Ilipoishia “Kama Maisha yangu yatakoma leo Ikulu, Sande uje kufanya hiiย kazi kuliokoa Taifa mara moja” Alisema Zola kisha choziย lilimtoka, akakata simu hiyo. Visa vya baadhi ya Askariย kupotea vilikuwa vingi katika Taifa hilo, Zola baada ya Masaaย mawili alikuwa akikaguliwa kwa ajili ya kuingia Ikulu,ย ilikuwa ni mara ya kwanza Zola kuitwa na Rais huyo, si Raisย huyu Pekee bali Zola hakupata kujulikana na Rais yeyoteย aliyepita, hii ilimpa shaka sana Zola kwanini Rais ampigieย simu wakati ambao alikuwa akimbana yule Askari amwambieย ukweli kuwa Nani anafanya Mauwaji yale.ย Endeleaย
SEHEMU YA SABAย
Upande wa Sande Olise, Chozi la Zola lilimkumbusha mbali sanaย wakati huo Zola alipokuwa akiogopa kwenda kufanya mafunzoย hayo ya Ujasusi na Upelelezi Nchini Mexico, mafunzo hayoย yaliambatana na Mafunzo ya Ukomando, Sande ndiyeย aliyemshawishi Zola kuingia huko laiti kama asingelimshawishiย basi Zola angekuwa Askari wa kawaida kabisa, Mafunzo hayaย hufanywa siri sana, kitengo cha siri cha Mzee Dawson ndichoย kilichokuwa kikifanya uchaguzi wa nani aende na Nani asiendeย hivyo Dawson alificha sana majina ya Askari wake wa siriย ambao ndio alikuwa akiwatumia kwenye majukumu mazito ambayoย Serikali ilimpa, haraka akafungua Kabati lake lililo chumbaniย kwake akaitoa simu ya Siri ambayo ilitumika kwa ajili yaย Mawasiliano yao ya Kiaskari, akampigia Mzee Dawson.ย
Mzee Dawson ( Google ) aliposikia sauti ya Sande alijuwaย kulikuwa na tatizo, akameza funda zito la Mate, sauti hiyoย hakuisikia kwa miaka mingi sana. Licha ya kuwa ni Mmoja waย vijana wake wa Kitengo lakini Sande alikuwa Botswana kwaย miaka mingi mno, alipojitambulisha ndio Mzee Dawson akapataย kujihakikishia zaidiย
“Sande! Bado unanikumbuka?” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaaย wasiwasi sana huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio, maraย nyingi hakuwa akipokea simu za siri sababu yeye ndiyeย aliyekuwa akiratibu kazi za Kijasusi hivyo yeye ndiyeย aliyekuwa Mpigaji mara zote kutafuta vijana wake, leoย alitafutwa yeye na Sande!!ย
“Naam! Mkuu wa Kitengo, Mimi ni P045! Simu ya dharura, narudiย Nchini kwa kazi maalum, nahitaji Baraka zako!!” Ilikuwa niย sauti iliyojaa uzalendo na ujasiri wa hali ya juu uliombatanaย
ย ย
na Utii sababu licha ya Mzee Dawson kuwa Mkubwa kiumri badoย alikuwa ni Askari mwenye Cheo kikubwa sana! Alikuwa ni kamaย Baba yao mzazi kwenye kazi za Kijasusi.ย
“Zola amewasiliana na wewe?” Aliuliza Dawsonย
“Ndio, yupo hatarini. Maisha yake yapo mikononi mwa Raisย Zagamba, narudi kumkomboa” Alisema Sandeย
“Uuuupss!!”ย
“Ndio Mkuu! Kwasasa Mkuu wa Nchi anawinda maisha ya Zola, niย ngumu kujuwa kama atatoka salama sababu yupo njiani anaendaย Ikulu ameitwa na Rais” Kauli hii ilimpa mshituko Mkubwa sanaย Mzee Dawson,ย
