Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Love & Pain Sehemu Ya Sita (06)
    Hadithi

    Love & Pain Sehemu Ya Sita (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 15, 2024Updated:November 21, 20249 Comments9 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Lucia alimpatia Noela bahasha hiyo yenye taarifa muhimu za  kesi, Desmond aliona makabidhiano hayo ya Bahasha kisha  wawili hao waliagana kila mmoja akashika barabara yake.  Desmond aliona ni bora amfuatilie Mpenzi wake Noela ili  kujuwa Bahasha hiyo ilikuwa na nini. Basi, baada ya kutoka  hapo Noela alielekea moja kwa moja nyumbani kwao, alipoingia  ndani aliiweka Bahasha hiyo kwenye Shefu maalum ya  kuhifahdhia nyaraka zake, alifunga kwa namba maalum kisha  alijipumzisha kitandani. 

    Akiwa hapo nje Desmond alipokea simu ya Polisi mpelelezi  akaambiwa anahitajika haraka kituoni, mara moja aliwasha gari  bila kumwambia Noela kuwa alikuwa nje ya nyumba yao,  akaelekea kituoni. Huko alioneshwa gari ambayo maiti  ilikutwa, gari hiyo ilikuwa ni Landlover ya zamani ambayo  ilidaiwa kuwa usajili wake haukujulikana. Endelea 

    SEHEMU YA SITA

    “Hii ndiyo gari yenyewe ambayo ilikutwa ndani ya Bahari ikiwa  na mwili wa Sanga, hadi kufikia sasa tumempoteza mshukiwa  namba moja ambaye angetusaidia kujuwa mambo mengi  yaliyojificha kuhusu kesi ya Mkeo” Alisema Polisi huyo wakiwa  wamesimama kando ya gari hilo, Desmond alilitazama sana gari  hilo alafu akakumbuka siku ya tukio kuwa gari aliyoitumia  ilikuwa ni Audi A4 na siyo Landlover hiyo chakavu. 

    Bado aliendelea kujiuliza Mtu wa tatu ni nani? 

    “Kwa maana hiyo uchunguzi wa kesi utaanza upya ili kumpata  mshukiwa mwingine wa matukio haya, inaonesha Sanga alifungiwa  ndani ya gari kisha akatupwa Baharini ili afe, yupo Muuwaji  nyuma ya hili” Alisema tena Polisi huyo huku Desmond  akijiambia 

    “Muuwaji ni Mimi lakini hamtokuja mnijuwe” alisema ndani ya  nafsi yake, basi baada ya kumaliza kufanya mazungumzo hapo  Kituoni aliondoka zake, alimfikiria sana huyo Mtu wa tatu  kisha akili yake ikawa inamwambia kuwa Mtu wa tatu ni Lucia 

    Akapata wazo la kutaka kujuwa Noela alipokea bahasha ya nini,  alimpigia Noela akamuuliza yuko wapi, Noela alimwambia kuwa  yupo Mjini anaangalia gauni la kuvaa siku ya kuvishwa pete,  basi Desmond aliutumia mwanya huo kwenda nyumbani anakoishia  Noela na Mama yake.

    Alisalimiana kwa Bashasha na Mama Noela, Mama huyo alikuwa  akimpenda sana Desmond amuowe Mwanaye hivyo kumuona hapo  ilikuwa ni jambo la furaha sana, Mama Noela aliingia jikoni  kumpikia Mkwe wake mtarajiwa, Desmond aliitumia nafasi hiyo  kuingia chumbani kwa Noela ili aitafute ile Bahasha maana  alijuwa tu inaweza kuwa na taarifa mbaya dhidi yake 

    Alipekua kila mahali hadi alichoka lakini hakufanikiwa  kuiyona ile bahasha, aliamini Bahasha ilikuwa mlemle ndani,  alizidi kuitafuta bila mafanikio, alitumia muda mrefu  kufikiria na kuitafuta Bahasha bila kuipata maana aliiweka  kwenye shefu ambayo aliificha mahali, jasho lilimtoka Desmond  huku akizidi kutafakari itakuwa ipo sehemu gani. 

    Baadaye alisikia mlio wa gari ya Noela, alipochungulia  dirisha alimuona Noela akishuka kwenye gari, haraka alijuwa  akikutwa hapo ndani bila taarifa atashtukiwa, aliangalia kama  kuna kitu ambacho hakikukaa sawa, haraka alikirudisha kisha  alitoka chumbani, alifuta jasho akaketi sebleni, uzuri ni  kuwa Mama yake Noela muda wote alikuwa jikoni hivyo  hakufanikiwa kujuwa kama Desmond aliingia Chumbani kwa Noela. 

    Alipoingia Sebleni alishangaa kumuona Desmond ambaye alikuwa  akimfahamu kama Joshua 

    “Eeeh Baby umekuja saa ngapi?” Aliuliza Noela akiwa mwenye  furaha na mshangao juu tena akiwa anaweka chini mizigo  aliyokuja nayo, kisha alimrudia Desmond 

    “Nimekuja muda mrefu sana, nimekaa hapa kwa muda mrefu  kukusubiria uje” Alijibu Desmond kama siyo yeye vile  aliyekuwa akipekuwa chumbani kwa Noela kuitafuta ile Bahasha. 

