Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Jasusi Sehemu Ya Tatu (03)
    Hadithi

    Jasusi Sehemu Ya Tatu (03)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 29, 2024Updated:December 1, 202414 Comments10 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Unatakiwa kuwa makini sana sababu kwa namna alivyo huyo MtuΒ  si rahisi akamuamini Mtu kwa Mara ya kwanza, unapaswa piaΒ  kujuwa kuwa ukibainika basi kila kitu kitaharibika. Zola niΒ  Jasusi mbobezi, kabla hujampeleleza anakuwa tayariΒ  amekupeleleza.” Alisema John Brain, kisha Malaika kasema

    “Zola anatumika kama Mwanvuli wa Serikali katika kutekelezaΒ  mipango ya siri, najiuliza aliwezaje kukwepa mtego wa Bomu” EndeleaΒ 

    SEHEMU YA TATUΒ 

    Yalikuwa ni maswali waliyoulizana, Muda huo Inspekta ZolaΒ  alikuwa kwenye gari yake akiwa anaelekea nyumbani kwaΒ  Marehemu Robert. Kichwani akiwa na mawazo lukuki akajikutaΒ  akimfikiria Msichana aliyeuwa polisi katika kituo cha polisiΒ  tena kwa Ustadi ambao hata Komando asingeliweza kufanya.Β  Akatikisa kichwa chake kisha katabasamu tuuΒ 

    Akaanza kuvuta picha namna Msichana yule aliyejitambulishaΒ  kama Judith alionekana, alikuwa mwembamba, mweupe na mwenyeΒ  sura ya upole sana. Pasipo kujuwa kuwa picha aliyokuwaΒ  akiiwaza Zola haikuwa halisi kwani, hakuitwa Judith baliΒ  alikuwa akiitwa Malaika, sura ile haikuwa halisi.Β 

    Alikanyaga mafuta bila kujuwa alikuwa akiwindwa sana auawe,Β  dakika Thelathini na tano baadae alikuwa akiegesha gari lakeΒ  katika uwa wa nyumba ya Robert. Huzuni ilikuwa imetanda sana,Β  Mama Robert alipomuona Zola alimtambua kama Polisi aliyekuwaΒ  akifwafilia tukio la vifo vile, akamkimbilia na kumwambiaΒ 

    “Mnipe mwili wa Mwanangu nimzike, Mnipe mwili nawaomba sana”Β 

    “Mama hebu tulia, nimekuja kwa ajili ya kuzungumza na wewe.Β  Hebu futa machozi Mama” Alisema Inspekta Zola akiwa amemshikaΒ  mabega Mama RobertΒ 

    “Hebu tuongee vizuri” Zola akapepesa macho yake, kulikuwa naΒ  Watu wengi pale Msibani akaona sehemu ambayo ilikuwa tulivuΒ  bila Watu, akamsogeza Mama yake Robert hukoΒ 

    “Mama hebu nieleze vizuri tukio lilitokeaje? Kuna utata sanaΒ  katika jambo hili” Alisema Zola huku akiwa makini kutakaΒ  kusikia ambacho Mama Robert angesemaΒ 

    Mama Robert akajifuta chozi na kujituliza kidogo kabla yaΒ  kumsimulia ZolaΒ 

    “Tulikuwa kanisani wakati tunasubiria ndoa iweze kufungwa,Β  ili Mwanangu Robert amuowe Sandra. Nilishtuka kusikia mlio waΒ  Risasi, nilipogeuka nikamuona Mwanangu akiwa ameshikiliaΒ  Bastola huku miili miwili ya Bosco na Sandra ikiwa chini,Β  katika hali ya taharuki kila mmoja akipiga kelele za woga,Β  Robert aliubeba mwili wa Sandra na kuondoka nao akiwa analia”Β  Mama Robert alianza kulia kwa uchungu hadi Inspekta ZolaΒ  alijikuta akidondosha chozi lake kwa jinsi ambavyo MamaΒ  Robert alikuwa akilia kwa uchungu.

