Ilipoishia “Sikia Dokta Simon, naomba hili jambo liwe siri Baina yetu.Β Baba yangu asijuwe chochote wakati ambao tunatafuta Figo kwaΒ ajili ya kunipandikiza” Alisema OsmanΒ
“Naweza kulificha lakini hali yako inaweza ikaniumbua mbeleΒ ya Baba yako, vyote nitafanya lakini vipi kama JacklinΒ akazikataa hisia zako huoni kama utakuwa umekula hasara wewe?” Alimuuliza swali gumu sana, Osman alikunbuka namnaΒ tukivyogombana kule Dubai, aliona Swali la Dokta SimonΒ lilikuwa na mashiko sana. Endelea
SEHEMU YA SITA
“Tuachane na hilo, naomba ufanye siri asijuwe Mtu yeyote naΒ pia tangaza dau kwa ajili ya kupata figo nyingine”Β
“Sawa kama unavyotaka” Alijibu Dokta Simon, Osman alitoa pesaΒ akampatia Dokta Simon kisha aliondoka hapo na kurudi nyumbaniΒ kwake.Β
Mimi nilikuwa nikifanya kazi zangu kama ambavyo Mama alikuwaΒ amenisihi nifanye ili nisimvunje moyo Osman, nilichapa kaziΒ hadi mida ya Jioni, muda wa kazi ulipoisha niliondoka nikiwaΒ nimechoka sana, nilimtafuta Mosses kisha alinielekeza wapiΒ natakiwa kwenda, nilipitia Benki kabla ya yote, nilitoa kiasiΒ kidogo kisha nilienda huko.Β
Nyumba ilikuwa nzuri sana, ilikuwa kubwa na yenye viungaΒ vizuri vya kupumzika. Tuliikagua kwa pamoja, pesaΒ zilizotakiwa kulipwa pale zote zilikuwa ni pesa zilizotokanaΒ na Osman, baada ya kuwa tayari tumemaliza kuikagua, nilifanyaΒ malipo kwa kutumia huduma za kibenki kwa simu. MalipoΒ yalikamilika, tuliandikiwa mkataba pale kisha zoeziΒ lililokuwa limebakia lilikuwa ni kununua fenicha zote zaΒ ndani ili nyumbani ipate kuitwa nyumba wanayoishi Watu.Β
Baada ya kuona nina pesa nyingi vile Mosses aliniomba pesa yaΒ mtaji ili afungue biashara, nilimwambia nitampatia baada yaΒ siku tatu, kuhusu Mosses nilikuwa sikifirii chochote kileΒ bali hisia za mapenzi ndizo zilizokuwa zikinisukuma kufanyaΒ kila kitu kwake.Β
Nilipomaliza kila kitu ndipo nilikumbuka kuwa nilikuwa naΒ maua ndani ya gari ambayo nilitakiwa kumpatia Osman iliΒ nimuombe msamaha, basi nilimdanganya Mosses kuwa naelekeaΒ nyumbani, kwa vyovyote asingeliweza kusema anisindikize maanaΒ alikuwa hapatani na Mama yangu. Nilimuacha hapo kishaΒ niliingia kwenye gari nikawasiliana na Osman, alinielekezaΒ mahali anapoishi, lengo langu lilikuwa ni kumuomba msamahaΒ kama ambavyo nilimuahidi Mama,Β
Safari ya kuelekea kwa Osman ilianza nikiwa ndani ya gari yaΒ kukodi, nikifikiria ni jinsi gani nitaongea na Osman iliΒ nipate kumuomba msamaha. Alionekana kunisubiria sana sababuΒ alikuwa akinipigia na kuniuliza nilikuwa nimefika wapi,Β mwendo wa saa moja na nusu nilifika nyumbani kwa Osman,Β alikuwa akiishi kwenye Bonge la Kasri, ndioo niliamini kuwaΒ Mwanaume huyu alikuwa tajiri sana.
