Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-09

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-08

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-07

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi (10)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Kumi (10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 23, 2024Updated:October 28, 202414 Comments6 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Macho  angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisema  Dokta Simon

    “Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twende  Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,  waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simon 

    Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,  aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.  Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuona  Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmke  ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.  Endelea

    SEHEMU YA KUMI

    “Zahra?” Aliita Osman akiwa anaendelea kumuangalia Zahra  ambaye alikuwa akitembea taratibu kuelekea kilipo kitanda  alicholala Osman, alitikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa ni  Yeye 

    “Baba! Huyu ni Zahra?” Osman alimuuliza Baba yake 

    “Ndiyo Osman huyu ni Zahra” Alijibu Mzee Dhabi, Chozi  lilimbubujika Osman, Dokta Simon alikuwa akiangalia  kilichokuwa kinaendelea kwa kutumia mlango 

    Zahra alisogea na kumkumbatia Osman akiwa analia, Osman  aliweka mikono yake kwenye mgongo wa Zahra. Muda huo Mimi na  Mama tulikuwa tumeingia wodini, tulikuta hali hiyo. Ilitubidi  Mimi na Mama kusizi kwa dakika ili kuangalia kilichokuwa  kikiendelea, walipoachana Zahra aligeuka nyuma alimtazama  Mzee Dhabi aliyekuwa akipepesa macho yake baada ya kuniona  Mimi 

    Macho yangu yaligongana na Macho ya Zahra, nilimtambuwa kuwa  ndiye Mwanamke aliyekuwa akiuendesha moyo wa Osman lakini  nilijiuliza aliweza vipi kurudi tena katika Maisha ya Osman,  roho iliniuma sababu alirudi wakati ambao nilikubali  kumsaidia Osman 

    Osman alinitazama, ukimya ulitawala huku kila Mtu akiwa  kwenye taharuki ya kilichokuwa kinaendelea pale. 

    “Baba! Nimerudi” Alisema Zahra akiwa analia, jinsi  nilivyomtazama niligundua alikuwa na jambo zito lililomfika  ambalo lilimrudisha kwa Osman 

    Nilihema sana nikihisi maumivu makali sana kifuani,  niliondoka nikaenda nje ambako nilijikuta nikiwa nimekaa peke  yangu usiku ule. 

    Mama hakuwa na neno la kuzungumza ilimbidi aangalie tu  kilichokuwa kinaendelea pale 

    “Zahra” Osman aliita, mara moja Zahra alimgeukia Osman

    “Ulikuwa wapi siku zote, nimekutafuta kila kona ya Dunia hii  bila mafanikio yoyote” Alisema Osman, Zahra alidondosha chozi  akasema 

    “Nisamehe Osman, najuta kwa Ujinga wangu, najuta sana.  Nimerudi kukufuta chozi lako” Alisema Zahra kisha alipiga  magoti akiwa analia, hata Mama alidondosha chozi lake 

    “Niambie nifanye nini Osman ili uamini kuwa nimerudi kwa  ajili yako, nimekukosea sana” Alisema Zahra akiwa anaendelea  kulia, Bilionea Dhabi alimsogelea Zahra na kumyanyua kisha  alimfuta chozi kwa kutumia mkono wake, akamwambia 

    “Osman anaumwa sana, hakuna tumaini la yeye kupona isipokuwa  kupata Figo na kumuondolea mfadhahiko” Alisema Mzee Dhabi kwa  sauti yenye kunong’oneza masikio ya Zahra, hii ilimshtua sana  Zahra alimfuata Osman alipolala kisha akamwambia 

    “Utapona Osman” Zahra alimshika mkono Bilionea Dhabi wakatoka  ndani, walinipita mahali nilipokuwa nimekaa, walielekea  ofisini kwa Dokta Simon 

    “Baba kama kutoa kiungo changu kutamfanya Osman awe salama  nipo tayari hata sasa hivi, pimeni figo zangu zikifaa mnitoe”  Alisema Zahra mbele ya Dokta Simon na Bilionea Dhabi ambao  walijawa na mshangao, chozi lilimtoka Bilionea Dhabi 

    “Zahra!” Aliita Bilionea Dhabi kwa sauti ya Chini sana, Zahra  alitikisa kichwa ishara kuwa alichokisema ndicho alicho  kimaanisha. 