    “Naomba msaada wako niipate maiti ya Mwanangu Robert iliΒ  nimzike Mimi”Β 

    “Sawa! Mwili wa Robert utaupata baada ya kumaliza uchunguziΒ  ambao kwa asilimia kubwa naweza kusema Umeisha, nisaidieΒ  namba ya Mama Sandra ili niweze kuzungumza nae”Β 

    Zola akapewa namba akaelekezwa anapoishi Mama Sandra,Β  akamuaga Mama Robert kisha akaingia kwenye gari yake ambayoΒ  ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuzuia risasi kuingia, gariΒ  hili lilinunuliwa na Mzee Dawson kwa ajili ya kazi zaΒ  kipelelezi.Β 

    Mwendo wa dakika arobaini na nane, Zola alikuwa ameshafikaΒ  alipoelekezwa, haikuhitaji sana ujuzi wa kutambuwa kuwa eneoΒ  hilo lilikuwa na tatizo licha ya ukimya na uchache wa WatuΒ  uliopo pale. Zola akajipenyesha hadi Ndani ambako Mama SandraΒ  alikuwepo lakini kabla hajafika huko alikutana na Baba SandraΒ  ambaye alimtambua Zola kabla hata hajajitambulisha.Β 

    “Umefanikiwa kujuwa chanzo cha kifo cha Binti yangu?”Β  Aliuliza Baba yake Sandra ambaye alikuwa na umri sawa na ZolaΒ 

    “Ngoma ngumu lakini tutafikia tamati hivi karibuni”Β 

    “Tutashukuru sana ili tuweze kumpumzisha Sandra katika nyumbaΒ  yake ya milele na hayo mengi tutayaachia jeshi la Polisi”Β 

    “Usijali! Nimekuja kuzungumza kidogo na Mama Sandra, hapanaΒ  shaka yupo Kushoto chumba cha mwisho” Alisema Inspekta ZolaΒ  huku akiachia tabasamu la kaziΒ 

    “Jicho lako la kipelelezi liko sahihi Afande, nenda tuuΒ  kazungumze nae” Zola aliposikia kauli ya utii namna ileΒ  aliona amtamzame Mzee huyo Usoni pake, akahisi jambo lakiniΒ  akaliweka kiporo kichwani pake. Hata alipokaribia mlango waΒ  chumba alichopo Mama Sandra aligeuka na kumuona Baba yakeΒ  Sandra akiwa bado anamfwatilia Zola kisha alipoona ZolaΒ  amegeuka akajifanya kuondoka pale. Zola akagundua jamboΒ  fulani, akabisha hodi kisha akaruhusiwa kuingia chumbaniΒ 

    “Pole Mama! Samahani naomba wote mtoke ili nizungumze na MamaΒ  Robert, Naitwa Inspekta Zola” Alisema kisha akatoaΒ  kutambulisho, Watu walioko mle waliondoka taratibu huku ZolaΒ  akipata nafasi ya kuangalia picha iliyopo Ukutani, ilikuwa niΒ  picha ya Sandra akiwa shuleniΒ 

    “Hapana Shaka huyu ni Sandra katika umri wa ukuaji wake?”Β  Alihoji Zola huku akiendelea kuiangalia, Mama SandraΒ  akaitikia kwa masikitiko

    “Ndio…Ameondoka nikiwa namuhitaji Mwanangu” AliposemaΒ  alijikuta akianza kulia upya ni kama vile aliweka chumviΒ  kwenye kidonda kibichi, Zola alisogea kisha aliketi chini kwaΒ  mtindo wa kufunga miguu yake kama Waislam wakaavyo.Β 

    “Mwanao alipaswa kuolewa na Robert, lakini Huyo RobertΒ  aliondowa uhai wake kabla hata ya harusi. Unafahamu nini katiΒ  ya hawa Watu watatu yaani Bosco, Robert na Sandra Mwanao”Β 

    “Sandra alifahamiana na Robert muda mchache sana ndipoΒ  akasema anataka kuolewa, lakini Robert na Bosco inasemekanaΒ  ni marafiki wa muda mrefu sana”Β 

    “Vifo vyao unaweza ukahisi vinatokana na nini Mama?” MamaΒ  Sandra alitikisa kichwa chake kisha akasemaΒ 

