Ilipoishiaย
“Ingia kwenye gari” ilikuwa kama ndoto vile, nilifunguaย mlango wa gari ili niingie kwenye gari. Kabla hata sijaingiaย nilihisi uzito kwenye mgongo wangu alafu nilipata nguvu yaย kuulizaย
“Nani wewe!” Niliuliza kwa sauti ya juu mno kisha nilionaย kama vile Dunia ilikuwa imesimama, ghafla nilisikia sauti yaย kugongwa kwa mlango. Mara nilijikuta nikirushwa pembeni,ย nilitumia nguvu ya mwisho kuangalia niliona pikipikiย ikianguka kando yangu ndipo nilipogundua kuwa nilikuwaย nimepata ajali ya Pikipiki. Sikuelewa kilichoendelea, mzimuย wa laana na matatizo uliendelea kuniandana. Endeleaย
SEHEMU YA SABA
Nilizinduka nikiwa Amana Hospital, daktari alikuwa kandoย yangu akiangalia jinsi nilivyokuwa nikiamka kutoka katikaย Usingizi mzito wa ile ajali, nilikuwa na maumivu makali yaย Mgongoย
“Tulia utakuwa sawa” Alisema Daktari huyo ambaye alianzaย kukagua macho yangu kisha aliniulizaย
“Unaitwa Nani?”ย
“Naitwa Jojo” nilijibu kwa maumivu makali sana.ย
“Unaishi wapi?” Aliniuliza, nilitikisa kichwa ishara ya kuwaย nilikuwa sina makaziย
“Ndugu zako wapo wapi?”ย
“Sina ndugu hapa, wapo Tabora…..aliyenileta hapa yupoย wapi?” Nilimuulizia yule Msaniiย
“Umeletwa hapa na wasamalia wema tu hata hivyo wameondokaย zao”ย
“Msanii hajafika hapa?”ย
“Hakuna aliyekuja kukuona” Alijibu yule Daktari kishaย aliniambiaย
“Unapaswa kwenda soba kwanza ili kukuondoa kwenye matumizi yaย madawa, vipimo vimeonesha damu yako inakiwango kikubwa chaย madawa ya kulevya” Alisema yule Daktari kisha alisemaย
“Gharama zote zitalipwa na Hospitali”ย
“Asante sana” nilisema, nilifurahi kwa upande mmoja sababuย sikupenda kuwa Mtumwa wa madawa ya kulevya tena.ย
Nilipopata unafuu nilipelekewa Soba, nilifundishwa vitu vingiย mno, nilikutana na wengine ambao walikuwa wameathirika zaidiย na Madawa ya kulevya, niliishi huko kwa zaidi ya miezi sitaย hadi nilipopona kabisa na kuacha matumizi ya dawa za kulevya.ย Baada ya hapo, nilikabidhiwa kwa Mama mmoja ambaye alikuwaย akiitwa Mama Zahara, alikuwa ni Mama fulani mnene hiviย
“Utaenda kuishi kwake sababu huna mahali pa kwenda kuishi,ย huko mtaani utarudi tena kwenye ulevi” Alisema Mtu wa Soba.ย Nilifurahia sana kwenda kuishi kwa huyo Mama, niliona naendaย kufungua ukurasa mpya wa Maisha yangu, ukurasa ambaoย utatengeneza upya Maisha yangu.
