Ilipoishia “Basi Maisha ndani ya Gereza yaliendelea, siku moja baada yaย kazi ilikuwa ni majira ya saa 7 Mchana, ulikuwa ni muda waย kupata Chakula. Tulikuwa tukipanga mistari miwili kwa ajiliย ya kupata Chakula, msitari wa kwanza nilikuwepo Mimi, sasaย katika tazama tazama nilistaajabu nilimuona Sarafina, yuleย Mdada ambaye alifukuzwa na Shonaa kisa Mimi, nilitamaniย kumuita ila nilikumbuka kuwa alikuwa na hasira na Mimi,ย nilimgeukia Isabela nikamuulizaย
“Yule yupo hapa kwa muda gani?” Nilimuonesha kidole Sarafinaย
“Nimemkuta hapa, anaonekana kahukumiwa muda mrefu ilaย inasemekana aliiba pesa kwa tajiri mmoja”ย
“Vipi unamjuwa?”ย
“Ndio namjuwa” Basi baada ya kuwa tumeshachukua chakulaย tulienda kula, Isabela aliniulizaย
“Unamjua vipi yule”ย Endeleaย
SEHEMU YA NANE
“Wakati nakuja hapa Dar ndio nilionana naye ila tuliachanaย kwa shari, aliniona mbaya akidai nimesababisha amefukuzwaย pale alipokuwa anaishi” Nilisemaย
“Mh! Sasa itabidi ujiadhari maana yule ana kundi lake hapaย gerezani ambalo linaendesha ubabe mwingi, akijuwa kama upoย hapa utaishi kwa shida sana” Alisema Isabela.ย
“Ni kweli lakini nitamkwepa vipi wakati tunaishi kwa uwaziย hivi, ikiwa mimi nimemuona nina imani na yeye ataniona tu.”ย
“Cha msingi ni kumkwepa vinginevyo utateseka sana hapa Jojo”ย
“Mh! Tutaona itakavyokuwa” Tulipomaliza kula tulirudiย kuendelea na kazi za Shamba, jioni tulihesabiwa kishaย tulikula na kurudishwa kwenye vyumba kwa ajili ya kulala,ย kila chumba kilikuwa na wafungwa 8 ambao tulikuwa tukilalaย humo. Bahati nzuri chumba chetu hakikuwa na muhuni hataย mmoja, kumbe taarifa ya Mimi kuwepo Gerezani alikuwa nayoย Sarafina, kama Isabela alivyoniambia kuwa Sarafina alikuwa naย kundi la ubabe pale gerezani.ย
Usiku tukiwa tumelala tena fofofo maana kazi za pale Gerezaniย zilikuwa ngumu mno hivyo Mtu akilala anakuwa kama amekufa.ย Nilishtuka geti la chumba chetu lilikuwa likifunguliwa alafuย tochi ilinimulika Usoni, aliingia mdada mmoja ambaye hakuwaย Askari, aliniambia nimfuate.ย
Niliamka kisha nilimfuata, niliingizwa kwenye chumba kimojaย kisha kilifungwa, kilikuwa ni chumba chenye giza mno kiasiย kwamba sikuweza kuona chochote kileย
“Nipo wapi?” Nilijiulza kwa sauti ya chini huku nikipapasiaย
“Dada yangu kwanini umenileta huku?” Niliuliza, sautiย ilijirudia tu katika kile chumba, sikujibiwa. Mara taaย iliwashwa, nilikutana na macho ya Sarafinaย
“Sarafina” Niliita kwa mshituko maana sikutegemea kamaย ningekutana naye katika Mazingira yale, kwa vyovyote vileย aliyenileta alijuwa nini anafanya.ย
“Karibu Jojo, Mungu wangu alinisikia kilio changu, hatimayeย nimekutana na wewe” Alisema Sarafina akipiga hatua ndogoย ndogo kusogea nilipokuwa nimesimama.ย
“Sarafina sikufanya chochote kibaya dhidi yako, sikutegemeaย kama ingekuwa vile. Nisamehe tafadhali, tuyamalize”
“Pengine umesahau Jojo, nilikuokoa yule Mwanaume asikubake,ย nilimpiga mbele yako kukuonesha kuwa sikupenda alichokifanya.ย Wema wangu kwako ndiyo uliozaa matunda yale, sikuwa na paย kwenda, nilikuacha pale lakini nilisema ipo sikuย nitakuonesha. Siwezi kuwa na haraka na wewe sababu upo kwenyeย himaya yangu” Alisema Sarafina akiwa anazunguka huku na kuleย
