Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Love & Pain Sehemu Ya Tisa (09)
    Hadithi

    Love & Pain Sehemu Ya Tisa (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 21, 2024Updated:November 25, 202410 Comments10 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “muda siyo mrefu sana alikuja na gari akasema umemuagiza na  alikuwa akijuwa hadi lilipokaa nikamiami, ina maana hukumtuna  Mtu?” aliuliza Mama Noela kwa mshangao, Noela hakujibu  alitoka akapanda gari kisha akaanza kumtafuta huyo Mtu,  alipita mitaa mbali mbali bila mafanikio yoyote yale hadi  alichoka. 

    Aliamuwa kurudi nyumbani, ndipo alipogundua huwenda kulikuwa  na jambo zito lilifanya Lucia auawe, akafikiria atapata vipi  kujuwa alichokuwa anatakiwa kufanya. Endelea  

    SEHEMU YA TISA

    Alitafakari kwa muda mrefu sana kisha akafungua Whatssap yake  akakumbuka kuna jumbe alizokuwa ametumiwa na marehemu Lucia  ila alikuwa hajazifungua. 

    Alikutana na Ujumbe wa sauti, alifikiria kusikiliza ujumbe  huo ila moyo wake ulijawa na woga akahofia kuijuwa hiyo siri  iliyopelekea kifo cha Lucia, basi akajipa moyo akakaza roho  yake. Alishtuka sana aliposikia sauti ya Desmond akizungumza  na Lucia tena wakionekana kujuwana kabisa. Alisikia maongezi  hayo yakisema 

    “Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone Mke  wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu na  ninekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaa  sawa” Alisema Desmond 

    “Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwa  katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndani  ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya miezi  mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodi  wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia 

    “Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tu  tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumia  mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond kwa  sauti ya kilio 

    “Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wako  usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa na  Mwanasheria” Alisema Lucia, 

    “Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wangu  kuhamishwa?” aliuliza Desmond 

    “Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujui  ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakalo  kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yote  kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakuja  kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenye  kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambia  Desmond 

    “Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenzi  mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada ya  kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawa  pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweli  utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia

    “Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema”  Alisema Desmond 

    Yalikuwa ndiyo maneno yaliyosikika, Lucia alichoka mwili na  akili alijikuta akikaa chini kama mzigo 

    “Joshua wewe ni Desmond? Umemuuwa Lucia? Una Mke Joshua?”  Alisema kwa suati ya chini iliyojaa mihemo ya kuchanganikiwa,  Ni mwanaume aliyetoka kumvisha pete siku iliyopita tu lakini  leo anagundua siri nzito za Mauwaji 

    Chozi lilimbubujika Noela, aliangalia kidole chake kilicho na  pete, 

    “Joshua…..Desmond…Una Mke ee!!” alisema kwa  kuchanganikiwa Noela 

    “Kwanini sikukusikiliza mapema Lucia, nisingefikia uamuzi huu  mbaya zaidi katika Maisha yangu” Alisema Noela, alijikaza  sababu ni Mpelelezi na mwanasheria Mkubwa tu Nchini, aliwaza  kisomi zaidi nini afanye 

    Akasikiliza tena huku moyo ukimuuma na chozi likimvuja, kisha  akakumbuka alipoenda kuangalia mwili wa Marehemu Lucia  alipelekwa pia kwa Mgonjwa wa Lucia, aliunganisha maelezo  akapata picha kamili huwenda mgonjwa wa Lucia ndiye Mke wa  Desmond…PATAMU HAPO!! 

    Alifuta chozi lake akaivaa elimu yake ya kipelelezi japo bado  moyo ulimuuma sana Noela, alitoka chumbani akakutana na Mama  yake, hakutaka Mama yake ajuwe chochote kile ila Mama Noela  alihisi Mwanaye alikuwa akilia>>>>>>>>>>>>>> 

    “Ulikuwa unalia?” alihoji Mama Noela 

    “Mama kuna rafiki yangu amefariki” Alisema Noela “Mmh! masikini pole sana, unaenda msibani?” 

    “Ndiyo Mama” Basi waliachana hapo, Noela aliingia kwenye gari  kwa ajili ya kuelekea Hospitalini. 