    “Ni ngumu sana kwa jinsi ambavyo walikuwa wakija hapa naΒ  kuongea kwa furaha sana, sijui nini kimesababisha haya yote”Β 

    “Asante Mama! Hii ni namba yangu ukipata chochote nijuze,Β  mtapewa mwili wa Sandra kwa ajili ya maziko huku uchunguziΒ  mwingine ukiendelea” Zola alijizoa na kuondoka pale hukuΒ  akili yake ikianza kumtafakari Baba yake Sandra kwaniniΒ  alikuwa akimtazama sana?Β 

    Akiwa kwenye gari Zola alionelea aelekee Hospitali ambakoΒ  miili ile ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi, alipofika alikutanaΒ  na mtaalam wa Maabara kutoka katika kitengo cha MPA Cha MzeeΒ  Dawson akamwambia kuwa ile miili miwili ipelekwe kwa wahusikaΒ  kwasababu ni miili halali ya wahusikaΒ 

    Zola aliondoka Hospitali na kuelekea katika makazi yake yaΒ  siri ambayo Watu wengi walikuwa hawayafahamu, wakati anafikaΒ  akakumbuka kuwa ujumbe wa picha ulikuwa umeshatumwa, akaingiaΒ  chumba cha siri kwa ajili ya kufanya alichokusudia, alihitajiΒ  kujuwa ule mwili bandia ni wa nani. Akaingiza picha katikaΒ  mashine yake ya Kazi akapata majibu yaliyomfanya afungeΒ  safari nyingine kuelekea Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mifupa.Β 

    “Namuulizia Anastanzia Nyange” Aliuliza Zola akiwa ameketiΒ  mbele ya Mkuu wa Chuo hicho ambaye macho yake yalikuwaΒ  yametua kwenye sura ya ZolaΒ 

    “Anastanzia Nyange?” Aliuliza Mkuu wa Chuo ambaye alikuwa naΒ  kitambiΒ 

    “Ndio, picha yake hii hapa” alimuonesha picha

    “Ameenda Field na wanachuo Wenzake Kaskazimi Mashariki mwaΒ  Mkoa jirani”Β 

    “Ok asante” Zola aliondoka pale, nyuma yule Mkuu wa ChuoΒ  akanyanyua simu ya mezani akapiga sehemu akaisikilizia hadiΒ  ilipopokelewa kisha akasemaΒ 

    “Amekuja hapa muda sio mrefu anamuulizia Anastanzia Nyange”Β  Aliposema hivyo hakuhitaji kusikiliza sauti kutoka upande waΒ  pili akakata simu kisha akaweka mikono yake juu ya meza hukuΒ  akionekana kuzama katika tafakari nzito sana.Β 

    Zola kabla hajaondoka pale Chuoni alikutana na MwanachuoΒ  mmoja akamuuliza kama anamfahamu Anastanzia, yule MwanachuoΒ  akamwambia Zola kuwa anamfahamu Anastanzia lakini hakuonekanaΒ  hapo chuoni kwa siku saba. Zola akajitambulisha kuwa niΒ  polisi akamuomba Yule Mwanachuo amueleze mahali ambapoΒ  Anastanzia alikuwa akiishiΒ 

    “Anaishi na Rafiki yake sio mbali sana ni nyuma ya HoteliΒ  mpya ya Sub Marine, ukifika utaona jengo la Njano lina vigaeΒ  ndio hapo hapo”Β 

    “Asante sana” Zola alifunga safari nyingine ya kuelekea hukoΒ  alipoelekezwa, alitumia dakika ishirini pekee kufikaΒ  akakutana na Mtu nje ya nyumba hiyo hapana shaka alionekanaΒ  kuwa mwenyeji hapo, Zola akamuulizaΒ 

    “Nimemkuta Anastanzia?”Β 

    “Salimia kwanza, waungwana husalimia sasa unapouliza tu HataΒ  hujui unayemuuliza kama ni Mzima au la” alifoka Mtu huyoΒ  ambaye alikuwa ni Msichana wa Makamo tuu.Β 