    “Ndiyo amekuja muda mrefu nikawa naandaa Chakula” Ilisikika  sauti ya Mama yake Noela ( Mlami ) kisha naye alisogea karibu 

    “Chakula tayari Baba” Mama Noela alimwambia Desmond 

    “Ah Mama asante sana” Alisema Desmond kisha alienda kupata  chakula wakati huo Noela akiwa amepumzika kwenye sofa  akionekana kuchoka, wakiwa mbali mbali Desmond alimtupia  Noela swali 

    “Unaoneakana umechoka sana vipi ulifanikiwa?” Aliuliza  kwasababu Noela alienda kuangalia gauni la kuvaa siku ya  kuvishwa pete 

    “Ndiyo nimefanikiwa lipo kwenye mfuko” Alijibu noela, Desmond  aliendelea kula hadi alipomaliza akaaga akaondoka zake bila kufanikiwa kuipata ile baasha ambayo ilikuwa ikimpa wasiwasi,  baadaye Noela aliingia chumbani lakini aliona kama kuna  baadhi ya vitu vyake vimekaa tofauti siyo kama alivyoviacha,  alipata shahuku ya kuzidi kukagua aliona ishara ile ile  akahisi moja kwa moja chumba chake kilipekuliwa, alirudi  sebleni kwa Mama yake akamuuliza 

    “Mama Nani amepekua chumbani kwangu?” Alihoji Noela akiwa  mwenye kushangaa 

    “Kupekua? Mmh mbona hakuna aliyeingia huko…” alijibu Mama  Noela sababu hakunuona Desmond akiwa ameingia huko 

    “Ina maana kumejipekua kwenyewe eti Mama? Vitu nilivyoacha  siyo nilivyokuta ndiyo maana nimekuuliza, Mlami utasemaje  hujui wakati upo nyumbani muda wote?” 

    “Aaah au Joshua aliingia huko? Lakini hapana mbona aliketi  hapa muda wote” 

    “aaah” Aligugumia Noela kisha alirudi chumbani, alichukua  simu akampigia Desmond akamuuliza kama aliingia chumbani  kwake, Desmond alimkatalia kuwa hakuingia huko, basi simu  ilikatika huku ikimuacha na maswali mengi Noela kuwa ni Nani  aliingia huko na alienda kufanya nini. 

    Ndani ya Hospitali kubwa, Desmond alienda kumuangalia Mke  wake ambaye ni adui mkubwa kwake, kilichomshangaza ni  kuzuiliwa kuingia kwenye chumba ambacho Mke wake Mandy  alikuwa amewekwa kwa ajili ya matibabu, yalikuwa ni maombi ya  Nesi Lucia kwa daktari mkuu wa Hospitali. 

    Alilalamika Desmond 

    “Nazuiliwa vipi kumuona Mke wangu wa ndoa? Kwanini anapelekwa  kwenye wodi nyingine bila kunitaarifu Mimi?” Alihoji akiwa  mbele ya nesi mmoja, Nesi Lucia alikuwa amejibanza mahali  akimfuatilia Desmond, alikuwa na mashaka sana na Desmond  tokea ile siku ambayo Desmond alienda na Mwanasheria pale  Hospitalini na kumsainisha Mandy kwa alama ya kidole. 

    Desmond alichanganikiwa kwa jambo moja, kama Mke wake ataamka  atasema Nani alimuuwa Mama yake Kitu ambacho Desmond  alipambana kuhakikisha hakuna siri inayotoka. 

    “Ni maagizo kutoka kwa Dokta Mkuu wa Hospitali nasi  tunayafuata” Alisema Nesi huyo wa kiume, Desmond hakutaka  kusema tena baada ya kusikia kuwa maagizo ya kuzuiliwa  yaliyoka kwa Dakatri Mkuu wa Hospitali hiyo. Alitembea kisha  aliketi kwenye Kiti akakumbuka jambo

    Alikumbuka siku moja mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, mvua hiyo  iliambatana na radi za hapa na pale, alikuwa akiendesha gari  huku akionekana kuwa mwenye kutafakari jambo zito kichwani,  nyuma yake kulikuwa na gari nyeusi iliyokuwa ikimfuata  taratibu, Desmond hakuiyona. 

    Gari hiyo nyeusi iliyo nyuma yake ndani kulikuwa na Mama Mtu  mzima, Mama huyo alikuwa ni Mama yake Mandy, Mama Mandy  alipata taarifa kuwa Desmond amepanga kukutana na Mwanasheria  wa Mandy kisha wabadilishe hati za mali za Mandy. 

    Mama Mandy alizidi kumfuatilia Desmond Usiku huo ambao  uliambatana na mvua na upepo, safari hiyo ilikita nje ya Mji  huo waliokuwa wakiishi tena katika ghofu moja ambalo  Mwanasheria wa Mandy aliyeitwa Joel alikuwa akimsubiria  Desmond. 