“Tuongee baada ya dakika chache” Alisema Dawson, kishaย alikata simu hiyo. Mara moja kanyanyua simu yake akampigiaย Zola ili kuthibitisha alichokisia, Simu ya Zola ilikuwaย imezimwa.ย
“Shit!!” Akasema Dawson kisha akatoka nyumbani kwakeย akaelekea Ikulu, Sande alikaa kusubiria simu ya Mzee Dawson!!ย
Alipofika Ikulu, Dawson alikaguliwa kabla ya kuruhusiwa, mojaย kwa moja akaelekea ofisini kwa Rais, akamsimamia Rais naย kumpigia Saluti kisha akaketi kwa heshimaย
“Dawson!! Kwanini umekuja kama Mkimbizi kutoka Somalia?”ย Alihoji kwa dhihaka huku akiwa anaandika kituย
Dawson alimtazama Rais Jacob Zagamba huku akili yakeย ikipingana na mawazo yake juu ya kuuliza kuhusu Inspektaย Zola, hakutaka ijulikane kuwa Zola ni Askari wake wa siri waย Kitengoย
“Nimekuja tuongee kuhusu Hii kesi”ย
“Umefikia wapi Dawson?”ย
“Bado uchunguzi unaendelea lakini nimefikia mahali pazuriย sana na siku si nyingi nitakupa mrejesho kuhusu Kundi laย Mafia Gang” Alisema Dawson huku macho yake yakionesha kuwaย sicho kilichompeleka pale.ย
“Dawson nahitaji hili jambo ulimalize ndio maana nikaliletaย katika Meza yako, ninachotaka kusikia siku moja ni kuwaย umeuwa Wahusika wote na kuileta miili hapa, hao Watuย hawatakiwi kuishi kabisa” Alisema Rais na kumpa maswaliย Dawson, kwanini Rais atake Watu hao Wauawe?
“Nitawakamata kisha watahukumiwa kufungwa kifungo cha Maisha,ย hiyo ni ahadi yangu kwako Mkuu” Rais akamtazama Dawson kwaย hasira kisha akagonga mezaย
“Nimesema nahitaji Miili yao, fyeka kundi hilo haramu naย mazalia yake hapa Nchini, Dawson narudia tena nahitaji miiliย yao, hawana kesi ya kujibu….hili jambo linapaswa kufanywaย siri, kinachotakiwa ni kuwa Watu hao wakifa basi vifoย vitakoma, hakuna atakayeuliza wako wapi, haya ni maagizoย yangu” Alisistiza Rais, muda huo akaingia Jamaa mmoja mweusiย aliyepanda Hewani, alionekana kuwa ni Usalama wa Taifa, Raisย akamuuliza Mtu huyoย
“Safari inaanza?”ย
“Ndio Mkuu” Alijibu kwa Utii, kisha Rais akachukua funguo yaย gari akampatia jamaa huyo, Dawson hakuelewa kilichoendeleaย pale japo hakujuwa Zola yupo wapi.ย
Baada ya jamaa huyo kuondoka Dawson akaaga ili aweze kuondokaย
Alipofika karibu na Lango kuu la Ikulu alikutana na walinziย wawili ambao ni dhahiri walikuwa wakimsubiria yeye ili wamtoeย nje, alipowafikia walimpa ishara kuwa wao walikuwaย wanamsubiria, Dawson akatupa macho yake huku na kule, Milangoย mingi ilikuwa imefungwa, walinzi hao ambao walivalia sutiย nyeusi waliongozana na macho makali ya Dawson ili kujuwaย alikuwa akiangalia nini, basi wakampa tena ishara kuwaย aongozane nao, wakati anatoka pale mlangoni macho yakeย yalitupa uangavu kuelekea kwenye maegesho ya Magari ya Ikulu,ย ndipo alipomuona Jamaa aliyetoka kuzungumza na Rais akiwaย amebeba begi kubwa lililomzidi uzito, Dawson alijikutaย akiingiwa na shahuku ya kutaka Kujuwa jamaa huyo alikuwaย akifanya safari gani. Akawageukia walinzi akawaambiaย