Jumba lilikuwa likiwaka taa nzuri zenye kuvutia sana, ilikuwaΒ ndiyo mara ya kwanza nafika kwa Osman, nilivuta picha yaΒ nyumba aliyotununulia japo ilikuwa ya kifahari ila nilionaΒ haiifikii hata theluthi nyumba ambayo Osman alikuwa akiishi,Β nilimpigia simu kisha aliwapa taarifa walinzi kuwa kuna ugeniΒ nje, nilifunguliwa geti kisha gari liliingia mara moja,Β ilikuwa ni mishale ya saa moja kasoro.Β
Alikuja Mdada mmoja kunipokea, tena alinipokea kwa bashashaΒ zote kama alikuwa akinifahmu vile, vile nilikuwa muelewaΒ nilijuwa tu ni kazi yake ya kupokea wageni ndiyo inayomfanyaΒ awe mchangamfu, nilimruhusu dereva aondoke, Mimi pamoja naΒ yule mdada tuliongozana kuelekea juu ambako Osman alikuwepo,Β jumba lake la kifahari lilikuwa la ghorofa tatu tu lakiniΒ lilikuwa la kisasa mno, ilinifanya niwe na hamu ya kumuonaΒ Osman.Β
“Osman yupo chumba hiki” Alisema Yule Mdada kisha akaongezaΒ kwa kusemaΒ
“Ingia tuu” Yule Mdada aliondoka zake, niliangaza huku naΒ kule kabla ya kufungua mlango huo ambao ulikuwa na kitasaΒ chenye mg’ao wa Almasi, ilikuwa ni kwenye floo ya mwisho yaΒ ghorofa. Nilipofungua mlango nilihisi kama nilikuwa nikiingiaΒ kwenye bustani fulani hivi, Osman aliidizaini nyumba yakeΒ mithiri ya Bustan ya Eden.Β
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na mandhari za kuvutia sana,Β hewa safi na upepo mwanana, mwenyewe Osman alikuwa amekaa juuΒ ya Kiti akicheza na samaki walio kwenye bwawa dogo laΒ kutengeneza. Aliponiona aliacha kila kitu kisha akaweka machoΒ yake yote kwangu, najuwa moyo wake ulimwambia kuwa Jacklin niΒ mrembo sana, maana alinitazama kutoka juu hadi chini kishaΒ chini hadi juu kabla ya kunisemesha chochote. Nilitabasamu tuΒ huku nikiwa nimeficha Mauwa nyuma kwa kutumia mkono wangu waΒ kushoto, alinifuata kama vile mzimu, alinisalimia kwaΒ kuhangaika kama si yeye aliyekuwa akiumwaΒ
“Ooh Jacklin! Karibu” Yaani Osman aliongea kama zuzu fulaniΒ hivi asiyejuwa nini kinaendelea au kama Mtu ambaye hakuwa naΒ taarifa kuwa ningefika pale wakati nilikuwa nikiwasilianaΒ naye kuwa naenda.Β
“Asante!!” Nilisema kwa tabasamu murua, Osman alihangaikaΒ kutazama ni wapi tungekaa.Β
“Kama hapa si sehemu nzuri tunaweza kwenda chumba kingineΒ chenye sinema tukaangalia filamu mpya” Alisema Osman
“Hapana Osman hapa pazuri panatosha, hewa yake ni safi sana”Β NilisemaΒ
“Basi tukae pale” Alinionesha mahali ambapo alikuwaΒ amepaandaa kwa ajili ya Mimi na yeye, hapo palikuwa na mezaΒ ya mawe na viti vya mawe, juu yake kulikuwa na juisi mbiliΒ ambazo ziliwekwa pambo la Ndimu, moyoni nikijikuta nikisemaΒ “Wow”Β
Kusema ukweli Osman alikuwa romantic sana, alijuwa nini MaanaΒ ya mapenzi, dakika chache tu za kuwa pale nilianza kuhisiΒ kumpenda Osman lakini nilimkumbuka Mosses nilisema na moyoΒ wanguΒ
“Hapana Jacklin, hapana una Mpenzi” Nilijisemea kishaΒ nililazimika kufanya haraka, hata sikusogea kuketiΒ alipopasema bali nilimwambiaΒ
“Osman! Lengo langu la kuja hapa kwanza ni kujuwaΒ unaendeleaje lakini pili ni kukuomba msamaha kwa kileΒ kilichotokea jana, haikuwa dhamira yangu. Nimejisikia vibayaΒ sana tena zaidi ya sana” Nilisema kisha nilimuona OsmanΒ akionesha kama vile tukio la jana halikumuumiza chochote kileΒ
“Aah usijali Jacklin, yameshapita hata hivyo wala sikuwekaΒ akilini sana, karibu tukae” Alisema Osman, nilitoa mauwaΒ nyuma yangu nikampatia, alikuwa ameduwaa mithiri yaΒ Mwendawazimu aliyeona jalala lenye chakula, alikosa hata nenoΒ la kusema, Mauwa ni ishara ya upendo hivyo ndivyo ilivyoingiaΒ katika akili yakeΒ