    Mama Mandy alionekana kuwa makini sana kumfuatilia Desmond,  alikuwa peke yake, hakujuwa kuwa Desmond alikuwa ameshashtuka  kuwa kuna gari iliyokuwa ikimfuatilia kwa nyuma, Mama Mandy  alipoona gari ya Desmond imesimama naye alisimamisha gari kwa  mbali kidogo kisha alishuka akawa anatembea kwenye mvua  taratibu huku akiwa makini mno, alisogea taratibu sana hadi  kwenye gari ya Desmond lakini hakumuona Desmond, Usiku huo  ulijaa giza kiasi. 

    Alipoangalia vizuri mbele aliona ghofu, alipata wazo kuwa  huenda Desmond atakuwa ameingia humo, basi alisogea hadi  ndani ya Ghofu hilo ambalo lilionekana kuwa kimya sana,  hakukuwa na Mtu yeyote yule kitu ambacho kilizidi  kumshangaza. 

    Akachukua simu yake ili ampigie Mandy amueleze mahali alipo  pia amwambie Binti yake juu ya Mchezo mchafu aliokuwa  akiufanya Desmond, kabla hata hajapiga simu alisikia hatua  nyuma yake alipogeuka alimuona Desmond akiwa amesimama nyuma  yake, alipoangalia mikono ya Desmond haraka aliona amevalia  Gloves. 

    “Desmond! Unataka kufanya nini?” Aliuliza Mama yake Mandy  akiwa anavujwa na maji kwenye mwili kutokana na ile mvua  iliyompiga kule nje 

    “Uchafu unaoufanya umefika mwisho Joshua, kila siku nilikuwa  nikimwambia Mandy kuwa wewe huna mapenzi naye bali unahitaji  mali za Mtoto wangu, Mwanasheria Joel yupo wapi?” Aliuliza  Mama Mandy, Desmond alihema kidogo kisha Joel alijitokeza

    “Hadi wewe Joel? Unajuwa ni kiasi gani familia inakuamini  Joel? Unashiriki uchafu mkubwa kama Huu, hili siwezi  kulifumbia macho, nyote mnaingia kwenye mikono ya sheria”  Alisema Mama Mandy kisha alionekana kutaka kupiga Simu lakini  haraka Desmond alimuwahi, akampora simu akaona alikuwa  anataka kumpigia Mandy 

    “Unataka kufanya nini Mama? Unataka nifungwe? Unataka niwe  Masikini au unataka Mtoto wako aniache? Hii ni siri ambayo  hukupaswa kuifuatilia Mama…..” Alisema Desmond huku  akijikaza lakini alikuwa akiumia sana ndani ya Moyo wake 

    “Mandy ni lazima atajuwa kuwa wewe si Mtu mzuri na nina  ushahidi wa video na picha ambazo nimetumiwa, umekuwa  ukikutana na Joel kila siku Jioni na kupanga mipango yenu  michafu..” Alisema Mama yake Mandy 

    “Pole Mama kwasababu hutoweza kufanya hivyo” alisema Desmond  haraka alikata waya uliokuwa ukining’inia kisha akamnyonga  Mama yake Mandy hadi alipofanikiwa kummaliza, Mwanasheria  Joel alikunja uso wake kuashiria kuwa jambo hilo halikuwa la  kawaida. 

    “Joel Mimi na wewe tumeuwa hapa sawa? Tunapaswa kuondoka na  kukaa kimya, nipe hizo nyaraka” Alisema Desmond, haraka  alipewa nyaraka kisha Joel alisema 

    “Bado saini ya Mtu mmoja tu, Mkeo Mandy” 

    “Nitajuwa nini cha kufanya” Alisema Desmond kisha haraka  walianza kutoka lakini Desmond aligeuka kuutazama mwili wa  Mama Mandy, alikuwa amevalia cheni ya Dhahabu yenye thamani  kubwa sana, alirudi akamvua kisha akaiweka kwenye koti la  suti yake, alafu alisema 

    “Sisi ni Watoto wa kimasikini sana” 

    Kumbukumbu ya Desmond iliishia hapo, alitikisa kichwa chake  kisha alielekea ofisini kwa Daktari wa Hospitali, Daktari  alipomuona Desmond alijuwa nini kimemleta, Desmond alianza  kumshambulia Daktari huyo kwa maneno 

    “Umeagiza Mke wangu apelekwe Wodi nyingine alafu Mimi  nizuiliwe kumuona si ndiyo? Hivi unajuwa ulichokifanya?”  Alisema Desmond kwa hasira 

    “Desmond hebu kaa kwanza tuongee, hili jambo siyo la  kulichukulia jazba, tulichofanya ni kupandisha daraja  matibabu ya Mkeo ili aweze kuamka haraka ” Alisema Daktari  huyo kwa upole sana

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

      

    Love & Pain
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.