Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Love & Pain Sehemu Ya Nane (08)
    Hadithi

    Love & Pain Sehemu Ya Nane (08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 20, 2024Updated:November 25, 202420 Comments7 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, Lucia  aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwao  Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongoza  Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambia 

    “Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe Mimi  siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa.. Endelea 

    SEHEMU YA NANE

    “Aaah usijali samahani kwa hilo, tunapita kushoto ili tuwahi  kufika” Alisema Mwanaume huyo kisha alikata kushoto lakini  Lucia alimuuliza 

    “Huko barabara imefungwa kuna ujenzi utapita vipi alafu kuna  pori kubwa huko” Alisema Lucia jamaa alizidi kuongeza gia  kisha alicheka, ndipo Lucia alipomkumbuka Desmond na kauli  yake, basi Lucia akaanza kuhangaika ili ashuke maana alijuwa  hapo ni lazima atafanyiwa kitu kibaya, kumbuka Tayari maagizo  ya kuuawa kwa Lucia yalikuwa yametolewa na Desmond, katika  pirikapirika gari hiyo ikajikuta ikipoteza uelekeo na kugonga  Mti. 

    Hali zao zilikuwa mbaya mno, Lucia alijitahidi kufungua  mlango akiwa hoi damu zikiwa zinamtoka, Mwanaume huyo naye  alikuwa akitokwa na Damu usoni, naye alifungua mlango akaanza  kumfukuza Lucia aliyekimbilia porini eneo ambalo lilikuwa na  mlima hivi. Akiwa anazidi kukimbia Lucia alimpigia sana simu  Noela lakini simu haikupokelewa, katika kukimbia akajikuta  ameindondosha simu yake. 

    Mwanaume huyo aliiokota simu ya Lucia kisha aliendelea  kumfukuza, bahati mbaya Lucia alijikwaa akaanguka chini, mara  moja Mwanaume huyo akiwa ana vuja damu alimfikia. 

    “Wewe ni Nani na unataka nini?” aliuliza Lucia akiwa katika  hali ya hofu sana huku akiwa amechoka. 

    “Unataka kujua mimi ni nani na Nataka nini kwako si ndiyo?  Mimi ni muuwaji nimekuja kuchukua roho yako Lucia” Alisema  Mwanaume huyo akionekana kumfahamu vizuri sana Lucia

    “Uniuwe kwa kosa gani mbona sikufahamu?” aliuliza Lucia akiwa  katika hali ya hofu huku maumivu ya Mguu yakizidi kumtafuna. 

    “Kosa lako ni Moja tu, kujifanya mjuwaji. Umeonywa mara ngapi  kuhusu Mandy wewe?” aliuliza Mwanaume huyo na kumfanya Lucia  sasa ajuwe kuwa Desmond alishatuma Mtu ili auawe. 

    “Ina maana umetumwa na Desmond si ndiyo? unafikiri ukiniuwa  itakuwa mwisho wa kila kitu? nakuhakikishia kifo changu  hakitofanya siri yenu isitoke, tena itatoka kwa kishindo  kikubwa sana” Alisema Lucia katika hali ya kujiamini sana  baada ya kujuwa kuwa alitakiwa kufa kwa maagizo ya Desmond 

    Yule Mwanaume alimbana vizuri Lucia pale chini akahakikisha  anakosa hewa kwa zaidi ya dakika moja kabla ya kunyonga  shingo ya Lucia, baada ya hapo alipiga simu mahali akasema 

    “Kazi imeisha” Alisema kisha aliubeba mwili wa Lucia akaenda  kuuweka kando ya Barabara hiyo ambayo ilikuwa na giza sana  kisha akaliwasha gari lake lililobamiza kwenye Mti kisha  aliondoka eneo hilo. 

    Shughuli ilikuwa imepamba moto, Noela hakumuona Lucia akienda  hapo licha ya kuarikwa, hakujuwa kuwa Lucia alikuwa ameuawa  porini. Desmond alimuuliza Noela alikuwa akifikiria nini  baada ya kumuona akiwa kama Mtu mwenye kutafakari jambo 

    “Rafiki yangu Lucia, alisema anakuja hadi sasa hivi, nampigia  simu hapatikani” Alisema Noela 

    “Atakuja tu, Watu wengine ndio kwanza wanaingia hivyo naye  ataingia tu” Alisema Desmond huku akijuwa fika kuwa Lucia  alikuwa ameuawa. 

    Muda ulienda bila Lucia kutokea eneo hilo, shughuli  ilifanyika kwa bashasha zote. Desmond akawa mchumba rasmi wa  Noela, ilikuwa ni siku yenye furaha sana Kwa Noela na Mama  yake sababu jambo hilo lilisubiriwa kwa muda mrefu, basi  zikapigwa picha za kutosha, Watu walikula hadi kusaza, Furaha  ilitawala usiku huo. Baada ya kuisha tukio hilo, Desmond  aliaga ili aondoke lakini alimuona Mtu mmoja aliyemfananisha  akiwa ameketi mahali anazungumza na Mwanume mmoja. 

    Desmond alimtazama sana Mwanaume huyo huku akijiuliza  alimuona wapi, akakumbuka alimuona siku ambayo aliliona gari  lake likiwa maegesho ofisini wakati gari hilo alilitumbukiza  baharini, alikuwa hamfahamu Mtu huyo na wala hakumuarika, ila  hakutaka kulipa uzito jambo hilo maana kama hakuarikwa na  yeye basi atakuwa amearikwa na Mpenzi wake Noela.