    “Samahani! Namuulizia Anastanzia”Β 

    “Chumba chake kile pale” alioneshwa kisha Zola akashukaΒ  kwenye gari na kuelekea kubisha hodi.Β 

    Kiatu cheusi cha Zola kilikuwa kinang’aa na kumfanya msichanaΒ  huyo kujuwa kuwa Mwanaume huyo alikuwa na pesa sana, kishaΒ  akapeleka macho yake kwenye gari ya Zola kisha akaingiaΒ  chumbani kwake.Β 

    Muda huo zola alikuwa akibisha Hodi huku macho yake yaΒ  Kijasusi yakiangaza huku na kule, ukimya uliomuitikia ulimpaΒ  wazo la kujaribu kufungua pale ili aweze kuchunguza vizuri,Β  akarudi kwenye gari yake kisha akafungua begi dogo akatoaΒ  rundo la funguo za Bandia, akachagua ambayo iliendana naΒ kitasa cha pale Mlangoni. Akarudi mlangoni na kufunguaΒ  taratibu sana bila hata sauti ya kufungua kusikika, sekundeΒ  chache akajikuta amefanikiwa kuingia ndani. Alikuwa makiniΒ  sana, sehemu hiyo ilikuwa na chumba na sebule.Β 

    Muda huu alikuwa pale sebleni, palionekana kuwa tulivu sanaΒ  huku feni ikiwa inaendelea kupepea, ilimfanya aamini kuwaΒ  kulikuwa na Mtu aliyekuwa akiishi pale, akili yakeΒ  ikayakumbuka maneno ya yule mwanachuo kuwa Anastanzia alikuwaΒ  akiishi na rafiki yake, Zola alimuhitaji zaidi huyo rafikiΒ  yake sababu alishafanikiwa kujuwa kuwa Anastanzia amekufaΒ  katika lile tukio kule kanisani, akanyata taratibu aliposikiaΒ  mlio wa simu ukilia kutokea chumbani, akapinda mkonoΒ  akachomoa Bastola yake yenye kiwambo cha kupoza sauti yaΒ  risasi itokapo.Β 

    Akageuka nyuma kuhakiki kuwa hakukuwa na Mtu pale sebleni,Β  kisha akaanza kuelekea chumbani ambako ile sauti ya simuΒ  kuita ilikuwa ikiendelea kusikika. Akameza mate taratibu hukuΒ  kijasho cha umakini kikiendelea kutiririka katika paji lakeΒ  la Uso, Kisha kwa mwendo wa haraka akaingia chumbani hukuΒ  akiangaza Bastola yake huku na kule, kitandani aliona MtuΒ  akiwa amelala huku sura ya huyo Mtu ikiwa inatazama ukutaniΒ  na kumpa wakati mgumu Zola kujuwa ni nani aliyelala pale,Β  taswira ilionesha ni Mwanamke kisha akili na moyo wa ZolaΒ  ukajipa tumaini la kumpata rafiki wa Anastanzia ambayeΒ  anaweza kuwa Mwangaza wa kumpa mwanga Zola kuhusu kesi ile yaΒ  Utata sana iliyoibua taswira ya nani alihusika na kifo chaΒ  Makam wa Rais..Β 

    Bastola ikiwa mbele Zola alionekana kuwa makini huku akizidiΒ  kusogea karibu na Mtu huyo ambaye hakumtambua hadi muda huo,Β  alipomfikia akamgeuza kwa kutumia bastola yake, mambo hayaΒ  aliyafanya akiwa na unri wa miaka zaidi ya 50 sijui alipokuwaΒ  kijana Zola alikuwa hatari kiasi gani kwenye upelelezi wake,Β  akashusha miwani na Bastola yake taratibu akapelekea kidoleΒ  eneo la shingo kisha kwenye pua, ubaridi wa Mtu huyoΒ  ulionesha kuwa alikuwa amekufa muda mrefu sana, povuΒ  ililikuwa likimtoka puani, alipomchunguza vizuri aliona ileΒ  alama ya vidole kwenye paja la Marehemu.Β 