    Mzee Dhabi alimkumbatia Zahra kwa Uchungu sana, alikuwa  ameshakata tumaini, Ujio wa Zahra ulimfanya Osman arudi  katika hali ya kawaida hata ile hali ya kunitaja ilikata.  Mama alimuuliza Osman kule Wodini 

    “Huyu Mwanamke ni nani?” 

    “Ni Mwanamke niliyampenda sana lakini alinikimbia na kwenda  Ughaibuni” Alijibu Osman 

    “Osman Mwanangu, Jacklin amekuja kwa ajili yako, yupo tayari  kufunga ndoa na wewe” Mama alisema kwa uchungu sana, Osman  alitikisa kichwa chake ishara ya kukataa huku akisema 

    “Jacklin hanipendi Mama, hawezi kukubali nimuowe” 

    “Tafadhali sana Osman, Jacklin anakupenda na yupo tayari”  Alisema tena Mama wakati huo Mimi nilikuwa ninachungulia mlangoni, niliumia sana. Sikuona umuhimu wa kubakia pale  Hospitali niliondoka zangu. Mama alijitahidi sana  kumbembeleza Osman lakini haikusaidia, kilichomtesa Sana Mama  yangu ni ule wema ambao Osman alitutendea na jinsi ambavyo  Mimi niliulipa wema huo kwa ubaya sana, Mama alilia sana hadi  Mzee Dhabi aliporudi akiwa ameambatana na Dokta Simon na  Zahra, Mzee Dhabi alimwambia Mama yangu 

    “Nashukuru kwa msaada na Mchango wako Mama Jacklin lakini  kwasasa wewe nenda” 

    “Lakini Mzee Dhabi…” Mama alikatishwa na Mzee Dhabi kisha  alipewa ishara ya kuondoka, chozi lilikuwa linamvuja Masikini  Mama yangu, aliondoka zake. 

    Mama alilia njia nzima hadi anafika nyumbani nguvu zilikuwa  zimemuishia, bahati nzuri nilikuwa sebleni. Nilipomuona  Nilimkimbilia na kumdaka asianguke, mwili wake ulikuwa wa  moto sana, jasho lilikuwa likimtoka, sikupata kumuona Mama  akiwa katika hali hii hata siku moja, nilimlaza kwenye Kochi  nikawasha Feni ili apate ubaridi kisha niliketi pembeni,  ukimya ukatawala huku nafsi yangu ikiwa imejaa majuto makubwa  sana, niliamini hali ya Mama ilitokana na makosa yangu. 

    “Jacklin” Mama aliita kwa Maumivu makali kisha alisema 

    “Tumechelewa lakini Mama yako nakupenda sana, Dunia nzima  inaweza ikakuona mbaya lakini Mama yako nitahangaika  kukusafisha. Osman amekataa kufunga ndoa na wewe” Alisema  Mama huku chozi likimbubujika, kusema ule ukweli niliumia mno  ndani ya nafsi yangu. 

    Moyo wangu nilishaufungua kwa Osman lakini niliufungua nikiwa  nimechelewa, nilijuwa Zahra ndiye aliyeharibu kila kitu,  nilimyanyuka na kuondoka nyumbani kwa hasira na maumivu  makali, sikutaka kujuwa kuhusu Hali ya Mama tena, kichwa  changu ni kama kilijaa moshi mkali sana. 

    Nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa 6 Usiku, nilimpigia simu  Mosses, zaidi ya mara sita mara ya saba ndio alipokea simu  yangu ikionesha kuwa alikuwa amelala. Aliniuliza nataka nini?  Nilimwambia nahitaji kuonana naye, aliniambia niende kwake,  nilianza safari ya kuelekea huko Usiku huo. 