“Asanteni! Nitafika” Alikuwa na nia ya kuwatoroka ili afanyeย upelelezi wake sababu bado kichwa chake kilikuwa kinaliaย alamu kuwa Zola yupo matatizoni,ย
“Ni wajibu wetu kukufikisha lilipo gari lako” Alisema mmojaย wa walinzi hao tena akiwa anatabasamu, walimjuwa vyema Dawsonย kuwa ni mmoja wa Askari waliotegemewa sana na Kila Raisย aliyepita, alikuwa na cheo kikubwa mno, pale pale Zolaย akapata akili, akakohoa na kutoa damu kitu ambachoย kiliwashtua wale Walinzi wakiamini anaumwa, ni kweli Dawsonย alikuwa anaumwa mapafu yake kutokana na uvutaji wa sigara ilaย hapa aliamuwa kucheza na akili za Walinzi hao ili awatoroke,ย taharuki ikazuka pale huku mmoja akijaribu kuita gari yaย wagonjwa
“Msijali nahitaji Kitambaa” Alisema Zola kwa sauti yenyeย kikohozi, Walinzi hawakuwa na kitambaa, mmoja akatoka kwendaย kuchukua tishu ili imsaidie Dawson, ulikuwa mtego. Harakaย Dawson akajikunjua na kumpiga ngumi kali sehemu ya shingo naย kufanikisha kumzimisha pale pale, akamburuza hadi maegesho yaย magari yaliyo karibu, Wakati huo yule Jamaa akiwa analipakizaย lile begi ndani ya buti.ย
Akamficha mlinzi yule kwenye maegesho, akaingia kwenye gariย yake na taratibu akaanza kulifuata gari hilo ambalo lilikuwaย likianza kutoka taratibu kuelekea getini, Naam!! Dawsonย aliliangalia gari hilo kwa taswira yenye mashaka sana hukuย akitilia mashaka lile begi, hakuacha hata hatua moja alikaaย nyuma ya gari hilo lililokuwa likiingia barabara kuuย iliyokuwa ikitoka Mjini, Gari hiyo ilibadilisha uelekeo naย kuelekea eneo la Bahari ambako ni nadra sana kuona Magariย yakiongoza huko, Dawson alisogea kwa spidi sawa na gari hiloย kisha mbele aliona gari hilo likiwa limesimama kando ya Mitiย ya Mikoko, Dawson akalipita gari hilo makusudi iliย kumuaminisha jamaa huyo kuwa yupo peke yake.ย
Alipofika mbele Dawson alisimama kisha akashuka ndani ya gariย akawa anarudi Taratibu liliposimama gari lile alilokuwaย akilifuatilia, walikuwa mbali zaidi ya Kilomita 15 kutokaย Ikulu, eneo hilo gari chache sana zilikuwa zikipita. Yuleย jamaa akafungua buti na kulitoa begi kisha akalitelekeza eneoย lile, Dawson alikuwa amejificha mahali, jamaa alipoondokaย Dawson alisogea na kulifungua.ย
Alijikuta akianguka kwa Mshituko huku macho yake yakishindwaย kuamini alichokiona ndani ya begi hilo, chozi lilianzaย kumbubujika Dawson, aliuwona mwili wa Inspketa Zola ukiwaย ndani ya begi hilo, Dawson alijikuta akiwa amepoteza mmoja waย Maaskari wake wa siri ndani ya Kitengo hicho, alilia kwaย uchungu sana! Maisha ya Inspekta Zola yalikuwa yametamatishwaย ndani ya Ikulu, mwili wake ulikuwa na vidonda na matundu yaย risasi, Dawson akalifunga begi hilo kisha akalivuta hadiย kwenye gari yake akaliweka kwenye buti akaondoka na mwiliย huo.ย