    “Shit!” Alisema huku akili yake ikimpa majibu kuwaΒ  waliohusika na matukio ya kikatili, waliomuuwa Makam wa RaisΒ  ndio waliosababisha kifo kile, haraka Zola akachukua simuΒ  yake na kumpigia Mzee Dawson ambaye alimpa kazi ile iliyojaaΒ  utata sana, Simu hiyo ilipokuwa ikiita Mzee Dawson alikuwaΒ  akistarehe na Msichana mmoja nyumbani kwake, alipoona simu yaΒ  Zola akaacha kisha akamwambia Msichana huyo avae aondokeΒ  haraka. Mzee Dawson akajitupa kitandani akiwa hoi kishaΒ  kapokea simu ya Zola

    “Unasemaje Zola?” Aliitika Mzee Dawson kwa sauti ya uchovuΒ  sanaΒ 

    “Unapaswa nawe kuingia kazini, vinginevyo mambo yanawezaΒ  kuharibika kabisa. Nilikuwa nafuatilia kuhusu vifo vya utataΒ  vilivyotokea kanisani, mmoja wa Watu ambao wangeliweza kunipaΒ  Mwangaza wa kesi hii nimemkuta akiwa amekufa nyumbani kwake,Β  Watu hawa wapo macho na wananifuatilia”Β 

    “Nilikueleza kuhusu hilo Zola, nilikupa pia msaidizi iliΒ  akusaidie lakini cha ajabu hutaki kuwasiliana naye kabisa,Β  unataka niingie kwenye majukumu hayo?”Β 

    “Dawson unajua fika huwa simuamini Mtu katika mambo yangu,Β  napenda kufanya kazi mwenyewe lakini hili linahitaji utulivuΒ  zaidi kitu ambacho maadui zetu hawataki kunipa”Β 

    “Aaaah Zola” ilisikika sauti upande wa Mzee Dawson, ikioneshaΒ  alikuwa akijigeuza.Β 

    “Hebu fanya taratibu tuonane ana kwa ana Mzee Dawson, nahisiΒ  kuchanganikiwa sasa” Zola alikata simu bila kusikiliza sautiΒ  ya Mzee Dawson, baada ya hapo akapiga simu sehemu nyingineΒ  ndani ya kitengo cha siri cha Mzee Dawson kinachoitwa MPA,Β  akaomba madaktari waweze kufika eneo la tukio, akawapa RamaniΒ  kamili lilipo eneo hilo.Β Β 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNEΒ  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ 

    Β Β 

    jasusi riwaya za kijasusi

    14 Comments

    1. G shirima on November 29, 2024 2:29 pm

      Mimi wa kwanza kusoma kazi nzur sana

      Reply
    2. Charz jr😎 on November 29, 2024 2:30 pm

      ✌️✌️

      Reply
    3. Abdurazack Hassan Mzale on November 29, 2024 3:30 pm

      Nzuri

      Reply
    4. Verena on November 29, 2024 3:50 pm

      Ngoma ngumu✍️✍️✍️

      Reply
      • Hamic on November 30, 2024 8:13 am

        Kama nimeielewa ivi

        Reply
    5. Jonathan Mushi on November 29, 2024 4:01 pm

      Bonge moja la kazi

      Reply
    6. Victor on November 29, 2024 4:24 pm

      Kazi Iko poa japo mmmmh

      Reply
    7. Cathbert on November 29, 2024 5:20 pm

      Iko poa sanaaaaa

      Reply
    8. Kikoba kitira on November 29, 2024 6:14 pm

      Noma sana

      Reply
    9. KingSam4321 on November 29, 2024 8:34 pm

      Kali sana

      Reply
    10. Given Gihsy on December 1, 2024 4:21 pm

      kama mimi tu navurugwa na mkasa huu je huyo zola😏, hapo kijiwen niπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ’―πŸ’―

      Reply
    11. Neema on December 1, 2024 5:54 pm

      Hatari sana

      Reply
    12. Fawziya Hassan on December 6, 2024 11:43 am

      Akakunja miguu kama wakaavyo Waislam 😊

      Reply
    13. Rogy on December 6, 2024 10:33 pm

      No!aaa sana

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi October 1, 2025

    In the name of LOVE – 12

    Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE Moyo Wangu na…

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.