Ilipoishia “Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani,Β alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwaΒ la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahiΒ kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijichekaΒ akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodiΒ Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao.Β
Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasiΒ kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipikiΒ alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywaΒ sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani. EndeleaΒ
SEHEMU YA NNE
“Lucia kwanini umekunywa hivi Mwanangu jamani” alisema MamaΒ Lucia akiwa anamuingiza Lucia ndani, alimpeleka hadi chumbaniΒ Kwake, alimuweka kitandaniΒ
“Lucia umepatwa na nini leo? Sijapata kukuona ukiwa umekunywaΒ kiasi hiki” Alisema Mama yake Lucia huku Lucia akianguaΒ kicheko kisha alisema kwa uleviΒ
“Ukiwa mzima kila Mtu atakupenda lakini kosa lako uumwe auΒ ufe, kila Mtu atakuwa adui wa Maisha yako Mama” Alisema LuciaΒ kisha alibeuwa kidogo, Mama yake alitamani kufahamu niΒ kwanini Lucia alisema hivyoΒ
“Kwanini unasema hivyo?” Alihoji Mama LuciaΒ
“Mama sisi Binadamu ni wabaya sana, tunacheka mbele kishaΒ nyuma tunanuna ha!ha!ha!” Alisema kisha alicheka lakini MamaΒ Lucia alihisi Mtoto wake pengine amekutana na jambo zitoΒ sana, ni kweli Lucia alikutana na janbo zito mnoΒ
“Pumzika Lucia tutaongea kesho” Alisema Mama Lucia kishaΒ alitoka chumbani humo, baada ya Mama kutoka Lucia alichukuaΒ simu yake akampigia Noela, alihitaji msaada kutoka kwa NoelaΒ
Wakati simu hii inapigwa usiku huo, Noela alikuwa amelala naΒ Desmond, Mara moja Noela alishtuka akaipokea huku akiwaΒ mwingi wa UsingiziΒ
“Hello?” Alisema Noela kwa sauti ya Usingizi, Desmond alikuwaΒ amelalaΒ
“Noela nahitaji msaada wako” Alisema LuciaΒ
“Msaada gani huo?” Aliuliza Noela huku akinyanyuka kitandaniΒ na kwenda dirishani ili tu asimpigie kelele Desmond
“Nataka msaada wa kisheria kwa mgonjwa wangu…ipo hivi….”Β Lucia alimuelezea Noela alichotaka kusaidiwaΒ
“Hivi una uhakika na unachokisema? Unaonekana umelewa sanaΒ kwanini tusiongee kesho hili jambo?” Aliuliza Noela, LuciaΒ alikubali kuzungumza na Noela kesho yake.Β
Simu ilikatika, kwa Mshituko Noela alipogeuka alimuonaΒ DesmondΒ
“Eeeeh Joshua umeamka?” Alihoji Noela kwa mshtuko maanaΒ hakutegemea kama angemkuta akiwa amemsimamia nyumaΒ
“Ulikuwa unaongea na nani?” Aliuliza DesmondΒ
“Aaah ni mteja wangu alikuwa anahitaji msaada wa kisheria,Β usijali Mpenzi twende tukalale” Alisema Noela, hakujuwa kamaΒ msaada alioombwa na Lucia ulimuhusu Mtu aliyekuwa naye UsikuΒ huo, Ndiyo!! Lucia alihitaji msaada wa kisheria kwa MandyΒ maana alichokiona pale kilimtisha sana.Β