    Hakutaka kupokea simu za Desmond sababu alijisikia vibaya  sana kutokana na alichokisikia hivyo alihitaji zaidi kupata  uhakika wa mambo, moja kwa moja alienda hadi kwa Mkuu wa  Hospitali hiyo. Alimuuliza kuhusu Mgonjwa wa Lucia 

    “Mgonjwa hali yake bado haijakaa sawa lakini tunajitahidi  kuhakikisha anaamka, yapo mambo ambayo Lucia alikuwa  akiyafuatilia kuhusu Mgonjwa..” alisema Dktari

    “Mgonjwa anaitwa Nani?” aliuliza maana kwenye ile sauti  alisikia kuwa anaitwa Mandy 

    “Mgonjwa anaitwa Mandy Desmond” 

    “Huyo Desmond ni Mume wake?” alihoji Noela kwa kujikaza sana  alitamani alie 

    “Ndiyo ni Mume wake wa ndoa” 

    Noela alimuonesha Daktari picha ya Desmond kwa kutumia simu “Ndiyo huyu Mume wake vipi unamjuwa?” alihoji Daktari “Hapana naifanya kazi yangu tu” 

    “Ooh! alafu kama sikosei yupo wodini, twende ukazungumze naye  huwenda ana la kukwambia” Alisema Daktari huyo akionekana  wazi kuwa alifahamu baadhi ya Mambo ila hakutaka kujiingiza  matatizoni baada ya kifo cha Lucia 

    Noela na Daktari waliongozana hadi wodini lakini bahati mbaya  Desmond alikuwa ameondoka wodini hapo muda mchache uliopita,  Noela alifanikiwa kuujuwa ukweli, pale pale aliingia yule  Polisi aliyekuwa akifuatilia hali ya Mandy, Alifahamiana na  Daktari wakasalimiana lakini pia alifahamiana na Noela sababu  alikuwa mpelelezi mzuri sana. 

    “Oooh Noela uko hapa, salam yako” Alisema Polisi huyo 

    “Hapana shaka unapeleleza juu ya kifo cha nesi wa mgonjwa”  Alisema polisi huyo 

    “Ndiyo! wewe umekuja kufanya nini hapa?” aliuliza Noela 

    “Huyu Mgonjwa ni Mtu ninayesubiria aamke ili anipe siri ya  kifo cha Mama yake” Alisema Polisi, Noela alishtuka sana 

    “Kuna kifo tena katika ugonjwa wake?” 

    “Ndiyo! kabla ya kukutwa na kilichomkuta alikuwa akiijuwa  siri ya kifo cha Mama yake, hivyo kuamka kwake kutafungua  kesi upya japo ni kesi ngumu sana” alisema polisi huyo na  kumuacha Noela akiwa njia panda, hakujuwa ashike lipi aache  

    lipi kila alilolisikia lilimpa stori mpya kichwani pake  akajiuliza haraka 

    “Kama Noela ameuawa na Mume wa Mandy maana yake ameuawa  kwasababu kuna jambo lilipaswa kufichwa, ina maana Desmond alimuuwa Mama yake Mandy! mbona nachoka” Alijisemea kisha  aliangusha tabasamu lenye maumivu makali sana ambayo si  rahisi mwingine akafahamu. 

    “Haya sawa” alijibu Noela kisha alitoka hapo, alienda nyuma  ya Hospitali alilia sana, aligundua Mwanaume aliyempenda  alikwua Muuwaji na Muongo, alijipa moyo na tumaini kuwa  atashinda kila jambo 

    Tuachane na kule Hospitalini, Mchana ulikuwa umeingia,  Desmond hakuwa na hili wa lile kuwa Noela alikuwa amesha  fahamu siri zake, alijaribu tena kumpigia Noela huku akiwa na  Mwanasheria wake wakiwa ndani ya gari wakijiandaa kuelekea  Hotelini. 

    Simu hiyo haikupokelewa kabisa 

    “Au amepata taarifa ya kifo cha rafiki yake imemchanganya?”  alihoji Mwanasheria Joel 

    “Sina hata ninalolifikiria kwasasa Joel, naona mambo yanazidi  kuwa magumu” Desmond aliwasha gari wakiwa na kitabu cha Hundi  ya fedha ambacho waliambiwa na Yule Mwanaume waende nacho  Hotelini 

    “Vipi umejaribu kumpigia Mtu wa tatu?” alihoji Desmond 

    “Naambiwa Namba haipo, huwenda anatumia simu kwa nyakati  anazohitaji yeye mwenyewe. Desmond alikanyaga Mafuta kuelekea  Hotelini wakiwa na tumaini kuwa wanaenda kujisafisha bila  kujuwa bomu jipya lilikuwa limelipuka. 

