Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Love & Pain Sehemu Ya Tano (05)
    Hadithi

    Love & Pain Sehemu Ya Tano (05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 13, 2024Updated:November 15, 20245 Comments7 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Haijulikani, mfumo hauitambui gari hiyo” Alisema Polisi huyo  kitu ambacho kilimshangaza sana Desmond, itakuwaje gari yake  isitambulike? Kibaya zaidi alikumbuka kuwa hakutoa chochote  kwenye ile gari ikiwemo kadi ya Gari kitu ambacho kingekuwa  rahisi sana kufahamika, pia alipokuwa akifanya hivyo alijuwa  wazi kina kile kirefu hivyo gari haiwezi kuonekana 

    “Gari haitambuliki?” Alihoji Desmond akiwa na presha. Endelea 

    SEHEMU YA TANO

    “Ndiyo, ngoja nitakupa taarifa zaidi” Alisema Polisi kisha  alikata simu hiyo. Desmond alishusha pumzi zake kisha  akajiuliza 

    “Gari yangu haitambuliki? Polisi walijuwaje kuwa kuna gari  eneo lile wakati kina chake ni kirefu sana?…” alijiwazia  bila kupata majibu huku kichwa kikizidi kumuuma, aliona  hawezi kuendelea kuwepo ofisini badala yake alionelea aelekee  nyumbani kwake. 

    Alichukua koti lake la Suti kisha alitoka, akaenda eneo la  maegesho ya Magari ya kampuni hiyo, wakati anaingia kwenye  gari aliona kitu kilichomchanganya zaidi, aliiyona ile gari  yake ambayo alimuulia Sanga kule Baharini tena ikiwa kavu  kabisa, alishuka akaenda kuiangalia kwa ukaribu zaidi! Ndiyo  ilikuwa ndiyo gari yake ileile aliyoitosa Baharini 

    “Gari hii imefikaje hapa?” Alijiuliza Desmond kwa mshituko  mkubwa, moja kwa moja akatambua kuwa kuna Mtu anayejuwa kila  kitu kuhusu Mauwaji yote yaliyofanyika, Desmond alichoka  mwili hadi roho 

    “Nani ni Mtu wa tatu?” Alijiuliza maana katika matukio yale  alikuwepo yeye na Mwanasheria wa Mandy aliyeitwa Joel, sasa  huyo Mtu wa Tatu ambaye anafuatilia na kujuwa kila kitu ni  Nani? Desmond alijikuta akiwa katika rundo zito la Mawazo  katika akili yake, aliegemea gari iliyo pembeni. 

    Mara alikuja Mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevalia miwani ya  macho, akamwambia Desmond 

    “Samahani nahitaji kuondoka na hii gari hapa” Alisema  Mwanaume huyo akiionesha ni mmiliki wa gari ambayo Deamond  alikuwa ameiegemea, Basi Desmond alimpisha Mwanaume huyo  akawa ameondoka zake na hiyo gari, Bado Desmond alijawa na  mawazo sana kuhusu huyo Mtu wa tatu 

    Alimpigia simu Mwanasheria Joel akamwambia waonane mara moja,  walikutana ufukweni ambako mara nyingi walikuwa wakikutana,  Desmond alimsimulia Joel kilichotokea, sasa huyo Joel alikuwa  muoga sana tofauti na Desmond akaanza kumlaumu Desmond 

    “Kwanini uliniingiza huku Desmond, ona sasa siri hii inaenda  kuvuja, tutaishia jela nakwambia” Alilaumu Mwanasheria Joel  huku akizunguka zunguka nje ya gari walipokuwa wanesimama 

    “Acha kubweka kama Mbwa koko, huu siyo muda wa kulaumiana ni  lazima tumtafute Mtu wa Tatu ambaye anajuwa kuhusu sisi”  alisema Desmond kwa hasira sana

    “Unafikiri ni rahisi kumuwinda Mtu anayejuwa kuwa anawindwa?  Usikute hata hapa tulipo anatuona” alisema Joel, ni kweli  mita kadhaa kutoka walipo kulikuwa na Hoteli iliyojaza  wazungu kadhaa, kulikuwa na Mtu mmoja ambaye alikuwa amevalia  Mask alikuwa akiwapiga picha Joel na Desmond. Mtu huyo  alikuwa ni Mwanaume, hakujulikana alikuwa ni Nani, alipopata  picha kadhaa aliondoka zake, huwenda ndiye ambaye alikuwa  akifuatilia jambo hilo 