“Utaishi kwangu kwa Muda kisha utaamuwa kama utaendelea auย utarudi kwenu Tabora” Alisema Mama Zahara, basi tuliingiaย kwenye gari yake kisha tulienda nyumbani kwake, alikuwa naย nyumba nzuri sana kubwa ambayo alikuwa akiishi na Wasichanaย waliotoka Soba.ย
Niliishi hapo kama Mwanafamilia, Maisha yalikuwa mazuri sana,ย tulipewa kila kitu, hadithi za walio wengi pale walikuwaย hawana makazi kama Mimi, wengine waliondoka na wengineย tulibakia.ย
Miezi miwili ilikatika nikiwa hapo kwa Mama Zahara, Siku mojaย Mama Zahara alisafiri, alituaga kuwa anaenda Mombasa Kenya.ย Alituhasa sana kuendelea kuishi kwa upendo wa hali ya juuย sana na pia kuishi kwa kujali afya na malengo yetu,ย alipoondoka kila mmoja aliachiwa pesa yake kwa ajili yaย kujikimu kidogo maana alikuwa anaenda kukaa huko kwa kipindiย cha mwezi mmoja.ย
Kulikuwa na Mdada aliyeiywa Salome, tulijenga ukaribu sana,ย alikuwa na hela nyingi kuliko Msichana yeyote pale, nilipataย shahuku ya kumuulizaย
“Hivi Salome hizo pesa unatoa wapi?” Kwanza alicheka kishaย alinijibuย
“Nazitafuta Jojo, unafikiria pesa inaokotwa?”ย
“Sijamaanisha kuwa inaokotwa ila nimeuliza ili nijuwe”ย
“Jibu zuri ni matendo, kesho ni Jumamosi, usiku tutoke”ย Alisema Salome, alikuwa ni Mdada fulani mnene kiasi mweusi,ย macho yake yalikuwa makubwaย
“Usiku tena?”ย
“Ndiyo, hofu yako ndiyo umasikini wako, ni lazima Jojoย ujifunze kutengeneza pesa kwa ajili ya Maisha yako,ย unafikiria siku ukiondoka hapa kwa Mama Zahara utapewa pesaย ya kuanzia Maisha? Utapewa nauli tu, sasa utaishi vipi hukoย kwenu?” Alisema Salome, maneno yake yalikuwa na mashikoย kwenye ufahamu wangu, alichokisema niliona kina ukweliย
“Sawa tutaenda” Nilimkubalia bila kujuwa alikuwa anatakaย kunipeleka wapi, wakati huo ule uzuri wangu ulikuwa umerejeaย tena kwa kasi sana sababu nilikuwa naishi vizuri sana paleย kwa Mama Zahara.
Siku iliyofuata Usiku tulitoka tukiwa tumevalia vinguoย vifupi, japo nilimuuliza tulikuwa tunaenda wapi ilaย aliniambia nitaona, nilimuamini sababu alikuwa ndiye rafikiย yangu pale kwa Mama Zahara.ย
Tulichukua Taxi hadi Magomeni, ilikuwa mishale ya usiku waย saa tano, tulipofika aliniambia tusubirie. Tulisimamaย barabarani tu, baridi lilikuwa kali sana pale kiasi nilikuwaย najikunyata.ย
“Tutasimama hadi saa ngapi Salome? Mimi nimechoka” nilisema,ย kiukweli tulisimama kwa zaidi ya nusu saa, alikuwaย akisimamisha magari binafsi ya Watu lakini yalikuwaย hayasimamiย
“Salome nimechoka mwenzio” Nilisema huku hasira ikianzaย kunishikaย
“Unataka kuharibu sasa si ndiyo?”ย
“Salome hii ni Biashara ya Ngono unaifanya si ndiyo? Sasa siย bora ungeniambia kule nyumbani unafikiri ningekuja huku Mimi?ย Yaani sijui mimi nakuwaje Aisee huwa naingizwa kwenye mamboย yasiyofaa kirahisi sana” Nilisema kwa kujilaumu, Salomeย alirudi kuendelea kusimamisha gariย
Nilikaa pembeni, Idadi ya Wanawake hapo ilianza kuongezeka,ย walivalia kama sisi tulivyovaa na wengine walikuwa wakivutaย sigara, niliyachukia Maisha yale kabisa, nilimfuata tenaย Salomeย
“Kama huwezi kuondoka na Mimi basi nitaondoka mwenyeweย Salome” Nilisemaย
“Nipe dakika tano tu nakuomba Jojo kisha tutaondoka” Alisemaย Salomeย
“Sawa ni dakika tano tu baada ya hapo sitakuwa na muda waย kuendelea kukusubiria” Nilisema kisha nilirudi kuketi kandoย kidogo ya waliposimama waoย
Baadaye niliona gari ikisimama, Salome alianza kuzungumza naย Mtu wa kwenye gari japo sikusikia walichokiwa anakizungumzaย ila nilihisi itakuwa amepata Mtejaย
Alikuja akaniambiaย
“Si ulikuwa unataka kwenda nyumbani? Basi wewe nenda mimiย nitarudi asubuhi” Alisema Salome
“Sasa ulichoniletea huku ni nini Salome? Aaah” nilisema kwaย kuchukia sanaย
“Nenda Jojo tutaongea nyumbani ila usimwambie Mtu yeyote”ย Alisema Salome kisha alikimbilia kwenye gari akapanda kishaย gari iliondoka. Nilichukia mno istoshe kiatu kilikuwaย kinanibana sana mguu wa kushoto, niliamuwa kukivua iliย nisizidi kuumia.ย