    Akaendelea kuaga Watu kwa ajili ya kuondoka eneo hilo, ghafla  aliguswa begani na Msichana mmoja ambaye alikuwa akihudumia  Watu vinywaji, msichana huyo alimpa Desmond ujumbe wa  karatsi, Desmond akamuuliza Msichana huyo 

    “Ametoa Nani?” 

    “Mkaka yule…” Msichana huyo alipoonyesha alipokaa Mtu  aliyetoa ujumbe huo hakuwepo hapo, akaanza kumtafuta kwa  macho lakini hakumuona ila Desmond alimuona mwanzo Mtu  aliyekaa hapo, alikuwa ni yule Mwanaume aliyemuona ofisini  kwake 

    “Haya sawa asante” Alisema Desmond, kisha alisogea pembeni  akafungua ujumbe huo akakuta maneno yaliyosomeka 

    “LUCIA AMEKUFA LAKINI SIYO MWISHO, TUKUTANE JUMATATU KATIKA  HOTELI YA HAVANA SAA 7 MCHANA!! CHUMBA NAMBA 43, NINA  USHAHIDI WA ULIYOYAFANYA” 

    Desmond alishtuka sana, alimtafuta Mwanaume huyo bila  mafanikio, alitoka nje kabisa lakini hakufanikiwa hata  kumuona Mtu huyo alijikuta akichoka mwili na akili, Mtu wa  tatu bado aliendelea kumtesa lakini bahati nzuri aliifahamu  sura yake, alimuita Mwanasheria Joel kisha waliondoka hapo  kwa ajili ya kujadili ni jinsi gani watamkabili Mtu huyo. 

    Noela alilala fofo baada ya kunywa pombe vya kutosha, aliamka  siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni Jumatatu, akili yake  ikamwambia kuwa siku hiyo hawezi kufanya chochote zaidi ya  kupumzika tu, lakini baadaye alifikiria kuhusu Lucia,  alijaribu tena kupiga simu ya Lucia lakini haikuita kabisa. 

    Alianza kupata mashaka pengine amepata tatizo ila hakuwa na  Mtu wa kumuuliza, aliwasha Tv ili aangalie habari za hapa na  pale, ndipo alipokutana na taarifa ya kifo cha nesi Lucia  aliyeuawa kwa kunyongwa shingo hadi kufa, Roho ilimripuka  sana Noela 

    Alishtuka sana kusikia taarifa hiyo na kibaya zaidi ni kuwa  aliacha Mama ambaye ni mgonjwa sana, mara moja Noela alivalia  nguo zake akamuaga Mama yake kisha akaelekea mahali ambapo  maiti ya Lucia ilikuwa imehifadhiwa, ni katika ile ile  Hospitali ambayo Lucia alikuwa akifanyia kazi, alikutana na  Daktari Mkuu wa hiyo Hospitali akawa anazungumza naye. 

    Mkuu huyo alimuelezea Lucia kwa jinsi alivyoweza mbele ya  Noela, kikubwa zaidi Noela alikufa akiwa masikini, pili  alikuwa na ndoto za kuja kuwa Nesi bora zaidi katika Hospitali hiyo na tatu aliacha Mgonjwa aliye katika hali  mbaya sana. 

    “Mgonjwa aliye katika hali mbaya?” Alihoji Noela 

    “Ndiyo! alikuwa akimuhudumia kwa kipindi chote, alikuwa na  ndoto ya kumuona Mgonjwa huyo anakuwa mzima tena lakini ndoto  ya Lucia imezimika ghafla kama Mshumaa” Alieleza kisha chozi  lilimtoka akalifuta, Noela alipelekwa hadi kwenye chumba  ambacho Mgonjwa wa Lucia alikuwa amelazwa, hakuwa mwingine  bali ni Mandy Mke wa Desmond. 

    Alimtazama Mandy kisha alisema 

    “Hakika Lucia amekufa na ndoto zake” Alisema Noela huku  akifuta chozi lake, alikumbuka mara ya mwisho alipewa kazi na  Lucia, haraka alitoka wodini ili alekee nyumbani kwake  kuangalia zile nyaraka alizopewa na Lucia. 

    Wakati anatoka Desmond alikuwa akiingia Hospitalini hapo,  wawili hao hawakuonana. Haraka akiwa na gari yake Noela  alifika nyumbani kwao, alimkuta Mama yake akiwa ameketi  sebleni, alitaka kumpita ila Mama yake alisema 

    “Amekuja Mtu uliyemuagiza amechukua sanduku” Alisema Mama  Noela na kumfanya Noela ashangae ni Nani alikuja kuchukua  Sanduku 

    “Mama unasemaje, sanduku la chumbani kwangu?” 

    “Ndiyo kwani hukumtuma Mwanaume mweusi hivi?” aliuliza Mama  Noela 

    “Mamaaaaaaa!!” aligumia Noela kisha alielekea chumbani kwake  haraka, kweli Sanduku liliondolewa chumbani hapo 

    Haraka alirudi Sebleni akamuuliza Mama yake 

    “Mtu huyo amekuja saa ngapi?” 

    “muda siyo mrefu sana alikuja na gari akasema umemuagiza na  alikuwa akijuwa hadi lilipokaa nikamiami, ina maana hukumtuna  Mtu?” aliuliza Mama Noela kwa mshangao, Noela hakujibu  alitoka akapanda gari kisha akaanza kumtafuta huyo Mtu,  alipita mitaa mbali mbali bila mafanikio yoyote yale hadi  alichoka. 

    Aliamuwa kurudi nyumbani, ndipo alipogundua huwenda kulikuwa  na jambo zito lilifanya Lucia auawe, akafikiria atapata vipi  kujuwa alichokuwa anatakiwa kufanya.

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TISA

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

    Love & Pain
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.