“Sarafina tafadhali sana, nisamehe hujui ni mambo mangapiย magumu nimekutana nayo, nimeishi Maisha magumu sana, hukumuย niliyopewa ni adhabu tosha kwangu…” Nilisema kwa uchunguย sanaย
“Lakini sio adhabu yangu, yangu itakuwa zaidi ya hiyo hukumuย uliyopewa, wema wangu ukageuka kuwa udhalilishaji, siri yaย ugonjwa wangu iliwekwa wazi, namjuwa Sana Shonaa kulikoย unavyomjuwa wewe ni lazima alinianika kwenye kila jambo”ย Alisema Sarafina akiwa amefika karibu zaidi na Mimiย
Nilipiga goti nikamuomba Sarafina asinifanye chochote kibayaย maana kama aliweza kupata funguo ya chumba chetu maana yakeย alikuwa na uwezo hata wa kuniuwa na hakuna ambaye angesemaย chochote kile.ย
“Magret” Aliita, yule Mdada aliyekuja kunichukua alikujaย ndaniย
“Mrudishe, nitamalizana naye” Alisema Sarafina kishaย nilirudishwa kwenye chumba chetu cha gereza.ย
Nilikuta Watu wa Chumba chetu wakiwa macho ni dhahiri kuwaย walisikia Wakati Mimi ninaondolewa pale gerezani. Mtu waย kwanza kuniuliza alikuwa ni Isabelaย
“Ulienda wapi Jojo?” Nilivuta pumzi nikamueleza nilipokuwaย
“Itabidi uwe makini sana Maana Sarafina ni Mtu mkorofi mnoย hapa gerezani, ipo namna anaweza akafanya maisha yako yakawaย si kitu hapa gerezani” Alisema Isabela akadakia Mwanamkeย mwingine akasemaย
“Wakati anafika aliwahi kupigana na askari Watatu naย akawadhibiti vizuri sana, tokea siku hiyo amekuwa na urafikiย na Mkuu wa Gereza hili, mara kadhaa amekuwa akitoka na kurudiย haijajulikana wana ajenda gani, hivyo unapaswa kuwa makiniย sana Jojo vinginevyo hata sisi tutakuwa hatarini. Ana kundiย lake hapa na linatambulika na Mkuu wa Gereza, wao hawafanyiย kazi yoyote ile zaidi ya kutoka na kurudi” Yalikuwa ndiyoย maelezo yake kuhusu Sarafina, hilo la kupiga Askariย halikunitisha sana maana nilikumbuka aliwahi kumpiga yuleย Mwanaume aliyetaka kunibaka.
“Ina maana anaishi humu gerezani kwa uhuru bila kubugudhiwaย na chochote?”ย
“Ndiyo! Ni Mtu hatari sana, anaendesha biashara ya kuuzaย Bangi na Unga hapa Gerezani, anachumba maalumu cha kulala naย anapewa mahitaji yote ayatakayo” alielezea huyo Mwanamkeย mwingine, kiukweli nilijawa na woga sana, nilipitia kote ilaย niliona dhahiri Maisha yangu yataishia ndani ya gereza,ย nilimuuliza Isabelaย
“Ndugu zako wanakuja kukuona?”ย
“Hapana nahisi hawajaambiwa chochote na Mume wangu”ย Alinijibu, lengo langu lilikuwa kama wanafika niwape maelezoย waende nyumbani kwetu Tabora wakauze kibanda chetu ili wajeย kunikomboa pale gerezani, nilichoka sana.ย
Wao walilala maana ulikuwa ni usiku mwingi, ila Mimi nilikuwaย macho hadi Alfajiri ambapo tuliamshwa kwa ajili ya kazi, sikuย zote nilikuwa napewa kazi nafanya na wenzangu ila siku hiyoย ilikuwa tofauti sana, kwanza nilipelekwa kwenye kuvunja maweย adhabu ambayo hupewa Wafungwa waliofungwa kwa kosa laย Mauwaji. Pili niliambiwa natakiwa kuwa peke yangu, basiย nilipelekwa huko na Askari mmoja, kulikuwa ni eneo lenye Maweย yaliyochimbuliwa, nilipewa nyundo kubwa nilianza kazi yaย kuvunja mawe, Mchana ulipoingia nilisikia kengele kwa ajiliย ya kwenda kupata Chakula lakini yule askari alinizuiaย akaniambia siruhusiwi kula kwa siku hiyo.ย