Nilisimama pembezoni mwa waliposimama wale wanawakeย wanaojiuza, nilikuwa nasubiria gari ya kurudi nyumbani.ย Ghafla nilisikia purukushani, nilipogeuka niliona waleย wanawake wakikimbia huku na kule huku wakipiga mayowe.ย Nilihamaki, nilihitaji kujuwa wamepatwa na nini, pundeย niliona Watu waliovalia sare za polisi.ย
Nami nilianza kukimbia, polisi wawili wakawa wananikimbiza,ย walinikamata mita chache tu kabla hata sijafika mbali.ย
“Naomba mniache tafadhali” nilisema wakiwa wananipelekaย kwenye gari ya polisiย
“Wanawake wa Siku hizi bwana, Mwanamke mzuri kama weweย ujiingize kwenye biashara ya ukahaba, twende tukakufundisheย kazi huku” Alisema Askari mmojaย
“Mimi siyo kahaba nilikuwa nasubiria gari nirudi nyumbani,ย sijawahi kuuza mwili katika Maisha yangu” Nilijaribuย kujitetea kidogo ili niachwe.ย
“Twende utajuwa huko huko kama ulikuwa ukiifanya hiyoย biashara au ulikuwa hauifanyi” Alinijibu yule askariย
“Kweli mimi sijafanya kama mnataka nimpigie ndugu yanguย ambaye nilikuja naye huku” Nilisema tenaย
“Ndugu yako atakuja kituoni kutoa maelezo huu siyo muda waย maelezo” Alinijibu Polisi mwingine, tayari tulikuwaย tumeshafika kwenye gari. Waliniingiza kwenye gari ya Polisi,ย Wale makahaba nao walikuwa wamekamatwa pia.ย
Tulipelekwa kituo cha Polisi, tulitupwa Mahabusu. Sikuย iliyofuata niliitwa na Polisi nikaambiwa niwapigie nduguย zangu ila kibaya sikuwa na simu wala namba ya Mtu kichwani,ย angalau ningempigia Salome au hata Mama Zahra lakini hataย hivyo Mama Zahra alikuwa nje ya Nchi ningempata vipi?ย
“Afande siijui namba ya Ndugu yangu hata mmoja ila naombaย nipo chini ya Miguu yako twende nyumbani kwetu,ย
watakuthibitishia kuwa Mimi sijiuzi kabisa” Nilisema, yuleย Polisi alicheka akasemaย
“Hayo ndiyo maneno yenu, nakusikitikia sana Ndugu yanguย sababu Rais ametoa maagizo makali sana kuhusu Biasharaย mnayofanya, siku tatu zijazo mtafikishwa mahakamani naย mtahukumiwa kufungwa Miaka mitatu au Faini isiyopunguaย Milioni 6” Alisema yule Polisiย
“Kaka yangu wewe una ndugu au hata Dada kama Mimi, naombaย usimame kama Kaka kwangu niangalie Mdogo wako ninavyoteseka”ย Nilisemaย
“Nikisema nisimame kama Kaka nitasimama kwa wangapi?ย Tutakomesha hii Biashara kweli? Nenda ukafunzwe na Walimwenguย huko uendako” Alisema kisha nilirudishwa Mahabusu. Ni Mimiย peke yangu ndiye niliyekuwa nikilia ndani ya Mahabusu sababuย sikuzoea maisha yale kabisa.ย
Nilionekana kero kwa wale mahabusu wengine wakawa wananisemaย sana nijikaze sababu Biashara ile ndiyo kila kitu, nilijaribuย kuwaambia kuwa Mimi siyo kahaba ila hawakutaka kunielewaย kabisa wakasema kama siyo kahaba nilifikaje pale? Naย nilijuana vipi na Salome wakati Salome ni kahaba wa mudaย mrefu?ย
Sikuwa na utetezi kabisa, niliishia kulia tu. Ukurasa wanguย mzuri wa Maisha ambao ulifunguka na kunipa furaha sanaย ulianza kuchanika, nilijikuta nikirudi kwenye Maishaย yaliyojaa giza tena, niliishi hapo kwa hizo siku mbili naย hakuna aliyekuja kunitafuta.ย
Siku ya tatu tulipelekwa Mahakamani, Polisi walisimama kamaย Mashahidi, nililia sana Mahakamani ili niachiwe lakiniย haikusaidia. Hakuna hata mmoja kati yetu aliyekuwa na kiasiย cha Shilingi Milioni 6 ili asifungwe, sote tulihukumiwaย kifungo cha miaka mitatu.ย
Tulipelekwa gerezani, siku tunavalishwa sare za Gerezani naย kukatwa nywele zetu ndipo nilipoamini kuwa nilikuwaย nimetumbukia kwenye shimo lenye giza, nilifikiria Miakaย mitatu ilivyokuwa Mingi nitaweza kuishi gerezani kweli? Kamaย kulia nililia sana hadi mwili ulishika moto lakini hakunaย kilichosaidia, kilio changu na machozi yangu yaligeuka kuwaย chozi la samaki lisombwalo na maji, hakuna aliyenisikia walaย kuthamini chozi langu, kila Mtu alikuwa na matatizo yakeย ndani ya Gereza hivyo isingelikuwa rahisi kusikilizwa.