    Walifika Hotelini kwa muda walioambiwa kisha walielekea  Kwenye chumba walichoelekezwa, waliamini watamkuta Mwanaume  huyo, walipofungua mlango walikutana na sanduku lililoibwa  kwenye chumba cha Noela, sanduku hilo Desmond alikuwa  akilijuwa alishtuka sana 

    “Hili ni sanduku la Noela, limefikaje hapa wakati  nililitafuta sana ili kuipata ile bahasha” Aliuliza Desmond,  walikagua chumbani humo na kujiridhisha kuwa hakukuwa na Mtu  yeyote, walipogusa mlango wa sanduku hilo dogo waliona  unafunguka kirahisi, sasa wakakutana na ile bahasha yenye  siri nzito sana. 

    Desmond na Mwanasheria Joel walizisoma nyaraka zilizo ndani  ya Bahasha hiyo, Desmond alikaa chini kwa kuchoka mno kisha  akamwambia Joel

    “Kama Noela atakuwa ameisoma hii Bahasha basi kila kitu  kimeharibika Joel” 

    “Kama angekuwa amesoma angekuuliza, kwanini hasemi chochote  hadi sasa?” aliuliza Joel 

    “Hajasema chochote lakini simu yangu hapokei tokea asubuhi  wakati Mimi ni Mume wake mtarajiwa, tumevishana pete jana tu.  Hapana shaka Anajuwa kitu fulani” Alisema Desmond kisha  alikunbuka kitu akasema 

    “Ni Nani huyu anayefahamu kila kitu?” aliuliza, kabla hata  hajapata jibu kutoka kwa Joel simu ya Desmond iliita, namba  iliyopiga ilikuwa ngeni kabisa machoni pake 

    “Pokea!!” alisema Joel huku akimuonesha kwa ishara Desmond  kuwa apokee haraka sana kabla haijakata, Desmond aliipokea 

    “Hello” Alisema Desmond huku simu ikiwa sikioni 

    “Desmond, mmeona kila kitu. Bahati iliyo njema ni kuwa Noela  hajui chochote hadi hivi sasa, laiti kama atagundua kuwa wewe  ni Muuwaji basi tegemea kuharibu kila kitu hata unachokitaka  hakiwezi kufanikiwa” Ilisikika sauti nzito ya kiume, sauti  hiyo haikuwa ngeni kwake ilikuwa ni sauti ya Mwanaume  aliyewaambia waende pale Hotelini 

    “Wewe ni Nani na unataka nini hasa?” alihoji Desmond 

    “Mimi ni Mr. Nobody ( Sijulikani ) kila wakati naokoa Maisha  yako sababu wewe ni mzembe sana Desmond, Hapana shaka umebeba  kitabu cha Hundi?” Alisema Mwanaume huyo aliyejitambulisha  kama Mr. Nobody 

    “Ndiyo lakini kwanini unafanya haya yote, unataka nini?”  Aliuliza Desmond 

    “Fuata nitakayokwambia, andika hundi ya Shilingi Milioni mia  tisa haraka sana kisha nitakuelekeza mahali unapopaswa  kuipeleka, ukifanya ujanja wowote ule Maisha yako yatakuwa  rehani sababu yapo mikononi Mwangu” Alisema Mr. Nobody,  Desmond alimtazama Mwanasheria wa Mke wake aliyeitwa Joel,  kisha alipewa ishara ya kuandika Hundi hiyo haraka sana ili  kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya Kampuni ya Mandy na  kupeleka kwa Mr. Nobody 

    Haraka Desmond akawa anaandika ile Hundi ili tu kujiweka  salama, lakini kwenye sura ya Mwanasheria kulijaa tabasamu  ambalo Desmond hakuliona, alipomtazama Joel alibadilisha sura 

    yake na kuwa ya hofu kama vile alikuwa akicheza mchezo mchafu  kwa Desmond. Baada ya kumaliza kuandika aliweka tena simu  sikioni 

    “Nimeshaandika, natakiwa kuipeleka wapi?” Aliuliza Desmond  baada ya kuwa ameshamaliza kuandika hundi hiyo yenye thamani  ya Milioni 900. 