Akiwa barabarani alionekana kuwa na hofu, nyuma yake kulikuwaย na lile gari lililotoka Ikulu lilikuwa likimfuatilia kwaย nyuma, Dawson aligundua hilo haraka akafanya ujanja iliย kulipoteza lakini gari hilo lilikuwa bado nyuma ya Dawson kwaย zaidi ya kilometa 35 kutoka usawa wa Bahari ambako aliuokotaย mwili huo ndani ya begi, Dawson alichofanya ni kutembea kwaย mwendo wa kawaida ili apambane na Mtu aliye ndani ya gariย hilo baada ya kuhisi kuwa hakukuwa na usalama wa Maisha yake,ย alisogea kwa umbali ndipo akaona kuna uzio wa Polisiย waliokuwa wakifanya msako barabarani, Dawson akagundua kuwaย kuna mchezo umechezwa ili yeye apotee, haraka akabadilishaย uelekeo na kuingia Barabara ya pili ambayo ilikuwa ya vumbiย kisha akaenda kutoka barabara nyingine, muda huo gari lileย lilikuwa nyuma yake.ย
Dawson alikuwa na sifa kubwa juu ya ujuzi wa kuendeshaย magari, sifa ambayo Zola aliwahi kuishuhudia siku mojaย alipotembelewa na Dawson, Naam! Akaongeza spidi kwa harakaย akachomoka kama ndege ya kivita, alifanya hivi makusudi iliย kulipoteza gari lile lililotoka Ikulu, dakika chache alikuwaย amesha lipoteza, akasogea hadi karibu na jengo moja chakavuย sana, Dawson aliona sasa Maisha yake yanaweza kuingia dosari,ย aliona kuna kila dalili kuwa Rais alikuwa na lengo laย kumpoteza baada ya kufanikisha kumfyeka Zola pale Ikulu, japoย alikuwa Mzee lakini nyakati hizi mbaya alijitahidi kulibebaย begi lenye mwili wa Zola akapanda nalo juu ya jengo hilo laย ghorofa ambalo lilikuwa halijaisha.ย
Hadi anafika juu alikuwa hoi, akajikuta akianguka chini kishaย akatoa simu yake yenye mkonga kutoka katika mfuko wakeย akapiga mahali.ย
“Sande! Zola ameuawa Ikulu muda mchache uliopita” Alisemaย Dawson huku akijifuta jasho, jioni ilikuwa ikiingiaย
“Unasemaje?” Ilisikika sauti ya Sande upande wa piliย
“Ndio hivyo, mwili wa Zola nipo nao hapa lakini hata Maishaย yangu yapo hatarini, huyu Rais ni Mtu hatari kulikoย inavyodhaniwa” Ilikuwa ni sauti iliyotoka kikomavu sana,ย Ghafla akasikia mchakacho, Dawson akakimbilia sehemu yenyeย uwazi kwa ajili ya kuchungulia chini, akaliona lile gariย jeusi lililotoka Ikulu, ni wazi kuwa Rais alituma Mtu kwaย ajili ya kumfuatilia Zolaย
“Mkuu mbona Kimya?” Aliuliza Sande Olise baada ya kuonaย ukimya umetawalaย
“Nacheza sarafu ya Kifo Sande!” Akakata simu mara moja baadaย ya kuwa ameshamuelekeza Sande, mara moja akatafuta sehemu yaย kujificha, begi lile lilikuwa katikati ya chumba kimoja.ย
Hakuwa Mtu mmoja bali walikuwa wawili wakiwa ndani ya sutiย nyeusi, mmoja akiwa amevalia miwani nyeusi na mwingine akiwaย na macho makavu sana, sura zao zilimtambulisha Dawson kuwaย Watu hao walitoka Kitengo cha Usalama wa Taifa Ikulu, Dawsonย alishazoea Maisha ya kuwindana akavuta pumzi zake mara mojaย kisha akajikunja mithiri ya nyani Mzee huku Mgongo wake ukiwa umevunjika vilivyo, masikio ya Dawson yalikuwa makini sanaย kusikiliza hatua za Wataalam hao ambao wazi walikuwa naย mafunzo maalum na walijuwa wanamtafuta Mtu wa namna gani,ย jinsi walivyokuwa wakipishana huku wakilindana ilimfanyaย Dawson afunge kiwambo cha kuzuia sauti ya Risasi kusikika.ย