    Nilipofika kwa Mosses kuna hali nilianza kuihisi ndani ya  nafsi yangu, niliona kabisa mapenzi kwa Mwanaume huyo  yalianza kuondoka ndani yangu, niliigiza tu na kumwambia kuwa  nammiss sana ila ukweli ni kwamba akili yangu ilikuwa kwa  Osman, kila nilipomfikiria Osman nilijikuta nikiumia tena kibaya zaidi nilipofikiria kuwa Zahra amechukua nafasi yangu  ndani ya moyo wa Osman ndiyo nilizidi kupagawa, hali hii  Mosses aliiona kwangu kwasababu mara nyingi nilikuwa nikitoka  kifikra akaniuliza 

    “Unawaza nini? Haupo kabisa” Aliuliza Mosses, huwezi amini  tulikuwa katikati ya tendo lakini akili yangu hata haikuwa  hapo, Mosses alishuka kisha alielekea Bafuni aliporudi  alihitaji majibu kutoka kwangu. 

    “Sijui Mosses! Najikuta tuu” Nilimjibu nikiwa ninavuta Shuka,  kweli mapenzi yanaumiza sana Aisee kumbe Osman aliumia hivi?  Sikuwahi kuumia kama ambavyo nilikuwa naumia 

    “Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwa  na tabia ya wivu sana 

    “Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanja  kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwa  ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bila  kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianza  kujichukia Mwenyewe. 

    Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, nami  nilitoa tabasamu 

    “Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadi  kulipopambazuka. 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MOJA Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

      

    Pumzi ya mwisho

    14 Comments

    1. catherine Arod on October 23, 2024 3:07 pm

      Dah fupi sana admin tuma mbili Leo Jana hukutuma hii pumz ya mwisho ni 🔥🔥🔥

      Reply
    2. Nelca on October 23, 2024 4:14 pm

      Waoooow 🥰💯

      Reply
    3. Happyness on October 23, 2024 4:47 pm

      Admin nyingn jmn 🔥🔥🔥🔥

      Reply
    4. yulia kimario on October 23, 2024 4:48 pm

      Admini hii ni ya jana bado ya leo

      Reply
    5. Calvin paul on October 23, 2024 5:20 pm

      Atleast sasa nimeanza kufurahi zahra kuwepoo

      Reply
    6. Chamalo on October 23, 2024 5:40 pm

      Jana hujatumia na leo ndio imeishia hapa

      Reply
      • Roda on October 24, 2024 3:56 pm

        Admin umerudia mbn 😭😭😭😭😭ila 🤣jack kaulambaaaaaaa akome ingekua mm toka kitamb san nihsaolewana huyoooo osman🤣hata hila kusem yy ungekuta nishamtongoza zangu🤣🤣🤣🤣🙌

        Reply
    7. Guyton on October 23, 2024 6:07 pm

      Hiyo ndo dawa ya wanawake kama kina jacklin….😏

      Reply
      • Lus twaxie on October 23, 2024 9:20 pm

        Akomee huyu dada ..pumbaf

        Reply
    8. Hamis on October 23, 2024 7:01 pm

      Adimin unasikia oja za ndugu zako tuma nyengne

      Reply
    9. Meows on October 23, 2024 10:24 pm

      Kusema ukwel j kayatimba hapo
      🌝🌝 Lakini atajua mwenyew cz aliyataka

      Reply
      • esthersafary on October 24, 2024 3:32 pm

        Leo n 11 jamn

        Reply
    10. yahaya on October 24, 2024 4:18 pm

      admn vp ten tuma ya 11 Leo bwan

      Reply
    11. Juju on October 24, 2024 5:42 pm

      Admin umezinguwa see ya 11 pumzi ya mwisho hujatuma ,

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 23, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-09

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nane “Nakufahamu Zahoro, wewe ndiye jibu la Laana hii.…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-08

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-07

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-06

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.