“Ja…jac…Jacklin” Aliniita kama Mtu asiye na uhakika waΒ jina languΒ
“Samahani na pia ugua pole” Nilisema kisha niligeuka naΒ kuondoka nyumbani kwa Bilionea Osman, nikiwa nje nilimuonaΒ akichungulia dirishani wakati huo giza lilikuwa limeingia.Β Ilipita Bajaji niliita kisha niliitumia kurudi nyumbani.Β
Osman nilimuacha akiwa na furaha ambayo aliipoteza mudaΒ mrefu, furaha ambayo Zahra aliichukua kwake lakini haikuwaΒ kwamba ndiyo nilikuwa naanza mapenzi na Osman japoΒ nilimuonesha ishara ya kumpenda, bado akili na mawazo yanguΒ yalikuwa kwa Mosses.Β
Kabla hata sijafika nyumbani Osman alimpigia simu Mama naΒ kumwambia kuwa nilienda kwake, Mama na Osman walikuwaΒ wameivana sana kiasi kwamba Mama alikuwa akinitaka niwe naΒ Osman. Waliongea kuhusu malengo na mawazo yao, nilipoondokaΒ
Hali ya Osman ilibadirika akakimbizwa Hospitalini, alikuwaΒ mgonjwa japo ugonjwa wake alikuwa hajausema popote zaidi yaΒ kwa Dokta Simon.Β
Nilipofika nyumbani nilishangaa kwa hali ambayo ilikuwepoΒ jana kati yangu na Mama yangu, nilistaajabu kumkuta akiwa niΒ mwenye furaha sana tena akiimbaimba nyimbo za kabila letu, niΒ muda mrefu Mama hakuwahi kuwa kwenye furaha namna hiyo.Β
Nililazimika kumfuata na kumuuliza kuliko alikuwa mwenyeΒ furaha sana.Β
“Nina furaha sababu Maombi yangu yanaenda kutoa majibu mudaΒ siyo mrefu, nilichokiwaza kinaenda kudhihirika hivi karibuni”Β Alisema Mama akiwa bizeΒ
“Mh! Mama uliomba nini na ulikuwa unawaza nini?”Β
“Siku zote Mama humuombea Mtoto wake na kumuwazia yaliyoΒ mema, ni furaha kwa Mama kuona Alichokiwaza kinaendaΒ kutendekea kwa Mtoto wake” Maneno ya Mama yalinipa tabasamuΒ japo yalijaa mafumbo, mimi ndiye Mtoto wake wa kipekeeΒ niliwaza atakuwa ameomba nini au kuniwazia niniΒ
“Mama unaniwazia nini Mwanao?” NilimuulizaΒ
“Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaΒ siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaΒ kumuuliza, nilimwambiaΒ
“Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”Β Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiΒ Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. HadiΒ naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naΒ kuambiana kuwa nilienda kwa Osman.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ


18 Comments
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Duuh tamu lkn fupi sanaa admin, all in all mapenzi ni ushetaniπ upofuuuu
Daaah Jacky hebu amka ktk isingiz huo wenye upof
Mpaka unaniumiza na mimi
Daaah mpaka najikuta nililia kila nikizidi kuiisoma hii riwaya inafundisha sana
Tupe na ya saba tu kwa leo hahahah π₯π₯π₯
Toa mbili mbili jamani
Osman nae anaumwa dah!! Hii kweli pumzi ya mwisho this is fantastic story π₯π₯π₯π₯
Nzuri sana πππ
Admin upewe maua yako… unajua bhan…ila t tunaomb isiwah kuish…ivute vute had tuone jacklin na osman wamependan na kuoan
Mmoja wao atakufa kati ya jack ama osmanπ₯²π₯²π₯²
Nzuri sanA natamani ya saba adminiπ€£π€£π€£π€£π€£π€£
ila co kwa wadada wa bongo ππ
admin pongezi sana
Kwa kweli jack ni muuaji kabisa kupenda gani huko anakompenda Moses mwanaume aliesema bora afe lakini yeye maisha yaendelee kwake
Ahahahahhaha eti kisa ndo mwanaume wake wa kwanzaπππ huo ni udwanziii
Bora figo yang nkaipa hata mbuzi ntaila hata nyama kuliko mwanamke
5s1klx
v087bk
5jkdy4