Hata kabla Dawson hajafyatua Risasi, alisikia mlio wa gari yaย polisi, kisha hatua za jamaa wale kukimbia zilisikika, Harakaย Dawson akaenda kuchungulia akawaona jamaa hao jinsiย walivyokuwa wakidanda kushuka chini kama nyani, akashushaย pumzi zake kisha akili ya kujuwa afanye nini ili polisiย wasiukute mwili wa Zola ilimjia, kando yake kulikuwa naย dirisha lililokuwa na mabomba mawili yaliyoshuka hadi chini,ย akajivuta haraka akalibeba begi na kuteleza nalo hadi chiniย kisha akajificha nyuma ya kichaka kwa umakini zaidi sababuย alijuwa maadui zake walikuwa eneo hilo, akanyata huku akiwaย amelibeba begi akakatiza mtaro wa maji machafu akaendaย kutokezea Barabarani akasimamisha Bajaji na kutokomea zake,ย Jamaa wale walipofika hawakujuwa Dawson aliondoka vipi pale,ย mmoja akavuta simu na kupiga mahaliย
“Mkuu!! Dawson ameyeyuka” Alisema kwa utii huku mkono wakeย uliobeba simu ukiwa na misuli na Glove!ย
“Mnamjuwa huyo Mtu vizuri, hakikisheni hachomoki” Ilikuwa niย sauti ya Rais Zagamba ikisikika katika sikio la Jamaa huyoย
“Sawa Mkuu!” Aliitikia kisha alikata simu.ย
MSAKO GIZANIย
Malaika, Six na John Brain baada ya kuona imekuwa ngumu kwaoย kumpata Mtu wao ambaye walihangaika Nchi nzima katika vituoย vyote vya polisi bila mafanikio, waliuwa Maafisa wengi waย polisi ili kumtisha Rais aamuru kuachiwa kwa Mtu waoย ilishindikana. John Brain akaja na Mpango wa kutaka kusambazaย Ugonjwa hatari wa Ebola, Kabla ya kuanza kwa mpango huo Johnย Brain alimpigia simu Rais ili kumtaka amuache Mtu wao harakaย sana.ย
Kilichowafanya Mafia Gang kuendelea kuwepo Nchini ni Mtu waoย ambaye alikamatwa, kesi iliyokuwa ikimkabili Mtu huyo ilikuwaย ni kesi ya Mauwaji ya Makam wa Rais. Muda huo Rais alikuwaย nyumbani kwake Ikulu akitafakari nini cha kufanya baada yaย kumkosa Dawson ambaye sasa alikuwa ameshaupata mwili wa Zolaย na kwa vyovyote Dawson atakuwa ameifahamu siri ya Mauwajiย yanayoendelea kutokea, mezani alikuwa na kikombe kidogo chaย Kahawa ambacho kilikuwa kikitoka mvuke kuashiria kuwa Kahawaย ilikuwa ya moto sana.ย
Simu ilipoita ilikuwa imemzindua kutoka Mawazoni, akaangaliaย ni nani aliyekuwa akipiga akaona ni John Brain. Akalambaย midomo yake kabla ya kupokea huku akiwa anaelekea Chooni.ย
“Kazi yako imeshaisha, tumekutoa katika kesi ya wizi naย ufisadi ambayo ushaidi alikuwa nao Makam wa Rais,ย kilichobakia kilikuwa ni kutupa Pesa zetu lakini cha ajabuย unamshikilia Mtu wetu hadi hivi leo, tumekupa taarifa kupitiaย vifo vingi tulivyovisababisha lakini inaonekana hujatakaย kuelewa”ย