    “Hebu tuliza akili yake Joel, haya maji tumeshayavulia nguo  ni lazima tuyaoge, huyo Mtu hana nia ya kutukamatisha  mikononi mwa polisi bali kipo anachokitaka, naamni atakuja  kukisema hicho anachotaka ndipo tutakapomjuwa na kummaliza  ili hii siri ibakie kwetu tu” Alisema Desmond, maongezi yao  yalichukua muda mrefu hapo Ufukweni, hawakufikia makubaliano  ya nini wafanye ili kujiweka mbali na mikono ya sheria maana  tayari walikuwa na kesi ya Mauwaji. 

    Desmond alijikuta akiwa kwenye matatizo mazito sana, jioni  alirudi nyumbani kwake, alipokelewa na shangwe za Watu  waliokuwa wakimsubiria huku wakimuimbia, Naam ilikuwa ni siku  yake ya kuzaliwa, alishasahu kutokana na msongo wa mawazo,  miongoni mwao alikuwepo mpenzi wake Noela. 

    “Mpenzi umesahau leo ni siku yako muhimu sana eeeh?” Alisema  Noela akiwa anatabasamu mbele ya Desmond, aliangaza huku na  kule akaona ni bora ajifanye hakumbuki 

    “Oooh nilisahau kabisa jamani, asanteni sana sana hakika nyie  ni Watu wangu wa nguvu sana” Alisema Desmond huku akiachia  tabasamu lililobeba mengi mazito, walikata keki, walikula na  kunywa, baadaye wengine waliondoka akabakia Noela na Desmond. 

    Walikunywa pombe kwa pamoja, Noela alionekana kunywa zaidi,  sasa huyu Noela alikuwa na tatizo moja, akinywa pombe  anaropoka siri nyingi anazozijuwa, Desmond alikuwa  akilifahamu hilo ila hakuwa na shaka na Noela, waliendelea  kugida unywaji wakiwa kwenye jumba hilo la hadhi ya juu sana  ambalo Desmond alilinunua ili kumfanya Noela awe anaenda hapo  na siyo kule ambako alikuwa akiishi na Mke wake Mandy hivyo  ilikuwa rahisi kwa Noela kutokufahamu kama Desmond ana Mke. 

    Usiku ulikuwa mwingi sana, Desmond alishangaa ni kwanini  Noela haropoki chochote wakati siyo kawaida ya mpenzi wake  huyo, alikunywa sana kisha alijikuta akipitiwa na Usingizi  akiwa amelala hapo kwenye kiti. Desmond hakulewa, alinyanyuka  ili amsaidie Noela kumuingiza ndani. 

    Wakati anajaribu kutaka kumbeba alimsikia akisema

    “Lucia tutalifanya hilo baada ya tukio la kuveshwa pete,  sitaki kuchanganya mambo kwa sasa…..Lucia hiyo ni kesi  nzito inahitaji utulivu sana” Alisema Kisha alikoroma, sasa  kutajwa kwa Lucia kulimfanya Desmond afikirie jambo fulani. 

    “Lucia ana kesi gani aliyompa Noela? Au amemwambia kuhusu  Mandy?” Alijiuliza Desmond kisha alikumbuka tukio la yeye na  Mwanasheria Joel kwenda wodini kwa Mandy na kumsainisha  mafaili kwa alama za kidole, akafikiria sana mwisho akasema 

    “Huwenda Mtu wa tatu akawa Lucia, inawezekana ananifuatilia”  Alisema Desmond, kisha alimbeba Noela akampeleka chumbani.  Aliwasha kompyuta yake akaanza kufuatilia taarifa za Lucia,  akajuwa hadi mtaa anaoishi. 

    Siku iliyofuata, Desmond alianza kumfuatilia sana Lucia  kuanzia alipotoka nyumbani kwake asubuhi. Lucia alionekana  kuwa mwenye jambo fulani kichwani pake, alimfuatilia kwa  karibu ili ajuwe ana fahamu nini kuhusu Yeye, siku hiyo Lucia  hakwenda kule Hospitali sababu alikuwa na uhakika na usalama  wa Mandy sababu aliwekwa kwenye chumba chenye uangalizi wa  daraja la pili, chumba ambacho hata yeye kwa daraja lake la  elimu hakupaswa kwenda huko kufanya kazi. 