Asubuhi mapema sana Lucia alienda Hospitalini kama kawaidaΒ yake, safari hii alikuwa makini zaidi na Mandy maana alijuwaΒ kuna jambo linachezwa nyuma ya ufahamu wake, alitembeaΒ taratibu akizunguka kitanda cha Mandy huku akijiuliza afanyeΒ nini kuzuia jambo hilo kutokea au kuwa baya zaidi. AlipataΒ wazo fulani, alimfuata Daktari Mkuu wa Hospitali akamuombaΒ Mandy aongezewe Huduma zaidi ili kuharakisha afya yake irejeeΒ kama mwanzo maana ilionekana kuwa na uwezekano wa MandyΒ kupona japo haikujulikana atapona lini licha ya wasiwasi kuwaΒ hata kama kiamka hatoweza kukumbuka chochote au anawezaΒ kukumbuka lakini akawa hawezi kuzungumza wala kufanyaΒ chochote kile.Β
“Kwanini umekuja kuniomba kuhusu hilo jambo?” AliulizaΒ daktari Mkuu wa HospitaliΒ
“Ni jukumu langu Kuhakikisha Mandy anakaa sawa haraka kulikoΒ ilivyo dhaniwa, naomba sana” Alizidi kuomba LuciaΒ
“Aah Lucia hilo jambo ni lazima tumshirikishe Mume wake, kamaΒ unavyojuwa yeye ndiye msimamizi wa kwanza wa Mandy” AlisemaΒ Daktari huyoΒ
“Hakuna haja ya kumuleza Desmond kuhusu hili jambo, naombaΒ asijuwe chochote kile” Alisema Lucia na kumfanya DaktariΒ ashangae, akamuuliza
“Kwanini hutaki ajuwe?” Nani atazilipa hizo gharama zaΒ ziada?” AliulizaΒ
“Kumbuka Mandy ni mfanyabiashara mkubwa sana hivyo akiamkaΒ atalipia hizo gharama” Alisema Lucia katika hali ya kuendeleaΒ kumuomba daktari akubali.Β
“Asipoamka?” Aliuliza DaktariΒ
“Jukumu letu namba moja ni kuhakikisha wagonjwa wanapona, niΒ lazima tufanye juu chini kuhakikisha tunasaidia Maisha yake”Β Alisema Lucia akiwa anamtazama Daktari huyo ambaye alionekanaΒ kuanza kumuelewa kidogo LuciaΒ
“Nakuamini Lucia usiniangushe katika hili, nitafanya kamaΒ unavyosema” Alisema Daktari huyo, Lucia aliweka mikonoΒ mdomoni kwa furaha kisha akasemaΒ
“Asante sana Mkuu! Umenipa thamani kubwa sana” Alisema LuciaΒ kisha alimuaga Daktari akaondoka zake, daktari huyo alikuwaΒ Mzee na ilionesha ndiye mmiliki wa Hospitali hiyoΒ
“Aaah” Alisema Daktari kisha alipiga simu alipopajua yeyeΒ akatoa maelekezo ya Mandy kupelekwa hatua ya pili yaΒ matibabu.Β
β’β’β’β’β’β’β’Β
Baada ya siku kama tatu kupita ilipatikana taarifa kutoka kwaΒ Askari polisi aliyekuwa akifuatilia kifo cha Mama Mandy,Β polisi huyo alimpigia simu Desmond akamwambia kuwa kuna gariΒ iliyopatikana kwenye Bahari, gari hiyo ilikutwa na maiti yaΒ Mtu. Desmond alichanganikiwa, alikuwa ofisini kwakeΒ akamuuliza polisi huyoΒ
“Gari! Maiti! Imefahamika gari ni ya nani na maiti ya Nani?”Β Alihoji Desmond akiwa amesimama huku macho yakiwa yamemtokaΒ pima, alijuwa tu ni ile gari yake aliyomuulia Sanga, harakaΒ akiwa anasubiria jibu la Polisi huyo alijiuliza kama gari ileΒ ikitambulika kuwa ni yake itakuwaje?Β
“Bado maiti imechukuliwa lakini kimekutwa kitambulisho chaΒ yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa ni mhisiwa namba moja waΒ Tukio la Mke wako ila mwili ulikuwa umeharibika hivyo imekuwaΒ ngumu kumtambuwa kwa macho. Mwili unafanyiwa vipimo kubainiΒ ni Nani” Alisema Polisi huyoΒ
“Vipi kuhusu gari imejulikana kuwa ni ya Nani?” AliulizaΒ Desmond kama Mtu mwenye haraka ya kutaka kujuwa, polisi hakutia shaka sababu aliamini Desmond alihitaji kufahamuΒ sababu Mandy ni Mke wake pasipo kujuwa Desmond ndiyeΒ aliyesababisha kila jambo na alikuwa akiwapiga changa askariΒ ili wasijuwe chochote kile, hata huyo Sanga aliyekuwaΒ akitafutwa ni yeye ndiye aliyemuuwa Hapo Baharini kwa kutumiaΒ gari yake.Β