Nilikubaliana na hali halisi, niliyaanza Maisha mapya ndaniย ya gereza. Maisha yaliyojaa ubabe, uonevu, utata, manyanyasoย na kazi ngumu sana. Tulifanya kazi ngumu na kupewa chakulaย kidogo tena hicho kidogo anakuja Mtu anakuchukulia kwa ubabeย wake na hakuna cha kumfanya.ย
Nilimpata rafiki ndani ya gereza, aliyeitwa Isabela nayeย alikuwa Mtu wa Tabora hivyo tulikuwa na memgi ya kuzungumza.ย Yeye alihukumiwa kwa kosa la kumkata Mkono kimada wa Mumeย wake, japo tulikuwa katika nyakati ngumu sana ila tuliishiaย kucheka tuu maana hakukuwa na njia nyingine zaidi kutumikiaย adhabu, Mume wake hakuwahi kuja kumuangalia Gerezani kwaย miezi zaidi ya mitatu. Isabela alihukumiwa kifungo cha miakaย miwili tuย
“Ukishamaliza kifungo una mpango gani?” Nilimuuliza Isabelaย tukiwa shambani tunalimaย
“Kurudi Tabora tu maana nimegundua Mume wangu hanipendiย kabisa licha ya kumzalia Mtoto mmoja, angekuja kunionaย angalau ningekuwa na tumaini. Ila najutia sana hasira zangu,ย ona nateseka mwenyewe kwa ajili ya mtu ambaye hajali chochoteย kuhusu Mimi” Alisema, niliona jinsi alivyokuwa na maumivuย moyoni, ghafla nilijiona sina matatizo kabisa.ย
“Pole sana Isabela, yataisha tu. Ukifika Tabora nendaย nilipokuelekeza waambie nipo Gerezani” Nilisema.ย
Basi Maisha ndani ya Gereza yaliendelea, siku moja baada yaย kazi ilikuwa ni majira ya saa 7 Mchana, ulikuwa ni muda waย kupata Chakula. Tulikuwa tukipanga mistari miwili kwa ajiliย ya kupata Chakula, msitari wa kwanza nilikuwepo Mimi, sasaย katika tazama tazama nilistaajabu nilimuona Sarafina, yuleย Mdada ambaye alifukuzwa na Shonaa kisa Mimi, nilitamaniย kumuita ila nilikumbuka kuwa alikuwa na hasira na Mimi,ย nilimgeukia Isabela nikamuulizaย
“Yule yupo hapa kwa muda gani?” Nilimuonesha kidole Sarafinaย
“Nimemkuta hapa, anaonekana kahukumiwa muda mrefu ilaย inasemekana aliiba pesa kwa tajiri mmoja”ย
“Vipi unamjuwa?”ย
“Ndio namjuwa” Basi baada ya kuwa tumeshachukua chakulaย tulienda kula, Isabela aliniulizaย
“Unamjua vipi yule”ย
Nini Kitaendeea?ย Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?ย
Usikose SEHEMU YA NANE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย
ย ย
7 Comments
Aiseee huyo dada nae kama chizi
Kila siku ni ukurasa mpya maishani
Asante
Looh jamani Jojooo anakuwa zuzu
sehemu ya nane please
Ndivyo mungu anatupitisha magumu ili kujifunza na kuwa bora zaidi
jv1556