    Desmond alijuliza ni kwanini Lucia haendi Hospitalini siku  hiyo badala yake alipanda taxi akaelekea Mjini, safari ya  Lucia iliishia kwenye moja ya Hoteli maarufu sana mjini hapo,  yote haya Desmond alikuwa akiyashuhudia kwa kutumia jicho  lake la udadisi, Lucia aliketi kwenye kiti mithiri ya Mtu  ambaye alikuwa Hotelini hapo kumsubiria Mtu. 

    Lucia aliketi hapo kwa kutambo kidogo baadaye Noela aliingia  Hotelini hapo, akaangaza huku na kule ndipo alipomuona Lucia,  ilionesha walikuwa na miadi ya kukutana hapo, Desmond alizidi  kujawa na mshangao huku akifikiria watakuwa wanazungumza  kuhusu nini, alikuwa amejificha nje ya Hoteli hiyo ila sehemu  ambayo alikuwa na uwezo wa kuwaona Lucia na Noela. 

    “Lucia hilo jambo ni zito sana ndiyo maana nimekwambia  subiria nivishwe pete kwasasa akili yangu inawaza pete tu,  sitoweza kuifanya hiyo kazi ngumu” Alisema Noela 

    “Najuwa Noela lakini hapa nazungumzia uhai wa Mtu, nakuomba  uchunguze kuhusu hili jambo ili ifahamike kuna jambo gani  lililo jificha” Alisema Lucia kisha akasisitza 

    “Tafadhali chukua hii Bahasha ina kila kitu, kuna picha za  huyo Mwanaume anaitwa Desmond, na baadhi ya taarifa  nilizoziandika humo, tafadhali sana Noela” Alisema Lucia

    “Ooooh Lucia haya nipe lakini hii kazi nitaifanya baada ya  kuvishwa pete” Alisema Noela bila kujuwa kuwa ndani ya  bahasha hiyo kulikuwa na picha ya Mwanaume wake ambaye yeye  alikuwa akimjuwa kama Joshua wakati jina halisi ni Desmond na  Mwanaume huyo alikuwa Muuwaji 

    Lucia alimpatia Noela bahasha hiyo yenye taarifa muhimu za  kesi, Desmond aliona makabidhiano hayo ya Bahasha kisha  wawili hao waliagana kila mmoja akashika barabara yake.  Desmond aliona ni bora amfuatilie Mpenzi wake Noela ili  kujuwa Bahasha hiyo ilikuwa na nini. Basi, baada ya kutoka  hapo Noela alielekea moja kwa moja nyumbani kwao, alipoingia  ndani aliiweka Bahasha hiyo kwenye Shefu maalum ya  kuhifahdhia nyaraka zake, alifunga kwa namba maalum kisha  alijipumzisha kitandani. 

    Akiwa hapo nje Desmond alipokea simu ya Polisi mpelelezi  akaambiwa anahitajika haraka kituoni, mara moja aliwasha gari  bila kumwambia Noela kuwa alikuwa nje ya nyumba yao,  akaelekea kituoni. Huko alioneshwa gari ambayo maiti  ilikutwa, gari hiyo ilikuwa ni Landlover ya zamani ambayo  ilidaiwa kuwa usajili wake haukujulikana. 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SITA

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain 

      

    Love & Pain

    5 Comments

    1. G shirima on November 13, 2024 4:18 pm

      Well done

      Reply
    2. Luse twaxie on November 13, 2024 4:45 pm

      Niceeeee

      Reply
    3. Fawziya Hassan on November 13, 2024 6:14 pm

      Mambo yanazidi kuwa sio mambo tena
      Stori tamu kuuzidi umbea😀
      Asante Mwandishi kwa stori nzuri
      More Love from Kenya ❤️

      Reply
    4. Hamis on November 13, 2024 7:03 pm

      Duh jamani mbona story fup ivi adimini

      Reply
    5. Tina on November 14, 2024 9:45 am

      Story ya kusisismua sana hii

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.