“Kazi hiyo inafanywa na kitengo husika ili kubaini gari hiyoΒ ilikuwa ni ya nani, ndani ya dakika kumi zijazo tutajuwa gariΒ ni ya Nani pia tutapata taarifa juu ya mwili ule kama ni WaΒ Sanga au ni wa Mtu mwingine tu” Alisema Polisi huyo kishaΒ alikata simu baada ya kuhakikisha kuwa alizifikisha taarifaΒ muhimu kwa Desmond akiamini ni Mtu mzuri anayepaswa kujuwaΒ kinachoendelea.Β
Ofisini kwa Desmond hapakukalika mchana huo kilaΒ alichofikiria hakikumpa jibu la moja kwa moja, alijuwa niΒ lazima gari itajulikana kuwa ni ya kwake na polisi watamuhisiΒ kwa namna moja au nyingine jambo ambalo litasababisha aanzeΒ kuchunguzwa kuhusu matukio taliyotokea, alizunguka ofisiniΒ hapo huku akifikiria afanye nini.Β
“Oooshit itakuwaje?” Alijiuliza sana Desmond, aliketi akaamkaΒ akaketi tena huku akitazama saa ya ukutani, alihesabu hadiΒ dakika kumi alizoambiwa na yule polisi mpelelezi zilipokatikaΒ kisha alishika simu yake huku akisubiria simu hiyo iite,Β punde simu iliita na mpigaji alikuwa ni yule polisi, mudaΒ aliosema kuwa atampa taarifa juu ya ule mwili pamoja na gariΒ uliwadia, taratibu aliipokea kisha aliiweka sikioni akiwaΒ amefumba macho yakeΒ
“Desmond! Mwili ni wa Sanga mshukiwa namba moja, kesi inazidiΒ kuwa ngumu na kuhusu gari kuna fumbo zito sana hapa ambaloΒ linahitaji umakini hasa ukizingatia gari ile…” alisemaΒ Polisi kisha Desmond alidakiaΒ
“Ni ya Nani?” Alihoji kwa hofu kubwa sana, ukimya ulitawalaΒ huku Desmond akisubiria neno kutoka kwa Polisi huyo, alisemaΒ
“Haijulikani, mfumo hauitambui gari hiyo” Alisema Polisi huyoΒ kitu ambacho kilimshangaza sana Desmond, itakuwaje gari yakeΒ isitambulike? Kibaya zaidi alikumbuka kuwa hakutoa chochoteΒ kwenye ile gari ikiwemo kadi ya Gari kitu ambacho kingekuwaΒ rahisi sana kufahamika, pia alipokuwa akifanya hivyo alijuwaΒ wazi kina kile kirefu hivyo gari haiwezi kuonekanaΒ
“Gari haitambuliki?” Alihoji Desmond akiwa na preshaΒ
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & PainΒ
Β Β
11 Comments
Admin
Ongeza nyingne sahz admin mda umewadia jamani tumepooza sanaaa
Ebwanaeeeh si mchezoooo
Tuma na ingine Admini ooooh ni π₯π₯π₯π₯π₯
Mbona sijasoma sanga alivyouuawa
Muda umewadia kukikaribisha kiza,jioni ya Leo tutakua na Simulizi zetu mpya Za Sofia Solo pamoja na NEGATIVE PLAN
Bila kusahau vipande vinne vya muendelezo wa Simulizi ya ZEE LA NYWILA,Simulizi isiyotabirika mpaka sasa…
Stay tuned kisha share sambaza upendo kwa uwapendao.
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/677
Mbona kama leo fupi san adimin
Nzuri sanaπ₯
Hee mbona nimesoma kwa dakika mbili leo
Sehemu ya 4 ni fupi hivi!!?
Afu Desmond kumbe alipoenda kijijini kwa kina Sanga kumbe alienda kumaliza uhai wake emmmahπ’
Anyway Asante kwa stori nzuri yenye mafunzo na maumivu ndani yake.
More Love from Kenya β€οΈ
Katiri uyu
Muache awe na presha tuu
lywwtt