    “Pembeni yako kuna Mwanasheria wa Mke wako mkabidhi hiyo  Hundi kisha Mwambie ailete Katika Baa ya Silva, nje ya Baa  ataiyona gari nyekundu, aiweke humo. Kumbuka anapaswa kwenda  peke yake” Alisema Mr. Nobody kisha alikata simu. 

    “Amesema nikupatie wewe Joel kisha utaipeleka Silva Baa,  utaona gari nyekundu utaiweka humo hii hundi. Nakuomba sana  Joel fanya kama alivyotaka” Alisema na kusistiza Desmond 

    “Amesema niipeleke Mimi? vipi kama akinidhuru huko, Mimi  naogopa Desmond” Alisema Joel. 

    “Sikia Joel acha woga nenda kaipeleke hii hundi, hakuna  kitakacho kupata laiti kama angekuwa na lengo la kukudhuru  amgekudhuru muda wote.” 

    “Haya sawa!” aliitikia Joel kisha walitoka hapo, nje alimpa  ile Hundi ili aipeleke huko ambako ilipotakiwa kufika, Joel  aliingia kwenye gari kisha akaondoka zake pale. 

    Wakati Joel anaondoka, simu ya Desmond iliita, aliyekuwa  akimpigia alikuwa ni Mchumba wake Noela, kwanza aliitafakari  hiyo simu kabla ya kuipokea maana alikuwa na hofu kubwa sana  juu ya mambo yao kugundulika, baadaye aliipokea 

    “Hello” Alisema Desmond 

    “Joshua naomba tuonane kwenye mgahawa muda huu” Alisema Noela  kisha alikata simu, Desmond alishusha pumzi zake baada ya  kujiridhisha kuwa Noela hajagundua lolote maana kama  angedungua asingemuita jina la Joshua bali angemuita Desmond,  kumbe Noela alishajuwa kila kitu, alikuwa katika upelelezi  wake binafsi 

    Desmond alipotoka pale Hotelini moja kwa moja alienda kuonana  na Mchumba wake Noela kama alivyoambiwa, alimkuta Noela akiwa  amejawa na tabasamu na bashasha kitu ambacho kilimfanya  Desmond azidi kujiamini kuwa Noela hajafahamu lolote lile,  waliagiza chakula huku Noela akizidi kumsoma Desmond, akili  ya Desmond haikutulia kabisa sababu alihitaji kufahamu kama  Joel alikuwa amefanikiwa kupeleka Hundi ile kwa Mtu wa Tatu

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA KUMI

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

      

    Love & Pain

    10 Comments

    1. Given Gihsy on November 21, 2024 11:37 am

      nimekuwa wa kwanz haya kiongoz. leo tulitakiw tuwe ya 11 malizia na hzo mbil😕

      Reply
      • Joyce on November 21, 2024 11:42 am

        Hahaaa uko makinj

        Reply
      • Robbiey on November 21, 2024 1:28 pm

        Mwanangu upo kama mimi inafikia hatua tunatembea tunawaza tu Desmond Lucy na Noela ila tulikua tukiangalia tunakuta patupu inabid atuombe radhi kwa hilo

        Reply
    2. Joyce on November 21, 2024 11:41 am

      Kwisha desmond

      Reply
    3. Verena on November 21, 2024 12:19 pm

      🤔🤔Joshua anazungukwa

      Reply
    4. Fawziya Hassan on November 21, 2024 2:11 pm

      Desmond anaenda kuisoma namba ya Joshua
      Simulizi ya 🔥

      Reply
    5. Sir, Yowas on November 21, 2024 4:29 pm

      Nikikisa bando najiskia ovyo kabisa sababu ya simulizi tamu

      Reply
    6. Halinga1 on November 21, 2024 6:05 pm

      Duuu kazi ipo

      Reply
    7. Cesilia Nkunga on November 21, 2024 11:41 pm

      Tabasamu la mwanasheria Joel 🥱🥱, mbona kama la kuchuma mali vile.

      Reply
    8. Ander on November 22, 2024 2:49 pm

      NiceOne

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.