zao, namba hiziΒ zilikuwa za siri sana, ilikuwa ngumu kugundua chochote lakiniΒ alizitambua kisha akampigia simu John Brain na kumuelezaΒ kuhusu Makaburi hayo manne yenye namba za siri, John BrainΒ alikuwa na mtandao mkubwa sana na alizijua siri nyingi zaΒ Mataifa mbalimbaliΒ
“Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupoΒ hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola,Β fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliaminiΒ Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake.Β
Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwaΒ bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenyeΒ kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwaΒ likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuiaΒ kufanya kazi yao,
Comments ziwe nyingi apa wikiendi itoke EPISODE NDEFU YA 10Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAΒ USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxΒ
Β Β
22 Comments
unyama
Kazi kazi
Toa hata tatu mzee baba
Weeknd usitubanie asee
Kila unaesima naomba ucoment please
Too hotπ
Ya motoo
.wendelzo jmn pia zilishwe hata tano kwa siku π₯°π₯°
Simulizi ya π₯
Mtunzi wa Simulizi hii anitafute kuna Zawadi yakeβ₯οΈβ₯οΈβ₯οΈ
Daah imefka penyew mkuu uwe unatoa hata mbili basi mkuu
Stor iko poa sana
Hatar iyooΓ³oo
Nzuri sana
Shusha chuma mkuu π€΄
Weeee
Kesho tuwahishie Basi pia ilefushe hata kidogo maana siku za mpira hua unabana Sana
Jmn huyu malaika na six. Si sande wawauwe fasta wasijeniulia Mzee wangu Dowson jmn
Admin story Kali sn ni km vile mtu unaangalia movie
Hili ni bomu la kutegwa ardhini kilo mia moja haponi mtu hapo ni mbele kwa mbele π€Έπ€Έπ€Έπ‘
π₯
Natamani ingekuwa movie kbs yani uwii admin upewe maua yako βΊοΈ
Kazi nzuri admin una jitahidi
3exvik