“Brain! Tukae mezani tulizungumze hilo”ย
“Michezo ya kitoto isiwepo tafadhali, kama utashindwaย kukubaliana na sisi basi tutahakikisha unang’oka madarakani”ย Alisema John Brainย
“Usijali Brain, hakuna kitakacho haribika” Rais alipotokaย Chooni alisimama kando ya mlango, Mlinzi wake alisogea naย kumuuliza kama yupo sawa!ย
“Hakikisheni Dawson anauawa haraka iwezekanavyo” Yalikuwaย ndio maagizo pekee aliyoyatoa Rais kisha akarudi ofisiniย kwake.ย
Mzee Dawson, akiwa ndani ya Bajaji alitafakari mambo mengiย aliyoyafanya na Rais huyo, jinsi alivyotumika kwa ajili yaย Taifa, hakuwahi kufikiria kama Rais angelikuwa ndiye tatizo.ย Alijikuta chozi likimdondoka baada ya kulitazama begi hiloย ambalo lilikuwa na mwili wa mmoja wa Askari wake wa siriย sana, akapiga simu sehemu kisha akatoa maagizo fulani ya siriย ambayo ni lazima uwe kwenye mfumo wake ili uweze kuelewa,ย hata dereva bajaji aliachwa njia panda, kisha akageuza naย kumpigia simu Sande Olise.ย
“Sande ni lazima urejee Haraka sana” Alisema Dawson kishaย alikata simu bila kusikiliza jibu la Sande Oliseย
“Hapo kunja kushoto! Ukiona kibao cha kanisa simama”ย Alielekeza Dawson, mara moja Bajaji lilifuata maagizo kishaย likasimama.ย
“Pesa yako hii hapa” Dawson alitoa noti ya Elfu kumi naย kumpatia dereva kisha akamwambiaย
“Chenji itakusaidia”
“Asante sana Kaka!!” Dereva alisema kisha akaondoka zake,ย Dawson alikuwa amesimama mbele ya geti la kanisa hilo. Wakajaย Vijana wawili ambao walikuwa wamevalia nguo za kitawaย wakalibeba begi hilo huku Dawson akiwa anatokwa na machozi,ย akawafuata huku vijana hao wakionekana kujuwa nini chaย kufanya.ย
Walitembea na kuingia kanisani, wakasogea hadi kwenyeย maegesho ya magari, wakaweka begi chini kisha, mmoja akaingiaย kwenye gari moja iliyokuwa hapo maegesho, akalisogeza mbeleย kidogo alafu akashuka, Kijana aliyebakia akafunua kitambaaย cheusi ambacho kilikuwa chakavu sana, pakaonekana kuwa naย andaki fulani, akafungua mlango mdogo uliokuwa na hadhi yaย mlango wa kisima cha maji, pakaonekana kuwa na ngazi yaย kushuka chini, kisha mmoja akaingia na begi hilo huko chini,ย mwingine akafuatia kisha Dawson akamalizia, walipofanikiwaย kuingia humo, akaja Mwanamke mmoja ambaye naye alikuwaย amevalia nguo za Kitawa kisha akafunga ule mlango, akawekaย kile kitambaa chakavu na kusali, alipomaliza akaingia kwenyeย gari na kulirudisha pale lilipokuwa mwanzo, huwezi kugunduaย kuwa kulikuwa na watu waliozama Ardhini.ย
Walipofika chini, waliwasha taa ndani ya andaki hilo ambaloย Mzee Dawson alikuwa akilitumia kwa ajili ya kazi zake zaย siri, vijana hao walikuwa ni wanafunzi wake. Mmoja aliitwaย Chande na mwingine Kisko, walikuwa ni vijana ambao alitumiaย gharama zake Binfsi kuwasomesha na kuwapeleka mafunzoniย Nchini Korea, walijiingiza Katika kanisa hilo ili wawezeย kufanya kazi na Mzee Dawson.ย