Nilikubaliana na hali halisi, nilifanya kazi kwa bidii sanaย bila hata kutegea sababu nilijuwa yalikuwa ni maelekezo yaย Sarafina, Jioni nilipelekwa kulala kwenye chumba cha pekeย yangu, chumba hakikuwa na taa wala sehemu ya kulalia,ย palikuwa pamemwagwa maji kwenye sakafu. Basi niliketi, japoย nililoa lakini ilinilazimu kwani nisingeliweza kusimama kwaย muda woteย
Kweli aliyesema Maisha ni popote, msemo ulikuwa na maanaย kubwa sana, licha ya kutokula chochote lakini nililala kwenyeย sakafu yenye maji, niliuchapa Usingizi kutokana na zile kaziย ngumu. Usingizi ulinipitiliza hadi asubuhi sana, jua lilikuwaย limeshatoka nilipata kuushuhudia mwanga wake kupitiaย kidirisha kidogo ambacho kilikuwa juu pale kwenye kileย chumba, mazingira ya chumba yalikuwa maalum, kilionekana kuwaย ni chumba spesho.ย
Tofauti na vyumba vingine, chumba hicho kilikuwa na getiย lisiloonyesha nje, kilikuwa na michoro ukutani na harufu kaliย sana ya uchafu, wadudu walikuwa wakitembea kwenye ukuta,ย nilijiinua na kuketi pembeni nikiwa nimeegemea ukuta,ย nilijiuliza kwanini sikuamshwa siku hiyo, masaa yalisogeaย njaa ilizidi kuniuma, kiu ilizidi kunishika maana tokeaย nilivyokula na kunywa maji siku iliyopita sikula wala kunywaย maji tena.ย
Siku iliisha bila geti langu kufunguliwa, giza liliingia, Kiuย ilinibana sana na njaa ilizidi kuniuma, niligonga nifunguliweย lakini hakuna aliyefungua mlango na hakukuwa na daliliย iliyoonesha kuwa kulikuwa na Watu karibu. Siku hiyo iliisha,ย Usiku uliingia, nilijaribu kuutafuta Usingizi lakiniย sikuupata, nilikaa macho hadi kulipopambazuka, mwili ulikuwaย na alama za kung’atwa na Wadudu na mbu.ย
“Mnifungulie nitakufa jamani” Nilisema kwa sauti isiyo naย nguvu kabisa, siku mbili bila kula tena nikitoka kufanya kaziย haikuwa rahisi kwangu kukabiliana na hali ile, haikusikikaย sauti yoyote upande ule, niligumia kwa muda mrefu hadiย nilikata tamaa ya Mtu kunisikia, nilirudi nikakaa chiniย nikaegemea ukuta nikiwa nimechoka sanaย
Baadaye kidogo nilisikia sauti ya geti langu kufunguliwa,ย niliamka haraka, ilitupwa bakuli moja kisha palifungwa,ย nilikimbilia kwanza getini kisha nilisemaย
“Mnitoe humu nitakufa, kwanini mnakuwa wakatili kiasi hicho,ย mnanitendea hivi kama nimeuwa?” Nilisema kwa sauti ya juu,ย sauti ya Mtu kutembea ilikoma kisha ukimya ulisikika,ย niligeuza macho yangu kwenye ile bakuliย
Nilisogea kuangalia kulikuwa kuna nini, niliifungua kishaย niliona Mchuzi mwepesi sana na kipande kidogo cha Muhogoย kilicho pikwa. Nililishika lile bakuri huku moyo ukiniumaย sana, yaani kukaa siku mbili bila kula alafu niletewe mchuziย na kipande kidogo cha muhogo? Nilitamani nimwage tu maanaย sikuona kama nilistahili, ila nilipokumbuka kuwa nipo Jelaย nilifakamia mchuzi huo kisha nilikula muhogo.ย
Angalau kidogo nilikuwa nimekata kiu lakini njaa ilibakiaย pale pale. Sekunde chache nilikuwa nimemaliza kula kishaย nilikaa chini, Muda ulizidi kwenda, siku zilienda nikiwaย ndani ya chumba hicho cha Mateso.ย
Macho yangu yakazoea giza, Uchafu ukatawala mwili wangu,ย nilikojoa humo humo na kujisaidia haja kubwa humo humo, njaaย iliponizidi nilikula kinyesi changu sababu nilikuwaย nikiletewa supu kila baada ya siku mbili, nilianza kukonda naย kudhohofika, sura yangu ilinyauka kutokana na kukosa chakula.
Usiku mmoja nilikuja kuchukuliwa nikiwa hoi bin taabani, haliย yangu ilikuwa mbaya kupita maelezo, nilikuwa nimelegea sanaย hata kuongea siwezi, nilichokuwa nasubiria ni ujio wa Malaikaย mtoa roho pekee aje anichukue maana sikuwa na tumaini tena laย kuendelea kuishi.ย
Nilipelekwa kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa na taa,ย mbele yangu kulikuwa na meza iliyokuwa na chakula chaย kutosha, niliambiwa nile nishibe. Taratibu nilianza kulaย chakula kile ambacho kilikuwa cha moto hivyo kilinipa nguvuย sana.ย
Angalau nilipata unafuu sana, mwili uliingia nguvu hadiย nilipata uwezo wa kumuuliza Mdada aliyekuja kunichukua kuleย kwenye chumna chenye matesoย
“Kwanini mlitaka kuniuwa?” Nilimuuliza kwa sauti ya uchovuย kiasiย
“Majibu utayapata muda siyo mrefu” Alisema, niliendelea kulaย huku nikisubiria hayo majibu. Punde aliingia Sarafinaย
“Jojo” Alisema kisha aliketi kwenye kiti, alichukua chakulaย kidogo akala kabla ya kusema chochote kile, nilimtazama sanaย Sarafinaย
“Kwanini ulitaka kuniuwa Sarafina, ni kosa gani ambaloย halisameheki hadi kufikia hatua ya kutaka kuondoa uhaiย wangu?” Nilimuuliza Sarafina huku chozi likianzaย kunibubujika.ย
“Kiukweli sikutegemea baada ya muda huo uliokaa kule ungetokaย ukiwa hai Jojo, hakika wewe ni miongoni mwa wachache wenyeย roho ngumu sana, wengi walifia mle ila wewe umetoka, Hongera”ย Alinipongeza Sarafina, ila niliona kama ananikaidisha tuย
“Unanipongeza kwa lipi ikiwa ulitaka nife? Wewe ni mnyamaย Sarafina…hadithi ya Maisha yangu imebadilika ghafla sana”ย Nilisema huku nikiwa ninafuta chozi languย
“Sarafina, kama kifo changu kitakuwa furaha kwako usisiteย kunimaliza ili nipumzike hii mitihani mizito ambayo imekuwaย ikiniandama baada ya Mama yangu kufa, sitaki kuingia kwenyeย mtihani mwingine, imetosha, nimeteseka sana Mimi Sarafina,ย ona nimedhohofika sina hata nguvu” Nilisema kwa uchungu sanaย huku nikiwa ninabubujikwa mchozi.ย
Sarafina alifuta chozi lake lililokuwa linaanza kumtoka,ย stori yangu ilimfanya alie kidogo japo baadaye alijifanyaย haijamuumiza
“Sikia Jojo, ukiishi kwa kuhitaji huruma ya wengine utaishiaย kuishi Maisha ya hovyo sana. Lengo la kukutoa mle ni kutakaย kufanya na wewe baadhi ya Majukumu kisha utaachiliwa huru”ย Nilishtuka sana kusikia kuna majukumu nataka kupewa, nilifutaย chozi kisha nilimuulizaย
“Majukumu?”ย
“Ndiyo! Kwasasa angalia Afya yako kwa mwezi mzima kishaย utakapokuwa sawa nitakuchukua tena” Hakunipa hata nafasi yaย kumuuliza chochote kile, aliondoka zake. Yule Mdada mwingineย alisogea akaniambiaย
“Unapaswa kwenda Hospitali” Alininyanyua kisha alinitoa pale,ย Ulikuwa ni usiku mwingi sana, nilipelekwa Kwenye hospitali yaย pale pale Magereza.ย ย
Nini Kitaendeea?ย Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?ย
Usikose SEHEMU YA TISA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย
9 Comments
Nomaaaa
Kazi nzuri๐ช๐ฅ๐ฅ
Kaz nzuri ๐ช๐ฅ๐ฅ
Nyie mnafikiri ni majukumu gani anapewa
Dah hii ya leo mpaka machoz
Dah pole Sana sarafina
Napenda tahalifa za kijiwen
f4lc82
tzbg6s