Andaki hilo lilichimbwa muda mrefu kabla ya Mzee Dawsonย kufadhili ujenzi wa kanisa hilo. Ilikuwa ni siri kubwa sanaย na Watu wengi hawakujua kama kanisani kulikuwa na andakiย lililotumika kufanyia kazi za Kijeshi, Mwanamke aliyekujaย kuziba pale juu alikuwa ni miongoni mwa Watoto ambaoย walipoteza Wazazi wao kutokana na visa mbali mbali,ย aliwachukua na kuwafundisha kazi za Kijeshi, Mwanamke yuleย aliitwa Jesca. Huyo ndiyo Mzee Dawson.ย
Huzuni ilikuwa imetanda ndani ya andaki hilo, Chande na kiskoย walimpa pole Dwson kwa kumpoteza rafiki yake Kipenzi naย Askari wake wa Siri aliyefanya naye kazi kwa muda mrefu, Zolaย alijulikana kama Polisi wa kawaida lakini nje alikuwa niย komando mwenye mafunzo ya Kijeshi na kijasusi.ย
Saa ya Dawson ilikuwa ikilia kushiria kuwa eneo hilo lilikuwaย kimya sana, Chande akaenda kufungua mlango mmoja ambaoย ulionekana kufungwa muda mrefu sana, wakaingia huko wakiwa naย begi, ndani ya chumba hicho kulikuwa na Makaburi matatuย lakini kulikuwa na mashimo mengine mawili ambayo yalionekanaย kuchimbwa muda mrefuย
Dawson akatoa amri ya kufunguliwa kwa begi hilo, hata akinaย Chande walijawa na maumivu ndani ya mioyo yao, Zola alikuwaย amekufa, wakamzika kwemye moja ya mashimo yale lakiniย lilikuwa limebakia shimo moja, Kisko akaulizaย
“Mkuu Mashimo manne yamepokea Watu, bado moja. Kwaniniย ulichimba matano?” Dawson alicheka kwa maumivu kisha akamjibuย Kiskoย
“Marafiki hukaa pamoja, hawa ni marafiki zangu pekeeย niliokuwa nawategemea katika Maisha yangu, wote wameniacha,ย hilo shimo moja ni kaburi langu mwenyewe” Chande na Kiskoย walimtazama Mzee Dawson kwa jicho lililojaa huzuni sana kishaย akawaambiaย
“Muda wangu ukifika mtanifukia hapo kisha mtaharibu kila kituย hapa, hamtaishi tena kanisani, mtakuwa huru kuyatumikiaย Maisha yenu, mna muda mchache sana wa kuendelea kuwa pmoja naย Mimi, nifuateni” Dawson alikaza sura yake kisha akaelekeaย mahali huku vijana wake wakimfuata huko.ย
Akafika mahali akasimama akawaambiaย
“Mwisho wa mtawala katili umefika, nawapa kazi ya kumfutaย haraka sana”ย
“Mtawala gani huyo?” Dawson akafunua Shuka sehemu ambakoย kulikonekana kuwa na mitambo mingi sana, akawasha Projektaย kisha akawaonesha picha ya Rais wa Nchiย
Vijana wake wakashtuka sana sababu Kwa muda mrefu Dawsonย alikuwa pamoja na Rais huyo, Chande akaulizaย
“Tumfute Mkuu wa Nchi?”ย
“Hafai kupewa hicho cheo, yeye ndiye chanzo cha Mauwajiย yanayoendeelea kutokea hapa Nchini, anapaswa kulipa kwa damuย alizomwaga, anapaswa kulipa kwa Kifo cha Zola, kama sio Ujuziย wangu basi nami ningekufa kama Zola” Wakashusha Pumzi zaoย kisha mmoja akaulizaย
“Tutaweza vipi kumfuta Mtu mwenye Ulinzi mkali, Mtu ambayeย anaishi Ikulu, Mtu mwenye jeshi?”ย
“Yupo atakayewasaidia”ย
“Nani huyo?”
“Anaitwa SANDE OLISE”ย
“Ndio Nani huyo?”ย
“Nalazimika kuvunja kanuni nilizowawekea, sikuruhusu Maย Ajenti kufahamiana lakini imenibidi, huyo ni P045 Olise”ย
“Familia inaungana” Alisema Kisko kisha wakampa salutiย Dawson, aliwatengeneza vijana wake kujuwa kuwa Ajenti wake niย Familia yao.ย
Jioni ya siku hiyo, katika Ukumbi wa Maktaba maarufu yaย vitabu iliyopo katikati ya Jiji, Rais alikutana na John Brainย kwa ajili ya mazungumzo, walitazamana kwa sura mbili hukuย kila mmoja akiwa na silaha inayomlinda, John Brain alikuwaย ameongozana na Malaika wakati huo Six akiwa kwenye moja yaย majengo akiwa ameweka Ulinzi kwa kutumbia Bunduki, alikuwa naย sifa nzuri sana ya Ulengaji wa shabaha kitu ambacho kilikuwaย kikimpa sifa na Umaarufu Mkubwa kwa John Brain, taa nyekunduย iliyoashiria kuwa Rais alikuwa akilengwa na Bunduki iligongaย kwenye kifua, huku John Brain akiwa ana tabasamu, walinzi waย Rais walipogundua hilo wakataka kuingia kazini lakini Raisย aliwazuia sababu alihitaji zaidi kuzungumza na John Brain.ย
Akaamuru Walinzi wake watoke nje kisha Kamwambia John Brainย
“Haina haja ya kuwindana, sisi ni marafiki John, badoย nahitaji kufanya kazi na nyie” Alisema Rais kisha akatoaย picha kutoka katika mfuko wake wa koti jeusi lililomshikaย vizuri,ย
“Huyo anaitwa Dawson! Ni mmoja wa Askari wa kutumainiwa zaidiย hapa Nchini, nahitaji mumpoteze sababu kuendelea kuishi niย sawa na Kuyaweka Maisha yangu rehani” Akasema Rais, Johnย Brain akaivuta picha hiyoย
“Namjuwa huyu nimewahi kumuona” Akasema Malaika kisha woteย wakamtazamaย
“Kama siyo huyu basi Zola alikuwa anakufa kwa mikono yangu”ย
“Hata hivyo Zola ameshakufa, aliyebakia ni huyo Mtu,ย anahitajika kumfuata Zola alipo haraka iwezekanavyo”ย Aliongeza Rais kisha picha ya Dawson ikarejeshwa mikononiย mwakeย
“Malipo kwanza kisha umuachie Mtu wangu ndipo kazi yakoย itafanyika, vinginevyo Nchi yako itatangaza Mlipuko waย Ugonjwa wa Ebola ndani ya wiki moja, Raia Watakufa kama Kuku, utakuwa ndio mwisho wa utawala wako” Akasema John Brain akiwaย amemtumbulia macho Raisย Comments zikiwa 100 naachia ya 8 leoleo
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABAย USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xxย
45 Comments
Zola amekufa daaah..๐ข
Unyama sana vita ya akil ila daah rip kamanda zola
Dah inaumiza na inasismua sana
Inshallah zitafika 100
Let’s continue
Zolaaa ๐ญ๐ญ
Jaman mambo ni mazito kwelikweli
Mfumo wa viongozi wengi ndo ulivyo dash hakika ni hatarii
โ
๐ญ๐ญzola
Lete kazi tajiri
Bado tu hazjafika comment 100
Zola ameishia dah
Pameanza kuchangamka sasa
Ndugu admini utengwe siyo kwa weredi huu wa kuteka akili zetu
Ya mia hii๐
Maskini Zola,๐ญ๐ญ๐ญ
Zola kaenda du
Congratualuons admin
Noma sana
Ya 99 hii hapa๐๐๐
Congratulations admin your are so talented
Olise is coming
Hatar ila Zola jaman
Duuuh
Mmmmmmh hatari
Jmn mbona Zola kafa kama utani vile๐ฅน๐ฅบ
Mpka chozi limenitoka
RIP kamanda ZOLA
๐ญ๐ญ๐ญ
Oyaaaaaa n ebiatar
Kimeniuma Zola kufa jamanii
Story moja tamu sana…ila zola daa ameondoka mapema sana
Zola why dah
Zola mbna naumia kama ukweli vile
Nzuri
Dah! Zola umeondoka hivi tunakuona jmn . Haya Sasa .sande njoo ingiaa kzn
Zola ameniuma๐ญ
Admin hongera sn unaweza alafu unaweza TN .Dah isiishe jmn
Ameniuma san zola๐ญ๐ญ
Jaman Zola sikuegemea Kama mwisho wake utakuwa hvyo ๐ข๐ข
๐ญ๐ญ๐ญ๐ญSasa Zola amekufaje jamani
Zola kafa mtu shupavu ,nasubiri mziki wa Sande Olise na vijana wa Dawson
Daah
Sasa picha ndio kwanza inaanza mzee Dawson fungua ukurasa mpya karibu sande olise
Daaaaah,aiseee kali xna hii simulizi
pta25q